Category Archives: Alpha being Alpha!

Jinsi nilivyo kuja Marekani!

Andrews university ndio chuo kilichonipa nafasi mimi ya kuja Marekani. Ngoja niwape story fupi ya safari yangu ya kuingia hapa.

Siku zote nilikuwa natamani kusoma /kuishi nje ya Tanzania.  Na mara nyingi nilikuwa napenda Australia, UK, na Marekani. Ilikuwa rahisi kujenga hisia zangu na maeneo hayo kwani mara nyingi nilivahatika kupata vijuzuu vinavyoonesha shule mbalimbali za nchi hizo. Basi, nikiwa katika muhula wa mwisho wa kumaliza chuo pale C.B.E siku moja nikiwa kanisani Temeke SDA, katika matangazo nikasikia wakitangaza kuwa chuo cha Andrew wanapokea wanafunzi kwa muhula wa Fall (Fall semester), na wakasema kuna vijuzuu kama kuna mtu angependa kwenda akachukue ili ujuwe jinsi ya kujiunga. Mara baada tu ya ibada, nikaenda kuchukua kijizuu. Baada ya siku kadhaa nikaenda kwenye intranet Cafe fulani ilikuwa karibu na chuo cha C.B.E. Ndio kwa mara yakwanza nafungua email akaunti yangu πŸ™ˆ Nikajaza fomu siku hiyo. Baada ya muda wa miezi kadhaa nilitumiwa barua kwa njia ya posta kuwa wamenikubali kuingia chuoni hapo kwaajili ya degree ya kwanza.  Wakati huo nilikuwa nimesha hitimu C.B.E sasa natafuta chuo cha kwenda.

Nakumbuka mmoja wa wadogo zangu (cousin sister) aitwaye Detta alikuwa akipenda kunitania kuwa “aah wewe ni wa hapa hapa tu” namwambia mie nakwenda zangu Marekani subiri utaona. Hapo sijajua kama nitachaguliwa au la! Ila yeye alikuwa anasema hivyo kwasababu dada yangu mkubwa alisoma China, kaka yangu alikuwa UK, na mdogo wangu yeye alikuwa anasoma South Africa. Hivyo akawa anasema mie nitabaki Bongo.

Ghafla, siku moja naletewa barua nikiwa job (niliajiriwa na Utegi Technical Enterprises Ltd baada ya kumaliza chuo), kuangalia ilipotoka nakuta ni Andrews University.  Nikaifungua haraka sana! Nikakuta ni barua ya kukubaliwa kujiunga na chuo ila sasa muda ulikuwa umebaki wiki 2 tu shule ianze πŸ™†πŸ½β€β™€οΈπŸ™†πŸ½β€β™€οΈ Nikachanganyikiwa maana hizo hela zinazo hitajika na muda uliobaki, dah! Yule mzee kutoka kanda maalum nitamuingiaje?! 🀣 Mtu wakwanza kumwambia alikuwa ni mama. Yeye akanipa moyo akasema hongera sana, mwambie baba haraka sana. Sasa kesho yake hasubui tumesha maliza kunywa chai tunataka kwenda kazini, mama akalipua bomu kimtindo. πŸ™†πŸ½β€β™€οΈ

Akasema “Umesha mwambia baba?”, nikajifanya kutoa macho πŸ˜… baba akauliza nini unataka kusema? Akasema (Akaniita kwa jina langu la kilugha) kaa chini “let’s talk ni nini”. Ikabidi nimwambie. Akasema sasa kwanini naogopa kusema jambo zuri kama hilo. Nikamwambie mzee nikienda siku yakwanza tu inatakiwa malipo ya awali ya nusu semester (muhula) au ada nzima. Kanijibu sasa tatizo ni nini? Kwani wewe ndio unatoa hizo pesa? Basi mzee wa watu siku hiyo akasimamisha shughuli zake zote, kuhakikisha napata documents zote zinazohitajika na kuzituma kwa njia ya fax na DHL. Chuo nao walikuwa shapu walipoamka tu wakatuma email kua sawa wanasubiria documents za DHL halafu watatuma I-20 (form maalum yakuombea viza ya shule). Mzee aliwaambia kutoka na muda watume kwa DHL halafu atawalipa hiyo pesa. Basi baada ya wiki 1-20 imefika. Nikaweka appointment ya kuomba viza. Tukaenda kwenye Viza, kumbuka nina siku tu zakuripoti shule, hivyo ticket ya ndege ilibidi nikate kabla hata ya kupata viza.
Kwenye viza si kidogo watuzingue! 🀣🀣

Basi, tumefika kwenye viza wala sikuhojiwa maswali mengi, wakasema kila kitu kipo vizuri lakini cheti changu cha form 4 ni “Fake”! πŸ™†πŸ½β€β™€οΈπŸ™†πŸ½β€β™€οΈ Wakadai tumepiga simu wizara ya elimu wamesema hizo namba sio zake. πŸ₯ΊπŸ₯Ί Wakasema kama mnaweza kwenda wizarani mkahakiki nendeni kisha mrudi hapa. Wakatupa reference namba, na jina la mtu walie ongea naye hapo wizarani. Basi, tukatoka mbio kwenda wizarani, tunafika getini tukasema jina la mtu tunayekwenda kumuona, wakampigia simu huyo mtu kumwambia kua kuna wageni hapa wanahitaji kukuona. Yule mtu akaomba aongee na baba, akasema samahani rudini ubalozini wanawasubiria kule tumesha tatua tatizo. Alikosea kusoma namba. 🀣🀣🀣 Baba akasema lakini nilimuuliza unahuwakika kuwa cheti cha binti yangu ni feki na akanijibu kuwa “100% sure”. Mzee hasira zikamshika lakini sasa atafanyaje inabidi turudi tena ubalozini. Sasa wakati baba anamaliza kuongea na yule.mtu wa wizarani, secretary wake akapiga simu muda huo huo akasema “baba mnatafutwa na ubalozi wa Marekani wamesema mwende sasa hivi”, baba akamwambia ndio tunaelekea huko, lakini hawa watu leo ndio watanijua mimi ni nani! 🀣🀣🀣 Usichezee mzee wa kutoka kanda maalum.

