Category Archives: Womanhood

Mwanamke ni mtu shujaa, mwenye hekima nyingi, na muerevu sana!

Embu leo tuongelee hichi kiumbe ambacho Mungu alikiumba baada ya kuumba kila kitu! Mungu aliumba vyote lakini akaona kuna mapungufu mahala yani kwa lugha zingine naweza sema hakuridhika na kazi yake ya uumbaji mpaka alipo muumba mwanamke akaona vyote ni mema sana na uumbaji wake ukaishia hapo!

Labda niseme kwa siku ya leo nia yangu si kuongelea uumbaji wa Mungu bali nataka kuongelea moyo au nguvu ya ushujaa, hekima, na uwerevu ambao mwanamke amepewa na Mungu mwenyewe lakini bado tunajiona wadhaifu, hatuwezi kufanya kitu bila nguvu ya mwanaume kwanini? Kwakweli hata mimi sijui sababu bado najiuliza kwani kitu ambacho wanawake karibia wote tuna “struggle” nacho hata mimi mwenyewe- hello! Yes, me too ? Msema kweli ni mpenzi wa Mungu!

Hivi umeshajaribu kutafakari kuwa Mungu baada ya kumuumba mwanaume akaona kuwa hajakamilika kuna kitu kinahitajika ili huyu mwanaume aweze kufanya kazi kamili na kuishi kama mwanadamu? Na kitu hicho ni mwanamke! Hivyo, ukitaka kulinganisha utagundua kuwa mwanaume anahitaji nguvu ya mwanamke zaidi ili kuwa kitu kamili lakini mwanamke anaweza akafanya kazi na kuishi bila kumtegemea mwanaume sana (mnaojua maandiko ruksa kunikosoa). Naomba nieleweke, sijasema mwanamke hamuhitaji mwanaume la asha! Kila kitu ili kifanye kazi vizuri lazima kuwe na nguvu za hasi na chanya (mkono wa kulia na kushoto) ambazo zimeunganishwa pamoja katika kuleta nguvu kamili! Lakini saa nyingine utakuta upande wa kulia hautoi joto / nguvu sawa na kushoto hivyo inailazimu upande wa kushoto kutoa nguvu zaidi ili kuweka balance!

Zari The Bosslady

Nguvu ya ushawishi na hekima ambayo mwanamke amepewa ni kubwa sanaaaa! Tukiacha kisa cha Eva alivyo mshawishi mumewe Adamu kula tunda la mti waliokatazwa na Mungu, embu tuangalie kisa ya Malkia Esther kwenye Biblia! Jinsi Esther alivyotumia ushujaa na hekima ya hali ya juu kumshawishi Mfalme (mumewe) mpaka kuokoa watu wakwao! Kutokana na sababu mbali mbali watu wote waliogopa kumfata mfalme, lakini Esther alipoambiwa akasema lazima nifanye kitu kwani alijua kunyamaza kwakwe kungetoa tafsiri ya kuwa ameunga mkono maadui. Esther akajua wakati ni sasa kama ni kufa basi acha nife lakini lazima nikamuone Mfalme na kuweza kuongea naye juu ya jambo hili. Esther akatumia uerevu wake na hekima kupanga nini cha kusema, mahali pakusema, na muda wa kusema! Namwishoe akashinda na kuonekana shujaa kwa watu wa kwao!

Labda nifupishe hii story kwa kusema kwanini nimeandika, nia yangu nikutaka kuwakumbusha wanawake kuwa sisi ni viumbe vya kipekee sana ambavyo tumebarikiwa sana na Mungu lakini muda mwingi tumekuwa tukijikatisha tamaa sisi wenyewe aidha kwa kujua au kuto kujua! Tumekuwa waoga wa kutoa sauti zetu zisikike mbele ya wanaume. Tumekuwa hatutaki kueleza hisia zetu halisi na kujikuta tunaishi maisha yasio na uhalisia na kile kilichopo moyoni mwetu! Tumeshindwa kutumia nguvu ya ushujaa na ushawishi ambazo tumepewa na Mungu kuleta mabadiliko mbali mbali ndani ya maisha yetu na katika jamii zinazo tuzunguka! Tumekuwa viumbe dhaifu wakati Mungu alituumba kama mashujaa mkombozi wa mwanaume!

