“Hata wakikucheka na kukudhihaki usiache endelea”-Dina Marios

Macho Kodooo hehehehe……Wiki iliyopita @efm_93.7 tulitangaza vipindi vyetu live kutokea Kibaha mkoa wa Pwani. Huu ni utaratibu wetu ambao tumeubatiza NJE NDANI.

Katika jukwaa la nje ndani tunafanya vipindi huku tukihusisha hadhira ambayo inakuja kutuona,wasaniii kuperfom, djs wetu kuturusha plus vipaji tunavyovikuta huko tuendako.fb_img_1476195416262Sasa siku hiyo kibaha alikuja kaka ambae ni mwana sarakasi na pia hasikii wala haongei kwa maana ni mlemavu. Kaka wa watu tulikutana nae mwanzo tukamwambia asubiri tutamuita kuperfom.Akasubiri masaa kama matatu mpaka muda wake ulipofika tukamualika jukwaani.

Muda wote alikuwa ni mtulivu hana kelele wala kihoro mpaka tulipomwambia sasa onyesha uwezo wako. Wakati anaanza kuonyesha sarakasi zake watu hawakumuelewa walimtukana, kumdhihaki, kumwagia maji, na kumrushia makopo. Kikubwa yeye hakuacha kuonyesha sarakasi zake na vimbwanga vyake kubwa zaidi alikuwa HASIKII watu wanasema nini au kumdhihaki maana ni kiziwi hasikii.

Wakati hayo yakiendelea nilikuwa najisikia vibaya natamani nimwambie ondoka lakini ile nguvu yake ya kuendelea na kutosikia ikanifanya nitulie.Kilichotokea kelele za kumdhihaki Zikaanza kupungua na baada ya Muda nasikia makofi ya kushangilia na kufurahi utadhani sio wao waliokuwa wakimtukana. Nikajifunza kuwa katika maisha wakati ukianza jambo sio wote watakuelewa ila wewe ndio unajielewa na kuelewa nini unafanya.Usiache kufanya au kupigania ndoto yako Hata kama watu hawakuelewi.Ipo siku wataelewa na salute watapiga.

Juzi nimekaa na bibi yake Zion nikawa namsikilizisha wimbo wa Salome wa @diamondplatnumz akaniambia huyu kijana wakati anaanza mziki watu walikuwa wanamsema na kumuita domo domo leo vipi? Wanamuita domo? au wanasikiliza mziki wake na kuimba na kucheza? Hahahaha yaani nilicheka sana nikasema bibi Zion amewaza nini?

Anyways @diamondplatnumz utanisamehe kwa mfano huu lakini sio mimi imagine bibi Zion anajua haya…lakini leo umekuwa inspirational ya vijana wengi katika muziki.

Ewe kijana Endelea kuwa wewe
Ewe kijana Fanya unachokiweza na unachokijua
Hata wakikucheka na kukudhihaki usiache endelea……. muda utafika wataelewa……. watashangilia,watapiga makofi, wataimba, watasimulia habari zako na watajivunia wewe!

Leave a Reply