ASANTE SANA ALPHA IGOGO.COM-Peter Sarungi

Na Peter Sarungi (Next Speaker, Baba Pilato)
Na Peter Sarungi (Next Speaker, Baba Pilato)

Dunia ina badilika kwa kasi ya ajabu, katika karne hii ya sasa tunashuhudia mapinduzi makubwa sana ya TEKNOHAMA yaani teknologia ya Habari na Mawasiliano. TEKNOHAMA ni kubwa sana na ilikuwepo tangu enzi na enzi hata kabla ya kuja kwa Yesu Kristu na Mtume Mohammad SAW na ndio maana kuna maandishi ya vitabu vitakatifu vilivyodumu kwa miaka Elfu na Elfu mpaka sasa. Kwa kizazi cha sasa ni ukweli ulio wazi kwamba TEKNOHAMA kwa sehemu kubwa imeegemea kwenye mitandao ya kijamii kama blogs, facebook, tweeter, whatsapp, youtube na mengine mengi yaliyopo duniani. Ukiangalia kwa makini mienendo ya hii mitandao ya kijamii, utagundua kuwa miaka inayokuja karibuni kutakuwa hakuna haja ya kununua magazeti, kusubiri saa mbili ili upate taarifa za habari za maredio na runinga, badala yake Taarifa zote na uchambuzi wote wa habari mbalimbali ngumu na nyepesi utazipata kwa haraka kupitia mitandao ya kijamii. Hivyo kwa wale tunaopenda kuchungulia fursa tunaona uwepo wa fursa kubwa sana katika mitandao ya kijamii. unaweza kutumia mitandao ya jamii kunadi na kufanya biashara mbalimbali, kufundisha, kutangaza na kueleza fikra zako, kutoa na kupokea taarifa na habari, na akaunti yako yaweza kuwa ni press coference yako na ikawa rasmi katika kutoa matamko na maelekezo yako.

Kutokana na fursa hizi ndio maana leo nimeona nimpongeze dada yangu Igogo Alpha aliye wekeza ujuzi na ubunifu wa hali ya juu katika TEKNOHAMA kupitia blogs yake ijulikanoyo kama AlphaIgogo.com
pamoja na hongera lakini pia nikushukuru kwa kuthamini makala zangu na kuzipa nafasi katika ubunifu wako maana nilivyopitia kazi zako nilikuta ume share nakala zangu karibia zote na kunifanya nijisikie kushare fan base yako kupitia nakala zangu. Wahenga wanasema undugu unakolezwa na urafiki, hivyo naona urafiki huu utakoleza undugu kati yangu na dada yangu alphaigogo. Tuendelee kushirikiana kwa kuonyana, kupongezana na hata tukiwa tofauti katika hoja bado tunaweza kukubaliana kutokukubaliana.

#Mytake
kuna haja ya kuwa na Fan base kubwa katika mitandao ya kijamii maana naona kuna fursa nyingi sana kama utawekeza ubunifu kama wa (www.alphaigogo.com) au zaidi ya hapo maana dunia inaelekea huko na hakuna jinsi zaidi ya kufuata fursa zilipo.

asante sana

fb_img_1472436063790Kaka yangu, asante sana kwa kuthamini huu mchango wangu japo ni kidogo sana. Ninachofanya hapa ni kutoka kwa dhati ya moyo wangu na kwa mapenzi yangu binafsi. Sifanyi ili nisifiwe na mtu yoyote yule, lakini hata hivyo siwezi dharau au kukataa kupokea shukrani pale mtu anapo guswa na hichi ninachokifanya. Hivyo asante sana…….. Makala zako zina tija kwangu mimi na ndio maana naona ni vizuri nika share na wengine waone. Naomba uendelee kuzitoa kwa wingi nami nitaziwakilisha!  Natumaini tunaweza kufanya mambo mengi na mazuri pamoja ambayo yatakuwa na manufaa kwa jamii yetu inayo tuzunguka………………….Thank you much. Be blessed always!

Leave a Reply