Japo kwasasa wanawake wengi wanaanza kuamka na kutambua hii siri ambayo ipo ndani yetu lakini bado inabidi tuamke zaidi! Mapinduzi yakweli yataletwa na mwanamke! Si unaona jinsi Eva alivyoweza mshawishi Adamu kula tuna na dunia yote sasa wanawake wanazaa kwa uchungu na wanaume wanaishi kwa jasho lao ?? Basi kama mnataka mabadiliko ya kuachana na siasa mbovu, kutokomeza ukatili wa aina zote, mazingira bora na salama ya kuishi n.k lazima muamke usingizini!

Usijione wewe hufai eti kwasababu unatabia kama za “Wema Sepetu” (sorry Wema I picked you), hapana! Mungu anapenda watu wote na anaweza mtumia mtu yoyote yule kufanya mabadiliko kwaajili ya utukufu wa jina lake! Kwa wale Wakristo kumbuka kisa cha Rahab au Ruth kwenye Biblia! Wanadamu tunatizama vitu kwa macho yetu haya ya dhambi hivyo nirahisi kuhukumu watu na kuona kuwa hawafai na hawana thamani lakini siku zote kumbuka kila mtu anathamani sana mbele za Mungu! Na kama Mungu ataamua kukutumia hakuna atakaye weza kuzuia! Kikubwa ni wewe kusikiliza ile sauti ‘ndogo’ inayo nena nawe kwa upole ndani ya nafsi yako kuwa badili njia zako!

Wanawake tunaweza kuibadilisha hii dunia kuwa mahala salama pakuishi tena kama hatuta waachia wanaume peke yao! Wanatuhitaji ili kuweza kuleta mabadiliko ya kweli! Siku zote kumbuka kuwa wewe ni shujaa, mwenyewe hekima, na muerevu sana!

****Zari’s picture has nothing to do with the story**

**Imeandikwa na Alpha Igogo

“SWEAR THERE WILL NEVER BE A PHOTOCOPY”

Regrann from @hollietheblogger - I SWEAR THERE WILL NEVER BE A PHOTOCOPY? THERE WILL NEVER BE ANOTHER OR A BETTER FEMALE WARRIOR THAN @zarithebosslady ?? IF THERE WAS A WAY I COULD PAINT OFF THAT VOMIT ? FROM HER LIFE I WOULD ‼️‼️ I hope there is a 12month ban in place so we can just focus on her growth and her life without any silly or stupid distractions. God I am on my knees please mysteriously delete any Tiffa and Nillan’s videos or pictures from LU-rope’s camera ? Abeg ??‍♂️‼️‼️ #temporarypost? - #regrann

“This lady has taught me, resilience, faith and self worth”

#RepostSave @hollietheblogger with @repostsaveapp There are four pictures that define @zarithebosslady for me! All these pictures paint her journey both physically and emotionally.  @1. When she had lost Ivan and her mum and was sitting by Ivan’s graveside and was quietly dealing with Hamisa’s child scandal because the instagram was on fire ? @2. When Hamisa decided to stalk her in Kampala during her annual white party☹️. @3' After dumping Baba tee. I had never prayed for anyone the way I prayed for this lady honestly. I was that ? and angry but helpless.  @4. MY BEST PICTURE her transformation!! She took control and had swam to the other side of the river. Duh! ??? ?. ??

This lady has taught me, resilience, faith and self worth. In three words what has this lady taught you?

“MWANAMKE USIPOJITAMBUA NA KUJIELEWA UKAJIAMINI UKAWA NA MSIMAMO BASI UJUE UTATUMIKA KILA SIKU NA KILA MTU KAMA KOPO LA CHOO CHA KULIPI”

Regrann from @open_kitchen2014 - Mwanamke anayejiamini she looks so sexy and classy mwanamke anayetambua thamani yake always anajiheshimu na anasimamia kile anachokiamini na hata mume wake atamuheshimu daima milele kwasababu anajua umuhimu wake na mchango wake katika familia ? ? Lakini pia heshima hiyo na kujiamini huko hakuji kwa urahisi kwasababu ni kitu ambacho anajengewa toka akiwa mdogo na wazazi (Mwenyezi Mungu awarehemu wazazi wangu ) lakini namshukuru sana mama yangu kwa kunilea na kunifundisha what it means kuwa mwanamke na sio mwanamke tu bali mwanamke anayejiamini 

Kila siku alikuwa anatufundisha ukijua kufanya kazi na kusimamia familia basi ujue kamwe hakuna atakaye kuangusha kirahisi utaheshimika kuanzia na wadogo zako mpaka watu wazima kila utakapo ingia mahali kila mtu atatambua uwepo wako na atakupa heshima yako iwe ni nyumbani kwako ,kazini kwako,au popote pale ?

