Category Archives: General education

Jinsi nilivyo kuja Marekani!

Andrews university ndio chuo kilichonipa nafasi mimi ya kuja Marekani. Ngoja niwape story fupi ya safari yangu ya kuingia hapa.

Siku zote nilikuwa natamani kusoma /kuishi nje ya Tanzania.  Na mara nyingi nilikuwa napenda Australia, UK, na Marekani. Ilikuwa rahisi kujenga hisia zangu na maeneo hayo kwani mara nyingi nilivahatika kupata vijuzuu vinavyoonesha shule mbalimbali za nchi hizo. Basi, nikiwa katika muhula wa mwisho wa kumaliza chuo pale C.B.E siku moja nikiwa kanisani Temeke SDA, katika matangazo nikasikia wakitangaza kuwa chuo cha Andrew wanapokea wanafunzi kwa muhula wa Fall (Fall semester), na wakasema kuna vijuzuu kama kuna mtu angependa kwenda akachukue ili ujuwe jinsi ya kujiunga. Mara baada tu ya ibada, nikaenda kuchukua kijizuu. Baada ya siku kadhaa nikaenda kwenye intranet Cafe fulani ilikuwa karibu na chuo cha C.B.E. Ndio kwa mara yakwanza nafungua email akaunti yangu 🙈 Nikajaza fomu siku hiyo. Baada ya muda wa miezi kadhaa nilitumiwa barua kwa njia ya posta kuwa wamenikubali kuingia chuoni hapo kwaajili ya degree ya kwanza.  Wakati huo nilikuwa nimesha hitimu C.B.E sasa natafuta chuo cha kwenda.

Nakumbuka mmoja wa wadogo zangu (cousin sister) aitwaye Detta alikuwa akipenda kunitania kuwa “aah wewe ni wa hapa hapa tu” namwambia mie nakwenda zangu Marekani subiri utaona. Hapo sijajua kama nitachaguliwa au la! Ila yeye alikuwa anasema hivyo kwasababu dada yangu mkubwa alisoma China, kaka yangu alikuwa UK, na mdogo wangu yeye alikuwa anasoma South Africa. Hivyo akawa anasema mie nitabaki Bongo.

Ghafla, siku moja naletewa barua nikiwa job (niliajiriwa na Utegi Technical Enterprises Ltd baada ya kumaliza chuo), kuangalia ilipotoka nakuta ni Andrews University.  Nikaifungua haraka sana! Nikakuta ni barua ya kukubaliwa kujiunga na chuo ila sasa muda ulikuwa umebaki wiki 2 tu shule ianze 🙆🏽‍♀️🙆🏽‍♀️ Nikachanganyikiwa maana hizo hela zinazo hitajika na muda uliobaki, dah! Yule mzee kutoka kanda maalum nitamuingiaje?! 🤣 Mtu wakwanza kumwambia alikuwa ni mama. Yeye akanipa moyo akasema hongera sana, mwambie baba haraka sana. Sasa kesho yake hasubui tumesha maliza kunywa chai tunataka kwenda kazini, mama akalipua bomu kimtindo. 🙆🏽‍♀️

Akasema “Umesha mwambia baba?”, nikajifanya kutoa macho 😅 baba akauliza nini unataka kusema? Akasema (Akaniita kwa jina langu la kilugha) kaa chini “let’s talk ni nini”. Ikabidi nimwambie. Akasema sasa kwanini naogopa kusema jambo zuri kama hilo. Nikamwambie mzee nikienda siku yakwanza tu inatakiwa malipo ya awali ya nusu semester (muhula) au ada nzima. Kanijibu sasa tatizo ni nini? Kwani wewe ndio unatoa hizo pesa? Basi mzee wa watu siku hiyo akasimamisha shughuli zake zote, kuhakikisha napata documents zote zinazohitajika na kuzituma kwa njia ya fax na DHL. Chuo nao walikuwa shapu walipoamka tu wakatuma email kua sawa wanasubiria documents za DHL halafu watatuma I-20 (form maalum yakuombea viza ya shule). Mzee aliwaambia kutoka na muda watume kwa DHL halafu atawalipa hiyo pesa. Basi baada ya wiki 1-20 imefika. Nikaweka appointment ya kuomba viza. Tukaenda kwenye Viza, kumbuka nina siku tu zakuripoti shule, hivyo ticket ya ndege ilibidi nikate kabla hata ya kupata viza.
Kwenye viza si kidogo watuzingue! 🤣🤣

Basi, tumefika kwenye viza wala sikuhojiwa maswali mengi, wakasema kila kitu kipo vizuri lakini cheti changu cha form 4 ni “Fake”! 🙆🏽‍♀️🙆🏽‍♀️ Wakadai tumepiga simu wizara ya elimu wamesema hizo namba sio zake. 🥺🥺 Wakasema kama mnaweza kwenda wizarani mkahakiki nendeni kisha mrudi hapa. Wakatupa reference namba, na jina la mtu walie ongea naye hapo wizarani. Basi, tukatoka mbio kwenda wizarani, tunafika getini tukasema jina la mtu tunayekwenda kumuona, wakampigia simu huyo mtu kumwambia kua kuna wageni hapa wanahitaji kukuona. Yule mtu akaomba aongee na baba, akasema samahani rudini ubalozini wanawasubiria kule tumesha tatua tatizo. Alikosea kusoma namba. 🤣🤣🤣 Baba akasema lakini nilimuuliza unahuwakika kuwa cheti cha binti yangu ni feki na akanijibu kuwa “100% sure”. Mzee hasira zikamshika lakini sasa atafanyaje inabidi turudi tena ubalozini. Sasa wakati baba anamaliza kuongea na yule.mtu wa wizarani, secretary wake akapiga simu muda huo huo akasema “baba mnatafutwa na ubalozi wa Marekani wamesema mwende sasa hivi”, baba akamwambia ndio tunaelekea huko, lakini hawa watu leo ndio watanijua mimi ni nani! 🤣🤣🤣 Usichezee mzee wa kutoka kanda maalum.

