Faraja Nyalandu: Sio nyakati zote nilikuwa napendeka wala kuvumilika

@Regranned from @farajanyalandu – Siku kama ya leo miaka kumi iliyopita niliitika ndio kukutunza, kukupenda na kukuheshimu mpaka kifo kitakapotutenganisha. Nilikuwa msichana, na sasa ni mwanamke. Katika wengi uliniona mimi. Umenivumilia, umenilinda, umenitunza na kunipenda. 

Sio nyakati zote nilikuwa napendeka wala kuvumilika. Kila tulilovuka limetuimarisha zaidi na si kwa uwezo wetu, bali kwa uwezo wa Mungu. Asante kwakuwanami. Asante kwaupendowako. Asante kwa Sarah Divine na Christopher Aman. Umekuwasehemu ya maishayangu, ndivyoilivyo leo, hatakeshohatamilele. Nakupenda sana. #10YearsOfLove #10thWeddingAnniversary – #regrann

Leave a Reply