Dr. Milton Makongoro Mahanga azikwa leo!

Marehemu Dr. Milton Makongoro Mahanga enzi za uhai wake!

Aliyekua Mwenyekiti wa Chadema mkoa wa kichama Ilala Dr Milton Makongoro Mahanga amezikwa leo majira ya mchana saa za Africa Mashariki katika makaburi ya Tabata-Segerea. Marehemu alizaliwa April 03, 1955 na kufariki dunia siku ya Jumatatu tarehe 23 mwezi huu, mwaka 2020 katika hospital ya Muhimbili alipokua anapatiwa matibabu. Marehemu ameacha mke, watoto, na wajukuu.

Kwaniaba ya familia ya mzee Otieno Olung’a Igogo naomba kutoa salamu za pole za dhati kabisa kwa familia ya marehemu, ndugu, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), majirani, pamoja na watu wote walioguswa na msiba huu.

Kama wewe ni mfuatiliaji mzuri wa alphaIgogo.com basi utakua ulishawahi soma huko nyuma post ambayo nilieleza uhusiano wa kidugu uliopo kati ya familia yetu na marehemu. Ilikua ni wakati wa msiba wa marehemu Dr. Didas Massaburi ????(https://www.alphaigogo.com/r-p-dr-didas-massaburi/) Kwa ufupi marehemu alikua anamuita baba yangu ‘kaka’ kwani mama zao ni madada. Marehemu Dr. Massaburi, marehemu Dr. Mahanga, pamoja na baba yangu mzazi hawa ni cousin-brothers mama zao ni ndugu wa damu. Basi kwa walio wengi wanamuangalia marehemu kama Mwanasiasa lakini kwa upande wetu ni mwana familia.

Na kwa wale mnao toka Rorya najua wengine nmnaweza jiuliza udugu wetu na marehemu Dr. Phenias Ziki Makoyo?! Dr. Makoyo naye pia ni cousin-brother wa baba yangu. Marehemu baba yake Dr. Makoyo, mama mzazi wa Dr. Massaburi, mama mzazi wa Dr. Mahanga, pamoja na mama mzazi wa baba yangu hawa ni ndugu wa damu!

Hivyo basi, baada ya kusema hayo, naomba ieleweke vizuri kabisa kua sijaweka hii post kuwakilisha chama chochote kile cha siasa hapa dunia! Hii post nimeweka hapa kwasababu marehemu ni sehemu ya familia yetu, pia hawa ndugu walikuwa marafiki wazuri sana. Natamani upendo waliokuaga nao wazazi wetu tungekua nao sisi watoto pia, lakini hichi kizazi cha Dot.com kina mambo mengi hivyo tuchukuliane tu hivyo hivyo ??

Pichani juu ni baadhi ya viongozi na makada wa CCM wakiongozwa na Katibu wa Itikadi na Uenezi Mr. Humphrey Polepole. Mr. Polepole alitoa salamu za rambi rambi kuwakilisha chama cha CCM ambapo marehemu ndipo alipo anzia mapambo yake ya kisiasa.

Ni vyema kuona mifano kama hii kwa viongozi wetu wa siasa a.k.a ‘wanasiasa’ ili Watanzania waweze kujifunza kutofautisha maswala ya kisiasa na mahusiano binafsi, itikadi za dini, na mambo mengine yote ambayo sio ya kisiasa. Siasa isimame kama siasa na isichanganywe na mambo mengine kama baadhi ya wanasiasa na “wanaharakati” wanavyotaka kuigawa taifa na familia za watu, tena wengine kwa makusudi tu na chuki zao binafsi!

Marehemu amefariki akiwa mwanachama wa Chadema lakini ikumbukwe kuwa alikuwa mwana CCM kwa muda mrefu, na huko alikuwa na marafiki, ndugu, na jamaa ambao bado ni wana CCM. Hivyo inapofika swala ambalo sio la kisiasa kama hili basi ni vyema wana siasa KUVUA KOFIA YA SIASA na kuweka swala la msingi mbele! Ni hatari sana kwa taifa kama wananchi wake wataweka siasa kwenye kila jambo. Kuna watu ambao hawapendi kujihusisha na vyama vya siasa ambao ni sehemu ya familia zetu na marafiki zetu basi ni busara, haki, na pia ni lazima maamuzi yao yaheshimiwe na kila mtu, msipende kulazimisha mambo eti kila mtu lazima awe mwanachama wa chama fulani cha siasa. Nope! Kila mtu ana hiyari ya kufanya maamuzi yake na hiyo ndio DEMOKRASIA.

“4 nao watajiepusha wasisikie yaliyo kweli, na kuzigeukia hadithi za uongo. 5 Bali wewe, uwe na kiasi katika mambo yote, vumilia mabaya, fanya kazi ya mhubiri wa Injili, timiliza huduma yako. 6 Kwa maana, mimi sasa namiminwa, na wakati wa kufariki kwangu umefika. 7 Nimevipiga vita vilivyo vizuri, mwendo nimeumaliza, Imani nimeilinda; 8 baada ya hayo nimewekewa taji ya haki, ambayo Bwana, mhukumu mwenye haki, atanipa siku ile; wala si mimi tu, bali na watu wote pia waliopenda kufunuliwa kwake.” 2Timothy 1: 4-8

  • Bwana alitoa na Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe milele zote. ????

Kumradhi!

Jana niliandika kua marehemu amezikwa jana 03/25/2020 jambo ambalo halikua sahihi. Marehemu amezikwa leo 03/26/2020 katika makaburi ya Tabata-Segerea.

Naomba radhi kwa kosa hilo ambalo nilitenda bila kukusudia, ni misunderstanding ya muda ndio ilitokea. ??

Leave a Reply