Dina Marios: Usifanye makosa ukaangalia safari ya mwenzako

Subira na Uvumilivu ni muhimu sana katika safari ya kukimbiza ndoto zetu na mafanikio yetu.

Ni muhimu kukubali kuwa matokeo mazuri ya juhudi zetu hayaji kwa haraka au Papo kwa papo. Lakini wakati ukipitia hatua muhimu ndogo ndogo za matokeo madogo madogo jua upo tayari njiani. Inawezekana unajua au hujui sababu wewe ni aina ya watu mnaotaka matokeo mazuri hapo hapo. Kuna aina ya watu wao hutaka matokeo ya juhudi zao hapo hapo…unataka yes hapo hapo…na ukikosa ni rahisi kuwa discouraged na kukata tamaa moja kwa moja.Kwa nini imekataliwa?kwa nini haijatoboza kama nilivyotaka?basi hili jambo naachana nalo…basi sitaki tena…mimi sio bora.

Na kuna watu wao ni kama marathoners wakimbia mbio ndefu. Anakimbia umbali mrefu km kadhaa lakini mdogo mdogo mpaka afikie finishing line.Njiani ataanguka,atasikia kiu, lakini amefocus kwenye finishing line yake.

Subira/Patience ni muhimu sanaa wanasema safari ya miles 1000 huanza na hatua moja. Ijue safari yako iwapo ni ndefu na inayohitaji hatua nyingi tena za taratibu au la.

Usifanye makosa ukaangalia safari ya mwenzako mbona fulani nimeanza nae juzi tu yeye kashafika? yeye kashafanikiwa? Ukaacha njia yako nakuanza kufata ya kwake…utapotea.

It’s owkey wakati mwingine kuanguka, lakini usikate tamaa…..Rise Up tena ukiwa na ari ya kufanikisha zaidi na zaidi.

Subira……..Uvumilivu kama haunao anza kuufanyia mazoezi ni muhimu sana.

Good Morning!
Dina Marios

                                              ***Baadhi ya maoni***

Leave a Reply