Kesha la asubuhi: Bidii Katika Kutoa Onyo la Mwisho

                *KESHA LA ASUBUHI*

                  Jumanne Mei 29, 2018

        *Bidii Katika Kutoa Onyo la
             Mwisho*_Baada ya hayo naliona malaika mwingine, akishuka kutoka mbinguni, mwenye mamlaka kuu; na nchi ikaangazwa kwa utukufu wake. Ufunuo 18:1_

? Siku hadi siku hupita na kuwa milele, ikituleta karibu zaidi na kufungwa kwa mlango wa rehema. Sasa inatubidi kuomba kwa jinsi ambavyo kamwe hatujawahi kuomba kwa ajili ya Roho Mtakatifu kuwekwa kwa wingi zaidi juu yetu, na lazima tutafute uwezo wake unaotakasa upate kuja juu ya watendakazi, ili watu ambao wanawafanyia kazi wapate kufahamu kuwa wamekuwa pamoja na Yesu na kujifunza kutoka kwake. Tunahitaji uwezo wa kuona kwa macho ya kiroho sasa kuliko wakati wo wote uliopita, ili tupate kuona mbali, na kwamba tupate kutambua mitego na njama za adui, na kama walinzi waaminifu kutangaza hatari. Tunahitaji nguvu za kiroho ili tupate kupokea kadiri ambavyo akili ya mwanadamu inaweza kupokea, mada kuu za Ukristo, na jinsi ambavyo kanuni zake ni za kudumu.

? Watu wa Mungu wanaponyenyekesha roho mbele zake, kama mtu mmoja mmoja akitafuta Roho Mtakatifu wake kwa moyo wote, itasikika kutoka katika vinywa vya wanadamu ushuhuda kama ule unaowasilishwa katika Maandiko: “Baada ya hayo naliona malaika mwingine, akishuka kutoka mbinguni, mwenye mamlaka kuu; na nchi ikaangazwa kwa utukufu wake” (Ufunuo 18:1). Kutakuwapo na nyuso zinazong’aa kwa upendo wa Mungu, zikisema, “damu yake Yesu, Mwana wake, yatusafisha dhambi yote.” (1 Yohana 1:7). Wale walioko chini ya uwezo wa Roho Mtakatifu wa Mungu hawatakuwa washupavu wa dini, bali watulivu, imara, huru kutokana na ubadhirifu. Lakini hebu wale wote ambao wameipata nuru ya ukweli ikiwaka wazi na dhahiri katika njia zao, wawe waangalifu katika jinsi wanavyotamka amani na usalama. Mwe waangalifu ni mvuto gani mnaoweka wakati huu.

? Yesu anatamani sana kuweka majaliwa ya mbinguni kwa kipimo kikubwa juu ya watu wake. Maombi yanapanda kwenda kwa Mungu kwa ajili ya utimilizwaji wa ahadi hii; na hakuna ombi hata moja lililotolewa kwa imani linapotea. Kristo alipaa juu, aliteka mateka, akawapa wanadamu vipawa. Wakati, baada ya kupaa kwa Kristo, Roho alipokuja chini kama ilivyoahidiwa, kama upepo wenye nguvu unaokimbia haraka, akijaza sehemu yote ambapo wanafunzi walikusanyika, matokeo yake yalikuwa nini?

Maelfu waliongolewa katika siku moja. Tumefundisha, tumetegemea kuwa malaika atashuka kutoka mbinguni, kwamba dunia itaangazwa kwa utukufu wake, pale tutakapoona uvunaji wa roho sawa na ule ulioshuhudiwa katika siku ya Pentekoste. - Home Missionary, Nov. 1, 1893.

*TAFAKARI NJEMA NA MUNGU AKUBARIKI*

Leave a Reply