? Malezi na misingi mizuri ya maisha ndio zawadi bora kabisa ambayo mama anaweza kumpa mtoto 

Ukimpenda sana mtoto wako lakini ukashindwa kumlea katika misingi mizuri na kumwongoza aweze kujua nini maana ya kujiheshimu ,kukuheshimu ,na kuheshimika ni sawa na kupaka chokaa kwenye nyumba ya nyasi TAFAKARI ?

MWANAMKE USIPOJITAMBUA NA KUJIELEWA UKAJIAMINI UKAWA NA MSIMAMO BASI UJUE UTATUMIKA KILA SIKU NA KILA MTU KAMA KOPO LA CHOO CHA KULIPIA ??????? - #regrann

Zari Hassan: I am The FOUNDATION Not The Roof

  Regrann from @zarithebosslady - Pale unaposkia pesa za urithi... apo vipi. Success isnt sexually transmitted my dear. Endeleeni kudanga thinking some rich guy will knock you off your feet and success will happen over night. Even if he did you will be like part of the furniture he has a right to take out old ones and bring in new ones, as for me its not easy to get rid of me. IAM THE FOUNDATION not the roof...haha.  Anyway we are commemorating Ivans one year since his passing and i thought I'd motivate someone out there with these old images.
Dont downlook broke guys, God is for all, tables turn! Poor thing worked day and night to get me this car at 22 because he saw the woman in me. And yes, it didnt work out no matter how much i tried, Started from the bottom, right! Rest his soul in peace! - #regrann  

Ni maneno mazito sana kaandika Zari katika kukumbukumbu ya mwaka mmoja tangu kifo  cha Ivan Ssemwanga ambaye alikuwa mume wake na walijaliwa kupata watoto watatu. Ujumbe huu mzuri sana kwa wale wanaofikiria na kutwa kumsakama Zari kuwa anafuataga pesa kwa wanaume aliokua nao. Haya ushahidi huo mmeuona sasa muache kumsakama mtoto wa watu na mumpe heshima yake anayostahili!!  Jibu safi sana kawapa  "I am the FOUNDATION not the Roof"?? Ten ? across the board!! Ngoja leo niseme; katika wanawake wote ninaowapenda kwenye Social media kwakweli I have to sincerely admit Zari is number one!! Nikiangalia alipotoka na mambo aliyopitia, na jinsi anavyo yakabili kwakweli she is MORE than 'Woman and half'!!  Hivi utawezaje kuvunja Msingi!! Kama ni nyumba inamaana lazima greda lipite nyumba yote idondoke ndio ufutilie mbali Msingi! Only fools do that!!!
Kama mnakumbuka huko nyuma niliwahi kuandika kuwa kuna wanawake wengine huwezi kupata "mbadala wake"  you can not  replace her no matter what (soma ? In loving memory of Ivan Ssemwanga: "I think I was prepared for death") na Zari ni one of those very few women! Yani kama vile Oprah, hakutakaa kutokee Oprah mwingine duniani! Wengine watajaribu kuwa kama yeye lakini they will never be her! Sio kwasababu ni wazuri wasura na maumbile, hapana! Is the Brain, the courage, behind that beauty is a whole game changer ma'am!! Unfortunately I have to say this, with all due respect to Ivan Ssemwanga, but he was part of Zari's journey and not the destiny!! The best of Zari is yet to come!! So do Diamond, yale yalikuwa ni mapito tuu lakini safari ya Zari inaendele na ni nzuri zaidi kuliko alivyokuwa na Diamond!! Just keep watching her. Yani naamini hata Diamond huko aliko anajuta sana kimoyo moyo kwani anajua kuwa hata hafanyeje haitokaa apate mwanamke kama Zari. Atapata hao wauza sura wakupenda drama na ujinga wa social media but not another Zari! He was just soooooo lucky to have Zari on his hands! Na bahati haiji mara mbili! Kwanza Zari sasa hivi ndio mambo  ??? Keep on shining Zari!  ? ❤ #IamTheFoundationNotTheRoof

Dina Marious: Nilipofikia sasa naweza Kufanya Official Launch ya product hii hapa Tanzania

Regrann from @dinamarious - Nilipopata mtoto Feb 2014 wakati nahangaika kutafuta mafuta mazuri ya mtoto nikashauriwa ya nazi. 

