Kesha la asubuhi: Ujasiri

```KESHA LA ASUBUHI```

*JUMATATU MACHI 26, 2018*

*Ujasiri*
_Basi msiutupe ujasiri wenu, kwa maana una thawabu kuu. Waebrania 10:35._

? Yohana anasema, “Na huu ndio ujasiri tulio nao kwake, ya kuwa, tukiomba kitu sawasawa na mapenzi yake, atusikia. Na kama tukijua kwamba atusikia, tuombacho chote, twajua kwamba tunazo zile haja tulizomwomba” (1 Yohana 5:14, 15). Hebu tudumishe zaidi wazo hili kwa watu, ili mawazo yao yapate kupanuliwa, imani yao iongezeke.

? Hebu watiwe moyo kuomba kwa upana zaidi na kutegemea bila mashaka utajiri wa neema yake; kwani kupitia kwa Yesu tunaweza kuja kwenye chumba cha kuzungumza naye Aliye Juu. Kupitia kwa stahili zake tunayo fursa ya kumfikia Baba kupitia kwa Roho huyu mmoja.

? Laiti tungekuwa na uzoefu mkubwa zaidi katika maombi! Tunaweza kumjia Mungu kwa ujasiri, tukijua maana ya kuwepo kwa Roho Mtakatifu na nguvu yake. Tunaweza kuungama dhambi zetu na pale pale, huku tukiomba, tujue kwamba Yeye anasamehe makosa yetu, kwani ameahidi kusamehe. Ni lazima tuiweke imani katika matendo na kudhihirisha uaminifu wa kweli na unyenyekevu.

? Kamwe hatuwezi kufanya hivi bila neema ya Roho Mtakatifu. Ni lazima tulale chini miguuni pa Yesu na tusiendekeze ubinafsi, tusioneshe namna yoyote ya kuiinua nafsi, lakini tumtafute Bwana kwa namna iliyo sahili, tukimwomba Roho wake Mtakatifu kama mtoto mdogo aombavyo mkate kutoka kwa wazazi wake. Ni lazima tufanye sehemu yetu, tumchukue Kristo kama Mwokozi wetu binafsi, nasi, huku tukisimama chini ya msalaba wa Kalvari, “Tutazame na tuishi.”

? Mungu anajitengea watoto wake kwa ajili yake mwenyewe. Nao wanapounganika Naye, wanakuwa na nguvu pamoja na Mungu na kushinda. Kwa uwezo wetu hatuwezi kufanya lolote; bali kupitia kwa neema ya Roho wake Mtakatifu, tunapewa uzima na nuru, nayo nafsi hujazwa na shauku ya dhati na hamu ya Mungu, na ya utakatifu. Hapo ndipo Kristo anapotuongoza kwenye kiti cha enzi cha neema na kutuvisha kwa haki yake; kwani Bwana Mungu wa mbinguni anatupenda.

? Kuwa na wakaidi na wenye mashaka kwa makusudi ndiko kunakoweza kutufanya kuwa na mashaka kwamba moyo wake huwa unatuelekea sisi. Wakati Yesu, Mpatanishi wetu, anapotuombea mbinguni, Roho Mtakatifu huwa anafanya kazi ndani yetu, kutaka kwenu na kutenda kwenu, kwa kulitimiza kusudi lake jema. Mbingu zote huwa zinapendezwa na wokovu wa roho moja. Sasa, tunayo sababu gani ya kuwa na mashaka kwamba Bwana anatusaidia na atatusaidia? –Signs of the Times, Okt. 3, 1892.

```MUNGU AKUBARIKI UNAPOTAFAKARI UJUMBE WA LEO```

Leave a Reply