Big-up Dr Asha-Rose Migiro

screenshot_2016-10-19-10-19-53-1Isn’t that something! Too cute! Unajua kuishi huku na wenzetu kuna mengi MAZURI yakujifunza pia na mengi MABAYA yakuto jifunza unaangalia tu nakuyaacha jinsi yalivyo!…… Sasa katika vitu vya kujifunza moja wapo ni KUWA WEWE KAMA WEWE! Yani mambo yale ya unafiki unafiki hakuna! Eti sijui kiongozi tena mwanamke wa umri wa Dr. Migiro  achezee mpira namna hii Tanzania?  Subutu! Labda awe Mwalimu wa Netball kama mama yangu mkubwa Mary Protuz?? Nakumbuka huyo mama yangu mkubwa watu walikuwa wakisema wee “behind her back” kuwa havaagi gauni wala sketi! Yani yeye ni mtu wa suruali, na short pants siku zote. Na wala huto mkuta akifunga Khanga labda anakwenda kuoga! ………Anyway big up Dr. AshaRose Migiro,  talent has no end, and there’s no age limit to have fun!

Leave a Reply