Category Archives: Leadership

Temeke SDA Nursery and Primary School watoa shukrani kwa mama Igogo!

Mama Igogo akitazama kwa furaha picha iliyochorwa kwa taswira yake.

Wanao onekana kwenye video hapo juu ni baadhi ya wafanyakazi wa Temeke SDA Nursery and Primary School walifika nyumbani kwa mama Igogo mchana wa jana tarehe 09/27/2021, masaa ya Africa Mashariki, kwaajili ya kutoa shukrani zao za dhati kwa mchango wake wa hali na mali ambao aliutoa toka kuwaza yakwamba kanisa la Temeke SDA linahitaji kuwa na shule, kuisimamia kuanzishwa kwakwe toka elimu ya awali ya chekechea (Nursery school) mpaka kufikia kuwa na darasa la kwanza mpaka la saba.

Kuhakikisha kuna kuwa na boarding (hostel) kwa wanafunzi wanao kaa mbali haswa wanafunzi wa jinsia ya kike! Mama Igogo alikuwa full time Mkurugenzi mkuu (Director) ambaye hakuwai kulipwa mshahara hata mara moja kwa miaka 7! Alifanya kazi ya kujitolea kwa asilimia 100%! Na baada ya miaka 7 aliomba “kung’atuka” na kuwaachia vijana waikimbize. Yeye alibakia kuwa mshauri kwenye bodi ya shule. Mungu ni mwema shule ilisimama na inaendelea vizuri! Mwanangu ni mmoja wa wanafunzi wa mwanzo kabisa wa shule hii! Alianzia  Nursery hadi darasa la sita. Mungu azidi wabariki wote walimu, wanafunzi, pamoja na watu wote wanaojitoa kwaajili ya huduma hii muhimu sana kwa jamii. ????

Kwenye video ya pili ni Mama Igogo akitoa shukrani zake za dhati baada ya kupokea shukrani na zawadi ya picha kutoka kwa wafanyakazi wa Temeke SDA Nursery and Primary School. 

Na hapa, mama Igogo akitoa ufafanuzi wa zawadi ya picha iliyochorwa kutoka kwenye moja ya picha zake ambazo alipiga akiwa kwenye Makao Makuu ya Wasabato ulimwenguni yaliopo Silver Springs, Maryland/ Washington DC eneo la kumbukumbu za Ellen G. White (mmoja wa waasisi wa dhehebu la Wasabato). Mama yangu hajatembea dunia nzima, Mungu ni mwema amembariki kutembelea nchi kadhaa hapa dunia na ameona mengi; lakini safari ya kutembelea kijiji cha history ya Wasabato huko Battle Creek, Michigan na safari ya kutembelea Makao makuu ya Wasabato ulimwenguni kwakweli ni moja ya safari ambazo zimemgusa sana moyo wake na siku zote huwa anaziongelea kwa hisia sana! Namshukuru Mungu kuwa amenichagua mimi binti yake kuwa kiungo kikuu cha mbaraka huo. Si kwamba asingeweza kufika Marekani hapana! Naamini Mungu kama alimpangia kufika angefika tu bila ya mimi kuwepo kama hizo nchi zingine alizo tembelea bila mimi kuwepo! Lakini kufika sehemu kama hizo kwa urahisi na kwa furaha kupitia mwanae naamini nikitu kinampa faraja kubwa sana moyoni! ?? No mama ain’t done yet! Mungu atupe uhai utakula more good time very soon! ?????

Mzee O.O Igogo, Magreth Otieno Igogo, na mama Igogo

Hapa juu ni moja ya picha waliyopiga wakati walikuwa wamekwenda kutembelea kijiji cha historia ya Wasabato huko Battle Creek, Michigan mwaka 2014 mwezi wa 11. Picha A siku hii zipo nyingi lakini zipo kwenye Flashdisk, sijapata muda wa kuziangalia.

Kama ulipitwa na picha za mama Igogo kutembelea Washington DC basi bonyeza ???? Safari ya mama Washington DC , na Safari ya mama Washington DC

Twamshukuru Mungu kwa yote kwani ni kwa neema yake tu ndio maana haya yote yanatokea. Sifa na utukufu ni zake yeye tu milele na milele. ????

R.I.P Kofi Annan

Another Africa greatest is gone! R.I.P Kofi Annan Africa will always remember you, your legacy shall forever live!……. Hivi mnajua hakuna kituo chochote cha TV hapa Marekani ambacho kimeongelea kifo cha kiongozi huyu mashuhuri aliyewahi kupewa  tuzo za Nobel Peace Prize? Halafu utakuta baadhi ya Waafrika haswa Watanzania wanavyo washobokea Wamarekani wakati wenyewe kama hawafaidiki na kitu hata siku moja hawakiongelei!!