Basi tukafika ubalozini, tukapokelewa vizuri, yule mdada akaomba msamaha kwa usumbufu, akachukua passport yangu akasema kesho asubuhi uje uchukue na nakutakia masomo mema. Mzee Igogo sasa akaanza, “young lady I need an official oppology letter” 🤣🤣 Eti huwezi kunifedhehesha mbele za watu halafu unaomba msamaha kiholela holela namna hiyo. 🙈🙈 Yani mie I was like just give my passport am ready to board. Nyie muendelee na drama yenu kimpango wenu. 🤣🤣 Nilipata passport asubuhi, usiku nikaondoka zangu siku hiyo hiyo.

Ilikuwa mara yangu yakwanza kutoka nje ya East Africa. Niliondoka na ndege ya British Airways, business class 😍😍 mzee Igogo sijui alifikiri nikipanda economy nitachelewa 🙈 Mwe! Nilifurahi sana. Tukafika UK, tukapelekwa hotelini kwa ajili ya kupumzika mpaka asubuhi kuanza safari ya kuelekea Chicago O’Hare International Airport. Baada ya kufika Chicago shulenilinielekeza kuchukua basi lakuelea Indiana. Waliniambia nishuke kituo cha mwisho ambapo ni Indiana Airport na hapo nitakuta gari la chuo cha Andrews likinisubiria. Nilifata maelekezo nikafika shule salama kabisa.

Nilifikia kwenye dormitories za chuo. Jamani acha tu! Unaingia kwenye dormitory ya chuo kama hotel vile. 😍 Nilikuwa na roommate mzungu kutoka Canada, alikuwa anaitwa Melissa Gonzalez. Vyumba ni self contained, mna bathroom na shower yenu kwa chumba, for a minute nikakumbuka mabafu ya C.B.E mabafu 3 watu zaidi ya 20 ni mwendo wa kusubiriana wengine wanaamua kuoga< kwenye kolido🤣🤣 Kwakweli,.Andrews ni shule nzuri sana sema gharama zake sasa! 🙆🏽‍♀️🙆🏽‍♀️Pasua kichwa.

Muhtasari wa matukio ya mwaka 2022 -sehemu ya kwanza.

Dec 2022

Mwaka 2021 niliufunga vyema na kuufungua 2022 vizuri sana. Namshukuru Mungu kwani umekua mwaka mwema sana wenye mibaraka mingi. Changamoto katika maisha hazikosekani kwani hatuwezi kujua tu imara kiasi gani kama hatutapitishwa katika changamoto hizo.

Daughter

Wanasema dhahabu au madini yoyote ya thamani hayapatikani juu ya barabara wala kando kando ya maji! Nilazima yachimbwe chini ya ardhi na yapitishwe kwenye moto mkali ndipo yawe haya madini tunayofurahia kuyaona. Hivyo, sikuzote tukipata changamoto tusikimbilie kusema “kwanini mimi?” Bali tumwambie Mungu najua hili ni darasa unanipitisha japo somo bado sijalielewa, naomba unipe HEKIMA ya kuweza kulielewa somo hili ili nifuzu mafunzo yangu vyema. Najua maumivu ninayopitia nikwaajili ya utukufu wako na mimi ndiye uliyenichagua kuwa kielelezo cha utukufu wako.

Basi kwa kusema hayo, naomba niweke kumbukunbu ya matukio yaliyozunguka maisha yangu mwaka huu wa 2022. Tukumbushane kushukuru katika kila jambo. Sikuzote tuhesabu mibaraka yetu kwani ni mingi mno sema tunafunikwa na upofu kwa kuangalia maisha ya watu wengine na kudhani kuwa wamebarikiwa kutuzidi. Hapana! Mungu anatubari sote kwa jinsi impendavyo yeye kwa wakati wake.

Hizi ni baadhi ya picha tulipiga mwanzoni mwa Dec 2021 tulikuwa maeneo ya tunako ishi karibu na NASA Space Center, Houston, Texas

Baadhi ya picha tulizopiga kwenye Christmas party 20021 iliyofanyika Hilton hotel, Houston, Texas.

2021 THC Thanksgiving Gala
April 2nd 2022

Mwenyezi Mungu alitubariki tukafurahia kuona mwanangu ameongeza mwaka mwingine. Ilikuwa siku ya Jumosi tarehe mbili mwezi wa Nne! Na zifuatazo ni baadhi ya picha ya siku hiyo.

Mama na mwana 😍

Mwanamke ni mtu shujaa, mwenye hekima nyingi, na muerevu sana!

Embu leo tuongelee hichi kiumbe ambacho Mungu alikiumba baada ya kuumba kila kitu! Mungu aliumba vyote lakini akaona kuna mapungufu mahala yani kwa lugha zingine naweza sema hakuridhika na kazi yake ya uumbaji mpaka alipo muumba mwanamke akaona vyote ni mema sana na uumbaji wake ukaishia hapo!

Labda niseme kwa siku ya leo nia yangu si kuongelea uumbaji wa Mungu bali nataka kuongelea moyo au nguvu ya ushujaa, hekima, na uwerevu ambao mwanamke amepewa na Mungu mwenyewe lakini bado tunajiona wadhaifu, hatuwezi kufanya kitu bila nguvu ya mwanaume kwanini? Kwakweli hata mimi sijui sababu bado najiuliza kwani kitu ambacho wanawake karibia wote tuna “struggle” nacho hata mimi mwenyewe- hello! Yes, me too ? Msema kweli ni mpenzi wa Mungu!

Hivi umeshajaribu kutafakari kuwa Mungu baada ya kumuumba mwanaume akaona kuwa hajakamilika kuna kitu kinahitajika ili huyu mwanaume aweze kufanya kazi kamili na kuishi kama mwanadamu? Na kitu hicho ni mwanamke! Hivyo, ukitaka kulinganisha utagundua kuwa mwanaume anahitaji nguvu ya mwanamke zaidi ili kuwa kitu kamili lakini mwanamke anaweza akafanya kazi na kuishi bila kumtegemea mwanaume sana (mnaojua maandiko ruksa kunikosoa). Naomba nieleweke, sijasema mwanamke hamuhitaji mwanaume la asha! Kila kitu ili kifanye kazi vizuri lazima kuwe na nguvu za hasi na chanya (mkono wa kulia na kushoto) ambazo zimeunganishwa pamoja katika kuleta nguvu kamili! Lakini saa nyingine utakuta upande wa kulia hautoi joto / nguvu sawa na kushoto hivyo inailazimu upande wa kushoto kutoa nguvu zaidi ili kuweka balance!