Nikazunguka kila kona nisiyaone ndio nikakata shauri la kutengeneza mwenyewe sababu najua kutengeneza. 

Lakini wakati natengeneza ndio likaja wazo la biashara nakumbuka kabisa nikishauriana na Da Husna mmiliki wa @zero2twelve maduka ya nguo za watoto akanishauri fanya.

Nilipoanza nakumbuka alikuwa mteja wangu wa kwanza alinunua carton 24

But ninachokumbuka nilipopata wazo sikulaza damu nikaanza mdogo mdogo kwa ugumu wake nikijaribu kujifunza na Mimi niwe na bidhaa yangu yenye jina langu.

Michakato ya kufungua kampuni Mimi ni mlipa kodi TRA kila mwezi sina malimbikizo ya madeni.

Kuyasajili TFDA yakaguliwe na kupata kibali yanafaa kwa watoto na watu wazima.

Kupata barcode pale GS1 ambapo Mimi ni mwanachama 

Na mambo mengi mengi.

Kwa sasa unaenda mwaka wa nne lakini ya milima na mabonde,kurudi nyuma kujifunza na kujipanga upya.

Kubwa nilichokuwa nataka ni kukuza Brand yangu ya mafuta ya nazi Dina Marios Baby Coconut Oil itambulike na iaminike sikuwaza pesa hata kidogo.

Nilipofikia sasa naweza Kufanya Official Launch ya product hii hapa Tanzania. - #regrann  

 Kwanza nianze kwa kusema hongera sana Dina Marious a.k.a Mama King Zion kwa  ubunifu na kuleta bidhaa bora! Natamani mama yetu Mh. Samia Suluhu ndio awe mgeni rasmi siku hii au baba yangu Dr Magufuli ili ajionee kuwa Wanawake tunaweza na azidi kutuunguka mkono kuwapa wanaume wengine motisha ya kuwanyanyua wanawake kwenda kwenye uchumi wa viwanda. 

Jamani mafuta haya ya Dina Marious coconut oil ndio mambo yote kwa ngozi nyororo yenye afya kwa mtoto wako. Ni mazuri sana sio tu kwa watoto hata watu wazima. Mimi niliyatumia sana nilipokuwa Bongo bahati mbaya sikubeba kuja nayo hivyo huku natumia Coconut oil ya Wamexico au Jamaica. Mimi natumia pure coconut oil wakati wote labda wakati wa baridi ndio natumia Nevea lotion kwasababu nataka kitu cha kuongeza joto. Nunua mafuta haya bila wasiwasi utunze ngozi ya mwanzo. Simmeona yamethibitishwa basi usiwe na hofu. Tumuunge mkono Mwanamke wa shoka halafu simnajua 10% inakwenda kwenye ile charity yake ya Dada Dina Marious kusaidia watoto, wamama, na watoto yatima. Tumuunge mkono, tujenge jamii zetu.

Madam Rita Paulsen: I can proudly say I know how she feels

Regrann from @mspaulsen - The smiles when a you are a single mother and get to wittness your daughter,s wedding...... I can proudly say I know how she feels. It's the best achievement and a blessing . The feeling is unexplainable. I wish this to all single mothers out there we rock ???thanks God and our daughters for making us proud - #regrann Maneno ya kugusa moyo haya kutoka kwa Madam Rita Paulsen. Je, wewe umeahawahi kukutwa na hali kama iliyomkuta Madam Rita? Yani ukaona mtu anapitia jambo au anakutwa na kitu fulani (jema au baya) halafu zile hisia zake ukahisi ni wewe kwasababu huwenda nawe unapitia kitu hichohicho au ulishawahi kupitia huko nyuma? Kwanini nime share nanyi hii " status" ya Madam Rita, nikuwa maisha ni fumbo, ukimwona kichaa yupo uchi usimcheke kwani hujui yakesho! Watu pekee ambao wanaweza kuelewa kwanini yule kichaa yupo uchi na nijinsi gani anajisikia niwale ambao walishawahi kuweuka! Nawale  ambao wanajua thamani ya kuwa na akili timamu niwale wale uliowahi kuwa vichaa. Ndivyo ilivyo hapa, only those who are or have been single mothers before ndio wanaoelewa ujumbe wa Madam Rita na furaha ya mama Princess Megan.  ***Siku zote dharau maiti siyo binadamu mwenye pumzi ya uhai***

