Jinsi nilivyo kuja Marekani!

Andrews university ndio chuo kilichonipa nafasi mimi ya kuja Marekani. Ngoja niwape story fupi ya safari yangu ya kuingia hapa.

Siku zote nilikuwa natamani kusoma /kuishi nje ya Tanzania.  Na mara nyingi nilikuwa napenda Australia, UK, na Marekani. Ilikuwa rahisi kujenga hisia zangu na maeneo hayo kwani mara nyingi nilivahatika kupata vijuzuu vinavyoonesha shule mbalimbali za nchi hizo. Basi, nikiwa katika muhula wa mwisho wa kumaliza chuo pale C.B.E siku moja nikiwa kanisani Temeke SDA, katika matangazo nikasikia wakitangaza kuwa chuo cha Andrew wanapokea wanafunzi kwa muhula wa Fall (Fall semester), na wakasema kuna vijuzuu kama kuna mtu angependa kwenda akachukue ili ujuwe jinsi ya kujiunga. Mara baada tu ya ibada, nikaenda kuchukua kijizuu. Baada ya siku kadhaa nikaenda kwenye intranet Cafe fulani ilikuwa karibu na chuo cha C.B.E. Ndio kwa mara yakwanza nafungua email akaunti yangu πŸ™ˆ Nikajaza fomu siku hiyo. Baada ya muda wa miezi kadhaa nilitumiwa barua kwa njia ya posta kuwa wamenikubali kuingia chuoni hapo kwaajili ya degree ya kwanza.  Wakati huo nilikuwa nimesha hitimu C.B.E sasa natafuta chuo cha kwenda.

Nakumbuka mmoja wa wadogo zangu (cousin sister) aitwaye Detta alikuwa akipenda kunitania kuwa “aah wewe ni wa hapa hapa tu” namwambia mie nakwenda zangu Marekani subiri utaona. Hapo sijajua kama nitachaguliwa au la! Ila yeye alikuwa anasema hivyo kwasababu dada yangu mkubwa alisoma China, kaka yangu alikuwa UK, na mdogo wangu yeye alikuwa anasoma South Africa. Hivyo akawa anasema mie nitabaki Bongo.

Ghafla, siku moja naletewa barua nikiwa job (niliajiriwa na Utegi Technical Enterprises Ltd baada ya kumaliza chuo), kuangalia ilipotoka nakuta ni Andrews University.  Nikaifungua haraka sana! Nikakuta ni barua ya kukubaliwa kujiunga na chuo ila sasa muda ulikuwa umebaki wiki 2 tu shule ianze πŸ™†πŸ½β€β™€οΈπŸ™†πŸ½β€β™€οΈ Nikachanganyikiwa maana hizo hela zinazo hitajika na muda uliobaki, dah! Yule mzee kutoka kanda maalum nitamuingiaje?! 🀣 Mtu wakwanza kumwambia alikuwa ni mama. Yeye akanipa moyo akasema hongera sana, mwambie baba haraka sana. Sasa kesho yake hasubui tumesha maliza kunywa chai tunataka kwenda kazini, mama akalipua bomu kimtindo. πŸ™†πŸ½β€β™€οΈ

Akasema “Umesha mwambia baba?”, nikajifanya kutoa macho πŸ˜… baba akauliza nini unataka kusema? Akasema (Akaniita kwa jina langu la kilugha) kaa chini “let’s talk ni nini”. Ikabidi nimwambie. Akasema sasa kwanini naogopa kusema jambo zuri kama hilo. Nikamwambie mzee nikienda siku yakwanza tu inatakiwa malipo ya awali ya nusu semester (muhula) au ada nzima. Kanijibu sasa tatizo ni nini? Kwani wewe ndio unatoa hizo pesa? Basi mzee wa watu siku hiyo akasimamisha shughuli zake zote, kuhakikisha napata documents zote zinazohitajika na kuzituma kwa njia ya fax na DHL. Chuo nao walikuwa shapu walipoamka tu wakatuma email kua sawa wanasubiria documents za DHL halafu watatuma I-20 (form maalum yakuombea viza ya shule). Mzee aliwaambia kutoka na muda watume kwa DHL halafu atawalipa hiyo pesa. Basi baada ya wiki 1-20 imefika. Nikaweka appointment ya kuomba viza. Tukaenda kwenye Viza, kumbuka nina siku tu zakuripoti shule, hivyo ticket ya ndege ilibidi nikate kabla hata ya kupata viza.
Kwenye viza si kidogo watuzingue! 🀣🀣

