Category Archives: Condolences

Pumzika kwa amani ya Bwana bibi Anna NYOLWENGO!

marehemu bibi Anna Nyolwengo akiwa na mwanandugu

“Ilianza kwa ajali ya kugongwa na pikipiki, ukavunjika mfupa wa nyonga, hospitalini ulikimbizwa kupata huduma, ukiwa umenyamaza kimya bila kujitambua, siku tatu baadaye uliizinduka na kuwatambua wanao, hata kwenye simu ukaongea na Otieno, kuimarika kwako iliwaruhusu madaktari kukusudia ufanyiwe upasuaji, wa kuunganisha palipovunjika, ukiwa na uhai wako wakakuchoma nusu kaputi, nayo ikazua balaa la kupoteza fahamu hadi jioni hii umetutoka Mama yetu ANNA NYOLWENGO, dada yako Rhoda alitangulia, ukabakia nasi ukooni, leo umetutoweka kwa utashi wa Mola TUNASHUKURU ????????” …… Sir O.O Igogo

Marehemu ni mdogo wake na bibi yangu mzaa baba! Pia mimi nilipewa jina la mama yao mzazi yani bibi yake baba mzaa mama! Jina langu hilo ni ARUA japo baba yangu huwa analiandika ARWA! ?? Marehemu bibi yangu mzaa baba wao asiliyao ni Kenya, ambapo ndipo na mdogo wake alipokuwa akiishi mpaka maiti ilipo mfika.

Hii wheelchair alinunuliwa wiki iliyopita wakiwa na tegemeo kuwa angetoka hospital salama baada ya kufanyiwa upasuaji. Wao walipanga kama wanadamu lakini mapenzi ya Mungu yametimuzwa! …… Poleni wanandugu na ukoo wote wa Nyolwengo. May our beloved grandmother Anna Rest In Eternal Peace! ????

“And said, “Naked came I out of my mother’s womb, and naked shall I return thither. The Lord gave, and the Lord hath taken away; blessed be the name of the Lord.” ………. Job 1:21

Sherehe ya maisha ya mwisho ya mama Yucabeth Atieno Chaulo!

Marehemu Mama Yucabeth Atieno Chaulo enzi ya uhai wake!

Siku ya Alhamisi ya tarehe 24, mwezi wa Sita, mwaka huu (06/24th/2021) familia ya marehemu mzee Androniko Chaulo walipatwa na msiba wa mama yetu Yucabeth Atieno Chaulo, kilichotokea mida saa mbili usiku huko Dar es salaam, Tanzania. Na amezikwa leo kwenye makaburi ya ukoo wa Chaulo yaliopo katika kijiji cha Buturi, wilaya ya Rorya mkoa wa Mara, ambako ndipo makazi ya kudumu ya ukoo wa Chaulo.

Pichani juu ni mama yangu mzazi (mwenye Tie dye) pamoja na marehemu. Mapema mwaka huu alipokwenda kutembelea makazi ya mama yangu huko Kibada, Dar es salaam.

Mama Yucabeth Atieno Chaulo ni mama mzazi wa Shemeji yangu mkubwa Mussa Chaulo a.k.a baba Danny. Shemeji Mussa amemuoa dada yangu mkubwa Elline Igogo a.k.a mama Danny takriban miaka 21 na miezi kadhaa sasa. Wamebahatika kupata watoto watatu Daniel, Chaulo, na Cecilia.

family!

Akiwa na baadhi ya watoto zake, wakwe zake, mama yangu mzazi, na mdogo wangu (mwenye darkblue), Kibada Dar es salaam.

Bahati mbaya miezi kama mitatu hivi iliyopita marehemu mama Yucabeth Atieno Chaulo alimzika mmoja wa binti zake ambaye yupo kwenye picha hii, (wapili kutoka kushoto mwa dada mwenye nguo Nyekundu, nyuma ya mama yangu naye amevaa Tie Dye)! ….. Roho zao zipumzike kwa amani ya Bwana.

Mama yetu alikua akisumbuliwa na mapafu kwa muda mrefu kidogo, alikuja Dar es salaam kwaajili ya matibabu na ndipo mauti ilipomkutia. Kwa asili yeye ni Mkenya (mzaliwa wa Kenya / mluo toka Kenya) ambaye aliolewa ujaluoni huko Buturi, na ndipo alipokua ameishi muda wote wa uhai wake.

