“WAISLAMU_NA_WAKRISTO SOTE TU TAIFA MOJA IMARA”

#WAISLAMU_NA_WAKRISTO SOTE TU TAIFA MOJA IMARASiku tukianza kukumbatia tofauti zetu za kidini (ukristo na uislamu) ni sawa na  kujichimbia kaburi la pamoja (mass grave) mchana kweupeeee kabisa.

Ukumbukwe tu ya kuwa si kitendo cha wakristo kuwatenga waislamu ndicho kitaweza kutuhakikishia maboresho katika mfumo wetu wa elimu ambao watoto wa dini hii kuu mbili wanapaswa kunufaika nao kama vijana tegemeo wa taifa la kesho, na wala si kwa;

kitendo cha waislamu kuwatenga wakristo ndicho kitahakikisha utatuzi wa changamoto ya upatikanaji wa maji vijijini ambapo takribani 90% ya watanzania waumini wa dini hizi kuu mbili wanapatikana.

Ili nchi hii isonge mbele, ni lazima tuhubiri umoja, na isiishie tu katika mahubiri, hapana, bali juhudi na mikakati ya makusudi kabisa lazima iwepo na itekelezwe ili kuhakikisha Tanzania inakuwa moja kwa leo na inaendelea kuwa moja na imara zaidi hata vizazi vijavyo.

Leave a Reply