Zari The Bosslady

Nguvu ya ushawishi na hekima ambayo mwanamke amepewa ni kubwa sanaaaa! Tukiacha kisa cha Eva alivyo mshawishi mumewe Adamu kula tunda la mti waliokatazwa na Mungu, embu tuangalie kisa ya Malkia Esther kwenye Biblia! Jinsi Esther alivyotumia ushujaa na hekima ya hali ya juu kumshawishi Mfalme (mumewe) mpaka kuokoa watu wakwao! Kutokana na sababu mbali mbali watu wote waliogopa kumfata mfalme, lakini Esther alipoambiwa akasema lazima nifanye kitu kwani alijua kunyamaza kwakwe kungetoa tafsiri ya kuwa ameunga mkono maadui. Esther akajua wakati ni sasa kama ni kufa basi acha nife lakini lazima nikamuone Mfalme na kuweza kuongea naye juu ya jambo hili. Esther akatumia uerevu wake na hekima kupanga nini cha kusema, mahali pakusema, na muda wa kusema! Namwishoe akashinda na kuonekana shujaa kwa watu wa kwao!

Labda nifupishe hii story kwa kusema kwanini nimeandika, nia yangu nikutaka kuwakumbusha wanawake kuwa sisi ni viumbe vya kipekee sana ambavyo tumebarikiwa sana na Mungu lakini muda mwingi tumekuwa tukijikatisha tamaa sisi wenyewe aidha kwa kujua au kuto kujua! Tumekuwa waoga wa kutoa sauti zetu zisikike mbele ya wanaume. Tumekuwa hatutaki kueleza hisia zetu halisi na kujikuta tunaishi maisha yasio na uhalisia na kile kilichopo moyoni mwetu! Tumeshindwa kutumia nguvu ya ushujaa na ushawishi ambazo tumepewa na Mungu kuleta mabadiliko mbali mbali ndani ya maisha yetu na katika jamii zinazo tuzunguka! Tumekuwa viumbe dhaifu wakati Mungu alituumba kama mashujaa mkombozi wa mwanaume!

Japo kwasasa wanawake wengi wanaanza kuamka na kutambua hii siri ambayo ipo ndani yetu lakini bado inabidi tuamke zaidi! Mapinduzi yakweli yataletwa na mwanamke! Si unaona jinsi Eva alivyoweza mshawishi Adamu kula tuna na dunia yote sasa wanawake wanazaa kwa uchungu na wanaume wanaishi kwa jasho lao ?? Basi kama mnataka mabadiliko ya kuachana na siasa mbovu, kutokomeza ukatili wa aina zote, mazingira bora na salama ya kuishi n.k lazima muamke usingizini!

Usijione wewe hufai eti kwasababu unatabia kama za “Wema Sepetu” (sorry Wema I picked you), hapana! Mungu anapenda watu wote na anaweza mtumia mtu yoyote yule kufanya mabadiliko kwaajili ya utukufu wa jina lake! Kwa wale Wakristo kumbuka kisa cha Rahab au Ruth kwenye Biblia! Wanadamu tunatizama vitu kwa macho yetu haya ya dhambi hivyo nirahisi kuhukumu watu na kuona kuwa hawafai na hawana thamani lakini siku zote kumbuka kila mtu anathamani sana mbele za Mungu! Na kama Mungu ataamua kukutumia hakuna atakaye weza kuzuia! Kikubwa ni wewe kusikiliza ile sauti ‘ndogo’ inayo nena nawe kwa upole ndani ya nafsi yako kuwa badili njia zako!

Wanawake tunaweza kuibadilisha hii dunia kuwa mahala salama pakuishi tena kama hatuta waachia wanaume peke yao! Wanatuhitaji ili kuweza kuleta mabadiliko ya kweli! Siku zote kumbuka kuwa wewe ni shujaa, mwenyewe hekima, na muerevu sana!

****Zari’s picture has nothing to do with the story**

**Imeandikwa na Alpha Igogo

Penda ndugu zako kwa matendo!

Wakulia amefurahia kumuona babu wakati wa kushoto amefurahia kumuona baba mkubwa! Ukitaka watoto zako wapende ndugu zako lazima uwafundishe muhimu wa ndugu zako kwako wakati wakiwa bado wadogo. Nasio kuwafundisha kwa maneno bali kwa vitendo. Siku zote watoto watasikia unachosema LAKINI watafanya kile ambacho wanaona mzazi unafanya. Wewe ndio ubao wao wakujifunza na watakusoma vizuri sana, basi hakikisha unacho andika kwenye ubao wako nikile ambocho kweli unataka watoto wako wajifunze toka kwako.

#ToGodBeTheGlor

hollietheblogger: So many people ask me If I get paid to promote

Regrann from @hollietheblogger - So many people ask me If I get paid to promote @zarithebosslady the answer is NO. But let me tell you what I gain and why I waste my time..it’s her rare STORY‼️ Rare because, she chose HER and HER KIDS above EVERYTHING something many women have no courage to do‼️ My benefits might NOT be in monetary terms but it’s in a sense of hope and reassurance. Reassurance that in future our daughters will NEVER have to sit silent in abusive relationships just because the society expect them to. But because of Zari’s and many other women’s experiences they will have the strength to reclaim CONTROL and emancipate themselves‼️ Just like you, in Zari I see my mother, my sisters, my aunties & best friends. Women who have been cheated on, abused and emotionally & physically trampled on. Women whose happiness have been snatched by another woman. Homes and children left fatherless, loveless, poor and homeless just because of men’s selfishness. Despite all these evil, society and some ignorant women still believe it’s ok for a man to disrespect a woman‼️ Religion & culture teach us that women are beneath men & aren’t allowed to be their own person. When a woman rises up to be her own voice there is so much noise surrounding her strength. Therefore if someone say that DP actions were innocent & didn’t mean any harm, I say that is nonsense. 

