Tanzia: R.I.P Kenneth Alexander Igogo

Marehemu Kenneth Alexander Igogo

Kwa masikitiko makubwa sana kwaniaba ya familia ya marehemu mzee Alexander Olung’a Igogo, familia ya mzee Otieno Olung’a Igogo, na familia yote ya babu mzee William Olung’a Igogo wa Utegi, Rorya, Mara. Naomba kutangaza kifo cha kaka yangu Kenneth Alexander Igogo a.k.a Ukombozi kilichotokea leo majira ya mchana saa za Africa Mashariki katika hospitali ya Bugando, Mwanza. Mipango ya mazishi inafanywa na ndugu wa marehemu. Mikusanyiko yote itafanyika nyumbani kwa baba mkubwa wa marehemu mzee Charles Olung’a Igogo pale Oyster Bay, Dar es salaam, Tanzania.  Kwafaida ya wasomaji wangu, marehemu ni kaka (tumezaliwa mwaka mmoja kasoro miezi) yangu mtoto wa marehemu baba yangu mkubwa. Baba yake ni tumbo moja na baba yangu ndio wanafuatana kuzaliwa. Marehemu ameacha watoto wawili, mama mzazi, dada wanne, na kaka watatu, pamoja na nieces, nephews, na mjukuu mmoja. Hii picha tulipiga mwanzoni mwa mwaka huu (February, 2017)  tulipokwenda kusalimia ndugu zetu kijijini kwetu Utegi ambapo marehemu alikuwa akiishi na familia yake.  Yeye ndio mwenye Tshirt yenye mistari ya kijani kifuani pembeni yangu. Mwenye nguo nyekundu ni mama mzazi wa marehemu. Hao wengine ni wadogo zangu Magreth na Guka. …..Kifo hichi ni chakusikitisha sana kwa jinsi kilivyotokea!! Sina lakusema zaidi ya Bwana alitoa na Bwana ametwaa. Jina lake lihimidiwe milele zote, Amen!

Leave a Reply