“ASANTE MUNGU” Maana yatupasa kushukuru kwa kila jambo

Kuna tajiri mmoja aliamka asubuhi akachungulia dirishani na kumkuta Maskini mmoja akiponda kokoto, alitema mate chini kisha akasema ee mwenyezi Mungu wewe ni mkuu mno nakushukuru sana Maana Mimi si kama huyu Maskini anayeponda kokoto hapa.Akisha kusema hivyo alimkejeri yule Maskini huku akimwambia we choko lazima ufe mapema. Lakini yule Maskini alimuangalia kwa uchungu kisha akasema, yeye anayenifanya niwe hai mpaka muda huu ndiye aujuaye hata mwisho wangu.

Mwanafunzi mmoja alifaulu peke yake darasani huku wenzake wote wakifeli lakini hakujisifu kwamba ana akili sana bali alipiga magoti akamshukuru Mungu akisema asante Mungu maana hii ni neema tu na wala si ujanja wangu.

Askari mwingine alinusurika vitani baada ya wenzake wote kuteketezwa, yeye hakujigamba kwamba ni mpambanaji sana bali alinyenyekea mbele za Mungu akasema asante Mungu maana wewe ndiye unayenipigania.

Mama mmoja alifiwa na mumewe akisha kulia sana alijifuta machozi yake huku akisema asante Mungu kwa yote haya yanayonipata Maana wewe ni mume wa wajane utanifariji.

Dada mwingine alisalitiwa na mpenzi wake lakini wala hakujiua bali alimshukuru Mungu huku akisema asante Mungu maana najua utanipa mume mwema.

Kaka mmoja alikataliwa na mpenzi wake na kukanwa hadharani lakini hakufa moyo bali alisema asante Mungu maana ndiwe utakaye nipatia mke mwema.

Mtu mwingine alikuwa msibani akiomboleza na kulia sana huku akisema asante Mungu maana najua unanipa wewe neema hii ya kuishi na siyo kwa nguvu zangu.
Picha credit: unknown
Kuna yatima walitengwa na ndugu zao na kudhurumiwa haki zao lakini hawakujikatia tamaa Maana walimshukuru Mungu wakisema asante Mungu maana tunakufahamu yakuwa wewe ni baba wa yatima utatutetea..

==>Hata wewe uliyeusoma ujumbe huu sema "ASANTE MUNGU" Maana yatupasa kushukuru kwa kila jambo, kumbuka hata huu uhai tulio nao tunapewa bure na wala hatuulipii.

*** Source unknown. Copy and paste  from Facebook ***

Leave a Reply