Category Archives: Inspirational stories

Jinsi nilivyo kuja Marekani!

Andrews university ndio chuo kilichonipa nafasi mimi ya kuja Marekani. Ngoja niwape story fupi ya safari yangu ya kuingia hapa.

Siku zote nilikuwa natamani kusoma /kuishi nje ya Tanzania.  Na mara nyingi nilikuwa napenda Australia, UK, na Marekani. Ilikuwa rahisi kujenga hisia zangu na maeneo hayo kwani mara nyingi nilivahatika kupata vijuzuu vinavyoonesha shule mbalimbali za nchi hizo. Basi, nikiwa katika muhula wa mwisho wa kumaliza chuo pale C.B.E siku moja nikiwa kanisani Temeke SDA, katika matangazo nikasikia wakitangaza kuwa chuo cha Andrew wanapokea wanafunzi kwa muhula wa Fall (Fall semester), na wakasema kuna vijuzuu kama kuna mtu angependa kwenda akachukue ili ujuwe jinsi ya kujiunga. Mara baada tu ya ibada, nikaenda kuchukua kijizuu. Baada ya siku kadhaa nikaenda kwenye intranet Cafe fulani ilikuwa karibu na chuo cha C.B.E. Ndio kwa mara yakwanza nafungua email akaunti yangu 🙈 Nikajaza fomu siku hiyo. Baada ya muda wa miezi kadhaa nilitumiwa barua kwa njia ya posta kuwa wamenikubali kuingia chuoni hapo kwaajili ya degree ya kwanza.  Wakati huo nilikuwa nimesha hitimu C.B.E sasa natafuta chuo cha kwenda.

Nakumbuka mmoja wa wadogo zangu (cousin sister) aitwaye Detta alikuwa akipenda kunitania kuwa “aah wewe ni wa hapa hapa tu” namwambia mie nakwenda zangu Marekani subiri utaona. Hapo sijajua kama nitachaguliwa au la! Ila yeye alikuwa anasema hivyo kwasababu dada yangu mkubwa alisoma China, kaka yangu alikuwa UK, na mdogo wangu yeye alikuwa anasoma South Africa. Hivyo akawa anasema mie nitabaki Bongo.

Ghafla, siku moja naletewa barua nikiwa job (niliajiriwa na Utegi Technical Enterprises Ltd baada ya kumaliza chuo), kuangalia ilipotoka nakuta ni Andrews University.  Nikaifungua haraka sana! Nikakuta ni barua ya kukubaliwa kujiunga na chuo ila sasa muda ulikuwa umebaki wiki 2 tu shule ianze 🙆🏽‍♀️🙆🏽‍♀️ Nikachanganyikiwa maana hizo hela zinazo hitajika na muda uliobaki, dah! Yule mzee kutoka kanda maalum nitamuingiaje?! 🤣 Mtu wakwanza kumwambia alikuwa ni mama. Yeye akanipa moyo akasema hongera sana, mwambie baba haraka sana. Sasa kesho yake hasubui tumesha maliza kunywa chai tunataka kwenda kazini, mama akalipua bomu kimtindo. 🙆🏽‍♀️

Akasema “Umesha mwambia baba?”, nikajifanya kutoa macho 😅 baba akauliza nini unataka kusema? Akasema (Akaniita kwa jina langu la kilugha) kaa chini “let’s talk ni nini”. Ikabidi nimwambie. Akasema sasa kwanini naogopa kusema jambo zuri kama hilo. Nikamwambie mzee nikienda siku yakwanza tu inatakiwa malipo ya awali ya nusu semester (muhula) au ada nzima. Kanijibu sasa tatizo ni nini? Kwani wewe ndio unatoa hizo pesa? Basi mzee wa watu siku hiyo akasimamisha shughuli zake zote, kuhakikisha napata documents zote zinazohitajika na kuzituma kwa njia ya fax na DHL. Chuo nao walikuwa shapu walipoamka tu wakatuma email kua sawa wanasubiria documents za DHL halafu watatuma I-20 (form maalum yakuombea viza ya shule). Mzee aliwaambia kutoka na muda watume kwa DHL halafu atawalipa hiyo pesa. Basi baada ya wiki 1-20 imefika. Nikaweka appointment ya kuomba viza. Tukaenda kwenye Viza, kumbuka nina siku tu zakuripoti shule, hivyo ticket ya ndege ilibidi nikate kabla hata ya kupata viza.
Kwenye viza si kidogo watuzingue! 🤣🤣

Basi, tumefika kwenye viza wala sikuhojiwa maswali mengi, wakasema kila kitu kipo vizuri lakini cheti changu cha form 4 ni “Fake”! 🙆🏽‍♀️🙆🏽‍♀️ Wakadai tumepiga simu wizara ya elimu wamesema hizo namba sio zake. 🥺🥺 Wakasema kama mnaweza kwenda wizarani mkahakiki nendeni kisha mrudi hapa. Wakatupa reference namba, na jina la mtu walie ongea naye hapo wizarani. Basi, tukatoka mbio kwenda wizarani, tunafika getini tukasema jina la mtu tunayekwenda kumuona, wakampigia simu huyo mtu kumwambia kua kuna wageni hapa wanahitaji kukuona. Yule mtu akaomba aongee na baba, akasema samahani rudini ubalozini wanawasubiria kule tumesha tatua tatizo. Alikosea kusoma namba. 🤣🤣🤣 Baba akasema lakini nilimuuliza unahuwakika kuwa cheti cha binti yangu ni feki na akanijibu kuwa “100% sure”. Mzee hasira zikamshika lakini sasa atafanyaje inabidi turudi tena ubalozini. Sasa wakati baba anamaliza kuongea na yule.mtu wa wizarani, secretary wake akapiga simu muda huo huo akasema “baba mnatafutwa na ubalozi wa Marekani wamesema mwende sasa hivi”, baba akamwambia ndio tunaelekea huko, lakini hawa watu leo ndio watanijua mimi ni nani! 🤣🤣🤣 Usichezee mzee wa kutoka kanda maalum.

