R.I.P mzee Naftali Kwang’a Adhero!

Kwa masikitiko makubwa sana kwaniaba ya familia ya Mzee Otieno Olung'a Igogo naomba kuchukua nafasi hii kutuma salamu  za pole za msiba wa mzee Naftali Kwang'a Adhero kwa familia ya marehemu, ndugu, jamaa, marafiki, na wana Kowak wote! Mwenyezi Mungu wa rehema awape faraja katika kipindi hichi cha maombolezo. Awape nguvu ya kuweza kuanza maisha mapya bila uwepo wa baba. Poleni sana familia ya mzee Adhero.
Marehemu mzee Naftali Adhero akiwa na baadhi ya wajukuu zake
"1 Nakuagiza mbele za Mungu, na mbele za Kristo Yesu, atakayewahukumu walio hai na waliokufa; kwa kufunuliwa kwake na kwa ufalme wake; 2 lihubiri neno, uwe tayari, wakati ukufaao na wakati usiokufaa, karipia, kemea, na kuonya kwa uvumilivu wote na mafundisho. 3 Maana utakuja wakati watakapoyakataa mafundisho yenye uzima; ila kwa kuzifuata nia zao wenyewe watajipatia waalimu makundi makundi, kwa kuwa wana masikio ya utafiti; 4 nao watajiepusha wasisikie yaliyo kweli, na kuzigeukia hadithi za uongo. 5 Bali wewe, uwe na kiasi katika mambo yote, vumilia mabaya, fanya kazi ya mhubiri wa Injili, timiliza huduma yako. 6 Kwa maana, mimi sasa namiminwa, na wakati wa kufariki kwangu umefika. 7 Nimevipiga vita vilivyo vizuri, mwendo nimeumaliza, Imani nimeilinda; 8 baada ya hayo nimewekewa taji ya haki, ambayo Bwana, mhukumu mwenye haki, atanipa siku ile; wala si mimi tu, bali na watu wote pia waliopenda kufunuliwa kwake." 2 Temotheo 4: 1-8
Mtoto wa marehemu John Adhero (Diaspora-U.S.A) na mama yake mzazi ambaye ni mke pekee wa marehemu
Pole sana John Adhero kwa kufiwa na baba, Mungu awe nanyi sasa na hata milele zote.

One thought on “R.I.P mzee Naftali Kwang’a Adhero!”

Leave a Reply