My son enjoying his New Year breakfast!

Yaas! That is my son! Enjoying his New Year breakfast in Nairobi. At age 2 1/2 he got all his table manners in place ?? way to go son! Wasichana itabidi wajipange sana tu! Kama hawakufunzwa ustarabu na mama zao wakwende huko hatuwataki sisi ?? We are raising a gentleman right here I hope someone is raising a Queen for him ??  maana Mimi mama mkwe nitamkagua kabla hajaingia ndani ya nyumba ya mwanangu ??? chezea mama mkwe wa dotcom! Kama tunataka tuondoe unyanjasaji na ukiritimba kwa wanawake inabidi wakina mama muwe teyari kulea vijana wenu katika maadili, na mambo yanayofaa! Na mambo hayo huanzia katika umri huu! Usisubiri akifika sijui miaka 6 that is way too late! Pia watoto wakike muwafunze tabia njema, kujithamini, good touch and bad touch mara tu wanapojua kuongea na kutembea! Usingoje mtoto sijui aote maziwa ndio unaanza "kubwabwaja"!! Kama tunataka ukombozi wa mtoto wa kike na mabadiliko ya tabia za wanaume wa Kiafrika basi wakina mama lazima mkubali kubadilisha tabia ya malezi yale ya kizamani kuwa mtoto wa kiume ni "King" na mtoto wa kike ni "servant"!! Kuwa mtoto wakiume haitaji kupewa malezi yenye maadili ya jinsi ya kuwa kaka, baba, mume, na raia mwema isipokuwa toto wa kike tu! Yeye ndiyo anatakiwe afunzwe kuwa dada mwema, mama mzuri, mke bora, na raia mwema,  swali linakuja awe mwema kwa nani?!! Mwaume mbakaji? Au mwanaume katili? Au a cold-hearted killer? Au mwanaume mnyanyasaji asiye hata na chembe chembe ya hofu ya Mungu?!! Mothers I'm raising my gentleman because I don't want him to be part of that ugly statistic!!What about you!! .........Happy New Year everybody!

Leave a Reply