Basi tukafika ubalozini, tukapokelewa vizuri, yule mdada akaomba msamaha kwa usumbufu, akachukua passport yangu akasema kesho asubuhi uje uchukue na nakutakia masomo mema. Mzee Igogo sasa akaanza, “young lady I need an official oppology letter” 🤣🤣 Eti huwezi kunifedhehesha mbele za watu halafu unaomba msamaha kiholela holela namna hiyo. 🙈🙈 Yani mie I was like just give my passport am ready to board. Nyie muendelee na drama yenu kimpango wenu. 🤣🤣 Nilipata passport asubuhi, usiku nikaondoka zangu siku hiyo hiyo.

Ilikuwa mara yangu yakwanza kutoka nje ya East Africa. Niliondoka na ndege ya British Airways, business class 😍😍 mzee Igogo sijui alifikiri nikipanda economy nitachelewa 🙈 Mwe! Nilifurahi sana. Tukafika UK, tukapelekwa hotelini kwa ajili ya kupumzika mpaka asubuhi kuanza safari ya kuelekea Chicago O’Hare International Airport. Baada ya kufika Chicago shulenilinielekeza kuchukua basi lakuelea Indiana. Waliniambia nishuke kituo cha mwisho ambapo ni Indiana Airport na hapo nitakuta gari la chuo cha Andrews likinisubiria. Nilifata maelekezo nikafika shule salama kabisa.

Nilifikia kwenye dormitories za chuo. Jamani acha tu! Unaingia kwenye dormitory ya chuo kama hotel vile. 😍 Nilikuwa na roommate mzungu kutoka Canada, alikuwa anaitwa Melissa Gonzalez. Vyumba ni self contained, mna bathroom na shower yenu kwa chumba, for a minute nikakumbuka mabafu ya C.B.E mabafu 3 watu zaidi ya 20 ni mwendo wa kusubiriana wengine wanaamua kuoga< kwenye kolido🤣🤣 Kwakweli,.Andrews ni shule nzuri sana sema gharama zake sasa! 🙆🏽‍♀️🙆🏽‍♀️Pasua kichwa.

Temeke SDA Nursery and Primary School watoa shukrani kwa mama Igogo!

Mama Igogo akitazama kwa furaha picha iliyochorwa kwa taswira yake.

Wanao onekana kwenye video hapo juu ni baadhi ya wafanyakazi wa Temeke SDA Nursery and Primary School walifika nyumbani kwa mama Igogo mchana wa jana tarehe 09/27/2021, masaa ya Africa Mashariki, kwaajili ya kutoa shukrani zao za dhati kwa mchango wake wa hali na mali ambao aliutoa toka kuwaza yakwamba kanisa la Temeke SDA linahitaji kuwa na shule, kuisimamia kuanzishwa kwakwe toka elimu ya awali ya chekechea (Nursery school) mpaka kufikia kuwa na darasa la kwanza mpaka la saba.

Kuhakikisha kuna kuwa na boarding (hostel) kwa wanafunzi wanao kaa mbali haswa wanafunzi wa jinsia ya kike! Mama Igogo alikuwa full time Mkurugenzi mkuu (Director) ambaye hakuwai kulipwa mshahara hata mara moja kwa miaka 7! Alifanya kazi ya kujitolea kwa asilimia 100%! Na baada ya miaka 7 aliomba “kung’atuka” na kuwaachia vijana waikimbize. Yeye alibakia kuwa mshauri kwenye bodi ya shule. Mungu ni mwema shule ilisimama na inaendelea vizuri! Mwanangu ni mmoja wa wanafunzi wa mwanzo kabisa wa shule hii! Alianzia  Nursery hadi darasa la sita. Mungu azidi wabariki wote walimu, wanafunzi, pamoja na watu wote wanaojitoa kwaajili ya huduma hii muhimu sana kwa jamii. ????

Kwenye video ya pili ni Mama Igogo akitoa shukrani zake za dhati baada ya kupokea shukrani na zawadi ya picha kutoka kwa wafanyakazi wa Temeke SDA Nursery and Primary School. 

