Huyu ndie Mwalimu wangu aliyenifundisha kuandika!

Leo naomba niwaonyeshe mama yangu kipenzi na Mwalimu wangu aliyenifundisha kuumba herufi, kutofautisha herufi  kubwa na ndogo na wapi pakuzitumia. Kisha akanifundisha jinsi ya kuandika neno moja moja, na jinsi ya kuandika maneno zaidi ya moja ili kuitwa sentence. 

Hili somo lilikuwa linaitwa "Mwandiko" nilikuwa darasa la kwanza pale Mgulani Chini Primary school! Yeye anaitwa Mwalimu Massam, lakini kwa heshima zaidi tulikuwa tunamuita Mwalimu-mama Massam! Kwani kwanza alitupenda wanafunzi kama wanae, alitufundisha kwa upendo na unyeyekevu mwingi sanaaaaaa! Such a humble Mwalimu. Pia alikuwa jirani yetu hivyo kumuita mama ilikuwa si jambo la kushangaza!
Mwalimu-mama Massam
Namshukuru sana kwa msingi wa elimu aliyo tupatia.......Pendo na wadogo zako najua mtasoma huu ujumbe tafadhali naomba mumfikishie ujumbe huu mama yangu. Mungu azidi mbariki sana. Nikija lazima nimtafute. 
#NeverForgetYourRoots 
#MyHumbleBeginnings

 

Leave a Reply