Category Archives: Relationship

Hongera sana Isaka na Sarah!

Mr and Mrs Isaka Alexander Olung’a Igogo

Hayawi hayawi sasa yamekuwa! Wamehalalishwa duniani na Mbinguni yakwamba wawili hawa ni mwili mmoja!

Sarah akila kiapo kitakatifu

Agano hili takatifu lilifanyika siku ya Jumosi tarehe 05 /08/2021 katika kanisa la viziwi lililopo huko Bunguruni, Dar es salaam. Tunawaombe baraka nyingi sana katika familia yao hii mpya walio ianzisha!

Bibi harusi

Bwanaharusi akihakikisha je kweli ni yeye?! Kabla ya kula kiapo, maana hukawii kubadilishiwa mke kama Jacob (Yakobo)! ? mjini mambo mengi jama! ?

Bwanaharusi amehakikisha na ameridhia! ?? Kama hujawahi sikia kisa cha Jacob (Yakobo) basi chukua Biblia yako na ufungue kitabu cha mwanzo sura 29 yote itakupa stori kamili!

Kwaufupi ni kwamba, Jacob baada ya kutumikia miaka saba kwa mzee Labani kama mahari ya kumuoa binti yake Rachel (Raheli), siku ya harusi akakuta amebadilishiwa mke anaye mpenda kwa dhati na kupewa Lea ambaye alikuwa ni dada wa Rachel (Raheli). Kwani kulingana na mila na desturi za kabila na ukoo wa mzee Labani ni kuwa mkubwa lazima aolewe kwanza ndipo mdogo anafuata. Kwa maana hiyo Jacob ilibidi atumikie miaka 7 mingine ili aweze kumpata Rachel. Kwa maana hiyo Jacob alitumikia miaka 14 kwa mzee Labani kama mahari ya kumuoa kipenzi cha roho yake! …… Sikilizeni wanawake wenzangu, kama mwanaume anakupenda basi hakuna gumu wala zito mbele ya macho yake! He will move mountains just to have you! Tena bila hiyana yoyote! Wanawake wazuri ni wengi sana lakini Mke ni mmoja tu ambaye kila mwanaume anajua hilo!

Maharusi na wapambe wao
Wasimamizi wao
Mchungaji aliye idhinisha ndoa hii

Sarah akisindikizwa na kaka yake aitwaye Alex ambaye ndiye aliyemlea toka wazazi wake wamefariki hadi leo hii anapokwenda kuanzisha nyumba yake mwenyewe. Kwa Sarah hamuoni Alex kama kaka bali ni baba yake mlezi na mke wa Alex ni mama yake mlezi, hao ndio wazazi wa Sarah.

Hapo juu ni baba mlezi wa Isaka ajulikanaye kama mzee O.O Igogo. Yeye ndio amemlea Isaka toka akiwa na miaka 5. Baba mzazi wa Isaka amefariki takribani miaka 7 iliyopita. Mzee 0tieno Igogo ni mdogo wake na marehemu mzee Alexander Igogo ambaye ndiyo Baba yake na Isaka.

Mama mlezi wa Isaka Mrs O.O Igogo akisalimia maharusi, nyuma yake ni mjukuu wake aitwaye Essy.

Mashangazi na mama wakubwa kwa wadogo upande wa bwanaharusi.

Baba mlezi akiwa na furaha nyingi usoni kwa kuongeza mtoto mwingine kwa familia.

Madada, mabinamu, na mashemeji wakiingia kwa shangwe!

Kutoka kulia, ni mdogo wa bwanaharusi aitwaye Blessing, akifuatiwa na mpwa (niece) wa bwanaharusi Essy, akifuatiwa na shemeji mkubwa Mrs. Vetto Igogo, na dada mkubwa (wapili kuzaliwa kwenye familia ya kina Isaka) Aphino Alexander Igogo (Mrs Ogoche).

Mdada mwenye nguo ya blue kutoka kushoto, huyo ndio kitinda mimba kwenye familia ya akina Isaka. Anaitwa Rhoda Alexander Igogo. Naye harusi yake ni mwishoni mwa mwezi huu. Wiki hii ni kitchen party yake.

Bibi harusi mtarajiwa Rhoda Alexander Igogo akiwa na maharusi Mr and Mrs Isaka Alexander Igogo.

Bibi harusi mtarajiwa, bi Rhoda akifurahia kaka kupata “jiko”!

Mama mlezi wa bwana harusi pamoja na baba msimamizi wa ndoa hii mzee Samuel Olung’a Igogo wakitoa nasaha zao.

Baba mlezi akitoa neno kwa niaba ya kamati!

Mama mlezi akiwa na maharusi

Maharusi wakikata keki!

Wapendwa, kwamahitaji yako ya Cake nzuri zenye ubora wake, juice fresh tamu, na Mc wa kitchen party, tafadhali husisite kumtafuta @isadoricakes_and_sassyjuice ndio habari ya taifa! ???

nnnnn

Maharusi wakifungua dancing floor kwa kucheza ziro-diatance music ?? asiye na wake akumbatie chupa ya soda! ???

Meza kuu upande wa bibi harusi

The Olung’as!

