Nawatakieni kheri katika kufunga mwaka na neema za mwaka mpya!

Wapendwa wasomaji wangu, ndugu jamaa, na marafiki, katika haya masaa machache yaliyobakia kumaliza mwaka huu wa 2017 napenda kuwatakia kheri katika kufunga mwaka na pia nawaombea neema na baraka zote za mwaka mpya ziwashukie na kukaa nanyi siku zote!   Blog hii nili register rasmi tarehe 15th Dec, 2015 hivyo mpaka sasa ninakuwa nimetimiza miaka miwili na wiki kama mbili hivi! Mwaka wa kwanza nilifanya vizuri sana tena sana! I was very proud of myself! Mwaka wa pili niliyumba kidogo kwasababu "vidudu mtu" wale mafundi wa majungu na fitina wakaingilia kati! Hivyo kimaendeleo ya blog sikufanya vizuri japo wasomaji wangu wameongezeka kwa zaidi ya 300%++ ukilinganisha na mwaka wa kwanza  Wanasemaga 'adui' ukimjua hakusumbui kichwa! Basi nami nashukuru kwa nafasi waliyonipa kwani nimewajua! Hawaniumizi kichwa, kwanza hata nguvu ya kusimama mbele yangu hawana! Wanajua sentence yangu moja inawatosha kuwapa "heart attack" ??  hawana uwezo wa kuniangusha mimi wamebakia kupiga majungu behind my back, and definitely that is where they belong "behind my back" I hope I "smell"  good enough to make them stay there forever ?? Siwapi nafasi tena! Yani huwezi amini wengine mpaka nacheka nao lakini akili kwa kichwa ati!!  2018 narudi kwenye mstari! Nawahaidi mambo mazuri kama yale ya mwaka wa kwanza! Tutajifunza na kucheka sana! Life is too short embu tujifurahie siye!.....Malengo yangu ni kwamba kila miaka 5 na make major move, lakini kama nitaweza kufanya hizo major move kabla ya miaka 5 nitashukuru sana! Just pray for me as I pray for you na sote tubarikiwe! Ukiona mapungufu yangu chukulia kama "fursa" kwako, kwani hata mimi niliona mapungufu ya wengine nikaona ni "fursa" yangu! Hivyo siku zote jifunze kutokana na makosa ya wengine siyo lazima yakukute wewe! Safari yangu ya kupunguza uzito! ?? Japo siwataharifu kila wiki kama nilivyo haidi lakini bado iko pale pale. Na ninepungua, sema lile tumbo la chini ndio bado?? Niliacha kuwapa progress kila wiki kwani ilikuwa inanikatisha tamaa kuona wiki nzima napungua 1Lb?? nikaona bora nifanye mazoezi na diet kimya kimya ikifika mwezi wa 5 mwakani nawapa report iliyo kamilika!   Nimepungua toka size 16 na 18 mpaka 12 na kuna nguo moja ndio 14, nafikiri inategemea na deaigner na material iliyotumika! Namshukuru Mungu kwa mambo mengi sana, na moja ya jambo ambalo ameweza kunibariki nalo mwaka huu ni kuonana na ndugu zangu. Miezi minne ya mwanzo mwaka huu nilikuwa Tanzania, nashukuru nimeweza kuonana na ndugu zangu wote! Mara nyingi nikiwa likizo kutoka na sababu za shule baadhi yao walikuwa nje ya Tanzania hivyo tulikuwa hatuwezi kukutana pamoja kwani ratiba zilikuwa tofauti sana. Mimi huwa siendi nyumbani mara kwa mara unless kuna kitu cha lazima ndio maana huwa nikienda nakaa miezi 3+! Mara nyingi kila baada ya miaka 2 ndio nakwenda. Kama kuna kitu nilifurahiya nilipo kuwa nyumbani ni kuwepo wakati wa birthday ya baba yangu! Miaka yote huwa na miss hii siku! Lakini safari hii Mungu alinibariki nilikuwa nyumbani na mimi ndio nilikuwa "master mind" behind hiyo surprise ?? Mimi hapa ndo huyo nimeshika camera ?? Kama kuna kitu namshukuru Mungu siku zote na nitamshukuru mpaka nakwenda kaburini ni zawadi ya hichi ? kiumbe! Sijui na wala sitaki kujua maisha yangu yangekuaje bila mwanangu! Mungu zidi kunilindia na kumbariki mtoto wangu! Jamani, nisiwachoshe na maneno mengi ?? Namshukuru Mungu kwa yote! Nawatakieni kheri ya kufunga mwaka na baraka na neema zote za mwaka mpya ziwashukie na kukaa nanyi! Happy New Year everybody! Love you all!

Leave a Reply