Basi tukafika ubalozini, tukapokelewa vizuri, yule mdada akaomba msamaha kwa usumbufu, akachukua passport yangu akasema kesho asubuhi uje uchukue na nakutakia masomo mema. Mzee Igogo sasa akaanza, “young lady I need an official oppology letter” 🀣🀣 Eti huwezi kunifedhehesha mbele za watu halafu unaomba msamaha kiholela holela namna hiyo. πŸ™ˆπŸ™ˆ Yani mie I was like just give my passport am ready to board. Nyie muendelee na drama yenu kimpango wenu. 🀣🀣 Nilipata passport asubuhi, usiku nikaondoka zangu siku hiyo hiyo.

Ilikuwa mara yangu yakwanza kutoka nje ya East Africa. Niliondoka na ndege ya British Airways, business class 😍😍 mzee Igogo sijui alifikiri nikipanda economy nitachelewa πŸ™ˆ Mwe! Nilifurahi sana. Tukafika UK, tukapelekwa hotelini kwa ajili ya kupumzika mpaka asubuhi kuanza safari ya kuelekea Chicago O’Hare International Airport. Baada ya kufika Chicago shulenilinielekeza kuchukua basi lakuelea Indiana. Waliniambia nishuke kituo cha mwisho ambapo ni Indiana Airport na hapo nitakuta gari la chuo cha Andrews likinisubiria. Nilifata maelekezo nikafika shule salama kabisa.

Nilifikia kwenye dormitories za chuo. Jamani acha tu! Unaingia kwenye dormitory ya chuo kama hotel vile. 😍 Nilikuwa na roommate mzungu kutoka Canada, alikuwa anaitwa Melissa Gonzalez. Vyumba ni self contained, mna bathroom na shower yenu kwa chumba, for a minute nikakumbuka mabafu ya C.B.E mabafu 3 watu zaidi ya 20 ni mwendo wa kusubiriana wengine wanaamua kuoga< kwenye kolido🀣🀣 Kwakweli,.Andrews ni shule nzuri sana sema gharama zake sasa! πŸ™†πŸ½β€β™€οΈπŸ™†πŸ½β€β™€οΈPasua kichwa.

Muwe na weekend njema, baraka za kufunga mwaka 2022 na kufungua mwaka 2023 ziambatane nanyi.

Muwe na weekend njema sana, sikuu njema ya kufunga mwaka 2022, na kheri na baraka ya kufungua mwaka 2023. Mbarikiwe sana. ❀️ Have a very wonderful weekend, great end of year 2022 celebration, and a peaceful beginning of 2023. Blessings to you all. ❀️

Baraka za kufunga mwaka 2022 ziambatane nanyi katika kufungua mwaka 2023 na zikae nanyi siku zote. ❀️

Muhtasari-sehemu ya saba: Kwaheri si neno rafiki sana.

Janeth, Alpha, Magreth, na Guka

ikafika muda wa kusema ‘kwaheri’ neno ambalo si rafiki kwa vinywa vya watu wengi kwasababu ya uhalisia wa neno hilo! Basi hii ndio ilikuwa siku yangu ya mwisho Tanzania kwa mwaka 2022. Pichani kutoka kushoto ni mdogo wangu Janeth (mzaliwa wa nne), mimi mwenyewe mtu kati hapo (mzaliwa wa tatu), Magreth Nyasungu (mzaliwa wa tano), na Guka (mzaliwa wa sita).

baba na mama Alpha 😍
Mama Bear and her cubs 😍

Our prayers warrior, the glue that keeps our family together, our iron lady , our super woman, the centerpiece of our blessings, mama Igogo we love you, Mama. May our Almighty God continue to keep you well.

Dubai
Tanzanite Business lounge-JKN International Airport

Namshukuru Mungu kwa yote naomba azidi kutupa afya njema na ulinzi wa kutosha ili tuonane tena na tena sio kwa ajili yetu bali kwa ajili ya utukufu wa jina lake. πŸ™πŸΏβ€οΈπŸ™πŸΏ

Muhtasari -sehemu ya pili: Jambo lililonifurahisha zaidi mwaka 2022 ….!

Mama na mwana 😍

Kamanilivyosema kwenye posti yangu iliyopita somahapa yakwamba mwaka 2022 ulikuwa na baraka zake nyingi sana. Basi katika kuhesabu mibaraka yangu naweza sema huu nao ni moja ya mbaraka mkuu. Ni jambo ambalo lilinifurahisha zaidi 😍😍 Ni surprise niliyo wafanyia wazazi wangu.

Tarehe 25 mwenzi wa Saba, mwaka huu wa 2022 (07/25th/2022) ilikuwa siku ya furaha sana baada ya mipango yangu ya kuwafanyia wazazi wangu haswa mama yangu safari ya kuwasalimia bila ya kuwapa taharifa kama ilivyokua huko nyuma. Nimpango ambao nilipanga na mdogo wangu aitwaye Magreth Otieno Igogo a.k.a Mrs Jacob Massawe kuwa tutamfanyia mama surprise wakati wa siku yake ya kuzaliwa ambayo ni tarehe 27th July. Bahati mbaya ratiba yangu ilibidi nifike siku mbili kabla ya birthday yake. Mimi nilichukua likizo na kuandaa safari bila kumwambia mtu yoyote nyumbani isipokuwa mdogo wangu, mume wake na mwanangu tu. Sikutaka mama ajue kabisa hivyo kuzuia wanafamilia wengine kujua hata marafiki ilikuwa muhimu sana. Nashukuru Mungu kila kitu kilikwenda vizuri kama tulivyopanga tuliomba kibali cha Mungu kwa kumkabidhi mipango yetu naye akaibariki ikatimia. πŸ˜πŸ™πŸΏπŸ˜Safari yangu ilianzia Houston, Texas.