Hawa ni baba zake Isaka, wadogo kwa wakubwa. Kutoka kushoto ambaye kichwa tu ndio kimeonekana ni mzee Samuel Olung’a Igogo (baba mkubwa na msimamizi wa ndoa hii), akifuatiwa na mzee Charles Olung’a Igogo (baba mkubwa), akifuatiwa na mzee Otieno Olung’a Igogo (baba mdogo na mlezi wa Isaka), akifuatiwa na Genga Olung’a Igogo (baba mdogo)

Walianza na Mungu, wakamaliza na Mungu. Mama mdogo wa Bwanaharusi Mrs Emmanuel Agonda Sassi Igogo akitoa sala ya mwisho!

Mathayo 19:5 “akasema, Kwa sababu hiyo, mtu atamwacha babaye na mamaye, ataambatana na mkewe; na hao wawili watakuwa mwili mmoja”!

Marko 10:9 “Basi, alichokiunganisha Mungu mwanadamu asikitenganishe” ….. I present to you Mr and Mrs Isaka Alexander Olung’a Igogo

Mc Rhevan mtu kati hapo

picha zote shukrani kwa Mc Rhevan studio. Ukitaka kuona picha za tukio nzima tembelea ????https://RHEVANSTUDIO2021.pixieset.com/isakaandsarahweddingphotos/

hollietheblogger: So many people ask me If I get paid to promote

Regrann from @hollietheblogger - So many people ask me If I get paid to promote @zarithebosslady the answer is NO. But let me tell you what I gain and why I waste my time..it’s her rare STORY‼️ Rare because, she chose HER and HER KIDS above EVERYTHING something many women have no courage to do‼️ My benefits might NOT be in monetary terms but it’s in a sense of hope and reassurance. Reassurance that in future our daughters will NEVER have to sit silent in abusive relationships just because the society expect them to. But because of Zari’s and many other women’s experiences they will have the strength to reclaim CONTROL and emancipate themselves‼️ Just like you, in Zari I see my mother, my sisters, my aunties & best friends. Women who have been cheated on, abused and emotionally & physically trampled on. Women whose happiness have been snatched by another woman. Homes and children left fatherless, loveless, poor and homeless just because of men’s selfishness. Despite all these evil, society and some ignorant women still believe it’s ok for a man to disrespect a woman‼️ Religion & culture teach us that women are beneath men & aren’t allowed to be their own person. When a woman rises up to be her own voice there is so much noise surrounding her strength. Therefore if someone say that DP actions were innocent & didn’t mean any harm, I say that is nonsense. 

Zari the real Bosslady

DP knew and still knows what he does. His actions were & are still emotionally abusive and were/are meant to break ZARI and leave her dependent and powerless just as he’s done to all his exes. DP has broken them all emotionally and left them powerless and dependent on him‼️If Zari had hold on to this nonsense this guy would have continued to demean her publicly to show her she’s worthless. These actions would have created fear and decreased her self esteem making her dependent on him‼️? So don’t expect the dirty ***  to move on or find happiness anywhere else because she’s EMOTIONALLY broken and will sit in that rented flat as a side fuck for the rest of her life?Compared to Zari who had a loving upbringing, these two are both as bad as each other because they both had a fucked up-bringing #revisitthispostinfuture #goodmorning - #regrann

Relationships is understanding beyond any reasonable doubt that NO ONE IS PERFECT‼️

#RepostSave @hollietheblogger with @repostsaveapp  Relationships are never going to be what you want, what you expect, what you need, what the society expects or what people will say. F*ck all that BS‼ Relationship is what YOU make of it. Relationship is what you dream of and wake up and put in time to get what YOU want. That’s why you see people investing in their spouses, children and partner and silly people want to snatch not knowing it’s someone’s effort for them to look the way they do??‍♂️Relationship is failing, making mistakes, learning and growing together. Relationships is understanding beyond any reasonable doubt that NO ONE IS PERFECT‼ Relationship is about saying sorry, acknowledging your failures and forgiving. That’s the best relationship that’s the lasting relationship! ? ?? For those who know about Tuckman’s theory well and good for those who don’t know I will sum up quickly. Tuckman believes that relationship is formed in 4 stages, forming, norming, storming and performing. Forming is when you meet someone for the first time and form a relationship. Norming is where you normalise stuff. You’ve known each other and now you go to get coffee together to normalise your relationship. Storming is where the PROBLEM IS‼ this is where hell breaks loose! Now that you have met, gone for a coffee you are now at a stage of knowing each other’s weaknesses‼‼?? This is where relationships break, die and murder happens BUT good news is that if you have survived this stage you’ve triumphed because performing stage you are just enjoying each other and it will take a miracle to break up or YOU AGAIN? However to get to performing it takes time, years to be precise. So to sum up Zari and her mother in law have passed the storming stage that’s why you see she’s comfortable with Wema visiting. So just remember when you are going through challenges in your relationship which stage are you at! ...?‍♀️?‍♀️???‍♂️

Haikutokea pasipo kuonyesha dalili za kifo!

Wapendwa wasomaji wangu haswa wanawake wenzangu, naomba msinishangae kwanini sijazungumzia vifo vya kinyama vya wanawake wawili vilivyotokea wiki iliyopita.  Kwanza nawapa pole wafiwa wote na familia zao,  Mungu awape faraja katika mapito haya.