Basi, tumefika kwenye viza wala sikuhojiwa maswali mengi, wakasema kila kitu kipo vizuri lakini cheti changu cha form 4 ni “Fake”! πŸ™†πŸ½β€β™€οΈπŸ™†πŸ½β€β™€οΈ Wakadai tumepiga simu wizara ya elimu wamesema hizo namba sio zake. πŸ₯ΊπŸ₯Ί Wakasema kama mnaweza kwenda wizarani mkahakiki nendeni kisha mrudi hapa. Wakatupa reference namba, na jina la mtu walie ongea naye hapo wizarani. Basi, tukatoka mbio kwenda wizarani, tunafika getini tukasema jina la mtu tunayekwenda kumuona, wakampigia simu huyo mtu kumwambia kua kuna wageni hapa wanahitaji kukuona. Yule mtu akaomba aongee na baba, akasema samahani rudini ubalozini wanawasubiria kule tumesha tatua tatizo. Alikosea kusoma namba. 🀣🀣🀣 Baba akasema lakini nilimuuliza unahuwakika kuwa cheti cha binti yangu ni feki na akanijibu kuwa “100% sure”. Mzee hasira zikamshika lakini sasa atafanyaje inabidi turudi tena ubalozini. Sasa wakati baba anamaliza kuongea na yule.mtu wa wizarani, secretary wake akapiga simu muda huo huo akasema “baba mnatafutwa na ubalozi wa Marekani wamesema mwende sasa hivi”, baba akamwambia ndio tunaelekea huko, lakini hawa watu leo ndio watanijua mimi ni nani! 🀣🀣🀣 Usichezee mzee wa kutoka kanda maalum.

Basi tukafika ubalozini, tukapokelewa vizuri, yule mdada akaomba msamaha kwa usumbufu, akachukua passport yangu akasema kesho asubuhi uje uchukue na nakutakia masomo mema. Mzee Igogo sasa akaanza, “young lady I need an official oppology letter” 🀣🀣 Eti huwezi kunifedhehesha mbele za watu halafu unaomba msamaha kiholela holela namna hiyo. πŸ™ˆπŸ™ˆ Yani mie I was like just give my passport am ready to board. Nyie muendelee na drama yenu kimpango wenu. 🀣🀣 Nilipata passport asubuhi, usiku nikaondoka zangu siku hiyo hiyo.

Ilikuwa mara yangu yakwanza kutoka nje ya East Africa. Niliondoka na ndege ya British Airways, business class 😍😍 mzee Igogo sijui alifikiri nikipanda economy nitachelewa πŸ™ˆ Mwe! Nilifurahi sana. Tukafika UK, tukapelekwa hotelini kwa ajili ya kupumzika mpaka asubuhi kuanza safari ya kuelekea Chicago O’Hare International Airport. Baada ya kufika Chicago shulenilinielekeza kuchukua basi lakuelea Indiana. Waliniambia nishuke kituo cha mwisho ambapo ni Indiana Airport na hapo nitakuta gari la chuo cha Andrews likinisubiria. Nilifata maelekezo nikafika shule salama kabisa.

Nilifikia kwenye dormitories za chuo. Jamani acha tu! Unaingia kwenye dormitory ya chuo kama hotel vile. 😍 Nilikuwa na roommate mzungu kutoka Canada, alikuwa anaitwa Melissa Gonzalez. Vyumba ni self contained, mna bathroom na shower yenu kwa chumba, for a minute nikakumbuka mabafu ya C.B.E mabafu 3 watu zaidi ya 20 ni mwendo wa kusubiriana wengine wanaamua kuoga< kwenye kolido🀣🀣 Kwakweli,.Andrews ni shule nzuri sana sema gharama zake sasa! πŸ™†πŸ½β€β™€οΈπŸ™†πŸ½β€β™€οΈPasua kichwa.

Leave a Reply