Na hapa, mama Igogo akitoa ufafanuzi wa zawadi ya picha iliyochorwa kutoka kwenye moja ya picha zake ambazo alipiga akiwa kwenye Makao Makuu ya Wasabato ulimwenguni yaliopo Silver Springs, Maryland/ Washington DC eneo la kumbukumbu za Ellen G. White (mmoja wa waasisi wa dhehebu la Wasabato). Mama yangu hajatembea dunia nzima, Mungu ni mwema amembariki kutembelea nchi kadhaa hapa dunia na ameona mengi; lakini safari ya kutembelea kijiji cha history ya Wasabato huko Battle Creek, Michigan na safari ya kutembelea Makao makuu ya Wasabato ulimwenguni kwakweli ni moja ya safari ambazo zimemgusa sana moyo wake na siku zote huwa anaziongelea kwa hisia sana! Namshukuru Mungu kuwa amenichagua mimi binti yake kuwa kiungo kikuu cha mbaraka huo. Si kwamba asingeweza kufika Marekani hapana! Naamini Mungu kama alimpangia kufika angefika tu bila ya mimi kuwepo kama hizo nchi zingine alizo tembelea bila mimi kuwepo! Lakini kufika sehemu kama hizo kwa urahisi na kwa furaha kupitia mwanae naamini nikitu kinampa faraja kubwa sana moyoni! ?? No mama ain’t done yet! Mungu atupe uhai utakula more good time very soon! ?????

Mzee O.O Igogo, Magreth Otieno Igogo, na mama Igogo

Hapa juu ni moja ya picha waliyopiga wakati walikuwa wamekwenda kutembelea kijiji cha historia ya Wasabato huko Battle Creek, Michigan mwaka 2014 mwezi wa 11. Picha A siku hii zipo nyingi lakini zipo kwenye Flashdisk, sijapata muda wa kuziangalia.

Kama ulipitwa na picha za mama Igogo kutembelea Washington DC basi bonyeza ???? Safari ya mama Washington DC , na Safari ya mama Washington DC

Twamshukuru Mungu kwa yote kwani ni kwa neema yake tu ndio maana haya yote yanatokea. Sifa na utukufu ni zake yeye tu milele na milele. ????

“SIMAMA KATIKA NAFASI YAKO, MUNGU ANAMAKUSUDI NA WEWE”

SIMAMA KATIKA NAFASI YAKO, MUNGU ANAMAKUSUDI NA WEWE
Ni wewe pekee mwenye kujua magumu unayoyapitia na uzito wa changamoto unazokumbana nazo katika maisha. Ni wewe pekee mwenye maelazo na lugha sahihi ya kumueleza Mungu juu ya shida zako, usikatishwe tamaa. 

Usinyamazishwe na watu ambao hawajui historia yako, hawajui shida yako, hawajui maumivu yako, na hawajawahi kuyapitia magumu yanayokusonga wala mazingira yako.

Ilikua rahisi watu kumnyamazisha Batimayo kwa sababu walikua hawajui nini maana ya UPOFU

°Usinyamazishwe na watu ambao wana wazazi wao kwa kuwa hawajui nini maana ya kuwa YATIMA

°Usinyamazishwe na watu ambao wako kwenye ndoa zao na hawajui nini maana ya kuachwa/kutelelekezwa, ujane /ugane, au kutalakiwa.

°Usinyamazishwe na wale walio na watoto na hawajui ugumu, maumivu ya kutokuzaa watoto

°Usinyamazishwe na wale walio na wenzi waaminifu na hawajui nini maana ya kusalitiwa.

°Usinyamazishwe na wale walio na kazi na hawajui ugumu wa kutafuta kazi miaka na miaka bila mafanikio.

°Usinyamazishwe na wale walio na watoto waaminifu/wasikivu na hawajui nini maana ya kuwa na watoto wakaidi, waasi, watukutu, walioshindikana.

°Usinyamazishwe na watu ambao wameshafanikiwa kimaisha na hawajui ugumu au shida ya kuwa masikini.

°Usinyamazishwe na wale wenye uwezo wakula Milo mitatu ya maana kwakuwa hawajui nini maana ya kulala na njaa

Wewe ndiye unajua uchungu unaoupitia, maumivu na upweke unajua wewe mwenyewe, kama Batimayo alivyoipaza sauti kwa Yesu, Endelea kuita na Yesu atakusikia hakika!

Nakutia moyo ya kwamba Mungu Yehova Yupo yeye aonae yupo, mwenye usemi wa mwisho juu ya maisha yako ni yeye!

USIOGOPE Yeye sio kipofu hata asione machozi yako, yeye sio kiziwi asisikie maombi yako, na hajakaa kimya kwa maumivu yako, Anajua, Anaona , anasikia atakutendea vyema hakika kwa majira na wakati unaofaa! 

Mungu akutie nguvu kusimama! 

Bwana akutendee vyema.

**by Melania Shedrack**

Reginald Mengi: I can, I must, I will

Regrann from @lemutuz_superbrand - Dk @regmengi akupa maisha yake katika kitabu

UNAWEZA kuwa na maswali mengi kuhusu Mfanyabiashara maarufu hapa nchini, Dk. Reginald Mengi,alivyoweza kufikia nafasi aliyonayo kwa sasa akimiliki makampuni kadhaa na mengine kuwa na hisa hapa nchini na ughaibuni.

Majibu ya maswali hayo na maelezo mengine yatapatikana katika kitabu chake cha kumbukumbu kuelekea utajiri ambacho kitazinduliwa Juni 30 mwaka huu.