Ibada ya kuuaga mwili , Dar es salaam

Beautiful and peaceful sendoff kwa mama yetu Yucabeth Chaulo yaliyofanyika nyumbani kwa mmoja wa watoto wake huko Mwanangati, Yombo Vituka, Dar es salaam. Kuishi maisha ya kumtukuza Mungu ni raha na amani tele! Amemaliza mwendo, tuonane asubuhi ile njema! ?? ……. Aneyeimba ni mwimbaji mashuhuri ajulikanaye kama Angela Magoti. Angela ameolewa na mjukuu wa marehemu.

“Nikasikia sauti kutoka mbinguni ikisema, Andika, Heri wafu wafao katika Bwana tangu sasa. Naam, asema Roho, wapate kupumzika baada ya taabu zao; kwa kuwa matendo yao yafuatana nao.” Ufunuo 14:13

Video hizi zote ni ibada ya mazishi yake leo hii 07/01/2021 huko Buturi, Rorya.

Video hii haina uhusiano na msiba huu! Japo wimbo wao huo ndio uliokuwa ukitumbuiza wafiwa.

“Bali wewe, uwe na kiasi katika mambo yote, vumilia mabaya, fanya kazi ya mhubiri wa Injili, timiliza huduma yako. Kwa maana, mimi sasa namiminwa, na wakati wa kufariki kwangu umefika. Nimevipiga vita vilivyo vizuri, mwendo nimeumaliza, Imani nimeilinda; Baada ya hayo nimewekewa taji ya haki, ambayo Bwana, mhukumu mwenye haki, atanipa siku ile; wala si mimi tu, bali na watu wote pia waliopenda kufunuliwa kwake.” 2Timothy 4:5-8

Bwana alitoa na Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe milele zote. Tuonane Paradiso mama yetu! ????

Video hii haina uhusiano wowote na msiba.

R.I.E.P uncle Zou Fu!

As family of O.O Igogo, we mourn the tragic death of our best friend, business partner, and family friend Sir. ZOU FU QIANG (in dark-red Tshirt) that happened in China earlier today! Our prayers go out to his family, friends, and everyone who is touched by his death!

From left Mr Molnar, Mr Igogo, and late Mr Zou

Mr Zou Fu a.k.a uncle Zou, he was one of the three founders and Shareholders of the on coming giant multi-millions Usd Copper Smelter and Gold Refinery entity, IGOZOMO ( IGOGO – ZOU – MOLNAR) Minerals Company Ltd, located in Mpwapwa district in Dodoma region, Tanzania.

2019 at Saba saba grounds!

Also, he was the owner and founder of Aloe vera herbal drug (Jufeel Aloe Vera juice) for human body immune boosting ……. Great human being to say the least! Such a beautiful soul gone too soon! We will surely miss you greatly!.????

“Rafiki yangu wa KWELI KIKWELI KWELI. MAREHEMU ZOU FU QIANG.(PUMZKA SALAMA.) MY DEAREST AND TRUETH FRIEND LATE Mr. ZOU FU QIANG. (REST IN PEACE)” by longtime best friend, brother, and business partner sir O.O Igogo.

Words of sympathy from Magreth
Words of sympathy from Magreth
Words of sympathy from Janet

“Thank you so much Arwa. That is a man who made me so popular and higly respected in the Chinese Communities, He was very loyal, honest, hard working, creative, excessfully kind to me and our family. I fail to stop crying whenever I recall his helping hand to all that I have gained since knowing him in 21 years. Let all of us in the family keep on praying for his Soul to rest in peace.???” ….. shukrani za baba kwa bintie Alpha kwa kutengeneza video ya baadhi ya matukio ya hivi karibuni ambayo marehemu alishiriki nasi.

R.I.P Kofi Annan

Another Africa greatest is gone! R.I.P Kofi Annan Africa will always remember you, your legacy shall forever live!……. Hivi mnajua hakuna kituo chochote cha TV hapa Marekani ambacho kimeongelea kifo cha kiongozi huyu mashuhuri aliyewahi kupewa  tuzo za Nobel Peace Prize? Halafu utakuta baadhi ya Waafrika haswa Watanzania wanavyo washobokea Wamarekani wakati wenyewe kama hawafaidiki na kitu hata siku moja hawakiongelei!!