Nakumbuka siku nakwenda airport tulimpigia mama simu, akiwa nyumbani na baba na shangazi yetu fulani wakipiga story zao, nikaanza kumuuliza anampango gani na birthday yake?! Akawa anasema nahamu namtoko fulani amazing πŸ˜…πŸ˜… lakini ameshapanga kwenda Fun city na watoto wake wa shule (school trip). Nikamwambia kwautani nikikutumia Dola Mia ($100) uongezee kwenye hiyo trip itatosha? akasema itatosha sana. Nikamwambia basi nitakutumia tarehe 25, ambayo ndio tarehe nilikuwa najua naingia nyumbani. πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜… Basi nikamalizia kwa kumwambia wakifunga shule apange trip yeye na wadogo zake na dada zake waende kutembea Zanzibar au mbuga za wanyama, wafanye bageti halafu anijulishe. Akashukuru kweli kweli bila kujua mimi hapo naingia uwanja wa ndege teyari kwa kum-surprise! 😍😍

Sasa, ilikuhakikisha chumba changu kipo katika hali nzuri mdogo wangu alimdanganya mama kuwa ana wifi yake anakuja toka Japan na ana mtoto mdogo hivyo anaomba aandae chumba cha dada Alpha (eeh usishangae sana, nina chumba changu kwa mama yangu 😍😍) ili afikie humo kwa siku kadhaa kabla ya kwenda Moshi. πŸ˜…πŸ˜… mdogo wangu wanaishi nyuma tu na kwa mama. Basi mama naye bila shaka wala kinyongo akamkubalia pasi kujua mwenye chumba yupo njiani. πŸ˜…πŸ˜…Nilipofika airport nilipokelewa na mdogo wangu pamoja na mume wake. Tukiwa njiani mdogo wangu akampigia mama simu akamdanganya kuwa amekutana na rafiki yake walikuwa wote huko kijijini Kowak (kijiji alipozaliwa mama yetu), na anasema hawezi kwenda kwake mpaka afike kumsalimia. Mama akanza kuuliza ninani? mdogo wangu alikataa kata kata kusema akamwambia ni surprise akifika hapo itabidi asikilize sauti yake ili amtambue ni nani! Mama alimbembeleza sana amwambie ni nani huyo lakini mdogo wangu alishikilia msimamo kuwa utamuona wakifika. Mama kidogo akawa kama amechukia kwani alikua anasema unakuja na mgeni mimi hata kupika sijapika hata juice ndo kwanza wanatengeneza sio vizuri na hapendi kabisa. πŸ˜…πŸ˜… mdogo wangu hakubadilisha msimamo wake mpaka tukafika nyumbani, na mengine yote yamebaki kuwa historia kama hiyo video ya tukio hilo inavyo onyesha. πŸ˜…πŸ˜…

Hii ni mara ya pili sasa nafanikiwa kuwa-surprise wazazi wangu. Tarehe 07 mwezi wa tatu, mwaka 2017 kwa kushirikiana na wadogo zangu pamoja na baadhi wafanyakazi wa Utegi Technical Enterprises Ltd (kampuni anapofanyia kazi baba yetu) tulifanikiwa kum-surprise baba yetu ofisini kwake, ilikuwa siku ya birthday yake. 😍😍 Tuliwahi sana ofisini kabla yake kitu ambacho hajazoea kwani siku zote yeye ndio anakuaga wakwanza kufika. Tukaingia ofisini tukazima taa sehemu ya mapokezi ili akiwa kwa nje ajue hakuna mtu. halafu tukamwambia mlizi arudishie tu mlango asifunge na funguo, na geti arudishie bila kuweka kufuli ili akifika tu ashtuke na akasirike (just to annoy him) kuwa waliacha mlango na geti wazi jana jioni. Sasa alipofika mlangoni anakuta ipo wazi akasema ooh! Tumesha ibiwa hapa, hasira zikamshika kuwa geti halikufungwa jana jioni. Halafu mdogo wetu aitwaye Guka ndio tulimuacha nje awe ana mmonita (monitoring him) kwa kutupa taharifa kwa simu kuwa ameshafika kwa parking lot. πŸ˜…πŸ˜… Na Guka alikuwa anawasiliana na dereva kusema wapo wapi. πŸ˜…πŸ˜… Tazama video hapo chini πŸ‘‡πŸΏπŸ˜…πŸ˜…

Basi, alipopita tu mapokezi kuingia eneo la secretary wote tukasema “surprise” kwa nguvu na furaha huku mmoja wetu alikuwa kwenye switch ya kwashia taa, tukaanza kuimba “happy birthday to you” πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜ alishangaaje, hasira zote zikaisha hapo hapo. πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜… Hakuamini kuwa watu waliweza kuwahi kazini mapema hivyo ilitu wam-surprise! Alishukuru sana na furaha nyingi mno.

unaweza itazama video yote ya surprise kwa kupitia YouTube yangu hapo chini πŸ‘‡πŸΏ

Baba na mwana 😍

Kwakweli ni furaha kufanya jambo ambalo linamfanya mtu mwingine kuwa na furaha na kujisikia vizuri kwa kujiona mwenye thamani, lakini nifuraha zaidi kufanya jambo linalowafurahisha wazazi wako. Nafurahia na najisikia vizuri pale ninapoweza kuwafanya wazazi wangu wafurahi zaidi. Ni mbaraka wa pekee. 😍😍 Counting my blessings ma’am! πŸ˜…πŸ˜

Chumba cha dada Alpha

Na story zitaendelea maana mama Igogo alikuwa haamini alichokiona. 😍😍

Surprise ya mwisho iliharibika πŸ˜…πŸ˜… tulitaka dada yetu naye am-surprise mama lakini dakika za mwisho akaamua kumwambia kua anakuja halafu hata hakutuambia kuwa kamwambia mama hivyo ikawa surprise kwetu. πŸ˜…πŸ˜…πŸ™ˆπŸ™ˆ kwakweli hii ni the best moment for 2022.

Cecy-mama mzazi

Miaka takriban 3 iliyopita dada yangu naye alim-surprise mama big time. Alikuwa mjamzito na wakati uchungu umeanza akampigia mama kumsalimia basi wakaagana vizuri. Ndani ya masaa 2 mume wake anampigia mama simu kuwa mama Dani amejifungua mtoto wa kike na wameamua kumrithisha jina la mama. Mama akawa hataki kuamini anasema mbona mama Dani nimeongea naye muda sio mrefu? 🀣🀣🀣 akaambiwa pale anakupigia alikuwa ameshikwa na uchungu na tulikua njia kwenda hospitali. πŸ˜…πŸ˜… Na mtoto mwenyewe ndo huyo hapo πŸ‘†πŸΏ juu. 🀩🀩

Muhtasari wa matukio ya mwaka 2022 -sehemu ya kwanza.

Dec 2022

Mwaka 2021 niliufunga vyema na kuufungua 2022 vizuri sana. Namshukuru Mungu kwani umekua mwaka mwema sana wenye mibaraka mingi. Changamoto katika maisha hazikosekani kwani hatuwezi kujua tu imara kiasi gani kama hatutapitishwa katika changamoto hizo.