Ingekuwa ni vita au vurugu mahala fulani huko African ungeona ambavyo kila kituo kinaonyesha kwasababu tu wanataka kuonekana wao ni bora kuliko wengine!! Napoa hapo wanajua ni sehemu ya kuuza silaha zao kama bunduki  hivyo ni lazima wamfanyie promo ya nguvu ili wauza silaha wapeleka huko!! Siku tutaacha kushabikia hawa wazungu na kujenga vyaketu ndipo tutaheshimika mbele zao!!

Anyway, may Kofi Annan soul’s R.I.P ??

Hongera sana Mh. Jokate Mwegelo

#RepostSave @jokatemwegelo with @repostsaveapp  Amini Mungu ni mwingi wa rehema kamwe hamtupi amtumainiye yeye!! Ahsante Mungu Wangu.

Labda ni-share kitu kidogo, kuna muda mwaka jana mwishoni nilikuwa so down nilitamani kukata tamaa na kila kitu kwenye maisha nilikuwa pia sijaelewa vizuri hatma yangu kwenye siasa. Nilikuwa kwenye mkutano mkuu wa chama kuna mdada mmoja kutoka Arusha akanikimbilia na kunikumbatia kwa nguvu sana alikuwa na mama mmoja hivi walikuwa wamekuja kupiga picha namimi. Huyo dada mdogo hivi akasema ananipenda sana sana na mimi ndio nilimfanya aingie kwenye siasa na akagombea nafasi kupitia mkoa wa Arusha akashinda!! Nikabaki natabasamu. Ikanipa nguvu kubwa ya kupiga moyo konde na kusonga mbele. Nilifurahi kuona kuna mdada nimeweza kumhamasisha na kumpa ujasiri wa kugombea. Unaweza ukawa unapitia mitihani migumu sana kwenye maisha yako lakini inakubidi usikate tamaa saa zingine kwasababu tu ya wale wanaokutegemea, wanaokuangalia na kuvutiwa nawe na kujifunza kupitia maisha yako. Lakini zaidi kwasababu safari ya mafanikio ina milima na mabonde, inabidi upambane na kiukweli hakuna mafanikio yasiokuwa na changamoto. Na kuna muda changamoto ndio haswa zinatengeneza “character” zetu. .

Kikubwa zaidi wakati wa changamoto tukumbuke kuwa wanyenyekevu, wenye kujishusha na kumuomba Mungu aendelee kutupa imani, hekima na busara ya kusubiri wakati wake. Tukumbuke Mungu hamtupi mja wake. Nawatakia Jumapili Njema. Nawapenda Sana. Ahsanteni ??”

Ninafuraha sanaaaa! Hongera sana mdogo wangu Muheshimiwa Jokate Mwigelo kwakuteuliwa kua  Mkuu wa Mkoa wa Kisarawe. Mwenyezi Mungu akuzidishie mibaraka yake, ukaongoze kwa hekima, na busara kwa faida ya wana Kisarawe na taifa la Tanzania kwa ujumla, zaidi ya yote utukufu wa Mungu ukapate onekana mbele za watu. Hongera sana tena sana! #WanawakeTunaweza

Hongera sana Mh. Jerry Muro

"Namshukuru Mungu kwa Kunipa Kibali cha Kumsaidia kazi Mhe, Rais, Dkt. John Pombe Magufuli katika Nafasi Ya Ukuu wa Wilaya ya Arumeru, Nakushuru Mhe, Rais, Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na Viongozi wote Waandamizi wa Serikali kwa kunipa Jukumu Hili la kuwatumikia wananchi wa Meru.#WakatiWetu #MeruYetu #TanzaniaYetu"
Naomba kutoa pongezi zangu za dhati kabisa kwa Mkuu wa wilaya mpya wa Arumeru Mh. Jerry Muro. Nakuombea uongozi bora wenye haki na tija  kwa maendeleo ya wilaya ya Arumeru na taifa kwa ujumla!. Hongera sana!