Alpha Igogo, blogger

Pili, mimi maswala haya ya domestic abuse haswa kwa wanawake nilishawahi waeleze huko nyuma kuwa ni mambo ambayo sina nguvu sana ya kuyaelezea kwani vinakuwa vinanikumbusha maumivu makali sana ambayo  sitaki kuyafikiria wala  kuyazungumzia kwa sasa. Siku nikijiona nina nguvu ya kuongelea  basi nitawaelezea. Ila kwa sasa acha watu kama akina Joyce  Kiria wayaongelee. Ndio maana hata yule dada  aliyeuliwa na mumewe kule London sikusema kitu siyo kwamba sijali ila ninakuwa na maumivu yaliyo changanyika na hasira hivyo naona ni bora kunyamaza kuliko kuongea nikiwa na hasira. 

Tatu, wanawake wenzangu, hawa wanaouliwa haikutokea tu pasipo kuonyesha dadalili za ukatili ambazo zitaashiria kifo! Haya mambo yanaanza kidogo kidogo na kadri unavyojaribu kuvumilia ukatili huo unao uona ni mdogo ndio unavyomjengea mazingira mazuri ya kukumaliza kabisa! Kataa ukatili wa aina yoyote ile, Hawaanzi kwa kupiga huwa wanaanza kwa kukutenganisha na ndugu na marafiki zako wa karibu ili usiwe na msaada wowote. Ukisha ona mumeo au mpenzi wako anaonyesha dalili za kutaka utengane na ndugu zako au wazazi wako basi anza kulala macho wazi!! Halafu utakuta yeye ndio anataka wewe uonekane mbaya yupo busy kuongelea udhaifu wako kwa watu bila kusema makosa yake ogopa sana! Kwanza mwanaume anayekupenda hata mgombane vipi hawezi zungumzia matatizo yenu kwa watu, mtagombana wenyewe na kuyamaliza wenyewe!! 
Ogopa sana mwanaume asiyejali hisia zako! Emotional abuse ni dalili kubwa ya pili katika maswala ya unyanyasaji. Akisha kutenga na ndugu zako basi lazima kinacho fuata ni ukatili wa kihisia na baada ya hapo atakupiga kama hata kuuwa basi atakuachia kilema cha maisha! 

Jamani hii ni karne 21 nani bado anataka kuishi maisha ya zama za giza?  Eti mwanaume anakupiga mpaka mimba inatoka halafu bado unamwita mume wangu? Au mtu eti mwanaume anakwambia utoe mimba kwasababu hataki watoto wa kike nawe unakubali??? halafu unjiita msomi?! ??

Jamani, Joyce Kiria anongea kwa sauti mwenye masikio na asikie asiyetaka shauri yake. Dalili huwa zinaanza mapema uwamuzi ni wako kuzikemea au kuzilea mpaka utolewe roho. Nachoomba tu tuwafundishe watoto zetu wa kike kwamba ukatili HAPANA! Napia watoto wetu wa kiume wafundishwe kupenda na kuheshimu wanawake kwani hata mama zao ni wanawake vile vile!

“If you find true love don’t look at limitations”

START TO SEE ADVERTSITY THE RIGHT WAY.

When life hits you with so much pain,so much hurt & disappointments, you need to find strength & comfort in knowing that God didn’t promise us days without pain, laughter without sorrow, or sun without rain, but He did promise strength for the day, comfort for the tears & light for the way.

If God allows it on you, He will also bring you through it all & you will never be the same again. Whatever you are going through – He has a reason.

Here she is;
Princess ? Meghan Markle
—————-

She is half black ,half white.(Biracial) African American origin.

Her parents got divorced when she was 6 years old

She was married before @30 years and divorced two years after .

Despite these factors you may consider as odds and a humble/not too smooth beginning, she rose above these circumstance and made a mark for herself.

She became a popular and successful actress

Became an advocate for gender equality and women empowerment.

Became a Global Ambassador for World Vision Canada

Became a UN advocate for women

Owns her own Clothing Line

She is Founder and Editor-in-Chief of her own blog.

And now at age 36 she is married to Prince Harry of England who is 34 years
Love is the way.she is making a grand entrance into The Royal Family! That is the story of MEGHAN MARKLE!

Amidst all, her family instead of supporting her new found journey to happiness, they’re busy putting her down. This coward brother writes to Prince Harry not to get married to a divorcee, old….
She’s an epitome of a true humble lady.

MORAL OF THE STORY:

1. Prince Harry followed his heart to beat all odds. If you find true love don’t look at limitations.

2. Your family background is not a limiting factor to anything.Do not let society define who you are, or friends telling you how old you’re and should be getting married!

3. The end of one marriage does not mean the end of your life!

4. Work hard to pick up the pieces of your life and start all over again! Do not give up on yourself .

5. Do not despise the days of humble beginning. Start small even as a brief case girl or tea girl or a secretary but don’t stay small. Dream and think big, stay focused , keep your eyes on the ball and aim for the stars.

6.. You may have to kiss a few frogs before you meet your Prince. Don’t give up on love ! You are lova

Never loss hope because Life can go from 0 to 100 Real Quick” ???.

Good Morning Everyone. Blessed Sunday. Ramdhan Kareem. NTV Mwasuze Mutya 9am.Every Weekday. NTV/Spark TV.