Daughter

Wanasema dhahabu au madini yoyote ya thamani hayapatikani juu ya barabara wala kando kando ya maji! Nilazima yachimbwe chini ya ardhi na yapitishwe kwenye moto mkali ndipo yawe haya madini tunayofurahia kuyaona. Hivyo, sikuzote tukipata changamoto tusikimbilie kusema “kwanini mimi?” Bali tumwambie Mungu najua hili ni darasa unanipitisha japo somo bado sijalielewa, naomba unipe HEKIMA ya kuweza kulielewa somo hili ili nifuzu mafunzo yangu vyema. Najua maumivu ninayopitia nikwaajili ya utukufu wako na mimi ndiye uliyenichagua kuwa kielelezo cha utukufu wako.

Basi kwa kusema hayo, naomba niweke kumbukunbu ya matukio yaliyozunguka maisha yangu mwaka huu wa 2022. Tukumbushane kushukuru katika kila jambo. Sikuzote tuhesabu mibaraka yetu kwani ni mingi mno sema tunafunikwa na upofu kwa kuangalia maisha ya watu wengine na kudhani kuwa wamebarikiwa kutuzidi. Hapana! Mungu anatubari sote kwa jinsi impendavyo yeye kwa wakati wake.

Hizi ni baadhi ya picha tulipiga mwanzoni mwa Dec 2021 tulikuwa maeneo ya tunako ishi karibu na NASA Space Center, Houston, Texas

Baadhi ya picha tulizopiga kwenye Christmas party 20021 iliyofanyika Hilton hotel, Houston, Texas.

2021 THC Thanksgiving Gala
April 2nd 2022

Mwenyezi Mungu alitubariki tukafurahia kuona mwanangu ameongeza mwaka mwingine. Ilikuwa siku ya Jumosi tarehe mbili mwezi wa Nne! Na zifuatazo ni baadhi ya picha ya siku hiyo.

Mama na mwana 😍

Happy birthday to me!

“Bwana ni mwema sana alitupa mibaraka ya mtoto wa kike usiku wa Alfajiri ya tarehe 26/06/1977 umekuwa mibaraka kwetu, umenifanya kutembea Merikani kama Queen Mungu asingetupa wewe ni nani angenipeleka kwa Hellen G. White, ni nani angenipeleka Washington DC nikaona ikulu ya Trump, ni nani angenifikisha Califonia nikaona Los Angeles, ni nani angenifanya nikaona HOLLYWOOD, na Golden Gate, umenifikisha Chicago, Michigan, Indiana, Houston, nimeona kaburi la mama Hellen G. White (Battle creek, Michigan). Kuishi kwako Merikani Mungu kanifuta machozi nami ninaongea kati ya wanawake. Ubarikiwe 100 times ningekuwa na uwezo ningekutumia nguo ya kuvaa leo lakini endelea kutuombea siku moja nami nikubariki mwanangu. Tunakupenda sana.” I LOVE YOU MORE Mama! ?❀

Blessed beyond measure! Forever grateful ???? #LovingFarther
thank you darling daughter! ?❀

Namshukuru Mungu kwa yote! Nimeuona mwaka mwingine. Happy birthday to me!

Nawatakieni kheri ya kufunga mwaka 2018 na baraka za kufungua mwaka 2019!

Katika mwaka 2018 kuna mambo mengi sana yametokea, mengine yalikuwa mazuri sana, mengine ya kuhuzunisha na mengine japo yalikuwa ni changamoto za kutesa moyo na hisia lakini yamezidi kutuimarisha sisi kama familia. Shetani alitujaribu sana lakini ametukuta tupo ngangari imani yetu kwa Muumba wetu haitetereki. Kwajinsi tulivyo pitishwa kwenye hayo majaribu ambayo makali yake yalikuwa kama makaa ya moto nabado tukaishika imani yetu!? Basi nina kila sababu ya kusema kuwa kamwe imani yetu haitokaa kutetereka kwani tumeuona mkono wa Mungu hatuto uwacha milele!Β 

Kama nilivyo amua kuishi maisha yangu kwamba siku zote nita ipa nguvu mambo ambayo yananipa furaha na sio huzuni. Basi kwa mwaka huu wa 2018 vitu vingi sana vimenipa hufura lakini hivi ni vilinipa furaha zaidi. Kutembelewa na mama yangu mzazi, wadogo zangu, na mama yangu mdogo hapa kwetu Houston, Texas ni mbaraka wa peke sana. Nina kila sababu ya kusema Asante kweli wewe ni Mungu! Nitalisifu jina lako milele!
Jambo lingine ambalo limenifurahisha sana mwaka huu ni ujauzito wa my best friend, a sister near and deer to my heart. Mungu amembariki mtoto wa kike na amemuita jina Mercy sawa na jina la mwanangu mimi. Kwakweli namshukuru Mungu sana kwa huu mbaraka. Tunaomba amlinde na amkuze mwanentu. Atupe hekima na busara za kuweza kulea vyema watoto wetu ??

Kila mtu huwa anafikiria tumbo lake kwanza!

Kila mtu anafanya kazi kwa kufikiria tumbo lake kwanza! Awe mfanya biashara, mwanasiasa, muajiriwa wa mahala popote pale au mwanaharakati wa jambo lolote lile wote kwa ujumla wao wanafanyakazi kwa kufikira matumbo yao kwanza! Na hakuna ubaya wowote kwani hizo ndio njia zao za kujipatia kipato ili waendeshe maisha yao.Β Huu ni ukweli ambao hauwezi pingika, ndio maana hakuna mtu atajiita mwanaharakati wa jambo fulani akaamua kupigania hicho anachokiamini kwa kutumia pesa zake mwenyewe na muda wake bila kujali ananufaika na nini! Wote wana angalia maslahi binafsi kwanza!

Mwanasiasa ili aweze linda cheo na maslahi yake lazima afanye kazi yake ya kuwatumikia jamii kwa nguvu zote. Mwanaharakati ili apate pesa kutoka kwa sponsors lazima apige kelele nyingi sana kuwashawishi watu kua anachokipigania ni sahihi. Mfanyakazi aliye ajiriwa ili adumu katika kazi yake lazima aongeze elimu na ufanisi kazini. Mfanya biashara ili azidi kukua na biashara yake idumu lazima aangalie jinsi ya kuongeza faida!Β Hivyo, hakuna mtu hapa duniani atafanya kazi bila kufikiria tumbo lake kwanza. Hata Mungu amesema, asiyefanya kazi naasile! Hata Wachungaji wanalipwa mshahara!