Zari the real Bosslady

DP knew and still knows what he does. His actions were & are still emotionally abusive and were/are meant to break ZARI and leave her dependent and powerless just as he’s done to all his exes. DP has broken them all emotionally and left them powerless and dependent on him‼️If Zari had hold on to this nonsense this guy would have continued to demean her publicly to show her she’s worthless. These actions would have created fear and decreased her self esteem making her dependent on him‼️? So don’t expect the dirty ***  to move on or find happiness anywhere else because she’s EMOTIONALLY broken and will sit in that rented flat as a side fuck for the rest of her life?Compared to Zari who had a loving upbringing, these two are both as bad as each other because they both had a fucked up-bringing #revisitthispostinfuture #goodmorning - #regrann

Kamwe usibishane na pepo!

Wapendwa wasomaji wangu, za siku mbili tatu ? Haya leo ngoja niongee kidogo kuhusu pepo au mapepo. Unajua humu kwenye mitandao au hata kwenye maisha yetu tumezungukwa na mapepo wachafu. Hao au hili pepo anaweza akawa ndugu, rafiki, mfanyakazi wako, au mtu baki kabisa ambaye hana undugu wala ujamaa na wewe. 

Utakuta hili pepo kazi yake ni kuchukizwa na wengine wakiwa na furaha. Yani akiona watu wengine wana amani hata kama ni masikini kuliko yeye basi yeye roho yake inatahabika sana! Kinachofuata nikutafuta kila njia ya kufanya ile amani au furaha uliyonayo itoweke! Kama ni familia inafuraha basi atatafuta kila njia ya kuondoa furaha kwenye hiyo familia. Atagombanisha watu hata kwa kutumia watu wengine ili yeye asijulikane! Hapendi kuona watu wanaishi kwa amani na furaha kugombanisha watu ndio furaha yake yeye!

Sasa hata humu kwenye mitandao yapo haya mapepo! Kwa sisi Wakristo, Bible inatuambia "utawajua kwa matendo yao"! Yani ukiona mtu kutwa yeye nikugombanisha watu kwenye hii mitandao, kutwa kutukana watu kwakutumia sababu yoyote ile, amekalia kuvuruga familia za watu kwasababu wanafuraha? Yani muongo na umbea ndio maisha yake; mpendwa, basi jua huyo ni PEPO! Kamwe! Nasema tena Kamwe! usijibishane na Pepo! Pepo unalikemea kwa Jina la Yesu! Ukijibishana na pepo atakuambukiza mapepo yake! Hivyo njia nzuri ya kulishinda pepo ni kulikemea likafie mbali huko, hakuna jina ambalo pepo linaogopa kama jina la Mungu. Wewe kemea usimpe nafasi ya kukusogelea!

Huwa napendaga sana huu wimbo wa Rose Muhando "Nipishe nipite" haswa kwenye chorus. Huu wimbo unamkemea pepo au kwa jina lingine shetani. Huu ni mfano mzuri kabisa, kuwa pepo unalipa 'amri' nasio kuongea nalo! 

"Wewe ulimwasi Mungu, nipishe nipite 

Uliwadanganya Adamu na Eva, songea nipite 

Dunia nzima imeharibika, kwa ujanja wako 

 wewe shetani mlaaniwa, mwenyeji wa kuzimu 

Sasa nipishe nipite "Wapendwa tukemee mapepo yanayotuzunguka na kutufata fata kwa nguvu usicheke wala kulemba lemba maneno kwa pepo! Mpe amri, mwambie wewe  ulimwasi Mungu songea nipite, wewe shetani mlaaniwa mwenyeji wa kuzimu nasema sasa sogea nipite katika jina la Yesu! 

*** Kama humjui huyo kwenye picha ni mdogo wangu kipenzi Jokate Mwegelo. Missing you, love you dearly****Wanaopenda kushangaa ndio wajanja!

Baadhi ya watu haswa sisi Watanzania huwa tunatabia yakutokupenda kuwa wadadisi wa jambo au mambo matokeo yake our ignorance is very High! 
Yani tupo radhi tuamini katika uongo au majungu / umbea kuliko kuchukua muda wako na kukisoma / chunguza kitu wewe mwenyewe ili uwe na huwakika wa kile unachokiongea. Utakuta mtu anahadithia kitu wewe utaamini ni kweli ameiona mwenyewe kwa macho yake au amesikia yeye mwenyewe kwa masikio yake kumbe naye kasimuliwa na rafiki yake ambaye nae huyo rafiki kasimuliwa na mtu mwingine ?‍♂️?‍♂️

Hiii no karai ya Chicago

Hii tabia kutopenda kuchukua muda wetu na kujifunza jambo fulani au kufatilia habari fulani bila ya wewe kuweka uongo wowote ndio imefanya Watanzania wengi wanapenda majungu sana, wanaamini ili uweze fanikiwa basi lazima umuharibie mwingine haswa kama yupo kwenye biashara au jambo ambalo na wewe unafanya! Inasikitisha sana kwani kwa hii tabia maendeleo ya taifa letu yatahitaji dictator!!  Juzi niliamua kwenda kuangalia hili 'karai' kubwa ambalo limeletwa hapa Houston, Texas kwenye chuo cha sanaa. Hili karai limetengenezwa Ulaya likaletwa hapa. Ni urembo wa aina unao vutia sana.  Katika mji wa Chicago nao wanao 'karai' kama hili limetengenezwa na mtu mmoja. Ila la Chikago limeinamishwa (kama inavyo onekana kwenye picha ya pili kutoka juu) hivyo watu wanaweza ingia katikati ya hili 'karai' nakupiga picha nzuri sana kama anavyoonekana mwanangu hapo pichani ☝ na pia tizama picha ya mama yangu na mdogo wangu hapo chini ?
Hizo picha zilipigwa miaka 6 iliyopita kwenye hilo karai la Chicago. Kwa maoni yangu binafsi mimi napenda ya Chicago zaidi kwani imewekwa vizuri kwa watu kupiga picha na kitendo cha kulazwa chini imefanya hiyo sehemu iliyoingia ndani kuwa sehemu ya kivutionzaidi cha kupigia picha. Halafu maua na urembo ulioko pembezoni unahakisiwa na hiyo karai ambayo pia nikivutio.
Nilichotaka kuwaambia Watanzania wenzangu ni kuwa usiogope kushangaa! Hakuna njia nzuri ya kujifunza kitu kama kushangaa. Tena ukimpata mtu anayekupa maelezo basi wewe zidisha kushangaa ili akupe maelezo zaidi. Wanaopenda kushangaa ndio wajanja!

