Dada wa Taifa aomboleza kifo cha mama Linah Mwakyembe!

 Kwakupitia mtandao ya jamii kwenye account yake ya Facebook dada wa taifa la Tanzania Mh. Shy-Rose Bhanji ametoa salamu zake za pole kwa waziri Mwakyembe pamoja na familia yake kwa msiba mzito uliowapata wakuondokewa na mke / mama / shangazi / bibi mpendwa mama Linah G. Mwakyembe.
Dada wa Taifa la Tanzania, Mh.ShyRose Bhanji
"Napenda kutoa pole za dhati kwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe kwa kufiwa na mke wake mpendwa Bi Linah Mwakyembe. Naiombea familia ya Dkt. Mwakyembe nguvu, uvumilivu na baraka katika wakati huu mgumu kwa wanafamilia. Mungu amlaze pema ??" >>>>>Mh. ShyRose Bhanji 
Nami naomba niungane na waombolezaji wengine kwa kutoa pole kwa familia ya Dr. Mwakyembe, ndugu, marafiki, na bila kumsahau Emelda Mwamanga na familia yake yote. Poleni sana wapendwa........Maisha ya mwanadamu ni kama maua uchanua, unyauka na kukauka kabisa! Yote ni mipango ya Mungu jina lake lihimidiwe milele zote! R.I.P mama Mwakyembe!

Leave a Reply