Asie na kasoro ni Mungu pekee -Dina Marios

Alikuwepo mfalme mmoja ambaye yeye alikuwa na tatizo katika jicho lake moja la kushoto na mguu mmoja alikuwa hawezi kusimama akiwa ameunyoosha. Jicho la kushoto limefumba halioni. Siku moja akahitaji wataalamu wa kuchora wa mchore kwa umahiri mkubwa picha yake ipendeze iwe na mvuto wa ajabu pamoja na madhaifu yake.

Wachoraji mbali mbali walijitahidi kufanya walichoweza kuhakikisha hili linawezekana maana waliahidiwa dau kubwa kutoka kwa mfalme. Walichora lakini bado ule udhaifu ulionekana wazi na hazikuwa na mvuto kama yeye alivyotaka.

Basi alitokea kijana mmoja ambaye yeye alimchora mfalme kama “muwindaji flani ambaye amefumba jicho moja na amekunja mguu mmoja akilenga shabaha kukipata kile anachokiwinda. Mfalme alifurahishwa sana na picha ile na kijana akashinda.

Katika maisha ni vema tujitahidi kuficha madhaifu ya wenzetu na kuchochea yale wanayoyaweza katika maisha ili kila mtu awe na furaha siku zote bila kujali muonekano na mapungufu yake.

Muda mwingi tunanyoosha vidole kudhihaki na kutangaza mapungufu ya wenzetu, maumbile n.k Tunajifunza kuwapenda watu ndugu zetu, jamaa, wapenzi, marafiki kwa kuyapa kipaumbele yale mazuri waliyonayo ukizitafuta kasoro za mwanadamu hutazikosa ni nyingi kweli na asie na kasoro ni Mungu pekee. FB_IMG_1465217175783Dina Marios!

Leave a Reply