Ingekuwa ni vita au vurugu mahala fulani huko African ungeona ambavyo kila kituo kinaonyesha kwasababu tu wanataka kuonekana wao ni bora kuliko wengine!! Napoa hapo wanajua ni sehemu ya kuuza silaha zao kama bunduki  hivyo ni lazima wamfanyie promo ya nguvu ili wauza silaha wapeleka huko!! Siku tutaacha kushabikia hawa wazungu na kujenga vyaketu ndipo tutaheshimika mbele zao!!

Anyway, may Kofi Annan soul’s R.I.P ??

R.I.P the King of Comedy!

R.I.P the King of comedy, the Legend mzee Majuto! You have fought a good fight your legacy will forever live in Tanzania entertainment industry! You will be dearly missed with not only Tanzanians but many around East Africa and Africa in general! Rest in Eternal peace mzee wetu . Bwana alitoa na Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe milele zote ??

Jokate Mwegelo: Ufike muda harakati za ukombozi wa mataifa ya Afrika zifundishe kwa nguvu zote mambo makubwa yaliyofanywa na akina mama wa mfano kama akina Bibi Titi wa Tanzania na Winnie Mandela wa Afrika Kusini

Regrann from @jokatemwegelo  -  What a love story! What a life! What a wife and mother! What a Human Being but most importantly what a WOMAN!!! A Force!! Unapologetic!! Political Activist to match non other. You went from being someone’s wife at a very tender age to being your own PERSON!! Having your own VOICE and CONVICTION which you pursued to your final breath. No matter how hard they try to taint your legacy by singling out some events notwithstanding what they did had so much more harm and adversity to your people, they made you when they cornered you, took you to solitary confinement which gave you strength instead of breaking you they actually made YOU- they saw your God see you through it all and you persisted like gold you came out stronger.  Even when your own people turned against you, you did not waiver. They know how much your strength and tenacity at times even more than men to fight for the total liberation and emancipation of your people will forever live on and inspire generations to come. 

In the struggle for the liberation of our African states WOMEN did play a vital role. It is sad that the role of women is eschewed and women who were fearless and did about anything for their people are labeled as angry or simply controversial. LoL. How funny and silly!!! The women are the ones who kept the struggle alive in this context, mobilized people for the cause while their husbands were jailed or exiled or even when some men went into hiding because they were scared!!!  Ufike muda harakati za ukombozi wa mataifa ya Afrika zifundishe kwa nguvu zote mambo makubwa yaliyofanywa na akina mama wa mfano kama akina Bibi Titi wa Tanzania na Winnie Mandela wa Afrika Kusini. Lazima watoto wakue wakijua kuna akina mama shupavu waliopitia mengi hata kuteswa na kunyanyaswa kwa ajili ya uhuru wa watu wao na hawakukata tamaa mpaka kilivyoeleweka. Yaani wanawake walionyesha tuna nguvu ya ajabu tukiamua jambo letu katika kupigania haki na maendeleo ya watu wetu kutoka kwenye utawala mbovu wa kibaguzi na kinyonyaji! Lala Ngoxolo Nomzamo Winnie  Madikizela Mandela. ❤️ #RIPWinnieMandela  - #regrann

Pumzika kwa amani Mwalimu Boaz Chumo!

Kwaniaba ya familia ya mzee Otieno Olung'a Igogo wa Utegi, Rorya, Mara. Naomba kutuma salamu za pole wa.msiba wa Mwalimu Boaz Chumo uliotokea leo katika hospitali ya Muhimbili majira ya asubuhi (masaa ya Africa mashariki). Salamu hizi za pole ziifikie familia ya marehemu mzee Boaz Chumo, ndugu wa marehemu, marafiki, pamoja na walimu na wanafunzi wote waliofanya kazi au kufundishwa na Mwalimu Chumo pale C.B.E  Marehemu Mwalimu Boaz Chumo enzi za uhai wake! Bwana alitoa na Bwana ametwaa lihimidiwe jina lake milele zote ? Marehemu Mwalimu Boaz Chumo akiwa na mkewe wa pekee Mrs Julita Chumo!..... Pole sana aunt kwa msiba Mungu awe nanyi wakati wote hasa katika kipindi hichi cha maombolezo. R.I.P uncle.

R.I.P mzee Naftali Kwang’a Adhero!