Zari Hassan: Success is not sexually transmitted

Wow! Word of centuries!! "Success is not sexually transmitted" kila mtu apambane na hali yake!! Hata ukiwa na mwanaume au mwanamke mwenye akili ya maendelo kama kichwa chako hakipo sawa yani hata ulale naye huyo mtu miaka na miaka hauta kuwa yeye!! Kama uwamini kamulize Gardner Habbash ??? (just kidding)...... Jamani ukimpata mtu mwenye akili ya maendelo basi nawe unaongezea na zako!!  Chuki wala roho mbaya haisaidii!! #SucessIsNotSexuallyTransmitted 

 ?

?

?

?


Regrann from @zarithebosslady  -  I repeat, success is not sexually transmitted!!!  - #regrann

Photo of the day: Emelda Mwamanga


The C.E.O herself! Beautiful Emelda Mwamanga a.k.a mama Gabby looking amazing ? Jamani kile kipengele chetu cha "Womanhood' siku nyingi tumekisahau eeh, nipeni muda kitarudi tena kwa kasi sana! Wanawake wenye miguu ya kuzalisha pesa simnawaona eeh walivyo tofauti na wale wenye

Joyce Kiria: Kila mtu ana njia yake …. Kila mtu kapewa msuli wa kupambana na matatizo yake

Regrann from @joycekiriasuperwoman - MAISHA YANGU BINAFSI NILIYAKUTA YAMEJAA CHANGAMOTO NYINGI, ELIMU SINA, FAMILIA YETU NI MASKNI, MIE NDO MTOTO WA KWANZA, YAANI MAISHA HAYANA HAMASA, HAYANA MATUMAINI, NOW NIKACHAGUA KUYAGEUZA NDO FURSA, YAANI NDO MTAJI WANGU... WEWE UNAONA NI MATATIZO MIMI NINAYAONA NI MGODI...  NILIAMUA KUPAMBANA NA HAYA MATATIZO YANGU KWA STAILI HII YASINIUMIZE KICHWA, BALI YANAPOKUJA TUU NINAYATAZAMA KWA JICHO LA FURSA! NAYAKUMBATIA NAYAONGEA KWA NGUVU ZANGU ZOTEEEE, NAPATA NAFUU LAKINI PIA NAPATA KAZI HAHAHAHA.

UJASIRI HUU NILIOJIPA NDIO UNAONIFANYA KUWA SUPER WOMAN, NANI ATAWEZA KUPITA HII NJIA?? UNADHANI WATU HAWANA MATATIZO? KWANINI WENGI WANAYAOGOPA?? KUKUBALI UKWELI WAKO BINAFSI SIYO JAMBO JEPESI, WENGI TUNAPENDA SANA KUJIONYESHA KWAMBA TUU WATAKATIFU...

MIMI NASIMULIA MAISHA YANGU BINAFSI, SIYASIMULII YA MTU, NASIMULIA NJIA ZANGU ZENYE LADHA YA ASALI NA MWAROBAINI KWA PAMOJA KWA AJILI YA KUJIFUNZA NA KUFUNDISHA WENGINE.... THAT IS MY PATH ... NJIA ZETU HAZIFANANI ... KILA MTU ANA NJIA YAKE ... KILA MTU KAPEWA MSULI WA KUPAMBANA NA MATATIZO YAKE... PIGANA NA YAKO.... AM SUPER PROUD TO BE ME... I AM A SUPER WOMAN #SUPERWOMAN - #regrann

Dina Marious: Angalia ndoto yako

Regrann from @dinamarious - Usiangalie magumu yanayokukabili na changamoto unazokutana nazo Leo angalia NDOTO yako.

Ndoto yako itatimia.......

 ndoto yako inawezekana.Kumbuka jinsi ulivyoiamini endelea kuiamini.