Ukikubali kuwaongoza lazima wakuhoji!

Kuhojiwa kwa vingozi wa jamii zinazo tuzunguka siyo jambo la kushangaza au la ajabu kwani halikuanza leo wala jana.Β Ukichukua mamlaka ya kuongoza watu basi lazima uwe teyari kuhojiwa kwani wana haki ya kufanya hivyo. Japo saa nyingine wanaokuuliza wanaweza wakakukwaza na maswali yao lakini kama kiongozi unakuwa hauna haki ya kuwakataza au kuwazuia kukuhoji pale wanapojisikia kufanya hivyo.

Kunawengine wanaweza kuhoji siyo kwamba hawajui ukweli, la hasha! Ni watu wenye ajenda zao mbovu, hivyo watakupa maswali ambayo wanajua majibu yake lakini wewe kama kiongozi inabidi utumie hekima yako kuwajibu na kutoa ushahidi ikabidi.

Kwa mfano, tunaona jinsi Yesu alipokuwa jangwani akifunga na kuomba, shetani alimuhoji β€œ....kama wewe ni Mwana wa Mungu, amuru jiwe hili liwe mkate.” Yesu akamjibu, β€œImeandikwa: β€˜Mtu haishi kwa mkate tu.’” Yesu alimjua huyu ni Shetani lakini kwakua alikuja kuwakomboa watu wote hivyo alitumia hekima yake ya juu kumjibu, bika kumzuia kumuhoji.Β 

Shetani aliendela kumuhoji Yesu kwa siku arobaini ambazo Yesu alikuwa Jangwani. Embu tafakari, pamoja na Yesu kushinda na njaa kila siku lakini bado Shetani alikuwa mbele ya uso wake akimpa maswali kila siku na Yesu akamuacha amuhoji. Siyo kwamba alishindwa kumnyamazisha Shetani au kumfukuza, hapana! Alimuacha Shetani atumie uhuru wake! Nayeye kama Mfalme atatumia hekima na mamlaka yake kumjibu.

Watu wenye tabia kama hizi za Shetani wapo miongoni mwetu na katika kila jamii. Niwajibu wa viongozi wetu kujua kua wapo kutumikia watu wa aina zote waliopo ndani ya jamii husika, hivyo hata wakija na maswali ya kukebehi au kukera ni wajibu wao kuwajibu kwa kutumia hekima na mamlaka waliyo nayo. Si busara kutishia watu wanapohoji viongozi, hekima itawale siku zote.

Mungu atusaidie.

Mungu ndiye muhasisi wa #Democracy

Demokrasia ni mfumo ulio hasisiwa na Mungu Mwenyezi. Mungu alikuwa mtu wakwanza alieanzisha Democracy pale kwenye bustani ya Edeni. 

Pamoja na kumpenda mwanadamua sana, na akampa masharti ya jinsi ya kuishi katika bustani ile ya Edeni lakini alimpa Adamu Uhuru wa kuchagua #Democracy kati ya mema na mabaya. Adamu alitumia uhuru wake kufanya maamuzi aliyo yafanya. 

Mimi huwa siku zote nasemaga sina "role model" ambaye natamani kuwa kama yeye isipokuwa Yesu mwana wa Mungu. Huyu ndio "role model" wangu siku zote, natamani kuwa kama Yesu na si mwanadamu mwenzangu. Don't get confused, kuna watu wengi sana wana ni inspire au motivate katika mambo mbalimbali na mtu wa kwanza au watu wakwanza kabisa ni Wazazi wangu! 

Kwanini Yesu ni "role model" wangu? Kwasababu, Yesu alitumwa na Mungu kuja kutuonyesha jinsi gani ya kuishi maisha yetu hapa duniani, siyo tu kiroho, kiakili, kiafya, na kimwili. Yesu alizaliwa kama mwanadamu mwingine yeyote yule, aliishi maisha yake kama mwanadamu, na alikufa kama mwanadamu. 

Hivyo, ametuonyesha ni jinsi gani tunaweza ishi na watu ambao hawana mtazamo wa mawazo kama sisi. Ametuonyesha jinsi gani tunatakiwa kuwapa watu uhuru wa kuamua nini wanataka nakuheshimu maamuzi yao hata kama hatukubaliani nao. Ndio maana Yesu alishiriki katika sherehe za harusi za ndugu zake na marafiki ambao walikuwa ni walevi japo Yeye binafsi si mlevi. #Democracy ilitumika! Alihubiri injili ya neno la Mungu lakini hakuwatenga au kuwachukia walio ikataa! Again, #Democracy ilitumika.

Shetani alikuwa mmoja wa Malaika waimbaji wakuu Mbinguni lakini alitumia uhuru wake na kufanya maamuzi kwa kutumia kiburi kumdharau Mungu. Na akachagua kuja duniani kutengeneza majeshi yake kama yanavyo onekana katika tabia za watu mbali mbali.

Kwa kumalizia, nasema mtu yeyote yule anayependa kuwapa watu #DemocracyΒ  basi atakuwa anatabia za 'kimbingu'! Kila mtu anahaki ya kuwa huru kufanya kile apendacho ilimradi hawaingilii uhuru, privacy za watu wengine au kuvunja sheria ya nchi husika. Demokrasia ni rahisi sana kuisema lakini kuitekeleza ni ngumu sana.Β  Mungu atusaidie!

Kunawakati utafika itabidi uwe mwenyewe…!