Kwa masikitiko makubwa sana kwaniaba ya familia ya Mzee Otieno Olung'a Igogo naomba kuchukua nafasi hii kutuma salamu  za pole za msiba wa mzee Naftali Kwang'a Adhero kwa familia ya marehemu, ndugu, jamaa, marafiki, na wana Kowak wote! Mwenyezi Mungu wa rehema awape faraja katika kipindi hichi cha maombolezo. Awape nguvu ya kuweza kuanza maisha mapya bila uwepo wa baba. Poleni sana familia ya mzee Adhero.

Marehemu mzee Naftali Adhero akiwa na baadhi ya wajukuu zake

"1 Nakuagiza mbele za Mungu, na mbele za Kristo Yesu, atakayewahukumu walio hai na waliokufa; kwa kufunuliwa kwake na kwa ufalme wake; 2 lihubiri neno, uwe tayari, wakati ukufaao na wakati usiokufaa, karipia, kemea, na kuonya kwa uvumilivu wote na mafundisho. 3 Maana utakuja wakati watakapoyakataa mafundisho yenye uzima; ila kwa kuzifuata nia zao wenyewe watajipatia waalimu makundi makundi, kwa kuwa wana masikio ya utafiti; 4 nao watajiepusha wasisikie yaliyo kweli, na kuzigeukia hadithi za uongo. 5 Bali wewe, uwe na kiasi katika mambo yote, vumilia mabaya, fanya kazi ya mhubiri wa Injili, timiliza huduma yako. 6 Kwa maana, mimi sasa namiminwa, na wakati wa kufariki kwangu umefika. 7 Nimevipiga vita vilivyo vizuri, mwendo nimeumaliza, Imani nimeilinda; 8 baada ya hayo nimewekewa taji ya haki, ambayo Bwana, mhukumu mwenye haki, atanipa siku ile; wala si mimi tu, bali na watu wote pia waliopenda kufunuliwa kwake." 2 Temotheo 4: 1-8

Mtoto wa marehemu John Adhero (Diaspora-U.S.A) na mama yake mzazi ambaye ni mke pekee wa marehemu

Pole sana John Adhero kwa kufiwa na baba, Mungu awe nanyi sasa na hata milele zote.

Vita vizuri mmevipiga na kazi mmemaliza. Pumzikeni kwa amani ya Bwana!

Mungu awape nguvu wanafamilia na wafiwa wote kuweza kukabiliana na maisha bila wapendwa wao! Poleni sana Watanzania wote. Wapumzike katika amani ya Bwana! Mungu ibariki ???

Tanzia: R.I.P Kenneth Alexander Igogo

Marehemu Kenneth Alexander Igogo

Kwa masikitiko makubwa sana kwaniaba ya familia ya marehemu mzee Alexander Olung’a Igogo, familia ya mzee Otieno Olung’a Igogo, na familia yote ya babu mzee William Olung’a Igogo wa Utegi, Rorya, Mara. Naomba kutangaza kifo cha kaka yangu Kenneth Alexander Igogo a.k.a Ukombozi kilichotokea leo majira ya mchana saa za Africa Mashariki katika hospitali ya Bugando, Mwanza. Mipango ya mazishi inafanywa na ndugu wa marehemu. Mikusanyiko yote itafanyika nyumbani kwa baba mkubwa wa marehemu mzee Charles Olung’a Igogo pale Oyster Bay, Dar es salaam, Tanzania.  Kwafaida ya wasomaji wangu, marehemu ni kaka (tumezaliwa mwaka mmoja kasoro miezi) yangu mtoto wa marehemu baba yangu mkubwa. Baba yake ni tumbo moja na baba yangu ndio wanafuatana kuzaliwa. Marehemu ameacha watoto wawili, mama mzazi, dada wanne, na kaka watatu, pamoja na nieces, nephews, na mjukuu mmoja. Hii picha tulipiga mwanzoni mwa mwaka huu (February, 2017)  tulipokwenda kusalimia ndugu zetu kijijini kwetu Utegi ambapo marehemu alikuwa akiishi na familia yake.  Yeye ndio mwenye Tshirt yenye mistari ya kijani kifuani pembeni yangu. Mwenye nguo nyekundu ni mama mzazi wa marehemu. Hao wengine ni wadogo zangu Magreth na Guka. …..Kifo hichi ni chakusikitisha sana kwa jinsi kilivyotokea!! Sina lakusema zaidi ya Bwana alitoa na Bwana ametwaa. Jina lake lihimidiwe milele zote, Amen!

