Joyce Kiria: MWANAMKE PIGA KAZI KWENYE NDOA FUATA MAHABA

IVI DUNIA YA LEO BADO KUNA MWANAUME ANAKATAZA MKE KUJITAFTIA KIPATO???? ------ Jamani Kuolewa kunatakiwa kukubadilisha tu kuwa umetoka kuishi mwenyewe na sasa unaishi na mwanaume lakini sio ubadilishwe kutoka kwenye kazi uwe mama wa nyumbani. Halafu kuna wanaume wanatumia hicho kama kigezo kisa kujifanya wana wivu kuhisi labda mwanamke akitoka kwenda kazini atakuwa na mchepuko. Yani wewe mumeo akisema acha kazi mwambie nipe kazi ingine ya kujiajiri na tena hiyo kazi nayo uwe na haki nayo sio umeachishwa kazi umefunguliwa kiduka siku mnaachana kiduka chake anachukua unaenda kuanza upya. Usikubali kupoteza kazi yako kisa ndoa tambua maisha ya leo yenyewe hayatabiriki wanaume wenyewe wa sasa maji kupwa maji kujaa sasa ndo uache kazi unajua umeolewa ukiachwa unaenda kuwa omba omba. Kwanza mwanaume mwenye akili atamuacha mke wake afanye kazi ili siku mambo yamekuwa mabaya kwake mke anaweza endelea kutunza familia. MWANAMKE PIGA KAZI KWENYE NDOA FUATA MAHABA... Kumekucha achia shuka bibi weeeeeee, SHAURILO

Leave a Reply