Kitabu hicho chenye taarifa muhimu kwanza za kumfahamu Mengi ni nani kisha safari yake ndefu kufikia ustawi alionao leo akiwa na makampuni yaliyotawanyika nchini na katika nchi za majirani na mataifa tajiri duniani lakini kubwa linakupa kanuni za kufikia na kumpita pale alipofikia yeye. Usikose kitabu hiki “I Can, I Will, I Must…The Spirit of Success” (Naweza, Nitaweza, Nitafanya na Moyo wa Mafanikio)

Dk Reginald Mengi Juni 30 anazindua kitabu chenye kujaa maarifa na taarifa. Kitabu hiki kimepongezwa na wanazuoni wastaafu wa Chuo Kikuu Cha Harvard, Profess Daniel Isenberg na Profesa Sujata Bhatia kutokana na kuelezea kwa ufasaha na kiufundi mifumo ya kiuchumi na kisiasa nchini kwa miongo minne iliyopita ilivyoweza kuathiri jitihada za ujasiriamali nchini Tanzania na kuelezea nini kinahitajika katika kutafuta mafanikio.

Unaweza pia kupata updates zaidi kuelekea uzinduzi wa kitabu chake kupitia akaunti yake ya twitter @regmengi
8 days to I CAN,I MUST,I WILL book launch #iCaniMustiWill #RegMengi ‭ - #regrann

“I always knew I wanted the good life, like I wont even lie about it”

Regrann from @zarithebosslady - WCW inspirational moment: I always knew I wanted the good life, like I wont even lie about it but then again dont we all? Well, at 30 I was already employing 258 employees and that alone on its own made me grow up mentally. The responsibility that comes with managing companies in a foreign country where you are always targeted as a foreigner least i forget the tight competition especially if your on top of your game wasnt easy...... so whatever you do, do it with passion. Fall down 99 times, get up the 100th. One day, and I say it again one day, the universe will respond. #Persistence #Consistence (See my life at 30, huge office with a personal boardroom?) me and Don started out in 2 offices, one PA, had just abit of ideas, got experts on board which we couldn't afford but they saw potential in us, did our logos which will forever remain a trademark and here is our recognized brand in the whole of SA www.brooklyncitycollege.co.za - #regrann Awiih! That's my gal! My true inspiration.  The real BossLady. Hakuiba kwa mume wa mtu akuuuu mtoto wa watu! Katafuta masiki mwenzake wakaanza kusaga visigido!! #I'mTheFoundationNotTheRoof ......I want good life too and hope to catch up with your achievement though I am in my 40s! Don't look down on me only God sits that high ? ??..... You go Zari! Keep winning! Keep shinning!

‘Life is just a moment’

“A man died…

When he realized it, he saw God coming closer with a suitcase in his hand.

Dialog between God and Dead Man: 

God: *Alright son, it’s time to go*

Man: So soon? I had a lot of plans…

God: *I am sorry but, it’s time to go*

Man: What do you have in that suitcase?

God: *Your belongings*

Man: My belongings? You mean my things… Clothes… money…

God; *Those things were never yours, they belong to the Earth*

Man: Is it my memories?

God: *No. They belong to Time*

Man: Is it my talent?

God: *No. They belong to Circumstance*

Man: Is it my friends and family?

God: *No son. They belong to the Path you travelled*

Man: Is it my wife and children?

God: *No. they belong to your Heart*

Man: Then it must be my body

God: *No No… It belongs to Dust*

Man: Then surely it must be my Soul!

God: *You are sadly mistaken son. Your Soul belongs to me.*

Man with tears in his eyes and full of fear took the suitcase from God’s hand and opened it…

Empty… With heartbroken and tears down his cheek he asks God…

Man: I never owned anything?

God: *That’s Right. You never owned anything*.

Man: Then? What was mine?

God: your *MOMENTS*.  Every moment you lived was *yours*.

Do Good in every moment

Think Good in every moment

Thank God for every moment

Life is just a Moment.

Live it…

Love it…

Enjoy it…… ”

#Mama

#AboutSabbathDay

#GodIsGood

Hekima za Mwl. Nyerere: Usikubali kuwa jiwe

https://youtu.be/TfbVbhvss2w

Kisa hichi kinanikumbusha story ya mke wa Lutu kwenye Biblia japo hakifanani sana lakini the moral of the story still the same. Ukitaka kusonga mbele na kuwa na mafanikio makubwa inabidi kuwa jasiri sana wakutosikiliza ya watu! Watu ambao wanajua kuwa “wamechemsha” kwa kutofata masharti ya kufika to their “promise land” or "destiny" wengine huwa wanakua na busara na kutumia experience yao kwa kuwafundisha au kuwaambia wengine wasifanye makosa waliofanya. Lakini kuna ambao wanakuwa na hasira sana na wengine na kuanza kupiga makelele kwa wale ambao wanaonyesha muelekeo wa kufika kwenye nchi ya asali…….. Watu hao ndo wazushi, waongo, wachonganishi, wapika majungu n.k hayo yote wanafanya kuwakatisha tamaa wale ambao wanaonyesha dalili ya kufanikiwa. DON’T  NEITHER LISTEN NOR  JOIN THE NOISE MAKERS! They are nothing but biggest losers! USIKUBALI KUWA JIWE!!

