Category Archives: Tanzania

Muhtasari wa matukio ya mwaka 2022 -sehemu ya kwanza.

Dec 2022

Mwaka 2021 niliufunga vyema na kuufungua 2022 vizuri sana. Namshukuru Mungu kwani umekua mwaka mwema sana wenye mibaraka mingi. Changamoto katika maisha hazikosekani kwani hatuwezi kujua tu imara kiasi gani kama hatutapitishwa katika changamoto hizo.

Daughter

Wanasema dhahabu au madini yoyote ya thamani hayapatikani juu ya barabara wala kando kando ya maji! Nilazima yachimbwe chini ya ardhi na yapitishwe kwenye moto mkali ndipo yawe haya madini tunayofurahia kuyaona. Hivyo, sikuzote tukipata changamoto tusikimbilie kusema “kwanini mimi?” Bali tumwambie Mungu najua hili ni darasa unanipitisha japo somo bado sijalielewa, naomba unipe HEKIMA ya kuweza kulielewa somo hili ili nifuzu mafunzo yangu vyema. Najua maumivu ninayopitia nikwaajili ya utukufu wako na mimi ndiye uliyenichagua kuwa kielelezo cha utukufu wako.

Basi kwa kusema hayo, naomba niweke kumbukunbu ya matukio yaliyozunguka maisha yangu mwaka huu wa 2022. Tukumbushane kushukuru katika kila jambo. Sikuzote tuhesabu mibaraka yetu kwani ni mingi mno sema tunafunikwa na upofu kwa kuangalia maisha ya watu wengine na kudhani kuwa wamebarikiwa kutuzidi. Hapana! Mungu anatubari sote kwa jinsi impendavyo yeye kwa wakati wake.

Hizi ni baadhi ya picha tulipiga mwanzoni mwa Dec 2021 tulikuwa maeneo ya tunako ishi karibu na NASA Space Center, Houston, Texas

Baadhi ya picha tulizopiga kwenye Christmas party 20021 iliyofanyika Hilton hotel, Houston, Texas.

2021 THC Thanksgiving Gala
April 2nd 2022

Mwenyezi Mungu alitubariki tukafurahia kuona mwanangu ameongeza mwaka mwingine. Ilikuwa siku ya Jumosi tarehe mbili mwezi wa Nne! Na zifuatazo ni baadhi ya picha ya siku hiyo.

Mama na mwana 😍

NAILILIA KAGERA (BUKOBA) YA WAJUKUU ZANGU-Peter Sarungi

fb_img_1473861345540
Peter Sarungi

Mimi babu yenu Peter Sarungi kutoka Mkoani Mara wilaya ya Rorya wa kabila la kimataifa la LUO, naandika salamu hizi kwa masikitiko makubwa na huzuni nyingi kwa janga la tetemeko lililowakumba wajukuu zangu. Najua mpo katika huzuni kubwa na inawezekana janga hili limewatonesha vidonda na majeraha makubwa mliyowahi kuyapata miaka ya nyuma, vidonda vilivyosababishwa na MV Bukoba, Vidonda Vilivyosababishwa na Vita vya Idd amin dada na Vidonda vilivyosababishwa na Chimbuko la ugonjwa wa UKIMWI. Hakika majanga haya yameacha vidonda na alama ya huzuni kwa wajukuu zangu kwa kuondokewa na wapendwa wenu wengi mliowategemea na kuwapenda. Niwatie moyo kwa kusema kuwa mimi Babu yenu nawaombea kwa Mungu awafariji na kuwavusha salama kutoka katika kipindi hiki kigumu na awasamehee, kuwalinda na kuwaepusha dhidi ya majanga mengine.

Nawapenda sanafb_img_1473861327089Mungu azilaze roho za wapendwa wajukuu zangu mahala pema peponi…Amin.

Historia imeandikwa: Kupatwa kwa jua, Rujewa, Mbeya, Tanzania

Screenshot_2016-09-01-11-12-46-1Siku ya leo (masaa ya Africa Mashariki) tarehe Mosi September, 2016 historia imeandikwa ndani ya  Rujewa, Mbeya, Tanzania ambapo tukio kubwa duniani la kupatwa kwa jua (Sun/Solar eclipse) limetokea. Soma  ?  KupatwaKwaJua2016  ili ujifunze zaidi! FB_IMG_1472746320110FB_IMG_1472746326305Watu wengi sana walijitokeza kushuhudia. Nitukio la kisayansi lenye faida nyingi kwa nchi yetu kihistoria, kiuchumi, na kiutalii! Tuna kila sababu ya kujivunia!  ??

Picha shukrani kwa Clouds FM