Toni Braxton akubali pete ya Mr Birdman

Je, wewe unampenda mtu kwa muonekano wake, taiba, familia aliyotoka, akili zake, sura, pesa, jinsi anavyokuonyesha heshima n.k?  Mwanamuziki Brian a.k.a The Birdman  anasema "so what? What that gotta do with love?"  Hayo yalikuwa ni maneno yake baada ya Talk show host Wendy Williams kusema kuwa yeye alikuwa mtu wa kwanza kusema "hapana" aliposikia Toni Braxton ana mdeti The Birdman! Wendy amemueleza Mr Birdman kuwa muonekano wake na Toni ni tofauti sana hapo ndipo Mr "The Birdman" akasema vinahusiana nini na kupenda?! Yeye ni 'certified gangsta' ?? aliye kuzwa na street kwasababu mama yake alikufa akiwa na miaka miwili (2), baba naye japo hakuwa sana kwenye maisha yake naye alikufa, kaka, dada, bibi, babu wote wamekufa hivyo vitu hivyo vinemfanya asijue nini maana na thamani ya upendo lakini siyo kwamba hajui kupenda!  "I’m just a gangster, that don’t mean nothing. Certified too. What that gotta do with love?" Wendy alishikwa na kigugumizi baada ya jibu hilo! 

Hilo nalo ni somo kwa wengi wetu tunaopenda kusema "kampendea nini?" Wewe ukiona watu wanapendana kama huna jema lakusema nyamaza lakini ukitaka kujua kampendea nini utaumbuka kwani hayo ni ya Ngoswe muachie Ngoswe mwenye! Kila mtu ana kitu chake ambacho anatafuta katika kumpenda mtu sasa mambo ya kujifanya  mimi sijui "Engineer" ooh mimi "mfanya biashara" sijui msomi gosh!! What that gotta do with love?!! Kwani siku ukiwa huwezi kunyanyuka kitandani hizo degree zako zitakunyanyua kitandani? ?? Watu wanaangali potential ulizo nano! Unaweza ukawa mzuri na elimu nzuri lakini akili ya maisha hauna azidi ya kutaka kuwa "trophy wife" au "Mario" ulishwe na kuvishwa na mwanamke halafu bado utake uitwe mume ? anyway, Birdman amemvisha Toni pete yenye thamani ya $5,000,000

The Birdman siyo mwanaume pekee ambaye anatarajia kufunga ndoa na mtu ambaye watu wengi walidhani haiwezekani.  Prince Harry naye mwaka jana mwishoni alimvisha pete ya uchumba muigizaji wa kimarekani ajulikanaye kama Megan Markle. Kwa hapa Megan ni mkubwa kwa Prince Harry kwa miaka mitatu (3yrs) na pia huko nyuma alishawahi kuolewa na kuachika. Ndoa yake ya kwanza ilidumu kwa miaka miwili (2 yrs) baada ya kudate kwa kwa muda wa miaka 6 ?? Hivi ndivyo vitu ambavyo sivielewi watu wadate kwa miaka sita halafu ndoa idumu kwa miaka 2 tu!! Tena hapo mpaka divorce imetoka ina maana atakuwa walitengana at least miezi 6 kabla ?‍♂️?‍♂️ Haya huyu Prince Harry ame mvika pete baada ya kumdate kwa muda wa miezi 15 (sawa na mwaka mmoja na miezi 3). Je, nitakuwa sahihi kusema ngoja tuone hii itadumu kwa muda gani au tuwatakie kheri tu ?

Btw, hata Toni Braxton hii itakuwa ndoa yake ya pili! Ndoa yake ya kwanza ilikuwa na mwanaume mwenye asili ya ngozi "nyeupe" ilidumu kwa muda wa zaidi ya miaka kumi na mbili (12  yrs) na alizaa watoto 2, Toni ana miaka 50 sasa.....Haya wale tunao pendeza hii show ya Braxton Family Values ndio tutakao faidi uhondo wote ? Siamini siku hizi nimemuambukiza mama yangu kupenda hizi show ?? anajua mpaka ratiba zake ??

Zari Hassan: I have decided to end my relationship with Diamond, as my RESPECT, INTEGRITY, DIGNITY & WELL BEING cannot be compromised

 @Regranned from @zarithebosslady - Understand that this is very difficult for me to do. There have been multiple rumors some with evidence floating around in ALL SORTS of media in regards to Diamond’s constant cheating and sadly I have decided to end my relationship with Diamond, as my RESPECT, INTEGRITY, DIGNITY & WELL BEING cannot be compromised. We are separating as partners but not as parents. This doesn’t reduce me as a self-made individual, and as a caring mother, and the boss lady you have all come to know. I will continue to build as a mogul, I will inspire the world of women to become boss ladies too. I will teach my four sons to always respect women, and teach my daughter what self-respect means. Unlike many, I’ve been in the entertainment industry for 12 years, and through all my challenges I came out a victor because I am a winner, and so are all of you Zari supporters. 
HAPPY VALENTINE'S - #regrann

Repost:- Je, Zari ataweza kubeba “bendera” za nchi mbili?