Wema Sepetu: Alafu sasa bado kuna wabishi watabisha

Regrann from @wemasepetu – Ninapokuita Mtetezi wa wanyonge Ninakuaga na Uhakika wa asilimia zoooooote… Alafu sasa bado kuna wabishi watabisha… Jamani eeh nasema hivi, “Kuna kufanya na Kuna kuthubutu…” Nini huwa kinaanza kati ya hayo mawili…??? Tunaanzaga kwa Kuthubutu alafu ndo tunafanya…… Kaka angu hapo juu, (sina haja ya kumtambulisha) alipothubutu kuliingilia swala zima la janga la kuuziwa makazi na malazi ya watu mbali mbali tena na mahakama wengi wenu mlimbeza na kurusha maneno ya kila aina… Oooh anakurupuka, oooh hana mamlaka, oooh HATOWEZA… Oooh Tutaona… Nadhani leo hii mmeinamisha vichwa chini kwa aibu… Na mimi nasema Aluta Continua… The Saga Continues.  Mwenyewe anasemaga kitu kimoja… Ametumwa kutetea wanyonge… Sio Mungu yeye wala Malaika kusema kwamba atafanya kila kitu Perfectly… Ila kwenye ukweli pasemwe ukweli… We are Blessed to have you as Our RC… Iko siku wataelewa tu… Na watakuwa wameshaelewa sema si unajua UBISHI ndo jadi yetu… Sana sana sisi Wana Mkoa wako… Umesaidia wengi sana na unazidi kuendelea kufanya hivyo kila iitwayo leo… Mungu anazidi kukupigania Mtumishi wake… Akupe Uhai mrefu… Uzidi kuona Juhudi na Uthubutu wako ukizaa matunda.Wana Dar tunakupenda sana… Mungu Ibariki Tanzania..

Mungu Ibariki Africa..

Mungu Mbariki RC Wangu..

Mungu Mbariki Rais Wangu…

Viva RC Viva…

@paulmakonda @paulmakonda @paulmakonda @paulmakonda

#IkikuchomaImeruhusiwa…??? – #regrann

HABARI NZURI KWA WATANZANIA WOTE

HABARI NZURI KWA WATANZANIA WOTE
•Ndege yetu aina ya Boeing 787-8 imemaliza hatua zote muhimu za uunganishwaji wa vifaa vya ndani kwa mafanikio makubwa.

•Zoezi hilo lililoanza 4/5/2018 na kumalizika 21/05/2018 linatoa picha ya ndege hii kuweza kuwa delivered kabla hata ya tarehe tajwa (9/7/2018).

•Hatua inayofuata ambayo kimsingi ndiyo ya mwisho ni Pre Flight preparation, testing and certification. Pre flight prep zitaanza leo mpaka pale watakapojiridhisha na kuset tarehe ya delivery.

•Ndege hii itakuwa na seat 22 za Business Class na seat 240 za Economy Class.

Heko kwa serikali ya JPM.

***Nimetoa kwenye Facebook ya UVCCM***

Mama Samia Suluhu ziarani Luanda nchini Angola

Regrann from @hoycetemu – Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. @samia_suluhu_hassan leo amehudhuria Mkutano wa Kawaida wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika unaojulikana kama (Extra Ordinary SADC Double Troika) unaowahusisha Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika unaofanyika kwenye mjini Luanda nchini Angola.

Makamu wa Rais anamuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika mkutano huo .

Nchi zilizoshiriki mkutano huo ni Angola, Tanzania, South Africa, Zambia, Namibia Lesotho na Congo DRC. – #regrann

Jokate Mwegelo: Ufike muda harakati za ukombozi wa mataifa ya Afrika zifundishe kwa nguvu zote mambo makubwa yaliyofanywa na akina mama wa mfano kama akina Bibi Titi wa Tanzania na Winnie Mandela wa Afrika Kusini

Regrann from @jokatemwegelo  -  What a love story! What a life! What a wife and mother! What a Human Being but most importantly what a WOMAN!!! A Force!! Unapologetic!! Political Activist to match non other. You went from being someone’s wife at a very tender age to being your own PERSON!! Having your own VOICE and CONVICTION which you pursued to your final breath. No matter how hard they try to taint your legacy by singling out some events notwithstanding what they did had so much more harm and adversity to your people, they made you when they cornered you, took you to solitary confinement which gave you strength instead of breaking you they actually made YOU- they saw your God see you through it all and you persisted like gold you came out stronger.  Even when your own people turned against you, you did not waiver. They know how much your strength and tenacity at times even more than men to fight for the total liberation and emancipation of your people will forever live on and inspire generations to come. 