Toni Braxton akubali pete ya Mr Birdman

Je, wewe unampenda mtu kwa muonekano wake, taiba, familia aliyotoka, akili zake, sura, pesa, jinsi anavyokuonyesha heshima n.k?  Mwanamuziki Brian a.k.a The Birdman  anasema "so what? What that gotta do with love?"  Hayo yalikuwa ni maneno yake baada ya Talk show host Wendy Williams kusema kuwa yeye alikuwa mtu wa kwanza kusema "hapana" aliposikia Toni Braxton ana mdeti The Birdman! Wendy amemueleza Mr Birdman kuwa muonekano wake na Toni ni tofauti sana hapo ndipo Mr "The Birdman" akasema vinahusiana nini na kupenda?! Yeye ni 'certified gangsta' ?? aliye kuzwa na street kwasababu mama yake alikufa akiwa na miaka miwili (2), baba naye japo hakuwa sana kwenye maisha yake naye alikufa, kaka, dada, bibi, babu wote wamekufa hivyo vitu hivyo vinemfanya asijue nini maana na thamani ya upendo lakini siyo kwamba hajui kupenda!  "I’m just a gangster, that don’t mean nothing. Certified too. What that gotta do with love?" Wendy alishikwa na kigugumizi baada ya jibu hilo! 

Hilo nalo ni somo kwa wengi wetu tunaopenda kusema "kampendea nini?" Wewe ukiona watu wanapendana kama huna jema lakusema nyamaza lakini ukitaka kujua kampendea nini utaumbuka kwani hayo ni ya Ngoswe muachie Ngoswe mwenye! Kila mtu ana kitu chake ambacho anatafuta katika kumpenda mtu sasa mambo ya kujifanya  mimi sijui "Engineer" ooh mimi "mfanya biashara" sijui msomi gosh!! What that gotta do with love?!! Kwani siku ukiwa huwezi kunyanyuka kitandani hizo degree zako zitakunyanyua kitandani? ?? Watu wanaangali potential ulizo nano! Unaweza ukawa mzuri na elimu nzuri lakini akili ya maisha hauna azidi ya kutaka kuwa "trophy wife" au "Mario" ulishwe na kuvishwa na mwanamke halafu bado utake uitwe mume ? anyway, Birdman amemvisha Toni pete yenye thamani ya $5,000,000

The Birdman siyo mwanaume pekee ambaye anatarajia kufunga ndoa na mtu ambaye watu wengi walidhani haiwezekani.  Prince Harry naye mwaka jana mwishoni alimvisha pete ya uchumba muigizaji wa kimarekani ajulikanaye kama Megan Markle. Kwa hapa Megan ni mkubwa kwa Prince Harry kwa miaka mitatu (3yrs) na pia huko nyuma alishawahi kuolewa na kuachika. Ndoa yake ya kwanza ilidumu kwa miaka miwili (2 yrs) baada ya kudate kwa kwa muda wa miaka 6 ?? Hivi ndivyo vitu ambavyo sivielewi watu wadate kwa miaka sita halafu ndoa idumu kwa miaka 2 tu!! Tena hapo mpaka divorce imetoka ina maana atakuwa walitengana at least miezi 6 kabla ?‍♂️?‍♂️ Haya huyu Prince Harry ame mvika pete baada ya kumdate kwa muda wa miezi 15 (sawa na mwaka mmoja na miezi 3). Je, nitakuwa sahihi kusema ngoja tuone hii itadumu kwa muda gani au tuwatakie kheri tu ?

Btw, hata Toni Braxton hii itakuwa ndoa yake ya pili! Ndoa yake ya kwanza ilikuwa na mwanaume mwenye asili ya ngozi "nyeupe" ilidumu kwa muda wa zaidi ya miaka kumi na mbili (12  yrs) na alizaa watoto 2, Toni ana miaka 50 sasa.....Haya wale tunao pendeza hii show ya Braxton Family Values ndio tutakao faidi uhondo wote ? Siamini siku hizi nimemuambukiza mama yangu kupenda hizi show ?? anajua mpaka ratiba zake ??

Jacqueline Mengi: The day @drntuyabaliwe_foundation will be able to put up libraries in all regions and hopefully all districts of Tanzania will be the peak of my happiness

Regrann from @j_n_mengi - There’s so much joy in seeing a dream become a reality,and how that dream can change other peoples lives.I can’t even put in words how lucky and blessed I feel to be able to fulfill my dream of encouraging and enabling kids to develop the habit of reading. The day @drntuyabaliwe_foundation will be able to put up libraries in all regions and hopefully all districts of Tanzania will be the peak of my happiness. - #regrann 

KUWA NA SHUKRAN

KESHA LA ASUBUHI

IJUMAA

16/03/2018

*KUWA NA SHUKRANI*

? _Shukuruni kwa kila jambo; maana hayo ni mapenzi ya Mungu kwenu katika Kristo Yesu. 1 Wathesalonike 5:18._

✍?Kuna mashaka mengi sana yasiyo ya muhimu, wasiwasi mwingi kwenye akili za watu, juu ya mambo ambayo mtu hawezi kuyabadilisha. Bwana anatamani watoto wake wamtumainie Yeye kikamilifu. Bwana wetu ni Mungu mwenye haki na mwaminifu. Yapasa watoto wake watambue wema na haki yake katika mambo makubwa na madogo ya maisha.

