Mungu ni mwema wakati wote!

Kwakweli sikuwahi kuwaza kuwa ipo siku nita post habari za misiba hapa kwa hii blog. Ila my “morals” inaniambia nilazima niweke haswa kwa sababu kuu mbili zifuatazo (1) ni ndugu zangu (2) ni blog yangu binafsi haiko sponsored na kampuni yoyote hivyo sina pingamizi. Basi kwa maana hiyo; kuwanzia leo kama kuna msiba wa ndugu yangu wakaribu au rafiki yangu wa karibu basi nita share nanyi kwa hii blog.

FB_IMG_1432478728295
R.I.P baba mdogo……you will always be missed

Wiki hii haikuwa nzuri kwetu kama familia na ukoo wa Igogo. Tumepatwa na misiba miwili ndani ya wiki moja na wamepishana only a day. Pichani ni marehemu baba yangu mdogo ajulikanaye kwa jina la Agonda, amefariki siku ya Thursday katika hospitali ya Bugando, Mwanza.

Ni baba yangu mdogo kwa pande zote mbili; yani kwa baba na kwa mama (Double undugu). Kwa baba, marehemu alikuwa ni mdogo wake baba kwa ukoo (au kwa lugha za wenyewe wanasema cousins). Marehemu alizaliwa katika kijiji cha Utegi, wilaya ya Rorya, mkowa wa Mara na huko ndipo atakapo zikwa.

FB_IMG_1432479047955
Kutoka kulia kwa chini-: 1st born: Felister Cornel Awiti (Mrs. Musira) 5th born: Cecilia Cornel Awiti (Mrs Igogo) last born: Magreth Cornel Awiti (Mrs. Sassi)

Kwa upande wa mama marehemu amemuoa mama yangu mdogo kitinda mimba (last born) kwa familia ya mama yangu mzazi (Familia ya marehemu mzee Cornel Awiti). Kama picha hiyo hapo juu inavyo jieleza. Basi ndio maana nimesema hapo mwanzo kuwa marehemu ni baba yangu mdogo kwa pande zote mbili.

2015-05-24 10.28.18Picha hapo juu ni marehemu alipokuwa kwenye graduation ya binti yake Dorice Sassi a.k.a Vumi.  Vumi kama wengi tupendavyo kumtwa, yeye ni mtoto wa pili kuzaliwa, lakini ni binti pekee kati ya watoto watatu wa familia hiyo. Mungu akupe nguvu Vumi, can’t imagine what you are going through right now and personally I don’t want to ever be in your shoes! So  sad to lose someone you truly loved and cared for. I have lost aunties, grandparents, uncles, cousin-sister, cousin-brother that were truly close to my heart, I know how it feels, but can’t imagine losing a father! Pole sana mdogo wangu, Mungu awape nguvu.

2015-05-24 10.57.37
R.I.P Jessica Kateti Sarungi

Msiba wa pili ni wa my niece Jessica Kateti Sarungi.  Huu msiba umetokea jana katika Hospitali ya Muhimbili. Marehemu Jessica alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa SickleCell na jana Mungu aliamua kumpunzisha.
FB_IMG_1432479118688Napenda kuchukua fursa hii kuwapa pole au salaam zangu za pole kwa familia ya kaka yangu Jamoko Kateti Sarungi (kwenye picha hapo juu). Kwa jinsi ninavyo mpenda mwanangu sipati picha ni maumivu ya namna gani waliyo nayo sasa kwa kuondokewa na binti yao kipenzi. Mungu awe nanyi katika kipindi hichi kigumu. Jessica atasafirishwa kwa ndege kesho hasubui kwenda kijiji Utegi ambapo ndipo wazazi wake wanaishi, pia ndipo Jessica alipo zaliwa na kukulia.

Picha za kuagwa kwa Jessica zimepostiwa na baadhi ya blogs, naomba niseme hili, binafsi sipendezwi na tabia ya watu au baadhi ya bloggers kupost picha za maiti kwenye mitandao. Ila hii link ambayo naweka ni blog ya mtu mwingine hivyo ipo nje ya uwezo wangu. Zipo Hapa

Najua kuna watu wanaweza kujiuliza kuwa nina undugu gani nao especially hiyo last name ya Sarungi kwasababu ni jina ambalo limezoeleka sana katika jamii ya Watanzania.

Kwa baadhi ya watu ambao hawatujui vizuri ngoja nifafanue kama ifuatavyo; Ukoo wa Marehemu Chief Igogo ni mkubwa sana. Hii inatokana na kuwa Chief Igogo alikuwa na wake 19 ooh yes! Nineteen wives! Sasa you can imagine huu ukoo ni mkubwa kiasi gani. Chief Igogo alikuwa babu yangu aliye mzaa babu mzaa baba (My partenal great grandpa) ambaye kwasasa naye ni marehemu. Yeye alikuwa anaitwa William Olunga’a Igogo. Kwa wale wanao jiulizaga kwanini baba yangu mzazi initials zake ni O.O.Igogo basi mtakuwa mmepata jibu. (Otieno ni first name, Olunga’a ni middle name, na Igogo ni m last name).

Sasa William (Olunga’a), Sarungi, Sassi, na wengine ambao sijawataja wote ni watoto wa marehemu Chief Igogo. Sasa nafikiri utakuwa umepata picha ya undugu wangu na wakina Sarungi, Sassi, na Igogo. Kama unaswali usite kuniuliza  🙂

Tunamshukuru Mungu kwa yote. Bwana alitowa, na Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe milele zote!

4 thoughts on “Mungu ni mwema wakati wote!”

  1. Umenigusa mno kwa upendo uliouonyesha kwa wapendwa wetu waliotangulia mbele za haki, pia na jitihada zako za pekee kuanzisha blog yako kwa kujitegemea.

Leave a Reply