Tanzia: Pumzika kwa amani Advocate Jacob Sarungi!

Marehemu Jacob Emmanuel Sarungi enzi za uhai wake

Kwamasikitiko makubwa sana naomba kuweka kumbukumbu hii ya kifo cha kaka yangu (first cousin brother) Advocate Jacob Emmanuel Sarungi kilichotokea siku ya Ijumaa tarehe 15, May; 2020 kwa ajali ya gari maeneo ya kona ya Mikese, Morogoro, Tanzania. Marehemu alikua akielekea Dodoma kikazi ndipo mauti ilipo mkuta. Marehemu ameacha mke na watoto, wazazi, pamoja na kaka na dada zake.

Kuna vitu vya kuandika lakini sio kifo cha mtu yoyote yule! Ni ngumu sana, haswa unapoona kijana ambaye ana maono makubwa, nguzo imara ya familia, moja ya watu ambao anategemewe katika kuongoza ukoo fulani, na nguvu kazi ya taifa inaondoka wakati ndio kwanza ameanza mwendo, amewasha mshumaa wake teyari kuimulika dunia halafu ghafla unazimika! Unajikuta unamaswali mengi sana lakini kwakua tunaimani katika Mungu hivyo tunaamini kazi ya Mungu haina makosa!

Natoa pole zangu za dhati kabisa kwa mke wa farehemu, watoto, wazazi, ndugu, marafiki, wanasheria wenzake wote walioguswa na msiba huu haswa chama cha wanasheria (Tanganyika Law society), wafanyakazi wenzake, pamoja na ukoo wote wa Chief Sarungi Igogo.

2 Timoth 4: 7-8 …. “7Nimevipiga vita vilivyo vizuri, mwendo nimeumaliza, Imani nimeilinda; 8baada ya hayo nimewekewa taji ya haki, ambayo Bwana, mhukumu mwenye haki, atanipa siku ile; wala si mimi tu, bali na watu wote pia waliopenda kufunuliwa kwake.”.

R.I.P brother! Bwana alitoa na Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe milele zote ????

Watu wengi wameguswa na msiba huu, na zifuatazo ni baadhi tu ya jumbe zilizo andikwa na ndugu pamoja na mara fiki

 • ???? Huo ulikua ni ujumbe wa masikitiko toka Mwanasheria mwenzake, na dada yake Janeth Igogo ambao aliuandika kupitia account yake ya WhatsApp
 • Naye dada wa marehemu Maria Sarungi-Tsehai kwa kupitia account zake ya Instagram na Facebook aliandika ujumbe huo ? hapo akionyesha ishara ya kuguswa na kusikitishwa na msiba huu.
Kwa kweli, kwa masikitiko makubwa sana nimepokea taarifa ya kifo cha kaka, ndugu, jamaa, rafiki na mwanasheria msomi mzuri kijana wetu damu ya Rorya Jacob Sarungi (Adv).Moyo wangu umeugua sana. Najikongoja kifikra kukubali kuwa Adv Jacob Sarungi ameaga dunia.Jacob alikuwa ni kijana mweye ndoto nzuri na pevu sana kwa ujenzi wa Rorya Mpya.Jacob ameacha familia changa sana nyuma yake na vijana waliomtegemea sana kujifunza katika tasnia ya sheria.Imeniuma sana. Jacob alitegemea njonzi yake ingekuwa angavu kwa maisha ya familia yake, wanarorya, jumuiya ya wanasheria na watanzania kwa ujumla.Tumbo la dunia lihifadhi mwili wake kwa amani. Namuomba Mungu mwingi wa rehema aipokee roho yake ikisubiri parapanda ya mwisho.Bwana alitoa, Ndiye ametwaa.Jina lake lihimidiwe. ??????                                                                 Maina Ang'iela Owino.©2020. 
 • REST IN PEACE BROTHER JACOB SARUNGI.Ni Mapema sana kuamini kwamba umerudi kwa Muumba wetu. Mungu akupe kauli thabiti huko uendako, nasi atupe uvumilivu wa kustahimili maumivu haya sisi tuliobaki.
 • Ujumbe huu ulitoka kwa mdogo wa marehemu Mwanasheria na mpatanishi wa serikali (government Arbitrator) Magreth Igogo ambao aliandika katika kupitia account yake ya WhatsApp

Kama ilivyo semwa na wengi kua ni ngumu kuamini lakini hatuna budi kukubali kuwa hiyo ndio hali halisi. Mungu awe nanyi wakati wote haswa katika kipindi hichi cha maombolezo.

Rest easy brother you are gone but you will never be forgotten ????

Leave a Reply