✍?Wale wanaoendekeza roho ya wasiwasi na manung’uniko huwa wanakataa kutambua mkono wake unaoongoza. Wasiwasi usiohitajika ni jambo la kipumbavu; nalo hutuzuia tusisimame katika nafasi zetu halisi mbele za Mungu.

✍?Roho Mtakatifu anapotujia moyoni, hatutakuwa na hamu ya kulalamika na kunung’unika kwa sababu ya kutokuwa na kila kitu tunachokitaka; badala yake, tutampa Mungu shukrani inayotoka kwenye mioyo iliyojaa kwa sababu ya baraka tulizo nazo. Kati ya wafanyakazi wetu leo, lipo hitaji kubwa la kuwa na shukrani zaidi; na wasipofikia hatua ya kuwa na roho hii watakuwa hawajajiandaa kuwa na nafasi kwenye ufalme wa mbinguni.

✍?Kazi kubwa yapasa ifanyike kwa ajili ya kila mmoja wetu.
 Huwa tunaelewa kidogo sana kile Mungu anachokusudia kufanya kupitia kwetu. Inatupasa tujitahidi kutambua upana wa mipango yake na tufaidike kutokana na kila fundisho ambalo Yeye amekuwa akijaribu kutufundisha.

``` ??‍♀Hali ya kudhamiria mabaya ipo kwa wingi mawazoni mwa mioyo na akili zetu tunapojitahidi kuenenda kwa namna yetu wenyewe kinyume na sheria ya wema. Hapa ndipo wengi wanaposhindwa. Huwa hatujengi welekeo wa wema; tunataka kila kitu kitujie kwa namna iliyo rahisi.```

```??‍♀ Lakini swali lenye umuhimu mkubwa zaidi kwa kila mmoja wetu haipasi liwe juu ya namna tunavyotekeleza mipango yetu wenyewe dhidi ya mipango ya wengine, lakini namna tunavyoweza kupata uwezo wa kuishi kwa ajili ya Kristo kila siku. Kristo alikuja duniani na kutoa uhai wake ili tupate wokovu wa milele. Anataka amzingire kila mmoja wetu kwa angahewa la mbinguni, ili tuweze kuupatia ulimwengu mfano utakaoiheshimu dini ya Kristo. – Loma Linda Messages, uk. 602.```

Akin-Al: RULE YOUR LIFE OR BE RULED FOR LIFE!

Your feminist sister who says you don't need no man in your life already had 3 kids from her ex-relationships and your egocentric brother who says you don't need no woman in your life already had 5 kids from different women... Your fanatic friend who says social media are distractions to get to the kingdom of God has flat screen TVs and unlimited internet in his house. 

My MCM is Edger Gasper, from Bongoland

Never allow the music in other peoples lives determine the dancing steps in your own life...RULE YOUR LIFE OR BE RULED FOR LIFE!..... Akin Al Ameen®™2017

***Edger picture has nothing to do with the story***

Uzalendo huanzia nyumbani kwako!

"Picha hii ilipigwa siku ambayo nilitangaza kuwa sitagombea tena Ubunge, baada ya kuwatumikia kwa miaka 10. Sita sahau hisia zetu siku hiyo, jinsi mioyo yetu ilivyo vunjika kwa kujua kuwa mazoea yetu yatabadilika. Nina uhakika upendo wetu umebaki daima. Ndugu zangu Singida mjini ninawakumbuka sana! ❤ MO" // This picture was taken the day I announced to my constituents that I won’t be running for parliament, after serving them for 10 years. I won’t forget our emotions that day, a deep sense of heartbreak knowing that our interactions will change but the love will forever remain. My fellow Singida Urban brothers and sister, I miss you dearly! ❤️ MO"

Biblia inasema kuwa mtu asiyependa wakwao ni mbaya kuliko mtu asiye amini! Yani ni bora  mpagani anaonekana mtakatifu mbele za Mungu kuliko yule anaye sema anamuamini Mungu wakati anachukia na kutojali wakwao! Kuna watu wengi sana tena wengine wapo mbele ya macho yetu kila siku baadhi yetu wanawachukulia kama "role model" wao bila kutafakari kwa kina kuhusu hao "role model" zao! Je,  umewahi kuwachunguza kama kweli wanapenda wakwao? Au ni watu wa 'mikakati' yani they have an hidden agenda ya kutaka kupata pesa kutoka kwa wazungu na sponsors wa mambo yao! Kama ni kusaidia je  umeshaona wakisaidia wakao? Au ndio wale watu ambao ndugu zao wote ni wa "mujini wenye pesa" ukiishi uswahili kwetu kule Keko wewe siyo ndugu yao hawakujui!! Uzalendo unaanzia nyumbani kwako kwani hata hao ndugu zako ni Watanzania hivyo ukiwasaidia unasaidia taifa la Tanzania. .............Binafsi naheshimu nakupanda  watu wenye tabia ya kutoa jasho lao na kusaidia watu bila kuomba au kubugudhi wengine. Mfano ni Mh. MO Dewji, ShyRose Bhanji, Dr. Ntuyabaliwe  Foundation, Rita Paulsen, Flaviana Matata Foundation, Kidoti na wengine. Sipendi mtu anayetaka kusaidia wengine kwa kulazimisha wengine wamchangie kwani kusaidia mtu ni ibada, hivyo ni siri ya mtu na Mungu wake. Usinielewe vibaya kuna kuchangia kwingine naunga mkono kabisa kama mambo ya cancer, shule, n.k (for special cause). Ninacho ongelea hapa ni kusaidia watu binafsi......... Anyway, napenda vile Mh. MO anavyo wajali watu wa kwao huko Singida mjini. Mfano mzuri wa kuwa uzalendo, unaanzia ndani ya nyumba yako!

