“….punguza kiburi, si ujanja kumnyanyasa mtu anayekupenda kwa dhati” Iddi Makengo Jr

Mwanamke anapokuomba msamaha baada ya wewe kumkosea usidhani ni mjinga, usijipe kiburi kwa kudhani labda hajui anacho kifanya, usivimbe kichwa na kujidanganya kua labda huyu hana pakwenda ndiyo maana ananinyenyekea. Usijisahu na kurudi kosa lile lile kisa unajua kuwa atakuomba tena msamaha na wala usijisifu kwa tambo kuwa wewe ni mjanja zaidi yake. fb_img_1477604978231Anakuomba msamaha kwasababu anfaahamu thamani ya ndoa yenu, anafahamu thamani ya mahusiano yenu, anajua gharama ya kutengana kwenu, anakumbuka yote aliyopitia mpaka kufikia hapo mlipo, anathamini yale mzauri kidogo ambayo ulishawahi kumfanyia na anajua kuwa katika mahusiano nilazima awepo mmoja wa kuyalinda. Usimsukume kusahau yote hayo.

Acha kumfanya kukata tamaa ya kulipigania penzi lenu, usimfanye kukata tamaa ya kusimama kwaajili ya ndoa yenu, usimfanye kukata tamaa ya kupata furaha tena kwa sababu mwanamke anapokata tamaa na ndoa jua hamna ndoa tena, hamna mahusiano tena, unacheka sasa kwakua bado anakuvumilia lakini siku akichoka kukuvumilia basi utalia lakini machozi hayatatoka, punguza kiburi, si ujanja kumnyanyasa mtu anayekupenda kwa dhati.

One thought on ““….punguza kiburi, si ujanja kumnyanyasa mtu anayekupenda kwa dhati” Iddi Makengo Jr”

Leave a Reply