In the struggle for the liberation of our African states WOMEN did play a vital role. It is sad that the role of women is eschewed and women who were fearless and did about anything for their people are labeled as angry or simply controversial. LoL. How funny and silly!!! The women are the ones who kept the struggle alive in this context, mobilized people for the cause while their husbands were jailed or exiled or even when some men went into hiding because they were scared!!!  Ufike muda harakati za ukombozi wa mataifa ya Afrika zifundishe kwa nguvu zote mambo makubwa yaliyofanywa na akina mama wa mfano kama akina Bibi Titi wa Tanzania na Winnie Mandela wa Afrika Kusini. Lazima watoto wakue wakijua kuna akina mama shupavu waliopitia mengi hata kuteswa na kunyanyaswa kwa ajili ya uhuru wa watu wao na hawakukata tamaa mpaka kilivyoeleweka. Yaani wanawake walionyesha tuna nguvu ya ajabu tukiamua jambo letu katika kupigania haki na maendeleo ya watu wetu kutoka kwenye utawala mbovu wa kibaguzi na kinyonyaji! Lala Ngoxolo Nomzamo Winnie  Madikizela Mandela. ❤️ #RIPWinnieMandela  - #regrann

President Lambert Tibaigana: Hatuta saidia mtu ambaye hasaidi wengine

Rais wa jumuiya ya Watanzania waishio katika jimbo la Houston, Texas Hon. Lambert Tibaigana akielezea kwa kina baadhi ya maazimio ambayo yalijadiliwa na kupitishwa na wana jumuiya hiyo na pia akigusia mambo machache ya msingi ambayo katiba ya jumuiya hiyo imezingatia.

Kama wewe ni Mtanzania unayeishi katika mji wa Houston na vitongoji vyake basi tunakuomba ujiunge na wanajumuiya wengine katika kuiendeleza jumuiya yetu. Tafadhali jiunge na jumuiya yetu, saidia viongozi wetu kwa kumtaharifu kila Mtanzania unaye mjua kuwa anaombwa ajiunge na jumuiya hii kwani inafaida sana kwa vizazi vyetu vilivyopo sasa na vijavyo! Mungu ibariki Tanzania. Mungu ibariki THC.

Rais Magufuli: Nimeviagiza vyombo vya dola kufanya uchunguzi na kuwachukulia hatua za kisheria

In God we trust!  R.I.P Aquilina  ??

Jokate Mwegelo: Hukustahili kufa kwa namna ulivyouawa

Regrann from @jokatemwegelo - Such a beautiful innocent young woman. ??❤ Aquilina Akwilini Baftaha, umefariki ukiwa kijana mdogo sana, kwa wakati ambao ndiyo haswa unatakiwa katika Jamii. Kifo chako kimetushtua na kimetugusa. Inawezekana tumeguswa kwa sababu mbali mbali na tofauti, ila tu uhakika ni kuwa imetuuma. Wengi tulikuwa hatukufahamu, lakini leo hii unawakilisha kundi kubwa la vijana wadogo kama wewe walio chuoni, na katika mioyo yetu tunajua inavyouma kumpoteza mtu wa hivyo. Haswa kwa namna ambayo umepoteza maisha kama mshumaa uliozimwa ghafla. Hukustahili kufa kwa namna ulivyouawa. Mwenyezi Mungu awape nguvu, imani na amani ndugu na jamaa wako wa karibu na kila aliyeguswa kwa kifo hiki cha kusikitisha. 
R.I.P Aqualina ❤ - #regrann

Jokate Mwegelo: Muhimu kujipanga kutumia fursa hizi zinazotengenezwa na serikali zetu hizi

Jokate Mwegelo

Tarehe 14/01/2018. Rais Magufuli wa Tanzania alimkaribisha Rais @paulkagame wa Rwanda, Dar es Salaam- Tanzania katika ziara ya kikazi.  Katika ziara hii walirejea mazungumzo juu ya ujenzi wa reli kati ya Isaka na Kigali lakini pia reli hii itaenda mpaka Musongati- Burundi kupitia Keza. Reli iliyopo hivi sasa ni kati ya Isaka ambako kuna bandari kavu na Dar yenye urefu wa kilometa 970- reli ya kati. Na hii reli mpya kati ya Isaka na Kigali itakuwa ya urefu wa kilometa 494. Ujenzi huu utasaidia usafirishaji wa bidhaa na watu kwa urahisi na kupunguza gharama za usafirishaji lakini pia itasaidia kuboresha maendeleo ya kiuchumi. Nchi za Rwanda na Burundi na mpaka DRC ambazo ni “landlocked” watazidi kuona unafuu katika kutumia bandari yetu kutokana na usafiri kuwa wa kuaminika. Mradi huu unabeba pia dhima za EAC, CEPGL na COMESA zenye kuhamasisha “inter-state transportation structures”. Hizi ni hesabu nyepesi. Kwa miaka mingi maendeleo ya biashara ya bidhaa, huduma na usafirishaji wa mazao ya kilomo, madini mbalimbali n.k kati ya nchi za Afrika zimekuwa zikikabiliwa na changamoto ya gharama kubwa za uzalishaji ambapo pamoja na sababu nyingi zingine zimechangiwa sana na ukosefu wa usafirishaji wenye kueleweka. Ujenzi huu utasaidia kufungua maeneo haya na kugusa makundi mengi hasa vijana kiuchumi. Muhimu kujipanga kutumia fursa hizi zinazotengenezwa na serikali zetu hizi. Tufuate kule serikali inapowekeza na kuona jinsi gani tutaweza faidika. Pia tupende kujifunza juu ya mipango ya serikali na tuone tunanufaika vipi na tuhoji. Niwatakie siku njema. ❤️ 