In loving memory of mzee Kimambi: Pole Mange na familia yako yote. May his soul continue to R.I.P

 Part 1. My late dad- in yellow and white. Mimi one of the little girls namwangalia babangu! . . Leo ni miaka 13 toka baba yetu atuache..??? Sitokaaa kuisahau siku ya Jumanne September 21 2004. Ilikuwa mida ya Sasa 1 usiku nikiwa mabibo hostel nilipigiwa simu na classmates wangu wa kiume @Gesona, Jerry Kajiru na wengine wakiniuliza nipo wapi wanataka twende sehemu nje ya mabibo hostel tukale chakula. Nikawaambia nipo block F basi wakanifata wakasema hiyo bar iko mbezi beach.Hao tukaondoka tukiwa njiani kuelekea huko nikapigiwa simu na Fideline Iranga, akiniuliza Mange uko wapi? Nikamwambia nipo njiani na washkaji tunaenda kula, akaniuliza ni kina nani? Nkamjibu huwajui, akawa very interested kujua niko na kina nani na tunaenda wapi mpaka nikastuka kidogo..Sjakaaa dakika 2 nikapigiwa simu na Carolyne Machange (Marehemu pia) akaniuliza Mange uko wapi? Mama yanguuuu nilitupa simu nkaaanza kuliaaaaaa sijui nalia nini?? Ila nilijua kuna tatizo kubwa na hakuna anaeweza kuniambia. Nikaannza kuwauliza washkjaji niliokuwa nao kwenye gari Jamani niambieni kuna nini? Something is wrong ? Wanajifanya kunishangaaa wananiuliza mange Unalia nini? Mbona hatukuelewi?? Nikawauliza Jamani mbona tunaenda Mbezi beach? Toka lini tunaenda kula mbali hivyo? Na huko ndo kwetu. Out of nowhere nilianza kuscream 'God Please not my dad' sijui why ila nilihisi ni babangu sababu watu wasingehangaika kunicheki vile Kama isingekuwa babangu coz wanajua nilikuwaje na babangu. Hapo rafiki zangu wananinyang'anya simu ili mtu mwingine asinipigie. Nalia kilio bila kujua nalilia nini. Nkachukua simu nkadial namba ya babangu ikawa imezimwa, mama yangu nikaanza kupiga mayoweeeeeeeeeeee why namba ya babangu imezimwa... gari ilivyoanza kuelekea kwetu nawauliza rafiki zangu mbona mnanipeleka nyumbani jamani?? Huku naliaaaa, wako kimya hawana jibu. . . Nakumbuka kama ilikuwa jana, tulivyofika kwetu mlinzi akaja kufungua geti nikawa namuuliza 'Babu kuna nini babu' Babu anaangalia chini, Hanijibu ile tunaingia nikaona gari ya babangu imepaki kidogo nkapata hope labda sio baba maana kama gari yake ipo it's means hajapata car accident na hawezi kufa kwa njia yoyote ile ingine sababu alikuwa mzima kabisaaa. Part 2. My dad (Mkandarasi) akikabidhi either College ya Veta au barabara (sikumbuki vizuri) kwa Mkapa . . . Basi nikashuka kwenye gari nakumbuka mtu wa kwanza kumuona alikuwa houseboy wetu Kaka Kibesa(marehemu pia) alikuwa houseboy wetu wa watangia Mimi sijazaliwa, aliletwaga na mama yangu mzazi kutoka Lindi, mmakonde mwenzie. Hata mama yangu alivyoachika Kaka Kibesa alibaki na aliendelea kunilea na alitulea watoto wote.R.I.P Kaka Kibesa. Kwa kumwangalia usoni tu nilijua ni baba, he looked so broken, nikamuuliza Kaka Kibesa naomba uniambie kuna nini, hakujibu kitu zaidi ya 'Panda juu Mange' . . Naingia ndani nakuta tayari kuna Watu wachache wamekaaa kwenye mikeka wanalia, mama yangu nilidataaaaaaa. Nilipanda zile ngazi kwenda upstairs Kama kichaaaaaaaaa, kuingia chumbani kwa baba na mama namuona step mom wangu kitandani analia huku watu wanambeleza, Mungu wangu nilianza kukaaaa chini na kusimama, najitupa