Je, unaheshimu mali za watu?!

Alpha Igogo, blogger Throw ? 2008

Mimi naheshimu sana kitu cha mtu yoyote yule! Yani mtu akiniazima kitu au kunipa kitu huwa nakitunza zaidi ya chakwangu! Naonaga mpaka mtu kutoa kitu chake kakupa au kukuazima inamaana sio tu amekuheshimu bali anakuamini! Trust is essential to me! Nina picha nilipewa na wanafunzi wenzangu Kowak Girls secondary school hizo picha mpaka leo ninazo hapa Marekani, sidhani hata kama wao wanakumbuka! Hivyo ndivyo nilivyo mimi! Na huwa nachukizwa sana nikiona mtu haeshimu kitu cha mtu mwingine kwani inaonyesha wewe unaweza kuwa na vielement vya tabia za kichawi chawi ???

Sasa jana jioni nilikuwa natafuta kitu kwenye closet (ambapo kuna washer and dryer sio kwenye nguo) nikakutana na hii GPS! Yes that how GPS monitors used to be ?? Wahenga mtatujua tu! ? ?Hii GPS niliazima kutoka kwa my good friend aitwae Sammy mwaka 2009. Alikuwa akihiitaji nampelekea nami ikitokea nahitaji naifata au ananiletea. Mwishowe ikaishia kwangu. Kusahau na mambo kuwa mengi sikufanikiwa kumrudishia.

Lakini kwakuwa nilijua niliazima sikupewa moja kwa moja miaka yote nimejisikia kuwa na wajibu wa kuitunza mpaka hapo nitakapo mpa tena. Believe me, nilipokuwa nahama Michigan to Texas, niliipaki vizuri nikaja nayo ?? nimeihifadhi vizuri sana mpaka stand yake ipo ? nafikiri it’s about time kumrudishia mwenye GPS yake akitaka kuitupa aitupe mwenyewe! Sindioo au niendelee kumtunzia kama yeye alivyokua akinitunzia vya kwangu ???? #HeshimuVyawatuZaidiYaChako

#NiMchezoWakutunzianaTu

 

 

“WAISLAMU_NA_WAKRISTO SOTE TU TAIFA MOJA IMARA”

#WAISLAMU_NA_WAKRISTO SOTE TU TAIFA MOJA IMARASiku tukianza kukumbatia tofauti zetu za kidini (ukristo na uislamu) ni sawa na kujichimbia kaburi la pamoja (mass grave) mchana kweupeeee kabisa.

Ukumbukwe tu ya kuwa si kitendo cha wakristo kuwatenga waislamu ndicho kitaweza kutuhakikishia maboresho katika mfumo wetu wa elimu ambao watoto wa dini hii kuu mbili wanapaswa kunufaika nao kama vijana tegemeo wa taifa la kesho, na wala si kwa;

kitendo cha waislamu kuwatenga wakristo ndicho kitahakikisha utatuzi wa changamoto ya upatikanaji wa maji vijijini ambapo takribani 90% ya watanzania waumini wa dini hizi kuu mbili wanapatikana.

Ili nchi hii isonge mbele, ni lazima tuhubiri umoja, na isiishie tu katika mahubiri, hapana, bali juhudi na mikakati ya makusudi kabisa lazima iwepo na itekelezwe ili kuhakikisha Tanzania inakuwa moja kwa leo na inaendelea kuwa moja na imara zaidi hata vizazi vijavyo.

Mwanaume kuwa na nyumba peke yake si tija…..!

Nakubaliana na Lemutuz kwa maneno aliyo andika hapo  chini lakini naomba niongezee kwa kusema kwamba; mwanaume kuwa na nyumba peke yake si tija bali kuwa na mji wako ndio mambo yote! Mwanaume sharti uwe na mji wako ndio utaheshimika! Hili hata kwenye Bible (kwa site tunao amini Bible) imesema. Siyo tu kufanya starehe halafu una lala na kuamka kwenye mji wa mwanaume mwenzio, kwani wewe unamatatizo gani?! Mwanaume kuuza sura hakukupi heshima au kukyongezea thamani yoyote bali kunaonyesha jinsi gani ulivyo na Itilafu kuchwani au mahala "fulanai" mwilini mwako!! Napia kuwa na nyumba nyingi kuna kufanya kuwa "baba mwenye nyumba" lakini hakukufanyi kuwa Baba Mwenye Mji (home)!! Kwa mwanaume kupata uwezo wa kusema nina kwangu au nina mji wangu lazima uwe na MKE!! Sijasema Kimada au Vimada hapana! MKE! Mwanamke uliyemuoa kihalali kwa kufata taratibu halali za kidini au lisheria! Nawala siyo mwanamke wa kufichia status kwa social media. Lasivyo hizo nyumba zako zinakuwa hazina uzito sana!! Nyumba hata Kunguni wanazo ?? Hivi bado kuna ndoa za kimila karne hii  ??Just asking ??Regrann from @lemutuz_superbrand - FACT: Hapa mjini kuna Baba mwenye nyumba ...sio Baba mwenye wabebez au magari na nguo ...hahahahahahaha.....NI BABA MWENYE NYUMBA TU! .....tuleni Batazzz lakini TUJENGE...Case Closed ....U know! - @lemutuz_superbrand - #regrann

why so many people like to talk down on the teaching profession?

