Jokate Mwegelo: Hukustahili kufa kwa namna ulivyouawa

Regrann from @jokatemwegelo - Such a beautiful innocent young woman. ??❤ Aquilina Akwilini Baftaha, umefariki ukiwa kijana mdogo sana, kwa wakati ambao ndiyo haswa unatakiwa katika Jamii. Kifo chako kimetushtua na kimetugusa. Inawezekana tumeguswa kwa sababu mbali mbali na tofauti, ila tu uhakika ni kuwa imetuuma. Wengi tulikuwa hatukufahamu, lakini leo hii unawakilisha kundi kubwa la vijana wadogo kama wewe walio chuoni, na katika mioyo yetu tunajua inavyouma kumpoteza mtu wa hivyo. Haswa kwa namna ambayo umepoteza maisha kama mshumaa uliozimwa ghafla. Hukustahili kufa kwa namna ulivyouawa. Mwenyezi Mungu awape nguvu, imani na amani ndugu na jamaa wako wa karibu na kila aliyeguswa kwa kifo hiki cha kusikitisha. 
R.I.P Aqualina ❤ - #regrann

Leave a Reply