nainuka , tumbo linaniuma, nilipata period hapo hapo, pale ndo nilipojua baba yangu kafariki. That was a defining moment.Nakumbuka sentensi ya kwanza nilisema ilikuwa ' Hakuna Mungu jamani, kungekuwa na Mungu asingemchukua babangu jamani' nikaanza kuuliza kafaje wakati gari yake ipo chini?? Hapo ndo nikaelezwa kajiua..... Dah sikuamini kajiua?? Ila it made sense!! . . Mara Kaka Kibesa akanitafa akanikabidhi barua aliyoniachia baba. Nkamuuliza aliacha barua ngapi akasema nne! Yangu, ya mke mkubwa, mke mdogo na ya kaka yake mkubwa!! Mikono ilikuwa inatetemeka kuifungua barua. Sikujua kama nilitaka kujua alichokiandika... Niliondoka nilipokua nimezungukwa na Watu nkajifungia nkaanza kuisoma. Like the true father that he was alikuwa kaniachia maagizo ya wapi ntapata pesa za school fees na matumizi mpaka Mirathi ikiwa settled! Na kuniagiza niwaangalie wadogo zangu. Nakumbuka sentensi ya kwanza ilikuwa ' Mwanangu Mange, utakapoipata Barua hiii nitakuwa nimeshatangulia mbele ya haki' Uwiii Barua ilijaaa machoziii. Wala hakugusia why kajiua Ila ni sababu alijua Mimi out of all people najua Sababu gani kajiua ??  Part 3. Msiba wa babangu ulikuwa kama movie kwangu. . . Baada ya hapo ilikuwa ni 2 long days za kuwasubiri wadogo zangu wa kiume waliokuwa wanasoma Kamuzu Academy-Malawi wafike nyumbani.nilikuwa nawawaza wao watahandle vipi situation sababu walikuwa wadogo.Nakumbuka sikuweza kutia kitu mdomoni toka nimeambiwa baba kafariki sababu nilihitaji kuwaona kaka zangu kwanza!Nakumbuka wadogo zangu walivyofika nilisikia tu vilio vimezidi nje. Niliwakimbilia nilihisi kama Baba anarudi.Tulihagiana wote wanne, Mimi, Step mom wangu,na wadogo zangu for the longest time. Na Nakumbuka ndogo wangu anaenifata alitake control of the situation mara moja, Yani alijua Sasa baba kaondoka lazma atake control. Alitukumbatia woooote akasema 'guys we will be okay' I swear hiyo sentensi ilinipa ahueni kubwa mnooo. Aliirudia ile sentensi kama mara 10 , ' We will be okay'. 30 mins later tulikaaa pamoja tukala chakula.?? . . Kifo cha babangu kinanisumbua mpaka Leo sababu I feel responsible somehow. I feel like I could have done something. I could have gotten him help. Baba yangu alikuwa ananitoa chuo kila siku anaiita ofisini kwake ananilalamikia about one thing and one person only.One of the 2 people aliemcause my father so much hurt ni Sumaye ndo maana mmeona issue yake ya kunyang'anywa Mashamba sikutaka kuposti.That time Sumaye alikuwa waziri mkuu. Labda Sumai hakufikiria kuwa threats alizomfanyia babangu kupitia mke mdogo na mali walizomfilisi yeye na mke mdogo zingeifikisha familia yetu hapo. Ntaishia hapo sababu nikiendelea itabidi nitaje na majina, kaka zangu hawatakagi niongeee hii issuie.Ila mke mdogo huwa siongei nae mpaka kesho. Nikimwonaga naskiaga roho inataka kunitoka? . . . Babangu aliondoka Kigoma 6 months before his death project ikiwa na matatizo na Sumaye akiwa anamwambia government haitomalizia malipo na ahand-in project ikiwa complete la sivyo anamfunga. Na hatokaaa kupewa tena projects za serikali na mkewe akawa kamchukua tayari. Remember babangu all his income zilikuwa ni project za serikali tu. All bank accounts zikawa frozen, Tanzania na Dubai......Let me end here ?