Inawezekana Leo umeamka una stress,huna hela,huelewi mambo yanavyokwenda.

Pamoja na yote endelea kuiamini NDOTO yako hata katika mazingira yanayokatisha tamaa.

Kumbuka wewe ndio una hiyo picha ya Kesho yako naamini ni picha nzuri sanaa na amini utaifikia.

Good morning! - #regrann

Mama Prince Kairo: Wipe their tears as you wiped mine father Lord

Regrann from @ladivamillen - I’m sharing my son’s pictures today not just for my supporters and followers to meet him, but  I needed to tell a different story.  Story of FAITH and HOPE. I needed to give hope by showing a picture of me holding my son, which I believe it could uplift and inspire someone out there. -Millen Magese .Catch my cover story interview Exclusively @genevievemagazine share it with that woman or family who lost Hope on Infertility battle. ?

 #NothingIsImpossibleWithHim #endometriosisawarenessmonth2018 #EndometriosisAndInfertilitySucks #SPEAKOUT #yellowdotfor1000needles #PutAStopOnEndometriosisAndInfertility. Custom dress by @eseazenabor you’re amazing.? - #regrann  Regrann from @ladivamillen - To read part of my story please check out the link on my bio for EMag then you can download. I look at your face my baby and can’t stop thanking God! My Miracle Worker ! Awesome is your name! Mighty is your name ooh God, I praise you, there is nothing you can’t do Lord! Do for other women as you did for me. Wipe their tears as you wiped mine father Lord. Let them experience the joy of carrying their own babies. You’re faithful God and awesome is your name?. Praying for all women out there to experience this joy soon ?#PrinceKairo???. Get to read our story @genevievemagazine .
Janeth Igogo: Whatever a man can do, a woman can do it better

The smile u make when u meet ur Secondary School Classmate n a Police Commissioner at Women’s Day Celebrations.. Whatever a man can do, a woman can do it better, Wanawake ni Jeshi Kubwa! WanawakeTunawezaa.. WanawakeOyeeee!!

Mwanamke wa Shoka 2018: Jiamini, Jitambue, Jikubali, Chapa kazi, Songa mbele

Regrann from @dinamarious - Sio kila jambo ni baya....wakati mwingine jambo zuri huanza kama baya....lakini baadae linakuja kukaa sawa katika uzuri wake unaostahili. Mwanzo wako unaweza kuwa mbaya lakini ikaja kuwa uhondoooooo. Changamoto zako zinaweza kuwa ngumu lakini kumbe baraka zako na mafanikio yako ndani ya changamoto hizo.

Inapofika mwezi wa tatu shamrashamra za kuelekea siku ya wanawake duniani huanza.Kubwa ni kusherehekea mafanikio,kutiana moyo na kupigania haki ya mwanamke hasa wale wanaonyanyasika.

Wanawake tunapitia changamoto nyingi sana lakini napenda nikwambie jifunge mkanda...pambana hakuna kujihurumia...dada utafika twende tukutane kwenye kilele.

Mwanamke wa Shoka.....jiamini, jitambue, jikubali, chapa kazi, Songa mbele tukutane Kileleni tuchape kazi ???
#Mwanamkewashoka2018 - #regrann

Zamaradi Mketema: Ni Makosa yetu wanawake

Miriam Kinunda author of  Taste Of Tanzania: Modern Recipe for the West https://www.instagram.com/miriamkinunda/

Regrann from @zamaradimketema -Kwenye comments nimegundua wanawake wanalalamika na mzigo wanaoubeba wao kwenye majukumu ya familia, ila MAKOSA mara nyingi yanaanzia kwetu, wanawake wengi WANAWALEMAZA sana wanaume wao wenyewe kwa kuhisi wanawasaidia, kwa bahati mbaya hii haina faida kubwa mbele ila hasara.