Je, umeshawahi kukutwa na hali kama hii? Hali ya kujishusha zaidi ya mtoto ili tu uweze kuwa na mtu au watu fulani katika maisha yako? Hali ya kujishusha  thamani yako na saa nyingine kupoteza utu wako ili tu fulani au kundi fulani likupende? (comprising your morals and values, loosing who you are for the sake of afraiding being alone). Kuna wengine mpaka wana acha kupigania ndoto zao kwasababu wanaona watapoteza baadhi ya watu katika maisha yao. Wengine wanaishi maisha ambayo siyo ya hualisia ili tu kuwafurahisha watu fulani ili waendelee kua kwenye maisha yao!Β Nikitu kibaya sana kama unaweza kupoteza nguvu uliyonayo ndani yako ambayo umepewa na Mungu eti kwasababu ya kutaka kukubalika na watu fulani au kwasababu unaogopa kutembea mwenyewe kwenye maishai yako. Duniani hapa kila mmoja amepangiwa safari yake na Mwenyezi Mungu, na wengine huwenda tumepangiwa safari zetu kuwa tutembee wenyewe sasa basi ukiona kama unapoteza hualisia wako na utu wako kwasababu ya kitu au mtu fulani au watu fulani, basi jua kua safari yako umepangiwa kutembea mwenyewe! Don't ever  sacrifice your happiness, morals, values, dignity, humanity kwasababu tu yakuogopa kutembea mwenyewe. Β Majasiri siku zote wanatembea wenyewe! Wanaweza wakachukua muda mrefu kufika lakini atafika akiwa salama na kwa ujasiri. Usiogope! Maana lazima kunawakati utafika itabidi tu uwe mwenyewe, anza sasa kabla hujachelewa ukaja sema "laiti ningelijua"! Usilazimishe mambo!  Anza safari mengine muachie Mungu!


	

Wanaopenda kushangaa ndio wajanja!

Baadhi ya watu haswa sisi Watanzania huwa tunatabia yakutokupenda kuwa wadadisi wa jambo au mambo matokeo yake our ignorance is very High!Β 
Yani tupo radhi tuamini katika uongo au majungu / umbea kuliko kuchukua muda wako na kukisoma / chunguza kitu wewe mwenyewe ili uwe na huwakika wa kile unachokiongea. Utakuta mtu anahadithia kitu wewe utaamini ni kweli ameiona mwenyewe kwa macho yake au amesikia yeye mwenyewe kwa masikio yake kumbe naye kasimuliwa na rafiki yake ambaye nae huyo rafiki kasimuliwa na mtu mwingine ?‍♂️?‍♂️

Hiii no karai ya Chicago

Hii tabia kutopenda kuchukua muda wetu na kujifunza jambo fulani au kufatilia habari fulani bila ya wewe kuweka uongo wowote ndio imefanya Watanzania wengi wanapenda majungu sana, wanaamini ili uweze fanikiwa basi lazima umuharibie mwingine haswa kama yupo kwenye biashara au jambo ambalo na wewe unafanya! Inasikitisha sana kwani kwa hii tabia maendeleo ya taifa letu yatahitaji dictator!!  Juzi niliamua kwenda kuangalia hili 'karai' kubwa ambalo limeletwa hapa Houston, Texas kwenye chuo cha sanaa. Hili karai limetengenezwa Ulaya likaletwa hapa. Ni urembo wa aina unao vutia sana.  Katika mji wa Chicago nao wanao 'karai' kama hili limetengenezwa na mtu mmoja. Ila la Chikago limeinamishwa (kama inavyo onekana kwenye picha ya pili kutoka juu) hivyo watu wanaweza ingia katikati ya hili 'karai' nakupiga picha nzuri sana kama anavyoonekana mwanangu hapo pichani ☝ na pia tizama picha ya mama yangu na mdogo wangu hapo chini ?
Hizo picha zilipigwa miaka 6 iliyopita kwenye hilo karai la Chicago. Kwa maoni yangu binafsi mimi napenda ya Chicago zaidi kwani imewekwa vizuri kwa watu kupiga picha na kitendo cha kulazwa chini imefanya hiyo sehemu iliyoingia ndani kuwa sehemu ya kivutionzaidi cha kupigia picha. Halafu maua na urembo ulioko pembezoni unahakisiwa na hiyo karai ambayo pia nikivutio.
Nilichotaka kuwaambia Watanzania wenzangu ni kuwa usiogope kushangaa! Hakuna njia nzuri ya kujifunza kitu kama kushangaa. Tena ukimpata mtu anayekupa maelezo basi wewe zidisha kushangaa ili akupe maelezo zaidi. Wanaopenda kushangaa ndio wajanja!

Je, unaheshimu mali za watu?!

Alpha Igogo, blogger Throw ? 2008

Mimi naheshimu sana kitu cha mtu yoyote yule! Yani mtu akiniazima kitu au kunipa kitu huwa nakitunza zaidi ya chakwangu! Naonaga mpaka mtu kutoa kitu chake kakupa au kukuazima inamaana sio tu amekuheshimu bali anakuamini! Trust is essential to me! Nina picha nilipewa na wanafunzi wenzangu Kowak Girls secondary school hizo picha mpaka leo ninazo hapa Marekani, sidhani hata kama wao wanakumbuka! Hivyo ndivyo nilivyo mimi! Na huwa nachukizwa sana nikiona mtu haeshimu kitu cha mtu mwingine kwani inaonyesha wewe unaweza kuwa na vielement vya tabia za kichawi chawi ???

Sasa jana jioni nilikuwa natafuta kitu kwenye closet (ambapo kuna washer and dryer sio kwenye nguo) nikakutana na hii GPS! Yes that how GPS monitors used to be ?? Wahenga mtatujua tu! ? ?Hii GPS niliazima kutoka kwa my good friend aitwae Sammy mwaka 2009. Alikuwa akihiitaji nampelekea nami ikitokea nahitaji naifata au ananiletea. Mwishowe ikaishia kwangu. Kusahau na mambo kuwa mengi sikufanikiwa kumrudishia.

Lakini kwakuwa nilijua niliazima sikupewa moja kwa moja miaka yote nimejisikia kuwa na wajibu wa kuitunza mpaka hapo nitakapo mpa tena. Believe me, nilipokuwa nahama Michigan to Texas, niliipaki vizuri nikaja nayo ?? nimeihifadhi vizuri sana mpaka stand yake ipo ? nafikiri it’s about time kumrudishia mwenye GPS yake akitaka kuitupa aitupe mwenyewe! Sindioo au niendelee kumtunzia kama yeye alivyokua akinitunzia vya kwangu ????Β #HeshimuVyawatuZaidiYaChako

#NiMchezoWakutunzianaTu

 

 

Where is my babysister?