Edward Julius: BABA WA FAMILIA NI LAZIMA ADUMISHE UHUSIANO MWEMA NA JIRANI ZAKE

Edward Julius

BABA WA FAMILIA NI LAZIMA ADUMISHE UHUSIANO MWEMA NA JIRANI ZAKE:

Kiongozi makini ni yule ambaye anatambua ya kuwa maendeleo ya kiuchumi ya nchi yake hayaji kwa nchi kujitenga na kujifanyia mambo yake peke yake, bali huletwa kwa juhudi za wananchi wake pamoja na kushirikiana vema na nchi majirani zake pamoja na jumuiya nzima ya kimataifa kwa mapana.  #VIVA_JPM

Mh.Edward Lowassa: Amenifanyia siku yangu kuwa njema sana. He has made my day

Siasa ni sera na itikadi siyo chuki wala uwadui! Wenyewe wenye lugha zao wanasema 'Politics is just a game'!  Na hapo ndio mimi nasema tusilazimishane kuupenda au kucheza mchezo huu!! Acha wale wanaopenda siasa wahubiri siasa, wale wanaopenda mambo ya kumtukuza Mungu wahubiri injili ya Mungu, wambea na wadaku wote washinde Facebook na Instagram kufuatilia maisha ya watu!! Kila mtu afanye kile kitu roho napenda!! Kwani siyo wote tunaoweza cheza mchezo huu wa siasa, wengine hatujui ku-control hisia zetu kuweka siasa kwenye maswala ya msingi!! Nasisitiza mimi sio mwanasiasa! Tusipangiane maisha!!

"He has made my day" hayo ni baadhi ya maneno ya Mh. Edward Lowassa baada ya kuonana na Rais Dr. John Pombe Magufuli siku ya jana. Naona wanachama wengi wa  Chadema wana lalamika kuwa wamesalitiwa??! Nikabaki kujiuliza, wamesalitiwa?? ?? na nani tena?! Kama ni usaliti basi ulifanyika 2015 pale kiongozi wenu alipo mchukua mtu ambaye hakuwa mwanachama wenu na kumpa nafasi ya kugombea urais bila hata aibu!! Ule ndio ulikuwa usaliti!!  Eti kwanini Mh. Lowassa hakushirikisha viongozi wa chama kabla ya kwenda kumuona Rais?!! ?? What a madness!! Are these people really know what they are saying! Hivi ukiwa mwanachama wa Chadema maisha yako yote ni mali ya chama??!! ?? ....Anyway Mh. Mbowe kawaelimisheni vizuri sana katika hili.  Msikilize hapo ?? Mh. Lowassa ni raia wa Tanzania kama walivyo raia wengine, kuonana na Rais ni haki yake kimsingi!! Haitaji kibali cha mtu yoyote yule kuendesha maisha yake nje ya chama.

Kuna maisha nje ya siasa na hayo ni maisha yako wewe mwenyewe  hayamilikiwi na mtu yoyote! Una uhuru wa kujumuika, kufanya biashara, kula, kuoa, kusali na mtu mwingine yoyote yule ambaye siyo adui (mf. Mtu ambaye gaidi) wa inchi yako! Siyo ndugu zako wote ni wanasiasa au wafuasi wa chama chako sasa utavunja undugu kwasababu ya Siasa?!! Kuna watu naona wanaingiza siasa mpaka kwenye maswala ya ndoa? Jamani hivi hii ni Siasa au ushetani!! Ndoa ni agano takatifu, leo hii mnataka watu waliokula kiapo mbele za Mungu waachane kwasababu ya Siasa?!! Huyu shetani anaye waingia Watanzania niwakukemewa kwa nguvu zote!! Embu turudi nyuma kidogo, sinimekwambia kuwa wenyewe wanasemaga Siasa ni mchezo tu! Sasa hapo mastering wa hii game kwa upande wa Chadema ni Mh. Edward Lowassa na Mh. Freeman Mbowe! Kumbuka Mh. Lowassa alijiunga na Chadema kwa mkataba wa kupewa nafasi ya kugombea urais na hiyo ndio imekuwa nia na lengo lake mpaka wiki kama tatu zilizopita, msikilize ?? akiwa bado anaomba Mungu amsaidie kushinda Urais 2020