Akin Akman inspirational: They call it pride, I call it class. Lions don’t mingle with cats.

They call it pride, I call it class. Lions don’t mingle with cats. No matter the economy of the jungle, lions will never eat grass. Respect everyone but never ever forget that you’re equally important. Be friendly to everyone but never try to be everybody’s friend. Be open but selective. If you flock with penguins, you will never fly like eagles. If you’re NOT being treated with love & respect, check your “price tag”. Perhaps you have marked yourself down. If you present yourself funny, people will treat you like a joke. No one can sit on your back if you’re standing on your feet. Sometimes where you stand determines how people values you in life, and the price you put on yourself determines your worth. Get off the “clearance rack” and get behind the GLASS where they keep all the “valuables and NEW ARRIVALS. Once you know your worth, how people values you becomes irrelevant. Akin Al-Ameen®™2017 . 

Augustine Mkude: Kile kipindi kigumu Cha maisha kilinijenga nifanye kazi zaidi na zaidi ili nisirudi nyuma


Sikiliza historia ya maisha ya mtanzania Augustine  Mkude ambaye anaishi hapa Marekani katika jiji la Houston, Texas Kama anavyojielezea kupitia show ya The Untold inayo ongozwa na mtangazaji mkongwe wa kimataifa Sunday Shomari!

Familia nyingi za kiafrika hulazimisha mambo yawe jinsi familia inataka bila kujua kila mtu Mungu amemuandikia safari yake kwa njia yake ya kipekee! Kitendo cha familia ya Augustine kukataa kumsaidia eti kwasababu amekataa kuwa Padri niseme kuwa ni hali halisi ya familia nyingi sana, nakwakweli si kizuri hata kidogo. Nafikiri Kuna haja ya kuelimisha jamii kuwa siyo kila mtu lazima aende Morogoro kwa kina Mkude kwa kupanda basi la Abood! Nasio wote watakao kwenda Morogoro kutoka Dar bila kushuka njiani au kupumzika. Just because my enroute is different from yours it doesn’t mean am in a wrong path!

I’m very impressed na huyu Augustine Mkunde. Anaoneka ni mtu mkarimu na mkweli. Wana Houston haya let support Mkunde, Safi sana! …….Hilo swala la kuulizwa “Do you speak English” hata mimi ilinikuta kwenye nursing home moja huko Michigan, sema mimi mgonjwa alisema  “Alpha can you speak English? this is America!” ???? jamani niliishiwa nguvu nikabaki kucheka tu!…….Anywa, nimependa sana hii show. But mbona sehemu ya nne na ya tano hazipatikani kwa YouTube? Mara yakwanza nipo angalia like a week ago kulikuapo zote sasa leo nimetafuta wee wapi naona mwisho sehemu ya tatu! Vipi? Nataka ile sehemu ya Kilimanjaro connection bwana  ?? that was naked truth ??

You see this lady!?! Don’t give up!

Zarinah Hassan: We have been created so different, the type of humans who can multi task

“There is so much in a woman that most people don’t know. We have been created so different, the type of humans who can multi task. A man can watch a game and not hear what one said while a woman can watch a movie and still hear, still know the stove is on, and so on (the list is endless). So here is to all the multi tasking women juggling through life as mothers, wives, momprenuers aka business women, caregivers and many more. You are appreciated! It’s all about knowing what comes 1st #prioritize. Salute? help me tag one woman who inspires you. @lukambaofficial ?” ——-Zarinah Hassan

RARE Magazine yatumia page mbili kuandika ‘Bio’ ya LB!

Kwakutumia social media accounts zake Linda Bezuidenhout alielezea furaha yake na kumshukuru Mungu kwa mibaraka hiyo kama unavyosomekahapa chini ? “Wow! Please zoom to read my bio and all the achievements Thanks to God Alhamdulilah ??. My bio keeps growing we now need 2 pages to complete all the awards and achievements WOW! The RARE Magazine based in NY used 2 pages just for my bio and other pages for my designs….. please if you haven’t seen the cover of the magazine with an LB dress go to @linda_bezuidenhout_couture …soon we will add the resent events on our website which are among the major events we participated (LB COUTURE ) My Accolade Media Award and to showcase for 50 Shades Of Pink.
One more Amazing event to come for this year InshaAllah ?? God Willing. Listen ? everybody Listen!! THANKS FOR YOUR LOVE AND SUPPORT. MashaAllah Bio yangu na matukio makubwa niliofanya ni mengi mpaka ina chukua kurasa mbili kwenye gazeti. Hilo kwenye gazeti kubwa sana la NY. Tukuio na tunzo niliopata za juzi juzi hatujaweka bado kwenye website … InshaAllah kuna tukio lingine kubwa moja kwa mwaka huu limebaki ??. NAWASHUKURU KWA MAPENZI YENU NA SUPPORT YENU ??” LB  Nami napenda kumpongeza sana Linda kwa mafanikio haya. Kweli Mungu si Athumani, nani alijua kuwa “Fundi cherehani” anaweza kutumia page mbili kuandikiwa Bio! Very inspiring! Ubarikiwe sanaaaaaa! ??

