“Mtoto Magazine”: Hongera sana Dina Marios

Nilipompata Zion kama mzazi yoyote ilikuwa ni furaha sanaa alileta furaha maishani mwangu na mwanzo mpya katika maisha yangu. FB_IMG_1456064695377Katikati maisha yangu yoote nilikuwa muoga sanaa kupata mtoto sikuwa najua nitaanzia wapi kumlea. Zile story za wakinamama waliotangulia kuwa kuzaa kunauma zilikuwa zinanipa stress saana. FB_IMG_1456070285421-1Lakini Nilimuomba Mungu nikifikisha miaka 30 Mungu anijaalie mtoto katika mahusiano yanayoeleweka. Zion hakuwa bahati mbaya siku ambayo baba yake alisema anatamani tupate mtoto Mungu aliweka tiki matamanio hayo  wiki iliyofuata nilishika ujauzito. 

Baba Zion, Zion, na mama Zion
 Baba Zion, Zion, na mama Zion kwenye ufunguzi wa Mtoto Magazine 

Nikiwa natimiza miaka 30 nilikuwa na mimba kubwa ya Zion na nikamzaa nikiwa na miaka 30 nikaamini ni mpango wa Mungu. Nilipopoteza leo tena nilihuzunika sana nikaanza kukufuru Mungu.Kwamba kwa miaka 8 mfululizo nimekilea kipindi leo nimeenda kujifungua narudi nakuta nafasi hiyo haipo kwa nini? kwa nini kuzaa kubadilishe tena ghafla? nakumbuka siku hiyo hata kunyonyesha sikuweza kabisa kabisa Lakini nikamuomba Mungu anipe muongozo anataka kunipeleka wapi?Kwa sababu ya Zion niliweza kuja na product ya mafuta ya nazi dina marios coconut baby oil. Screenshot_2016-02-21-10-26-53-1Alipotimiza mwaka mmoja picha za birthday yake ndio zilileta wazo la kuanzisha magazine ya parenting/malezi. Later nikajoin @efm_93.7 radio nakuanza kipindi kipya cha UHONDO. Screenshot_2016-02-21-10-23-37-1Na magazine cover story toleo la kwanza yupo Zion na mimi mama yake kukusimulia mengi maana yeye ndio inspiration ya hiyo magazine.Nilianza upya na MTOTO wangu Zion ndio inspiration ya mwanzo wangu mpya. Baada ya mwaka mmoja kupita wa kulipika wazo jana nikafanikiwa kutambulisha magazine ya MTOTO kwa ndugu, jamaa na marafiki waliokuja katika birthday party ya Zion. Screenshot_2016-02-21-10-22-17-1Lolote tunalomuomba Mungu atatupa lakini sio kwa picha ile tunayoitaka ni kwa namna apendavyo yeye na anavyoona inakufaaa. Usikose nakala ya MTOTO magazine kuanzia wiki ijayo kusoma mengi yahusuyo malezi ya watoto wetu . Litauzwa Tsh 5,000 tu! Screenshot_2016-02-21-09-59-26-1Hongera sana tena sana Dina kwa kuonyesha mfano mzuri sana katika jamii yetu. Mungu akuongoze ujalie mafanikio makubwa zaidi ya hapa ?

Source: Dina Marios Facebook account 

Leave a Reply