I don't get why so many people like to talk down on the teaching profession. It baffles me because teaching is no different than being a doctor, an engineer, a lawyer, all the other jobs that are deemed more important to society. These careers are seen as practices and people forget that Teaching is also a practice. It's a learning experience just like those other jobs. You see teachers literally everywhere. I always ask myself ...without teachers would we have doctors, lawyers, and engineers? People aren't born with all that knowledge they are TAUGHT it by TEACHERS. So, why the bad rep? Teachers are the backbone of all society and yet...never get that recognition. (Yes there are bad teachers, but there are far more good ones. But one should also research why there are bad teachers, what is so messed up about the education system that even ALLOWS bad teachers?) Of course many people who go into education don't do it to be noticed. But is it wrong to want to be respected? Is it wrong to want to know that your community understands your importance and impact on a student's life? Is it wrong to ask to be provided with resources needed to help reach student's success without having to constantly prove that they are essential? It seems like many people forget that it's not just the teachers but it's the students who also are affected. And how can a teacher do their job of educating these students when most of them don't even have the tools,support etc to achieve this goal? Everyone has a story about a teacher who has helped them, gone the extra mile, simply been there for them. Who would you be without them? - Rant ended***by Sarah, teacher to be***

Dina Marious: Angalia ndoto yako

Regrann from @dinamarious - Usiangalie magumu yanayokukabili na changamoto unazokutana nazo Leo angalia NDOTO yako.

Ndoto yako itatimia.......

 ndoto yako inawezekana.Kumbuka jinsi ulivyoiamini endelea kuiamini.

Inawezekana Leo umeamka una stress,huna hela,huelewi mambo yanavyokwenda.

Pamoja na yote endelea kuiamini NDOTO yako hata katika mazingira yanayokatisha tamaa.

Kumbuka wewe ndio una hiyo picha ya Kesho yako naamini ni picha nzuri sanaa na amini utaifikia.

Good morning! - #regrann

Hujafa hujaumbika: Mariah Carey amegundulika na Bipolar disorder

Wahenga walisema hujafa hujaumbika hawakukosea bali walitaka watu wajifunze kuishi kwa unyenyekevu bila kudharau wengine kwani kama bado hatujakuchimbia kaburi lako tegemea kupatwa na kitu chochote kila kibaya au kizuri! Just be humble! Kuna watu wengi ukiwaona utadhani wapo vyema kabisa kiafya na kiroho, kumbe ni wagonjwa kama siyo kiroho, basi kimwili, au kiakili! Tena humu kwenye social media ndio nirahisi sana kuwagundua ?? Wewe angalia sana watu wanaofanya vitu extreme just to get attention fanya kuwachunguza utagundua kuna shida mahala! Siyo tu wanao post matusi au picha za uchi, hapana! Hata wale ambao kutwa picha zao lazima ziwe na muonekano fulani "perfectly put together" the "divaish" behavior. Au mwingine kazi yake ni kupiga picha na viongozi wa siasa na "celebrates" tu haonyeshi maisha yake halisi zaidi ya hizo picha yani watu kama hawa wengi ni wagonjwa! Wengine ni waongo spare zake hakuna!!

Lakini  hakuna haja ya kumcheka mgonjwa japo saa nyingine katika hali ya kiubinadamu wengi tumejikuta tukifanya hivyo haswa kwa wale ambao wameumiza roho zetu! Kumbuka 'hujafa hujaumbika'! Wewe ona mtu kama Mariah Carey  uzuri na pesa zote alizo nazo bado amekutwa na huu ugonjwa! Bipolar siyo Ukichaa ila usipo tibiwa kwa muda mrefu unageuka kuwa kichaa kabisa. 

Mariah Carey aligundulika kuwa na huu ugonjwa mwaka 2011, ameficha kwa muda huo wote lakini sasa imefikia hali ambayo haufichiki tena. Kwa kuhofia kuwa ipo siku mtu angetoa hivyo siri kabla yeye hajasema imembidi sasa aende hadharani na kutangazia dunia kuwa yeye ni mgonjwa wa akili, hivyo dunia impokee na kumkubali jinsi alivyo!.....Kabla ya kuhukumu mtu jaribu kumjua kwa kiundani unaweza tena dhambi mbaya sana! #HujafaHujaumbika

Kwenye hili la Makonda na ‘watelekezwa’…….!

Regrann from @mutwiba - MJADALA 

Kwa wale wenye uelewa wa maswali yajayo naomba tusaidiane kuyatafakari na naamini tutapata majibu ama maswali zaidi yatakayohitaji ama kuleta majibu zaidi. Kwenye hili la Makonda na 'watelekezwa' nimejiuliza baadhi ya maswali. Na kwa kuwa penye wengi haliharibiki neno, wacha niulize hapa ili ukiweza jibu lolote kati ya maswali haya.

MJADALA WA HESHIMA UTATHAMINIWA

1: Hili la wanawake kutelekezwa na watoto wao linatokea Dar tu ama hata mikoani lipo?

2: Wanaotajwa Dar wakikimbilia mikoani ambako mpango ama mkakati huu haupo, watasakwa ama? Na watakaotajwa kwa chuki na kuharibiwa mahusiano yao ya sasa watafidiwa?

3: Hili la kuwataja wanaume wanaoaminika kutelekeza watoto linatendeka kisheria ama ni ubunifu wa mkuu wa mkoa? Kama ni kwa mujibu wa sheria, si lifanyike nchi nzima? Kama ni ubunifu wa Mkuu wa Mkoa, akiacha ama kuachishwa kazi na ubunifu wake usio katika maandiko unakuwa umefia hapo?

4: Hudhani kwamba ingekuwa vema kuandaa workshop ama hata matangazo ya radio ya kuwafunza sheria za ndoa / mahusiano wanawake waliotelekezwa na wanaotaka kuingia kwenye mahusiano?

5: Mhe. Mkuu wa Mkoa akishakutana nao, wakishawataja watu waliowatelekeza, atawatatulia tatizo lao ama atawaelekeza Mahakamani ambako sheria ambazo zipo tayari zinastahili kuchukua mkondo wake?

6: kilichoonekana juzi ni kipi? (i) wanawake waliotelekezwa? (ii) wanaume waliotelekeza? (iii) mfumo wa sheria usiotenda haki kwa wanawake? (iv) wanawake wasiojua haki zao ambazo walistahili kuzisaka na kuzipata kabla ya kumfikia Mkuu wa Mkoa?

Yaani kilichodhihirika leo ni jambo la kuihurumia jamii yetu kwa kutojua ama kupuuza sheria

Na kwa kuwa na imani katika njia isiyotufikisha tunakotakiwa kwenda.

My two cents.

Na natunza haki ya kukosea na kukosolewa.