Yuko wapi Jokate wangu? Jojo, where are you at? Hope all is well with you, don't let those haters take you down baby gal!Β Β Just give me Β some days I will destroy them like tornado ? Seriously nawauliza waungwana where is my babysister at? Sipendi! Sipendi! @ brother Paul Makonda can you kindly check on my babysister please? Kamanda Sirro, where is Jokate Mwegelo?? Jamani this ain't funny!Β Jojo, just know I love and missing you. Come back please!Β ??

Kuna watu ambao wapo hatarini kufutiwa uraia wa Tanzania!

Hii ni kwa wana Diaspora wenzangu tu wengine someni halafu mpite kimya! Kabla hamjaweka miguu yenu barabarani kwenda huko mnako kwenda naomba kwanza uhakiki uraia wako. Je, wewe bado ni Mtanzania au ulisha ukana uraia wako? Kumbuka Tanzania haina Dual citizenship! Na kama bado wewe ni raia wa Tanzania je, umeshaagana na ndugu zako kwamba hata kama hamta onana tena basi iwe hivyo na kuwa ni salama rohoni mwako?!Β Maana unaweza usiwaone tena, siyo kwasababu ya kifo hapana, kwasababu huwezi kukanyaga ardhi ya Tanzania!Kwanini nimesema haya niliyo yasema, ni kwasababu ninaona dalili za baadhi ya watu kuja kufutiwa haki yao ya kuzaliwa kama Mtanzania (uraia wao kufutwa kabisa) na wengine ambao walisha ukana Utanzania wanaweza kuwekewa "Red flag" na wasiruhusiwe kukanyaga Tanzania for a very long time! Sounds like a joke, huh! Wrong! This is not a joke so kindly take it very seriously!! Kumbuka ofisi ya Rais ni tasisi inayo jitegemea ambayo inauwezo na mamlaka ya kufanya hivyo pale watakapokuwa na sababu tosha kufanya hivyo!Β 

Vile vile kumbuka kuwa Rais ndio mtu peke anaweka signature kwenye Hati Miliki ya viwanja na pia anauwezo wa kuifuta na kuweka majina ya wamiliki wapya, hivyo kua muangalifu na maamuzi yako. Ukitaka kupambana na serikali lazima uwe umejipanga uwe na plan A to Z! Siyo plan A, B, sijui na C hapana! Uwe na plan zooote intact!!  Nimewatolea siri tusije laumiana huko mbele ? Otherwise, nawatakieni matembezi mema kwa wale mtakao kwenda matembezi ? #NotWorthIt

Watoto wa mwenye haki! Zaburi 37:25-26

Zaburi 37: 25-26 :-

“25 Nilikuwa kijana na sasa ni mzee;

kamwe sijaona mwadilifu ameachwa na Mungu,

au watoto wake wakiombaomba chakula.

26 Daima huwapa wengine kwa furaha na kukopesha,

na watoto wake ni baraka.”
❀
❀
❀

Psalms 37: 25 -26 :-

“25Β  I have been young, and now am old,

yet I have not seen the righteous forsaken

or his childrenΒ begging for bread.

26Β  He is ever lending generously,

and his children become a blessing.”

Hello there…….!

Β Hello wasomaji wangu, mambo ni aje! Kumepooza humu eeh? Msijali, simnajua mkiona kimya jua ratiba imegoma, majukumu na kubeba mabox basi ni shida tupu ??....... Nitarejea! Kaeni teyari kwa kuifurahia Hottest And Best Couple ya 2018! Simnajuaga mie sibabaishagi? Basi nitawaletea couple nyingine ya ukweli mtaipenda!....... Haya muwe na wiki njema mpigie picha hizo za  Valentine week Β muwarushe roho wenye mapenzi fake ???

Some people need Jesus not you!

Usitake kujifanya wewe ni Yesu mwana wa Mungu kwa kujifanya “shujaa ushwara” wa kubeba mizigo ya watu ambao hawabebeki! Hata Yesu yalipomfika akaona kikombe hakibebeki alimuomba Baba yake kuwa “Baba yangu, ikiwezekana kikombe hiki kiniepuke”!! Some people need Jesus not YOU!! Β Β 

Mzaha, mzaha, hutumbua usaha!

Katika maisha kuna vitu vya kufanyia mzaha na vingine usijaribu hata siku moja! Kitu chochote kinacho husisha HISIA za mtu usifanyie mzaha hata siku moja! Kumbuka hisia za mtu ndizo zinazomfanya huyo mtu kuwa mtu, sasa kuzichezea hisia za mtu kwanza ni unyanyasaji wa hali ya juu, pili unaweza kuleta madhara makubwa sana kwa muhusika ambayo saa nyingine yanaweza sababisha kifo! Siku zote kumbuka Β "mzaha, mzaha utumbua usaha"!Β Naomba niongee na watoto wa kike kwa hili, ogopa sana mwanaume anayekufanyia vituko halafu badala ya kukuomba msamaha anakimbilia kwa ndugu na marafiki zako kujisafisha kuwa alikuwa anatania tu au kukufanya wewe uonekani ni mtu ambaye ni tabu to get along with! Kama hujaoana na huyo mtu basi kaa naye mbali kabisa kwani huyo mtu ni MNYANYASAJI! Na anachokifanya hapo ni kuweka mazingira mazuri ya kukunyanyasa pindi atakapo kuoa na wewe usiwe na pakukimbilia kwani amesha "brainwashed" watu wako wakaribu kuwa wewe ni hard personal to get along with au wewe ni mtu unayechukulia kila kitu too seriously!!Β 

Mtu anayecheza na Β hisia zako bila ya huruma huyo mtu ni wakuogopa kwani hisia za mtu siyo jambo la kuchezea! Halafu unapo taka kuliongelea wewe ndio mtu mbaya?! Kwa mfano, eti mtu anakudhalilisha kwa kupiga picha na mwanamke aliye zaa naye au mwanamke aliyekuwa akimdeti kabla yako nakuweka hizo picha kila kona za media halafu anasema "was just a joke"?! Tena anafanya hivyo zaidi ya mara moja? My friend, mkimbie huyo mwanaume kama unavyoweza kukimbia kifo! Unless unataka kuwa "celebrity" basi utakubaliana na unyanyasaji huo simnamuona Zari anavyo fanyiwa na Diamond?? Ndo Ucelebrity huo ??? No! Ain't Zari! I'm just a normal girl from KekoJuu who deserves love, respect, and happiness ??  Au kwa mfano, mlisikia ile mvua kubwa iliyonyesha hapo Dar es salaam Β ambayo ikasababisha maafa makubwa sana na watu kupoteza maisha? Sasa wewe ndio mwanamke unaishi Dar es salaam, maeneo ya Jangwani, halafu mwanaume yupo Morogoro cha ajabu hata kukupigia simu kujua kama upo salama au umekufa hakuna! Tena unamuona yupo online akifanya yake? Then mtu huyu akisema anakupenda wewe Β mtoto wa kike bado unamuamini?!! ??? Unless you want to marry your killer ndio utakubaliana na huo upuuzi kwani wanaume wa hivyo hakuheshimu wewe wala mahusiano yenu! Mwanaume wa hivyo hakujali wewe wala roho yako! Yani kifo chako hakimsumbui!Β 