  Katika Biblia kuna maneno yanasema ‘hakuna mtu awezae kutumikia mabwana wawili’! Yani kiufupi lazima mmoja utampendelea na mwingine utamuonea kwa mapenzi ya uwongo! Sasa, wote tumeshuhudia maisha ya Zari na Ivan mpaka kuachana kwao. Lakini pamoja na hayo Ivan bado hakuona mtu mwingine ambaye angefaa kulinda mali zake, watoto wake, na kuhakikisha kuwa his Legacy forever lives zaidi ya Zari. Na Zari mwenyewe kwa mdomo wake alitamka mbele ya kadamnasi siku ya mazishi ya Ivan Ssemwanga  (SomaHapa) kua atavaa viatu vya Ivan Ssemwanga, kwani yupo tayari, anaona kama she was prepared enough for it!!  Na kwamba she will do it for his boys, his family, friends, and his legacy!  Swali ambalo ninajiuliza will Zari be able to be a “flag bearer” for the two men from different countries?!  Can she honestly, sincerely, and lovingly serve the “two masters”! ……..Personally, I’m not sure but very curious to see how will this go down considering one of her “men” is still living and 100%  involving in her life!………Will Zari disappoint many or will she continue to shine and come-out as a shero? Will this be Zari’s downfall as she may lose some sort of “respect” from Ugandans who are / were hardcore fans of the “Rich Gang” particularly  The Don- Ivan Ssemwanga?! Will Watanzania accept Zari and give her 100%  support to carry their flag as Diamond’s wife especially after his bizarre behaviors of abusing and disrespecting women!?! Remember “The B**** is dying for fame”  and “the baby is not mine”! And finally, the boys are growing up, one day they will have bunch of questions to ask! How will her children feel? Will they feel a sense of betrayal from their own mother; the only living parent?! Can’t get any better than this!! I will surely keep up with the story. And You be the judge!

 

 

*** Hii ni Repost, niliandika August 31st  mwaka jana. Tujikumbushe na tutafakari kama niliyosema yametokea au bado au kuna dalili ya kutokea!****

Msikilize Aunty Ezekiel akieleza historia yake na Moses

 Kama kuna wapendanao ambao nawapenda sana kwenye hii kitu inaitwa Bongo movie / Bongo flava basi ni hii couple! Mie sijawahi kaa kuangalia Bongo movie toka enzi ya Mambo Hayo (wahenga mtatujua tu ?) hata movies za marehemu Kanumba sijawahi kaa nikaangalia!Mimi siogopi kusema ukweli as truth will always set me free napia inanipunguzia marafiki wasio na tija ?? Mambo ya hawa wasanii wa siku hizi honestly yana nikera sana! Wengi tunawajua kwa scandle zao kuliko talent zao! Lakini kwakweli lazima nikubali kuwa Aunty na Moses wamenifanya nianze kuwachambua mmoja mmoja nakugundua kuwa kumbe kuna wengine wanajielewa na huwenda ipo siku moja nitakaa chini kuangalia Bongo movie tena! Natamani wasanii wakike wa aina zote wangekataa huu udhalilishaji wa wanawake unaotumiwa na promoters na media eti "kutafuta Kiki" kwa kuwekwa kwenye scandle zisizo na kichwa wala miguu ili kazi yako au kipaji chako kionekane! Huu ni udhalilishaji period!! Kama mtu ana talent tafuta njia sahihi ya watu kuona talent yake nasio kuwapa kashfa za kutembea na wanaume!! If someone got talent people will see it!! Chema chajiuza kibaya chajitembeza!!!

Anyway, back to Aunty Ezekiel na Moses wake, kumbe jina la Aunty ni jina lake halisi aliyopewa na baba yake! Mimi nilifikiria ni jina la kuigiza ? ......Halafu wewe Moses wewe huyo shetani aliyekuingia sijui alitokea wapi, sasa sisi tungemuona wapi Cookie?! ......... Please people interview ipo very raw  yani Aunty Ezekiel kafunguka haswa lakini usishangae sana kwani hayo ya kutoa mimba na kwenda kwa waganga ni mambo alifanya wakati huo yupo kwenye "giza nene" Ni mambo ya kale! Don't judge  if you know what I mean ???  Hey every Saint has a past, every sinner has a future, and who are you to judge anyone!

RC Paul Makonda: haikuwa rahisi kama siyo Mungu kuwatumia wateule wake sijuwi leo nigekuwa wapi

@Regranned from @paulmakonda - Mwaka 2017 ni mwaka watofauti sana kwangu. Leo tunapojiandaa kupokea Mwaka 2018. Ni vyema nikayatazama maisha yangu ndani ya mwaka 2017 hakika huu ulikuwa mwaka wa aina yake. Ni mwaka ulionipa marafiki wa kweli, lakini kubwa kuliko ni Upendo na Maombi niliyoyapata kutoka Kwa Kipenzi changu Maria. Nikuambie kitu ndg msomaji...... haikuwa rahisi kama siyo Mungu kuwatumia wateule wake sijuwi leo nigekuwa wapi. Nimepewa kila jina baya, kila jambo baya nimefanya mimi ,matusi yote yalikuwa yangu na hata watu kutamani nisiwepo duniani. Lakini kwako Mpenzi ilikuwa tofauti, ulinitia moyo Kwa sauti ya upole,uliniombea na kunifuta machozi bila kuchoka. Tena Kwa kusema Nanukuu, Paul Mungu hajawahi kukuacha hata kama Dunia yote inakuona haufai nataka nikuambie Mungu amekupaka mafuta Kwa kazi hii simama na usonge mbele. Mwisho wa kunukuu”.Ndg zangu na wananchi wenzangu ni vyema mkajua kila mtu anayo hadithi ya kumweleza mwenzake ila kwangu inahitaji kitabu kuyaeleza mapito na njia nyembamba niliyoipita mwaka 2017. Itoshe kusema Mungu wa haki iko siku atasimama na kutoa hukumu ya kweli Kwa watu wote. Kwani yeye anatujua kila Mtu na matendo yetu tena kwake hakuna Siri ya maisha yetu.Nakupenda sana Maria wangu na ninathamini sana Mchango wako ktk utumishi wangu hapa Duniani. Uzidi kuwa Imara simba wangu ili niyafanye yote mema ambayo Mungu amepanga Kwa watu wake. Asante sana Mungu Kwa kunivusha mwaka 2017.