Mzee wa Changamoto - #regrann

Joyce Kiria: Wamejikuta wanakubaliana na IMANI ya KUVUMILIA hali walizonazo

Regrann from @joycekiriasuperwoman – Watu wengi wamenasa katika mtego wa kuamini kuwa hawana uwezo wa kupata ufumbuzi wa matatizo waliyonayo, kwa sababu wamejikuta wanakubaliana na IMANI ya KUVUMILIA hali walizonazo.
Wacha nikwambaie, Haujaumbwa ili kuvumilia matatizo yanayokukabili, umeumbwa ili UYATATUE na upige hatua. Chunguza matatizo yanayokuzunguka Leo na ujiambie nafsi yako ” HATA TATIZO HILI LINA UFUMBUZI, SITAKUBALI KUSHINDWA KULITATUA”
**
**
Kila Changamoto inayokukabili Leo inahitaji UWEZO Mkubwa zaidi wa kufikiri au MAARIFA ili uweze kuitatua. Kinachofanya Changamoto iwe ngumu, siyo kwa sababu ya jinsi ilivyo Bali kwa sababu ya UWEZO Mdogo wa MAARIFA uliyonayo.
**
**
Katika Changamoto ulizonazo jiulize unahitaji maarifa gani katika hilo Eneo ili uweze kukabiliana nayo na kuishinda… Good morning
**”
Top from @lizycollections @lizycollections – #regrann

Chumba chako cha kulala siyo sehemu ya michezo!

Zari, my dear umeona nowadays I don't post you like I used to right? Honestly, you have disappointed so many of us!! Never in a million times  wouldn't  have ever thought you could stoop yourself so low like that?! Honestly, for what?!! Because I'm sure you are not happy right now! So for what?! Don't you see how  Diamond is abusing your love?! Playing with your feelings, disempower you every day, and literally tarnishing your brand and you think it's okay cause?! Anyway, it's your life my dear the rest of us are just "hand clappers" ??? wishing you the best!

Hayo ya Zari tumuachie Zari mwenyewe embu tuongee kuhusu mada yetu ya leo! Eti wewe unakiwekaje chumba chako cha kulala? Unaruhusu watu kuingia na kucheza kama hapo kwa Zari au una mipaka?! Kuna kitu kinaitwa "self discipline", Kama mtu hauna self discipline basi hautajua  wapi kwa kuweka mipaka yako! Hautojua wapi niseme ndio na wapi niseme hapana! Yani Mimi hapa nawaonyesheni chumba ninacho lala sasa hivi kwasababu bado sijaamia kwenye my "dreamed bed room" ?? kweli kabisa siku nikiingia kwenye hicho chumba hamta kaa muone chumba changu cha kulaka kwa social media!! Nope! Labda wale watakao nitembelea ndio watabahatika kukiona tena tuwe tumezoeana sanaaaaaaa!! Hivi mlishaona mtu Kama Madam Rita Paulsen, Oprah Winfrey, au Jacqueline Mengi wakiwaonyesha vyumba vyao wanavyo lala?! You just have to leave something to yourself! Chumba chako cha kulala nikama your private part keep it private! Labda wale wanaokuja kukutembelea ndio utawapa house tour! Soon nitakuwa kama Mrs Mengi haonyeshagi nyumba yake yote  nikwa nje  na kwenye ngazi tu! Hata jiko hajawahi onyesha ?? Nahiyo ndio inaongeza heshima na watu kujua mipaka  ya urafiki! Chumba chako is not a game room ambapo watu wanaingia bila mpangilio tena wanapanda mpaka kwenye kitanda chako! Always have a self discipline!

Uzalendo huanzia nyumbani kwako!

"Picha hii ilipigwa siku ambayo nilitangaza kuwa sitagombea tena Ubunge, baada ya kuwatumikia kwa miaka 10. Sita sahau hisia zetu siku hiyo, jinsi mioyo yetu ilivyo vunjika kwa kujua kuwa mazoea yetu yatabadilika. Nina uhakika upendo wetu umebaki daima. Ndugu zangu Singida mjini ninawakumbuka sana! ❤ MO" // This picture was taken the day I announced to my constituents that I won’t be running for parliament, after serving them for 10 years. I won’t forget our emotions that day, a deep sense of heartbreak knowing that our interactions will change but the love will forever remain. My fellow Singida Urban brothers and sister, I miss you dearly! ❤️ MO"

Biblia inasema kuwa mtu asiyependa wakwao ni mbaya kuliko mtu asiye amini! Yani ni bora mpagani anaonekana mtakatifu mbele za Mungu kuliko yule anaye sema anamuamini Mungu wakati anachukia na kutojali wakwao! Kuna watu wengi sana tena wengine wapo mbele ya macho yetu kila siku baadhi yetu wanawachukulia kama "role model" wao bila kutafakari kwa kina kuhusu hao "role model" zao! Je,  umewahi kuwachunguza kama kweli wanapenda wakwao? Au ni watu wa 'mikakati' yani they have an hidden agenda ya kutaka kupata pesa kutoka kwa wazungu na sponsors wa mambo yao! Kama ni kusaidia je  umeshaona wakisaidia wakao? Au ndio wale watu ambao ndugu zao wote ni wa "mujini wenye pesa" ukiishi uswahili kwetu kule Keko wewe siyo ndugu yao hawakujui!! Uzalendo unaanzia nyumbani kwako kwani hata hao ndugu zako ni Watanzania hivyo ukiwasaidia unasaidia taifa la Tanzania. .............Binafsi naheshimu nakupanda  watu wenye tabia ya kutoa jasho lao na kusaidia watu bila kuomba au kubugudhi wengine. Mfano ni Mh. MO Dewji, ShyRose Bhanji, Dr. Ntuyabaliwe Foundation, Rita Paulsen, Flaviana Matata Foundation, Kidoti na wengine. Sipendi mtu anayetaka kusaidia wengine kwa kulazimisha wengine wamchangie kwani kusaidia mtu ni ibada, hivyo ni siri ya mtu na Mungu wake. Usinielewe vibaya kuna kuchangia kwingine naunga mkono kabisa kama mambo ya cancer, shule, n.k (for special cause). Ninacho ongelea hapa ni kusaidia watu binafsi......... Anyway, napenda vile Mh. MO anavyo wajali watu wa kwao huko Singida mjini. Mfano mzuri wa kuwa uzalendo, unaanzia ndani ya nyumba yako!