“Mitihani ni sehem ya Maisha na Huletwa na Mwenyez Mungu”~~~~~Diamond

Mitihani ni sehem ya Maisha na Huletwa na Mwenyez Mungu , na Siku zote huletwa kwa sababu, na ndiomaana tumefunzwa kushukuru kwa kila jambo..... Allah nakushkuru kwa yote, Nakushkuru kwa kunifikisha Uganda na Kumaliza kila jambo salama....Naomba pia Uniongoze katika safari yangu hii ya sasa ya Kuelekea Dar es Salaam....na unitie nguvu siku ya kesho nikiwa kazini pale Leader Club... ? @mama_dangote

Pumzika kwa amani mama Zari!

R.I.P mama Zari

Zari and her mother

" It's with deep sorrow that my family and I announce the death of our lovely mother who passed on this morning. May her soul rest in peace, May Allah forgive you your sins and grant you Jana. You will forever be loved our Old Sun, us as your kids were given the best from God as our mother. We appreciate all you did for us. We will forever cherish you Mama. Sleep well? " >>> Announced the BossLady through her Instergram A/C 
 Zari my dear,  just know there are so many of us who have been touched with the death of your mother, we mourn with you and your family!...... I imagined how will I feel and what will I do if I was in your position right now; the feeling is unexplainable, terrifying to say the least! Just keep the faith, believe that if God brings you to it, He will bring you through it!  Stay strong darling!

A  family that plays together stays together! God be with you all!

Sending my deepest condolences to your family, your 4 soldiers, and beloved daughter- Tiffah! May mama's soul R.I.P ......... Bwana alitoa na Bwana ametwaa libarikiwe jina lake milele zote ?

 

Dada wa Taifa aomboleza kifo cha mama Linah Mwakyembe!

 Kwakupitia mtandao ya jamii kwenye account yake ya Facebook dada wa taifa la Tanzania Mh. Shy-Rose Bhanji ametoa salamu zake za pole kwa waziri Mwakyembe pamoja na familia yake kwa msiba mzito uliowapata wakuondokewa na mke / mama / shangazi / bibi mpendwa mama Linah G. Mwakyembe.

Dada wa Taifa la Tanzania, Mh.ShyRose Bhanji

"Napenda kutoa pole za dhati kwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe kwa kufiwa na mke wake mpendwa Bi Linah Mwakyembe. Naiombea familia ya Dkt. Mwakyembe nguvu, uvumilivu na baraka katika wakati huu mgumu kwa wanafamilia. Mungu amlaze pema ??" >>>>>Mh. ShyRose Bhanji 
Nami naomba niungane na waombolezaji wengine kwa kutoa pole kwa familia ya Dr. Mwakyembe, ndugu, marafiki, na bila kumsahau Emelda Mwamanga na familia yake yote. Poleni sana wapendwa........Maisha ya mwanadamu ni kama maua uchanua, unyauka na kukauka kabisa! Yote ni mipango ya Mungu jina lake lihimidiwe milele zote! R.I.P mama Mwakyembe!

Rest In Eternal Peace mama Janet Leah Anyango Owino!

Janeth Igogo -the daughter inlaw to the late mama Janet Leah Anyango Owino

It’s painful and hard to believe. I’ve lost a good friend, my ONLY in law who could call and ask “nyar Igogo why are you so quiet……na huyo kijana wangu anakuangalia vizuri kweli…….wacha kupotea hivo mamaa……I love you my daughter” Her heart was pure and filled with joy, will miss her dearly. +254 will never be the same without you mamaa! Until we meet on that beautiful shore; Sleep well my beautiful aunty in law.

The late mama Janet Leah Anyango Owino and her son

Faith Mbori-daughter to the deceased mama Janet Leah Anyango Owino

My only regret is that , I didn’t get home in time to take you to our trip we had talked about .Please join me and my family in prayers. We lost our Beautiful Beloved Mother. I am still in Shock . I think I am dreaming . Maybe I will wake up and hear her voice . Awuoro tho. Rest In Peace Alei Nyar gi Pastor. Awuoro tho . We loved you but God loved you most. I know I will meet you in Heaven. I know you are now singing with the Angels . Awuoro tho . Awuoro. The death that took my father, now My mother? Awuoro.

Mama Janet Leah Anyango Owino and her children

Alpha Igogo -blogger, and sister to Janeth Igogo,

I am deeply sadden by the death of our aunt inlaw mama Janet Leah Anyango Owino! It hurts for no one can be prepared or get used to the loss of our beloved ones!  However, it takes comfort knowing that they are resting  in peace and one day we will meet again in that beautiful shore! With all due respect and honor, on behalf of Mr and Mrs O.O Igogo’s family and the Rhoda Nyolwengos’ household,  I’m sending my sincere condolences to my “International brother-in-law”  and his entire family, the Nyagilos’ family in Kagan, Kenya, the Owinos’ family in Kenya, the Omboris’ family here in U.S.A and Kenya, and without forgetting the Atengs’ family here in U.S.A, Nairobi, and Kagan, Kenya!…….. Mama has departed physically from us, but her good deeds will forever live in our hearts and minds! “Naked I came out of my mother’s womb, and naked shall I return thither. The Lord gave, and the Lord hath taken away; blessed be the name of the Lord” Job 1:21……. R.I.P mother inlaw!