“Hatuna formula sometimes hata hatuelewi what we are doing…ila tunachojua tunapendana”

My 2017 best Tweet: “You are the air that I breathe”Kuna comment nyingi kwenye hii tweet ambazo zinachekesha sana sema nimechagua hizo tu!    

Ngoja niwaambie, kwakweli hakuna kitu kizuri kama kumuona mtu kama Dr Mengi anajishusha na kumuheshimu. kumpenda  mwanamke namna hii! Yani inavutia sana kuona mtu mwenye elimu yake nzuri sana, anapesa zake, na all the power kwenye public and yet he can humble himself like that! "You are the air that I breathe"! Hivi niwanaume wangapi wa Kitanzania ambao wamesoma labda wana Masters tu wanaweza kusema maneno Kama haya kwa mkewe ambaye elimu yake ni sawa na "sifuri" kwake?!! Enyi vijana wa Kitanzania jaribuni kuiga wazee kama akina Dr Mengi mtabarikiwa zaidi! ........And Nope! Wakubwa hawafaidi!! Muheshimu na umpende mkeo kwa dhati in private and in public nawe uone kama hauta faidi!! Muache ukatili!!!...........Kwa maana hiyo hii imekuwa my best tweet for 2017! Kama mjuavyo hii blog upendo ndio dini yetu, basi tumefurahi sana na hii tweet!

Baba_Dangote: when I say I love you true means it agah!…..The only thing I have in my life is you!

Love in the air! Hivi mnakumbuka wakati nilimtakia mama Diamond kheri ya kutimiza  miaka 50 nikauliza where is "step dad" kwasababu miaka khamsini bado kijana kabisa! Embu soma hapa (kheriyamiaka50MamaDiamond) Eeh, unajua haikukaa sana tukaanza kusikia fununu kuwa mama yake Diamond kaolewa!

Mama Diamond siku ya harusi yake

Najuzi kati kwenye harusi ya Romy Jones akatokea naye pia  mama Diamond alisema rasmi kuwa kaolewa na tusubirie mziwanda anakuja ?? uzee mwisho 'kanda ya Ziwa' huku Pwani wote baby ???

Sasa naona kila mtu ameshakubaliana na hiyo hali na baba wa kambo naye kawa huru hata kumposti mkewe na familia yake kwenye social media! Baba kafa kazimia kwa mama, mpaka kaamua kujiita "baba Dangote" kwenye account zake za Instagram ili kuendana na jinsi mama yake Diamond anavyo jiita kwenye social media. Binafsi, I don't see a big deal at all!! After all ni mumewe halali siyo boyfriend so what the fuzzy is all about! Ingekuwa just a "strange man" sawa lakini huyu kaka kafuata mila na sheria zote za dini ya Kiislamu kuoa hivyo sasa kunatatizo gani mtu kumposti mkewe wapekee hakuna maswala ya ukewenza kusema anampendelea?!! Jamani life is too short let others be!

Baba na binti yake

Maisha ya wanawake wengi wa Kiafrika ni ya shida, many don't get the privilege to enjoy their youth! Yani kuna maisha yaliyopangiliwa na familia pamoja na jamii mtu binafsi hupati nafasi ya Ku experience life and choose what is best for you! Nakama bado haitoshi, wengi wanafiikiria ndoa zitawapa furaha matokea yake emotional abandonment is all they experiencing!!.......... Kama kwa wenzetu Waislam wanaruhusiwa kuachana kiurahisi hivyo wanawake wengi wanaishia kuteseka kulea watoto wenyewe bila msaada wa baba zao! Hivyo, pale mwanamke anapopata mtu wa kumfanya ajisikie 16 again why not?!! Let her enjoy the youth life that was once snatched away from her!! Mimi hizi double standard za Wabongo hata sizielewi!! Wanaume wanaoa wasichana ambao wamepishana hata zaidi ya miaka 30 na watu mnaona sawa tu! Lakini mama wa watu wamepishana miaka kumi tu inakuwa shida?! Ni wivu ama?? Tatizo Nyota aa  ???  Haya, wenzenu wako honeymoon South Africa wakati nyie mnaojiona wasichana wabichi mnaambulia kupelekwa  Ramada Inn Bagamoyo, kwani mmekuwa waganga wa kienyeji  ??  ??? napenzi kama bia nileweshe ee chupa kilo mia nibebeshe ee ??  Halafu Baba Dangote handsome boy kweli kweli, he truly needed a "Nanny" to babysit him ?? BTW, hivi huyu stepdad hana watoto eeh? Mbona anasema "the only thing I have in my life is you"?! Kama hana basi hapo bi Sandra ata enjoy sana maana hakuna mambo ya ada za shule sijui uniform za watoto, Mara oh, watoto wanaumwa makamasi ?? inahusu?!????  #RULE YOUR LIFE

Mama Diamond amsifia mkwewe!