Umemsikia eeh! Wakati huo huo Mh. Mbowe ameshaona kuwa Mh. Lowassa is not a great candidate kwa 2020 hivyo target yake ni Mh. Tundu  Lissu.  Lakini kwakuwa bado anamuhitaji Mh. Lowassa kwaajili ya nguvu ya umma na kifedha inabidi aendelee kumlaghai akae ndani ya chama mpaka 2020 halafu wamfanyie ule mchezo aliomfanyia Dr. Slaa  ?? but Mh. Lowassa is too smart for that ndio maana anaanza kuwafanyia maigizo kwani ameshaona dalili za yeye kufanyiwa mchezo aliomfanyia Dr Slaa! ??? Hivi huwa wanasema eti "Karma is a........" and what goes around always huwa linarudi kinyume nyume eeh ?? I love it when politicians played themselves! Mh. Edward Lowassa amekwishaona hana tena maslahi yakudumu na Chadema sasa sibora arekebishe huku kwingine before it's too late! Nammemsikia akisema anaona miaka mingine 5-10 ya uongozi bora wa Dr Magufuli ??? should I say CCM oyee ee on behalf of CCM members or will I be morally wrong since I am a blogger I should stay neutral and keep my mouth shut ?? #IHatePolitics #HeHasMadeMyDay  Btw, swala la Mh. Lowassa kuwa ni mtu muungwana na mstarabu hata mimi niliwahi sema huko nyuma, soma ?? Mr&MrsMkapaGoldenAnniversary
NilisemagaHukoNyuma

2020, je! Oprah Winfrey atajitosa kugombea urais wa Marekani?!

Hatuba fupi aliyoitoa Oprah Winfrey wakati akipokea tuzo za Cecil B. de Mille Awards kwenye Golden Globes hapo juzi kati imefanya watu wengi wajiulize kama mwanadada huyo ambaye ni billionaire mwenye mvuto mkubwa wa kushawishi watu atakuja kugombea kiti cha urais ifikapo 2020! Oprah Winfrey aliongea kwa hisia kali kuelezea jinsi wanawake wanavyokuwa wakinyanyasika, kudhalilishwa katika nyanja zote za maisha, malalamiko yao yamekuwa yakipuuzwa siku zote nasasa wakati wa hawa wanaume wanyanyasaji  umefika mwisho, "their time is up" Oprah alisema kwa ushujaa huku watu wakimshangilia. Embu msikilize kwanza ?

Kwakweli mimi nilikuaga siyo mapenzi au shabiki sana wa kuona Rais mwanamke, lakini jinsi nilivyokaa nikachukua muda wangu kuwatizama hawa wanasiasa wa kiume, honestly I now strongly supporting for a Female President! Their time is up for real! Labda tukiwa na viongozi wakuu wakike wengi kwenye dunia hii hali itabadilika kidogo, we may make this world a better place to live again! Hawa wanaume hakuna wanafanya zaidi ya ku-feed their stupid ego and using women as tools!!

Oprah Winfrey na mpenzi wake Stedman Graham

Kama Oprah aliweza kumfanikisha Rais Baraka Obama kuwa Rais wa kwanza mwenye ngozi nyeusi hapa Marekani, trust me with what is going on right now in America? Oprah Winfrey will definitely be the First Female President in America and she is BLACK!! .......Katika tuzo hiyo Oprah Winfrey ndio mwanamke wa kwanza muafrica aliyewahi pata tuzo hiyo. Sydney Portie're ndio alikuwa muafrica wa kwanza kupata, hivyo mpaka sasa ni hao wawili tu kwa upande wa watu weusi ambao wamefanikiwa kupata tuzo hiyo!