Tukirudi kwenye nature mwanamke ameumbwa kutunzwa hata vitabu vyote vya Dini vinasema hivyo, na ndiomana ikiwa tofauti madhara tunayaona, mwache mwanaume awe mwanaume hata kama umemzidi kipato, nature ya mwanaume ni KUTOA na kujihisi ANAMILIKI na ndio uanaume wake unapokuja, anapokutunza anafeel uanaume wake, hata uwezo wa kunguruma anaupata ndani, mpe hiyo nafasi usimnyime, hata kama wewe una mia yeye ana kumi hakikisha katika kumi yake lazima utaratibu wake wa kulisha nyumba ubaki palepale kwa kidogo chake hikohiko, we utatumia tu akili jinsi ya KUMSAIDIA ila usimlemaze akaona wewe ndio kilakitu na kumpa nafasi ya kutulia, hakikisha kila anapotoka anaacha kinachostahili hata kama ni mia tano, mfanye awe mume, maana athari za wewe kuibeba familia mara nyingine zinaenda pabaya zaidi hadi kuharibu mahusiano.

Na ndiomana kuna fikra isiyo rasmi kuwa wanaume wengi wanaoishi na wanawake wenye uwezo zaidi yao hutafuta nyumba ndogo pembeni za hali ya chini na kuzihudumia kwa hikohiko kidogo, lengo ni kutaka kuutoa uanaume wake, anataka mamlaka yake yaonekane, anataka akiongea asikilizwe, mpe nafasi hata kama una uwezo, hiyo ndiomaana ya kuwa KICHWA mfanye awe kichwa kwa vitendo, hata kwa umasikini wake onesha unamtegemea yeye na umtie moyo afanye kadiri ya uwezo wake, sio ndio unazo basi yeye anakuwa kama mtoto mdogo sasa ndani unamuacha moja kwa moja hapana, au unajifanya huhitaji kitu kwake unakosea. Ukitaka kujua hii ni nature hata kwa upande wa wanawake ndiomana hakuna feeling nzuri kama kupewa/kutunzwa na mwanaume wako hata kama una kilakitu, sababu nature iko hivyo!! Ndiomana si ajabu kukuta mwanamke tajiri lakini akamtamania mwenzie wa hali ya chini kwa kununuliwa mkufu tu, pamoja na kupata kilakitu kwa jasho lake bado kuna kitu kinamiss, kuona mtu anasimama kwake kama MLINZI na mtunzaji wa maisha yake, MUNGU ndio kaumba hivyo!! Ila siku hizi eti wanaume ndio wanalindwa. Ni Kosa!! Regrann from Zamaradi Mketema

Mother and daughter moment

Pretty-pretty-pretty! Such a lovely priceless moment, mama Cookie na Cookie wake! ???....... Jamani Valentine's moments unaweza ukachagua mtu yoyote umpendaye  uka dedicate mwaka huu kwake! Anaweza akawa mama yako mzazi, baba, dada, mtoto wako n.k! Yoyote yule amabye yupo karibu na ndani ya roho yako! Ila kama ni mume / Mke lazima awe amehalalishwa na mamlaka husika kama serikali, kanisa, au msikitini!  

Joyce Kiria: Haya MACHOZI yangu namlilia Mungu wangu aliye juu, yeye ndo ataamua

@Regranned from @joycekiriasuperwoman - Changamoto kubwa 2018 #Kipigo
Sikutegemea kama ipo siku kwa mkono wako ungeunyanya KUNIPIGA @kilewo2020mwanga ???? * Ukasahau kabisa! Ukasahau yooooote.. nimeharibu career yangu kupigania ndoto yako kwa kugawa watu wangu kwenye biashara zangu, nimepoteza ndugu jamaa na marafiki, umeniachia nimebeba mzigo wa familia kwa muda wote... Malipo yako ni KUNIPIGA/ KUNIDHALILISHA/ KUNITOA MACHOZI???

Umenipiga kwa sababu Mimi Ni MNYONGE siyo! SINA NGUVU, kwa sababu ni MWANAMKE Sina nguvu za kupigana na MWANAUME ... Umeniumiza mwili wangu unauma kila mahali umefiria damu na kichwa ukanigongesha kwenye gari, ili iweje? Nia yako ilikuwa ninini? kuniua??? Mungu amenipigania.

 Haya MACHOZI yangu namlilia Mungu wangu aliye juu, yeye ndo ataamua...?????? Kama NI Mimi niliandamana na watoto, nikakufanyia kampeni na deni kubwa nikaingia mpaka nikafungiwa Kipindi hewami, ninakutunza wewe na Watoto wako kwa miaka yote, MUNGU YUPO.... LEO UMENIPIGA @kilewo2020mwanga ??? Sawa watakusifia hao wanaokusifu ujinga, wanaokuambiaga Mimi sikuheshimu, badala wakwambie ufanye kazi utunze familia, Leo watakuona wewe ni MWANAUME kwa KUNIPIGA... - #regrann

Is baby number 2 on the way?!….if so; hongera sana Madam Rita!

