Kamwe usibishane na pepo!

Wapendwa wasomaji wangu, za siku mbili tatu ? Haya leo ngoja niongee kidogo kuhusu pepo au mapepo. Unajua humu kwenye mitandao au hata kwenye maisha yetu tumezungukwa na mapepo wachafu. Hao au hili pepo anaweza akawa ndugu, rafiki, mfanyakazi wako, au mtu baki kabisa ambaye hana undugu wala ujamaa na wewe. 

Utakuta hili pepo kazi yake ni kuchukizwa na wengine wakiwa na furaha. Yani akiona watu wengine wana amani hata kama ni masikini kuliko yeye basi yeye roho yake inatahabika sana! Kinachofuata nikutafuta kila njia ya kufanya ile amani au furaha uliyonayo itoweke! Kama ni familia inafuraha basi atatafuta kila njia ya kuondoa furaha kwenye hiyo familia. Atagombanisha watu hata kwa kutumia watu wengine ili yeye asijulikane! Hapendi kuona watu wanaishi kwa amani na furaha kugombanisha watu ndio furaha yake yeye!

Sasa hata humu kwenye mitandao yapo haya mapepo! Kwa sisi Wakristo, Bible inatuambia "utawajua kwa matendo yao"! Yani ukiona mtu kutwa yeye nikugombanisha watu kwenye hii mitandao, kutwa kutukana watu kwakutumia sababu yoyote ile, amekalia kuvuruga familia za watu kwasababu wanafuraha? Yani muongo na umbea ndio maisha yake; mpendwa, basi jua huyo ni PEPO! Kamwe! Nasema tena Kamwe! usijibishane na Pepo! Pepo unalikemea kwa Jina la Yesu! Ukijibishana na pepo atakuambukiza mapepo yake! Hivyo njia nzuri ya kulishinda pepo ni kulikemea likafie mbali huko, hakuna jina ambalo pepo linaogopa kama jina la Mungu. Wewe kemea usimpe nafasi ya kukusogelea!

Huwa napendaga sana huu wimbo wa Rose Muhando "Nipishe nipite" haswa kwenye chorus. Huu wimbo unamkemea pepo au kwa jina lingine shetani. Huu ni mfano mzuri kabisa, kuwa pepo unalipa 'amri' nasio kuongea nalo! 

"Wewe ulimwasi Mungu, nipishe nipite 

Uliwadanganya Adamu na Eva, songea nipite 

Dunia nzima imeharibika, kwa ujanja wako 

 wewe shetani mlaaniwa, mwenyeji wa kuzimu 

Sasa nipishe nipite "Wapendwa tukemee mapepo yanayotuzunguka na kutufata fata kwa nguvu usicheke wala kulemba lemba maneno kwa pepo! Mpe amri, mwambie wewe  ulimwasi Mungu songea nipite, wewe shetani mlaaniwa mwenyeji wa kuzimu nasema sasa sogea nipite katika jina la Yesu! 

*** Kama humjui huyo kwenye picha ni mdogo wangu kipenzi Jokate Mwegelo. Missing you, love you dearly****Leave a Reply