RC Paul Makonda: haikuwa rahisi kama siyo Mungu kuwatumia wateule wake sijuwi leo nigekuwa wapi

@Regranned from @paulmakonda - Mwaka 2017 ni mwaka watofauti sana kwangu. Leo tunapojiandaa kupokea Mwaka 2018. Ni vyema nikayatazama maisha yangu ndani ya mwaka 2017 hakika huu ulikuwa mwaka wa aina yake. Ni mwaka ulionipa marafiki wa kweli, lakini kubwa kuliko ni Upendo na Maombi niliyoyapata kutoka Kwa Kipenzi changu Maria. Nikuambie kitu ndg msomaji...... haikuwa rahisi kama siyo Mungu kuwatumia wateule wake sijuwi leo nigekuwa wapi. Nimepewa kila jina baya, kila jambo baya nimefanya mimi ,matusi yote yalikuwa yangu na hata watu kutamani nisiwepo duniani. Lakini kwako Mpenzi ilikuwa tofauti, ulinitia moyo Kwa sauti ya upole,uliniombea na kunifuta machozi bila kuchoka. Tena Kwa kusema Nanukuu, Paul Mungu hajawahi kukuacha hata kama Dunia yote inakuona haufai nataka nikuambie Mungu amekupaka mafuta Kwa kazi hii simama na usonge mbele. Mwisho wa kunukuu”.Ndg zangu na wananchi wenzangu ni vyema mkajua kila mtu anayo hadithi ya kumweleza mwenzake ila kwangu inahitaji kitabu kuyaeleza mapito na njia nyembamba niliyoipita mwaka 2017. Itoshe kusema Mungu wa haki iko siku atasimama na kutoa hukumu ya kweli Kwa watu wote. Kwani yeye anatujua kila Mtu na matendo yetu tena kwake hakuna Siri ya maisha yetu.Nakupenda sana Maria wangu na ninathamini sana Mchango wako ktk utumishi wangu hapa Duniani. Uzidi kuwa Imara simba wangu ili niyafanye yote mema ambayo Mungu amepanga Kwa watu wake. Asante sana Mungu Kwa kunivusha mwaka 2017.

RC Paul Makonda ndani ya jiji la Suquian, China!

@Regranned from @paulmakonda – Nikiwa na Meya wa jiji la Suquian Bw. Wang Tianqi,jiji la jimbo la Jiangsu. Hili ni jiji jipya kati ya miji mingi iliyopo nchini China(limeanzishwa mwaka 1996). Jiji hili lina ukubwa wa km za mraba 8555 km na Wananchi milioni 4.7. Nikiwa jijini Suquian nimepata bahati ya kutembelea maeneo ya kiuchumi mbalimbali likiwemo eneo la *Suquian National Economic and Technological Development Area* (eneo la viwanda) lenye viwanda vya kati na juu kama viwanda vya chakula, mbao,mvinyo (Yanghe Breweries Industry),viwanda vya nguo n.k. Uchumi huo wa viwanda umesaidia Pato la mwananchi kufikia hadi Yuen 40930 kwa mwaka, sawa na $ 6292 ambayo ni sawa na tshs 14,124,910 2018niMwakaWauwekEzAjI

Wema Sepetu: Katika vitu ambavyo Dar pia inatakiwa kujivunia ni kupata RC mwenye akili nyingi

 @Regranned from @wemasepetu - Tanzania Kwanza....... Katika vitu ambavyo Dar pia inatakiwa kujivunia ni kupata RC mwenye akili nyingi.........Mungu akakutangulie katika kazi zako za lengo la kuijenga Tanzania yako izidi kuwa zaidi ya ilipo sasa........... Ipo siku wataelewa tu......... The Man Himself....... Call Him Mr Dar-es-salaam...... Viva RC wangu....... Viva Rais wangu...... #UzalendoKwanza ... cc @paulmakonda May everything you wish well for your Nation Be.... We support you fully... ?????? - #regrann

 

Uzalendo huanzia nyumbani kwako!

"Picha hii ilipigwa siku ambayo nilitangaza kuwa sitagombea tena Ubunge, baada ya kuwatumikia kwa miaka 10. Sita sahau hisia zetu siku hiyo, jinsi mioyo yetu ilivyo vunjika kwa kujua kuwa mazoea yetu yatabadilika. Nina uhakika upendo wetu umebaki daima. Ndugu zangu Singida mjini ninawakumbuka sana! ❤ MO" // This picture was taken the day I announced to my constituents that I won’t be running for parliament, after serving them for 10 years. I won’t forget our emotions that day, a deep sense of heartbreak knowing that our interactions will change but the love will forever remain. My fellow Singida Urban brothers and sister, I miss you dearly! ❤️ MO"

