Safari ya mama Washington DC

 Siku iliyofuata, tuliamka na kupata breakfast, kisha tukaendelea na mizunguko yetu.     Nilitaka mama aone Washington DC yote kila jengo la office na majumba ya matajiri wa huko. Bahati mbaya au nzuri mama alikataa kutembea alidai amechoka kwasababu ya mizunguko ya jana yake. Hivyo, ikabidi tuchukue tour bus ambayo ilituonyesha sehemu zote tulizopenda kuona. Of course, nimuhimu kusalimiana na wapendwa wako pale unapopata nafasi. Basi hapa tutakutana na cousin yangu (mtoto wa mama yangu mkubwa, mama yake ni wapili kuzaliwa katika familia ya mama yangu) Dr. Joseph Obure yeye anafanya kazi hapo Washington DC. Mama na wanae Mama na kijana wake  wakisogoa story za miaka mingi ? 

Mama na binti yake katika pozi ?


Siku ilyofuata, tulianza kwa kununua green tea na pumpkin bread (my all time favorite breakfast) katika cafe ya Starbucks, tuliungana na aunt yangu aitwaye Sophie au mama AnnaD na baadaye kuanza safari ya kuelekea Makao Makuu duniani ya kanisa la Wasabato.  

Hili eneo ni kubwa sana kama utabahatika kutembelea basi panga angalau masaa azidi ya matatu ili uweze kufaidi na kujifunza kidogo. Mama yangu alifurahia sana. 

  

Basi safari yetu kwa siku hii ikaishia napa, tukaenda kula na kufanya mizunguko kidogo ya dakika za mwisho kwani muda wetu ulikuwa unatupa mkono.    
Nawatakieni maandalizi mema ya Sabato na Sabato njema kwa waumini wote wa dhehebu la Wasabato duniani ?

One thought on “Safari ya mama Washington DC”

Leave a Reply