Mama Samia Suluhu ziarani Luanda nchini Angola

Regrann from @hoycetemu – Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. @samia_suluhu_hassan leo amehudhuria Mkutano wa Kawaida wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika unaojulikana kama (Extra Ordinary SADC Double Troika) unaowahusisha Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika unaofanyika kwenye mjini Luanda nchini Angola.

Makamu wa Rais anamuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika mkutano huo .

Nchi zilizoshiriki mkutano huo ni Angola, Tanzania, South Africa, Zambia, Namibia Lesotho na Congo DRC. – #regrann

Leave a Reply