Biblia inasema kuwa mtu asiyependa wakwao ni mbaya kuliko mtu asiye amini! Yani ni bora  mpagani anaonekana mtakatifu mbele za Mungu kuliko yule anaye sema anamuamini Mungu wakati anachukia na kutojali wakwao! Kuna watu wengi sana tena wengine wapo mbele ya macho yetu kila siku baadhi yetu wanawachukulia kama "role model" wao bila kutafakari kwa kina kuhusu hao "role model" zao! Je,  umewahi kuwachunguza kama kweli wanapenda wakwao? Au ni watu wa 'mikakati' yani they have an hidden agenda ya kutaka kupata pesa kutoka kwa wazungu na sponsors wa mambo yao! Kama ni kusaidia je  umeshaona wakisaidia wakao? Au ndio wale watu ambao ndugu zao wote ni wa "mujini wenye pesa" ukiishi uswahili kwetu kule Keko wewe siyo ndugu yao hawakujui!! Uzalendo unaanzia nyumbani kwako kwani hata hao ndugu zako ni Watanzania hivyo ukiwasaidia unasaidia taifa la Tanzania. .............Binafsi naheshimu nakupanda  watu wenye tabia ya kutoa jasho lao na kusaidia watu bila kuomba au kubugudhi wengine. Mfano ni Mh. MO Dewji, ShyRose Bhanji, Dr. Ntuyabaliwe  Foundation, Rita Paulsen, Flaviana Matata Foundation, Kidoti na wengine. Sipendi mtu anayetaka kusaidia wengine kwa kulazimisha wengine wamchangie kwani kusaidia mtu ni ibada, hivyo ni siri ya mtu na Mungu wake. Usinielewe vibaya kuna kuchangia kwingine naunga mkono kabisa kama mambo ya cancer, shule, n.k (for special cause). Ninacho ongelea hapa ni kusaidia watu binafsi......... Anyway, napenda vile Mh. MO anavyo wajali watu wa kwao huko Singida mjini. Mfano mzuri wa kuwa uzalendo, unaanzia ndani ya nyumba yako!

Ruge Mutahaba: lazima tufanye kitu kikubwa kwa ajili ya historia ya nchi hii

@Regranned from @cloudsfmtz - Hatujahitimisha bado huu ndiyo mwanzo hatuwezi kuishia hapa tukaliacha kama Tamko sisi kama CMG tutalibeba kama Azimio kufika mwisho. Tumezunguka zaidi ya miaka 5 tumesikia vilio vinavyofanana kwa Vijana kabla hatujakwenda mbele lazima tufanye kitu kikubwa kwa ajili ya historia ya nchi hii. Jana tumeanza kwa kujiuliza Kwa swali Je tunaimba wimbo mmoja kwa Sauti zenye kufanana? Inawezekana hadi tunaondoka hapa bado hatujapa Sauti moja Lakini naimani tutafikia lengo. Tunaposema anzia sokoni lazima tuangalie Uongozi wa kimasoko namna gani tunaweza kushindana pasipo kushushana kwenye mazingira ya ushindani, Ubakie kwenye maneno tu na Vitendo vionekane Sokoni.  Hebu tujaribu kutafuta taarifa na lazima wote tukubaliane kusaidia na maafisa kilimo na viongozi katika kuodoka katika Kilimo cha Kisasa. Sababu kilimo chetu kimepitwa na wakati. Kama tuna uwezo wa kupata mifumo bora zaidi katika huduma za kijamii tujipe Moyo na wala tusivutane kama kuna Fursa zipo tuzikimbilie katika kuzalisha huduma bora zaidi. Misingi yetu lazima ijikite katika namna ya kusolve tatizo bila kulalamika, Malalamishi tunayoishi nayo yageuke kuwa changamoto ambazo ni fursa kwetu tutengeneze kitu kinachoitwa Problem Solving Skills. Ndani ya Mwezi mmoja unaofuata kuanzia sasa kupitia WAMANTA waliopo hapa, Watu wa kwenye mitandao pamoja na wengine walio pamoja nasi tutatengeneza timu kwa ajili ya andiko la Azimio la Kagera. kabla ya Bunge la bajeti 2017/18. Hili #AzimioLaKagera Leo kwa pamoja tumeandika historia kubwa sana namshukuru mwenyezi Mungu kupata viongozi wa dini ambao tumeshindana nao kuanzia siku ya Jana hadi leo ni faraja kwetu. Kwasisi tuliobahatika kuishi leo lazima tubadilishe mtazamo wa kuitengeneza Kagera mpya yenye mtazamo mpya kama mipaka ya kiuchumi na siyo eneo la Ulinzi wa mipaka yetu.

 Muasisi wa Fursa
 Ruge Mutahaba.
 #AzimioLaKagera @tatumzuka - #regrann