In loving memory of Ivan Ssemwanga: “I think I was prepared for death”

“I think I was prepared for death,……for some reason on the back of my mind I knew what is going to happen!…… I have 3 boys to raise it’s a full church  here but three months down the line I’ll be by myself! So I’m strong! Ammm, I’m ready to raise them!  I’m very strong! If you trust me I moved on he never moved on! He knew I’ll do the right thing not just for the boys for his legacy; Ivan  knew Zari is the right person! So, I’ll do it for him, for the boys, and for the legacy, and the  family, and the fans, and  everybody else  Ivan was reattached with! So for me,  I don’t mourn  Ivan I celebrate him! He’ lived his life to the fullest”  Zari Hassan  

Kuna kitu lazima watu mkubali kuwa kuna wanawake wengine ni IRREPLACEABLE na Zari is just one of them! Ivan never moved on because he was searching for another Zari out there without knowing some people has no photocopy! Naamini ndio maana aliamua kuishi a “party” lifestyle ili kumuondoa Zari katika mawazo yake but deep inside his heart he was lonely and depressed! So sad!………..Zari take God on board as you will need Him now more than ever before! With Him on your side I know you will make it and your boys are going to be very proud of you!……….R.I.P Ivan Semwanga!

R.I.P mama Tenga!

Naomba nitoe pole zangu za dhati kabisa kwa familia ya Mchungaji Rashid Tenga na ukoo wote kwa msiba wa mama / bibi yetu mama Tenga. Pole sana dada yangu Penninah Tenga kwa msiba wa mama. Mungu awe nanyi katika kipindi hichi cha maombolezo na wakati wote!……..Kwa faida ya wengi, marehemu mama Tenga ni mke wa Mchungaji mstaafu Rashid Tenga wa kanisa la Wasabato.  Pia ni mama yake mzazi na mwanasheria maharufu Tanzania Ringo Tenga. ………..Bwana alitoa na Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe milele zote!

R.I.P Ivan Semwanga!

Jamani, Ivan what have you done to your boys jamani! Boy! Mbona huyu Ivan ameniuma hivyo yani nikifikiria jinsi alivyokuwa anawapenda watoto wake mwe! So sad! Sincere condolences to Zari and her “soldiers”! Ma’am! Those children are way too young to be fatherless! Honestly, Ivan had his own issues but when comes to his children!? He was a very responsible, dedicated father! I think ndio maana imeniuma sana kifo chake kwani there are not so many committed / dedicated  responsible fathers in this world; to lose one is just too plenty!!……Gone too soon my age mate!  R.I.P Ivan Semwanga!

R.I.P sister Maimuna Rajabu Sarungi!

May your soul rest in eternal peace my charming sister Maimuna Rajabu Sarungi! I glorify the name of the Lord for the time we spent together and the love  we shared during my visit to Utegi earlier this year and all other times! We shall meet again on that beautiful shore!   ………. I’m sending my sincerely condolences to my late BabaMkubwa Rajabu’s family na wana ukoo wote! Bwana alito na Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe milele ?

“Together we will get through this, God bless you we love you “~~~~ Idris Sultan

Wapendwa, huu msiba umeumiza watu wengi sana! Binafsi nikiona hii picha ya hawa watoto nashikwa na butwaa, huzuni inanijaa! Kuna post ya kuchekesha nilitaka kuweka kile kitendo cha kufungua blog na picha ya kwanza nakutana nayo ndiyo hiyo ya watoto hao washule yani nikajikuta nakuwa mdogo kama sisiminzi!! Nikaona ngoja niipotezee kwa leo. Seriously, the nation is still grieving, I don’t know how people will transit from this tragedy to their normal lives?!! O’Lord of mercy see Tanzanians through this!!…………  Basi nikaingia Instagram ndo nakutana na huu ujumbe wa Idris Sultan kwa Watanzania wote. Very touching, embu usome na wewe…..!