Pale mama mkwe anapokuwa msemaji wa penzi lako! Well!! Inakufanya ujisikie vizuri lakini bado huwalisia utabaki pale pale! Kama mwanaume hakupendi kwa dhati nawala hakuheshimu hata mama mkwe akupende vipi haitobadili kitu! Heshima na mapenzi yako kutoka kwa mumeo ni lazima mumeo haonyeshe mwenyewe nasio mama mkwe wala wifi zako au ndugu wa mumeo! …..anyway, yangoswe hayo ngoja tumuachie ngoswe mwenyewe!

Tamar Braxton amekwenda mahakamani kuomba talaka!

Nashindwa kuelewa ni kitu gani huwa kinatokea, ndani ya miezi michache watu wanakataa kabisa kuwa ndoa yao ipo sawa na hizo rumors ni maneno tu yamtaani!! Wanathubutu hata kumtaja Mungu!! Halafu hamjakaa sawa mnasikia wame file for divorce kuwa wameshindwana! Sasa najiuliza why lying!?! Kama ndoa inamatatizo si unasema tu, kuwa ndoa yetu haipo sawa lakini we are working on it, just pray for us!! Kuliko kudanganya!! Kama hapo ?kwenye video Tamar na mumewe walivyo jieleza kwenye Wendy Williams show mwezi wa tatu mwaka huu embu wasikilize

Kana kwamba hiyo haitoshi hata mwezi uliopita alipo ulizwa akasema yupo teyari kufanya chochote kile kulinda ndoa yake. Na hivyo kitu chakwanza ambacho anafanya ili kuokoa ndoa yake ni kuachana na "showbiz business" ataacha kutengeneza album za nyimbo mpya! Sasa within 30 days inakuwaje mtu huyo huyo ndio anakuwa wakwanza kudai talaka ??  I don't get it!.......

Lakini ukiangalia kwaundani utagundua huyu Tamar kuacha kuimba siyo kwasababu alikuwa anataka kuokoa ndoa yake bali ni njia ya kumuondoa mumewe kuwa Manager na producer wake. Kama mnakumbuka how Lady JayDee alivyo mfanyia Captain Garnder Habash ?? smart lady huh! .......Jamani let your husband be your husband! Mambo ya mumeo kuwa Manager wako kwakweli naona ndoa nyingi zinavunjika ni wachache mno wamefanikiwa. Labda kama huyo mumeo hachukui pesa yoyote kwenye hiyo production yako. Your husband / wife is your business partner and advicer but not someone to manage you everyday, no no! You can only meet at the board meetings or kwenye weekly business meeting. Lakini kila mtu awe na ofisi yake na wafanyakazi wake nafikiri kwa njia hii itapunguza tension fulani zisizo na ulazima!

Halafu pia kitu ambacho nimeona wanandoa wengi ambao wako kwenye the same industry ndoa zao hazidumu au zinakuwa na matatizo sana. Kwamfano, hapa Tamar ni muimbaji na reality TV star wakati mume wake ni producer mkubwa kwenye music na TV show hivyo wote wapo kwenye spotlight na mzunguko wa watu hao hao kila wakati! Lazima wanandoa wawe makini sana mnapokuwa kwenye maswala ya business ili ndoa yenu iwe na amani.  Sasa Tamar na Vince walipo owana hawakupeana "prenuptial agreements" kwani walikubaliana kuwa divorce is NOT an option! Sasa pale divorce inapokuwa ni the only option sijui itakuwaje kwani Tamar anataka full custody ya mtoto wao na pia anasema Vince asipewe spouse support. Kumbuka wakati Tamar anaolewa na Vince, Vince ndio alikuwa anatengeneza pesa nyingi lakini baadaye Tamar akawa super star na kutengeneza pesa nyingi zaidi ya Vince hivyo sasa itabidi Tamar amlipe Vince pesa za kujikimu baada ya divorce..... Vince ni yatima na kwao alizaliwa mwenyewe hivyo hana ndugu wa tumbo moja wala wazazi! So sad!

Couple nyingine ambayo imeshangaza watu ni ya huyu mwanadada wa The Real talk show ?? Jeanie Mai na mumewe Fredy! Hapa mwanamke ndiye aliyesema kuwa yeye hataki kuwa na watoto kwani haoni kama atakuwa mama mzuri kwani kulea kiumbe kingine na kumfanya awe ni kiumbe bora is a tough job ambayo yeye hawezi. Pia kwasasa yupo busy na "carrier" yake wakati mumewe anataka wazae watoto kitu ambacho hawezi fanya. Kutokana na history yake ya kutoka kwenye familia duni wazazi wake waliangaika sana wakaja Marekani kutafuta maisha bora haswa kwa watoto wao. Hivyo kuwa na watoto kuta slow down dream zake ambazo yeye na wazazi wake wameteseka sana kuzipata. Nabado kuna watu masikini kwenye familia yake ambao anaona kuwa anawajibu wa kuwasaidia hivyo kuleta watoto duniani itakuwa ni mzigo mwingine wa watu wanao mtegemea! Hayo ni maisha ya Marekani kule kwetu Africa masikini ndio wanazaa zaidi ya matajiri wanajua mjomba/ baba mdogo au shangazi atawalea tu bila shida ??

Hivi, mimi nashindwa kuelewa hivi dunia hii kunawatu wanaowana bila kujadili kama wanataka watoto au hapana!! Hivi si vitu vinajadiliwa kabla hata ya kuchumbiana au mie ndio sijui ?? nielewesheni ?? mie I would love to know what am I signing up for, sorry naogopa sana kujifunga kitanzi mwenyewe! Naogopa surprises .........Kumbuka Tamar Braxton alikuwa kwenye show hii kabla ya ufukuzwa mwaka jana!