A day in the life: Siku ya maisha yangu na Emelda Mwamanga

Emelda Mwamanga (Kushoto) pamoja na Dorothy Kipeja ambaye ndiye mmiliki wa show hii ya A day in the life

Wow! I’m super happy Bang Magazine is coming back!!! My wishes came true! Ni miezi michache iliyopita nilikuwa nauliza kuhusu Bang Magazine kama itarudi sokono (SomaHapa), na katika video hii fupi inayo onyesha maisha ya Mama / Mke / C.E.O / Entrepreneur lady / Motivational speaker and now what an Author?!  (ma’am this lady can do it all huh!! I only have this blog and can’t even keep up with it ????)  Emelda Mwamanga ambaye ndiye mmiliki wa Bang Magazine ametamka kuwa Bang Magazine inarudi sokoni muda si mrefu! ………So happy for you Emelda! Nice show, good job! Love it!!

Jacqueline Mengi: Love is an act of endless forgiveness!

Nimeenda kuchungulia kwa Mrs Mengi nikakutana na picha nzuri sana zakwake na maneno Fulani amazing hivi, "love is an act of endless forgiveness"! Haya ni maneno rasmi aliyo yatamka Beyonce baada ya kumsamehe Jay Z kwenye ile "cheating scandle" nakusema kuwa amejifunza upendo ni tendo la kusamehe bila ukomo / kukoma! Dah! Haya maswala ya mapenzi namwachia Jacqueline na Dr Mengi wake maana site wengine tulishaga achana nayo  ????. 
Kuna mtu aliandika article akisema Beyonce amemsaidia sana kwa maneno yake hayo ............."The best part of the show is when Beyoncé gives us the quote about forgiveness.

Love is an act of endless forgiveness. Forgiveness is me giving up my right to hurt you for hurting me. Forgiveness is the final act of love” 

All this while getting shot in a wedding dress. Yes, shit gets THAT real.
We’ve all been there for before where we wanted to hurt the one we love because they hurt us. Why? Because no one can hurt you more than the ones you care for. They know you best and you feel so vulnerable to them.

It is a valuable lesson to be learned here. In order to sustain love, you have continuously BE love. You have to be willing to love through thick AND thin. It’s easy to stop loving once you’ve been hurt but as the late Maya Angelou once said, “Have enough courage to trust love one more time, and always one more time.”

If two people can put aside their ego and realize that mistakes will be made; and know that nothing worth having will come without HARD work to keep it, you can really have that ever lasting love you seek." ............unaweza soma article you kwa kubonyeza ?? (LoveIsAnActOfEndlessForgiveness).  

“If you are happy with yourself it’s very easy for others to make you happy”JNM……….Umependeza sana! Super clean and beautiful!

Zamaradi Mketema: Usiangalie mawe kama SILAHA ukayakimbia ila badala yake yafanye ZANA katika kusimamisha himaya yako. MAWE yanasaidia KUJENGA!!

Sisi Binaadamu wengi ni watu tunaohofia MAWE, tunaishi katika hali ya kutafuta njia za kila aina za kukwepa kabisa kurushiwa na kuziba mianya yote itayoweza kutoa chakusema kwa adui zako kitu kinachopelekea kujikuta unaishi hadi maisha FAKE kwa kuhofia tu binaadamu, bila kufahamu mara nyingine ni vizuri kuyaacha yaje ili kujua yanatokea upande gani, yana sababu gani, yatakusaidia vipi na yatabadilisha nini pia kwenye maisha yako. Kwa upande wangu NIMECHAGUA kuyaokota na kujengea NYUMBA yangu, kila jiwe litakalorushwa kwangu nahakikisha siachi lipotee, nitaliokota na kuliongezea tu kwenye ujenzi wa nyumba yangu, hata kama lengo la mawe ni kuniumiza, nitahakikisha yananisaidia pia. Mawe ni BARAKA, mawe ni ongezo, na ni mafundisho pia. Tunajifunza mengi kupitia mawe yanayorushwa kwetu, tunakua zaidi, tunaimarika na kujijenga, tunafahamu nguvu tulizonazo na zaidi tunajifunza hata KUJIHADHARI Kupitia unavyonifikiria na kuyawaza juu yangu unafanya nijue nini natakiwa kufanya, unanifundisha wapi sitakiwi kuwepo nakadhalika, kiufupi UNANIAMSHA, na hata ule udhaifu unaohisi unaniumiza nao usichofahamu unanifundisha jinsi ya kuishi nao na zaidi kuufanyia kazi na kuufuta kabisa kama upo. Unaposema na kunisimanga juu ya jambo ni kunizindua juu ya jambo hilohilo hivyo kama lengo ni kukomoa unajikuta unafeli maana athari njema ulizoziacha utakuja kugundua ni nyingi kuliko zile mbaya ulizodhamiria.

Angalia kila jambo katika hali chanya na utaona faida yake, Usiangalie mawe kama SILAHA ukayakimbia ila badala yake yafanye ZANA katika kusimamisha himaya yako. MAWE yanasaidia KUJENGA!!