Rais Magufuli aonyeshe hasira zake dhidi ya Ufisadi kwenye huu ufisadi mkongwe wa IPTL- Zitto Kabwe

fb_img_1474302356894Nimesoma ‘ arbitral award ‘ ambayo Benki ya Standard chartered wametunukiwa na ICSID ( case no. ARB/10/20 ) na kuumizwa sana kutokana na kwamba hoja zote ambazo zimetumika kuwapa ushindi SCB ndizo Kamati ya PAC ilizijenga kwenye Taarifa yake Maalumu iliyopitishwa na Bunge na kutolewa maazimio 8. Ndio hoja hizo hizo zilibezwa na Serikali chini ya Waziri Sospeter Mwijarubi Muhongo na umma kuambiwa kuwa TANESCO hawatakuwa na madai dhidi Yao.

Mahakama hii ( tribunal ) ya ICSID imethibitisha maonyo ya PAC kwamba hasara Kwa Nchi kwenye kashfa ya #TegetaEscrow itakuwa Ni mara mbili ya Fedha zilizochotwa kwani mwenye Mali akijulikana tutapaswa kumlipa tena. Tulimpa Harbinder Singh Seth tshs 306 bilioni na tunapaswa kuwalipa SCB tshs 320 bilioni. Jumla tshs 626 bilioni. Na bado tunamlipa Seth kila Mwezi $4m Kwa umeme wa mtambo alioupata kitapeli.

ICSID imesema IPTL Ni Mali ya Standard Chartered Bank.

Rais John Magufuli ana fursa ya kihistoria kumaliza kabisa huu mtandao wa wizi na utapeli uliodumu toka mwaka 1995.

Leave a Reply