You deserve!

You Deserve

 Make room in your life for what you really deserve instead of settling for a comfortable compromise. Join her on a journey to forgiveness.
Iyanla Vanzant
Photo: Gary Lupton/Studio D
Some years ago, I was shopping and came upon a beautiful red dress. The color, style and length were perfect. But the store didn’t have it in my size. It did, however, have the same dress in navy, which I wasn’t crazy about. Then I noticed a pair of blue shoes nearby that complemented that blue dress. (I didn’t love those, either.) So what did I do? I bought both. I was afraid I wouldn’t find anything else, so I settled. (It won’t surprise you to learn that I’ve never worn the dress or the shoes.)

You’ve probably heard the saying “Better the devil you know than the devil you don’t.” Here’s a question: Why put up with any devil? Why not give ourselves only good things? When we believe we cannot have what we desire—when we lack faith in ourselves and in the goodness of life—we settle for less. We decide that whatever is in front of us is better than nothing. But believe me when I tell you that better than nothing isn’t good enough.

I often see people settle for less than they deserve in personal relationships: accepting bad behavior, excusing broken promises, accommodating people who take more than they give. Why? Because doing things we’ve grown accustomed to is familiar, comfortable.

Which is why sometimes it can be tough to gauge whether we’re settling: When we tell ourselves that things are fine, we soon forget that they could be better. Here’s how to know whether you’re putting up with less than you deserve:

 • When you have to work yourself into a state of excitement rather than naturally experiencing joy and passion, you’re probably settling.
 • When you bargain with yourself about what you can do without rather than feeling gratitude for what you already have, you’re probably settling.
 • When your focus is on the time and energy you’ve invested in an endeavor rather than the love, joy and gratification you’ve gained, you’re probably settling.
 • When you’re making excuses about why you should stay put rather than going for what you truly want, you’re probably settling.
 • When you spend more time complaining about what you have than appreciating it, you’re definitely settling.

  But there is a lesson to be learned in everything. When we realize we’ve been settling, we discover what we actually believe. We learn that we perhaps think ourselves undeserving of happiness and find how susceptible we are to outside influences—because often we settle when others convince us it’s the right thing to do. Most important, we learn that we are not standing fully in our truth. Armed with this information, we can make new choices that support our desires—by beginning to believe that we can have what we really want.  Iyanla Vanzant is the host of OWN’s Iyanla: Fix My Life and the author of Peace from Broken Pieces.

 • Read more: www.Oprah.com

Dina Marios: Usifanye makosa ukaangalia safari ya mwenzako

Subira na Uvumilivu ni muhimu sana katika safari ya kukimbiza ndoto zetu na mafanikio yetu.

Ni muhimu kukubali kuwa matokeo mazuri ya juhudi zetu hayaji kwa haraka au Papo kwa papo. Lakini wakati ukipitia hatua muhimu ndogo ndogo za matokeo madogo madogo jua upo tayari njiani. Inawezekana unajua au hujui sababu wewe ni aina ya watu mnaotaka matokeo mazuri hapo hapo. Kuna aina ya watu wao hutaka matokeo ya juhudi zao hapo hapo…unataka yes hapo hapo…na ukikosa ni rahisi kuwa discouraged na kukata tamaa moja kwa moja.Kwa nini imekataliwa?kwa nini haijatoboza kama nilivyotaka?basi hili jambo naachana nalo…basi sitaki tena…mimi sio bora.

Na kuna watu wao ni kama marathoners wakimbia mbio ndefu. Anakimbia umbali mrefu km kadhaa lakini mdogo mdogo mpaka afikie finishing line.Njiani ataanguka,atasikia kiu, lakini amefocus kwenye finishing line yake.

Subira/Patience ni muhimu sanaa wanasema safari ya miles 1000 huanza na hatua moja. Ijue safari yako iwapo ni ndefu na inayohitaji hatua nyingi tena za taratibu au la.

Usifanye makosa ukaangalia safari ya mwenzako mbona fulani nimeanza nae juzi tu yeye kashafika? yeye kashafanikiwa? Ukaacha njia yako nakuanza kufata ya kwake…utapotea.

It’s owkey wakati mwingine kuanguka, lakini usikate tamaa…..Rise Up tena ukiwa na ari ya kufanikisha zaidi na zaidi.

Subira……..Uvumilivu kama haunao anza kuufanyia mazoezi ni muhimu sana.

Good Morning!
Dina Marios

                                              ***Baadhi ya maoni***

Joyce Kiria: MWANAMKE PIGA KAZI KWENYE NDOA FUATA MAHABA

IVI DUNIA YA LEO BADO KUNA MWANAUME ANAKATAZA MKE KUJITAFTIA KIPATO???? ------ Jamani Kuolewa kunatakiwa kukubadilisha tu kuwa umetoka kuishi mwenyewe na sasa unaishi na mwanaume lakini sio ubadilishwe kutoka kwenye kazi uwe mama wa nyumbani. Halafu kuna wanaume wanatumia hicho kama kigezo kisa kujifanya wana wivu kuhisi labda mwanamke akitoka kwenda kazini atakuwa na mchepuko. Yani wewe mumeo akisema acha kazi mwambie nipe kazi ingine ya kujiajiri na tena hiyo kazi nayo uwe na haki nayo sio umeachishwa kazi umefunguliwa kiduka siku mnaachana kiduka chake anachukua unaenda kuanza upya. Usikubali kupoteza kazi yako kisa ndoa tambua maisha ya leo yenyewe hayatabiriki wanaume wenyewe wa sasa maji kupwa maji kujaa sasa ndo uache kazi unajua umeolewa ukiachwa unaenda kuwa omba omba. Kwanza mwanaume mwenye akili atamuacha mke wake afanye kazi ili siku mambo yamekuwa mabaya kwake mke anaweza endelea kutunza familia. MWANAMKE PIGA KAZI KWENYE NDOA FUATA MAHABA... Kumekucha achia shuka bibi weeeeeee, SHAURILO

Blog