Haya kuna huu ubuyu nawaletea wapenda ubuyu wenzangu ??? Niliona hii picha wiki imepita sasa, kimoyo moyo nikasema “she looks like pregnant” lakini nikadharau! Sasa juzi kinaenda kuchungulia tena Instagram page yake nikaona no update! Nikasema mbona siku hizi anapotea sana kwa social media!! basi nikaamua kusoma comments chini ya hiyo picha si ndio naona watu wengi wakimpongeza na kumsifia kuwa mimba imempendeza! 

Honestly, nimefurahi utafikiri mie ndio Madam Rita ?? huyo atakuwa mtoto wake wa pili baada ya miaka zaidi ya 20 kama ni kweli mjamzito! Isijekuwa mtu amevimbiwa maharagwe ya Mbeya sisi tunampa pongezi ?? …………anyway, Madame, please rusha basi picha nyingine tukuone mpenzi ?? Hongera sana, Mungu awe nawe ?

I am a woman-So what?!

           I AM A WOMAN!!! -So what?

I get into an argument with a man, he slaps me, I feel the pain, yet they tell me I provoked him. I should have been quiet, I should have been patient. I should apologize to him.

I get into an argument with a man, I slap him, they tell me I have no respect, no home training. I should have been quiet, I should have been patient. I should apologize to him.
Because I am a woman, I don’t have a right to be angry. So, the degree of my innocence is directly proportional to the degree of my silence in the face of oppression and brutality….. Because I am a woman, my husband cheats on me, I am told to tolerate it to save my marriage. The barbaric and stupid excuse is that ”it is in their nature to cheat, I should slim down, dress better, cook better, pray harder and be more pleasant to him”

I cheat, and I am called a whore, I have committed an abomination, I have no right to look elsewhere for the love and emotional support I lack at home, I am an irresponsible mother.

So I am sent packing, from the home we both built, with all my earthly possessions stuffed into a tiny box on my head. I am henceforth forbidden from seeing my two older children, I’m lucky to be allowed to go with my little one still suckling on my left breast. Three years later, the little one is tagged a bastard. Now, my new name is “after-three”, because I am a woman.

He is 28 and runs a company. He’s tagged wonderful, hardworking, focused, career oriented, successful at a very young age.

I am 28 and I run a company ” Hmmmm, she is not even married, unserious, can not order her priorities right, a hustler, loves money, let her go and get a husband oh”

And I wonder if being successful has anything to do with a person’s gender.

Because I am a woman,
I am not allowed to have wits or be a prodigy, I cannot be financially buoyant, professionally successful or be treated with respect without a man beside me.

Then I am tagged a generous leg opener, “a runs girl”. They never see the possibility that I actually had to go through ups and downs to get to where I am.

Because I am a woman.

A man looses his wife to death and remarries a year after, he did the right thing, he’s being praised and congratulated for moving on, after all life is for the living.

A woman looses her husband to death and remarries after 4yrs, “ahhh! so early? Are u sure she wasn’t sleeping with that man even when her husband was alive? That was why she killed her husband. She’s a witch! ” Because she’s a woman.

Because I am a woman, this post will be considered controversial, and everyone will try to correct me.

But don’t forget, that I am a woman and it does not make me less human!!!

Good Morning Everyone. NTV Mwasuze Mutya 9am-11am NTV/SparkTV Monday to Friday.

Mama Salma Kikwete ndani timu ya netball!

Mama yetu kipenzi mama Salma Kikwete ndani ya kivazi mwanana kabisa teyari kwa kuingia uwanjani kucheza mashindano  ya netball za timu za Wabunge wa Africa Mashariki hapo juzi kati! Inapendeza sana, inavutia, na kutia moyo wanawake wengine na mabinti unapo ona powerful figure Kama mama yetu hapo akijishusha kwa unyenyekevu na kufurahia maisha na watu wengine! Safi sana na hongera nyingi mama yetu!………… Mwaka jana naye Dr. AshaRose Migiro alituonyesha ujuzi wake wakupiga dana dana  tazama ?? BigUpDrAshaRoseMigiro