Ukiyakubali mambo kama hayo kabla hujaolewa halafu ukaja olewa na huyo mtu basi tegemea hizo tabia ataendelea nazo mpaka ndani ya ndoa yenu na hautakuwa nalakusema! Atakapo sema mbona hayo nilikufanyia kabla ya ndoa na ukakubali kunioa utasema nini?! Au mfano mwingine, mwanaume anataka kukuoa wewe lakini mipango ya maisha yenu anaongea na watu wengine bila kukuhusisha?! ?? What does that tell you? You are just going to be a "trophy wife"!! definitely that is not a man to have family with!! Ipo siku atataka kukutoa roho yako halafu atasema alikua anataka kuona how will you react!! Emotional abuse siyo kitu cha kufanyia mzaha hata kidogo kwani mzaha, mzaha hutumbua usaha!

Nawatakieni kheri katika kufunga mwaka na neema za mwaka mpya!

Wapendwa wasomaji wangu, ndugu jamaa, na marafiki, katika haya masaa machache yaliyobakia kumaliza mwaka huu wa 2017 napenda kuwatakia kheri katika kufunga mwaka na pia nawaombea neema na baraka zote za mwaka mpya ziwashukie na kukaa nanyi siku zote! Β Β Blog hii nili register rasmi tarehe 15th Dec, 2015 hivyo mpaka sasa ninakuwa nimetimiza miaka miwili na wiki kama mbili hivi! Mwaka wa kwanza nilifanya vizuri sana tena sana! I was very proud of myself! Mwaka wa pili niliyumba kidogo kwasababu "vidudu mtu" wale mafundi wa majungu na fitina wakaingilia kati! Hivyo kimaendeleo ya blog sikufanya vizuri japo wasomaji wangu wameongezeka kwa zaidi ya 300%++ ukilinganisha na mwaka wa kwanza Β Wanasemaga 'adui' ukimjua hakusumbui kichwa! Basi nami nashukuru kwa nafasi waliyonipa kwani nimewajua! Hawaniumizi kichwa, kwanza hata nguvu ya kusimama mbele yangu hawana! Wanajua sentence yangu moja inawatosha kuwapa "heart attack" ??Β  hawana uwezo wa kuniangusha mimi wamebakia kupiga majungu behind my back, and definitely that is where they belong "behind my back" I hope I "smell"  good enough to make them stay there forever ?? Siwapi nafasi tena! Yani huwezi amini wengine mpaka nacheka nao lakini akili kwa kichwa ati!! Β 2018 narudi kwenye mstari! Nawahaidi mambo mazuri kama yale ya mwaka wa kwanza! Tutajifunza na kucheka sana! Life is too short embu tujifurahie siye!.....Malengo yangu ni kwamba kila miaka 5 na make major move, lakini kama nitaweza kufanya hizo major move kabla ya miaka 5 nitashukuru sana! Just pray for me as I pray for you na sote tubarikiwe! Ukiona mapungufu yangu chukulia kama "fursa" kwako, kwani hata mimi niliona mapungufu ya wengine nikaona ni "fursa" yangu! Hivyo siku zote jifunze kutokana na makosa ya wengine siyo lazima yakukute wewe!Β Safari yangu ya kupunguza uzito! ?? Japo siwataharifu kila wiki kama nilivyo haidi lakini bado iko pale pale. Na ninepungua, sema lile tumbo la chini ndio bado?? Niliacha kuwapa progress kila wiki kwani ilikuwa inanikatisha tamaa kuona wiki nzima napungua 1Lb?? nikaona bora nifanye mazoezi na diet kimya kimya ikifika mwezi wa 5 mwakani nawapa report iliyo kamilika! Β  Nimepungua toka size 16 na 18 mpaka 12 na kuna nguo moja ndio 14, nafikiri inategemea na deaigner na material iliyotumika!Β Namshukuru Mungu kwa mambo mengi sana, na moja ya jambo ambalo ameweza kunibariki nalo mwaka huu ni kuonana na ndugu zangu. Miezi minne ya mwanzo mwaka huu nilikuwa Tanzania, nashukuru nimeweza kuonana na ndugu zangu wote! Mara nyingi nikiwa likizo kutoka na sababu za shule baadhi yao walikuwa nje ya Tanzania hivyo tulikuwa hatuwezi kukutana pamoja kwani ratiba zilikuwa tofauti sana. Mimi huwa siendi nyumbani mara kwa mara unless kuna kitu cha lazima ndio maana huwa nikienda nakaa miezi 3+! Mara nyingi kila baada ya miaka 2 ndio nakwenda.Β Kama kuna kitu nilifurahiya nilipo kuwa nyumbani ni kuwepo wakati wa birthday ya baba yangu! Miaka yote huwa na miss hii siku! Lakini safari hii Mungu alinibariki nilikuwa nyumbani na mimi ndio nilikuwa "master mind" behind hiyo surprise ??Β Mimi hapa ndo huyo nimeshika camera ??Β Kama kuna kitu namshukuru Mungu siku zote na nitamshukuru mpaka nakwenda kaburini ni zawadi ya hichi ? kiumbe! Sijui na wala sitaki kujua maisha yangu yangekuaje bila mwanangu! Mungu zidi kunilindia na kumbariki mtoto wangu!Β Jamani, nisiwachoshe na maneno mengi ?? Namshukuru Mungu kwa yote! Nawatakieni kheri ya kufunga mwaka na baraka na neema zote za mwaka mpya ziwashukie na kukaa nanyi! Happy New Year everybody! Love you all!