 

Mpende akupendae…….!

Mpende akupendae asiyekupenda achana naye! Acheni wenye ndoa zao halali wajishaue babu! Kwa raha zao ??

“Nitakulinda nitakupenda na kukuombea pia hiyo ndio kazi yangu.” ~~~Mrs Paul Makonda

“Nitakulinda nitakupenda na kukuombea pia hiyo ndio kazi yangu.Mengine tumwachie yeye aliye juu ayatimize kwa wakati usiogope Mimi ndio askari wa Mungu niko kazini ?❤️❤️❤️❤️❤️?  ” ~~~~~~ Mrs Paul Makonda

Jamani!! Huyu wifi yangu siyo wa dunia hii kwakweli!! Hivi anawezaje kusimama strong na kutembea bila woga wakati shetani na majeshi yake yanamuandama kila kona!!! Kweli Mungu ni muweza wa yote!! Such a phenomenal woman! Great role model to many of us!! May Almighty God richly keep blessing you. ?❤

Mh. Paul Makonda: Endelea kuniombea na kunielekeza pale ninapokosea kwani mimi ndiye mwanao wa kwanza hapa duniani.

Namtukuza Mungu kwakunipa Maria, umefanyika baraka na furaha ktk kila nyakati nilizopitia,hadi kufikisha leo miaka 6 ya Ndoa.hujawahi hata siku moja kukata tamaa pale ambapo Dunia ilikata tamaa, hujawahi kusahau upendo wangu hata pale ulipokuwa mbali na familia yako. Umekuwa mnyenyekevu, mpole na mpenda Amani. Mwisho wa yote umenivumilia Kwa nyakati zote huku ukiniombea Kwa machozi na kufunga ili Mungu aendelee kuonekana katika majukumu yangu. Hakika sinachakukulipa zaidi ya kusema asante Kwa Mungu kwakunipa wewe katika maisha yangu. Bado ahadi yangu niliyoitoa tareh 23/10/2011 bado iko palepale. Endelea kuniombea na kunielekeza pale ninapokosea kwani mimi ndiye mwanao wa kwanza hapa duniani.

***Soma ujumbe wa Mr Paul Makonda kwenye 5th anniversary yao hapa ?? (MrAndMrsMakonda)***

Winny Edwin Kihore: Living in love

                                      LIVING IN LOVE
 I once heard about a husband and wife who were so upset after a big argument that they refused to speak to each other. That night, not wanting to be first to break the awkward silence, the man left a note on his wife's side of the bed that read, "wake me up at 6 o'clock in the morning ". The next morning, by the time the husband woke up, it was already 8 o'clock. Furious, he roared, "where is she?" and was about to chew out his wife when he found a note on his side of the bed : "lt's six o'clock; wake up." If we're going to live in love, we have to learn to forgive one another. The Bible says, "Do not let the sun go down on your anger, but instead, forgive. And above all things, put on love. " EPHESIANS 3:17- That we would be "rooted and established in love so that we would have power together with all the saints " when we choose to walk in love, we have the power of God in our lives, as well as healthier relationships. We should always look for the best in each other. That's one of the things l love my husband Edwin Kihore. I used to think that he didn't see the things that l did wrong. Then l realized: it's not that he doesn't see them ; he choose not to focus on them. Let 's learn to walk in love and see the best in everyone. A house divided will fall. That's why it's so important to keep peace in your home. Be the first to apologize. Be quick to forgive. You need to remind yourself that God has put that person in your life, and He's got good things in store. If you will do your part by being kind, respecting one another, treating each other the way you want to be treated, God will do his part, and you can live in love!

Jacqueline Mengi: Apendwae akajua haachi kujishauwa!

If the only prayer you said in your whole life was “thank you” that would suffice. Meister Eckhart

Nimekwenda kwenye Instagram page ya Jacqueline Mengi nikakuta ame post msemo huu “Apendwae akajua haachi kujishaua”!………… Kwakweli hata mimi nakubaliana na huo msemo! Raha sana kupendwa na mtu anayekupenda kwa right reasons and in a right way!! Kuna watu wanaweza kukupenda in a wrong way kama Bobby  Brown na Whitney Houston! Bobby Brown alikiri kuwa alimpenda Whitney Houston but he didn’t love her in a right way!! Sikiliza sehemu ya hiyo interview hapa ??

Hapo ni vile mtu anakupenda lakini anashindwa kukukataza au kukuzuia kwenda kwenye njia mbaya badala yake na yeye ana support njia zako mbovu in the name of “LOVE” halafau wote mnaangamia. Sasa kwa hawa aliye salimika ni Bobby peke yake Whitney na binti ya ke BobbiChristina wakafariki kwa drugs….. Mtu anyekupenda katika njia sahihi na kwa sababu zilizo sahii siku zote ata wish to see the best of you! Mtu huyo atapigana mchana na usiku kuwakikisha hauingii gizani na kupotea. ………Hivyo ukimpata mtu wa namna hiyo huna budi kushukuru Mungu na kama binadamu basi kujishaua lazima!…….. Wewe jishaue tu Mrs Billionaire, acha wenye wivu wajinyonge tu ??? kama hawana kamba tutawanunulia waseme tu ???