Category Archives: General education

KILA MTU ABEBE MZIGO WAKE….. LASIVYO, MWAFA! -Peter Sarungi

Peter Sarungi a.k.a The Next Speaker-Baba Pilato!

Naunga mkono kauli ya Mkuu wa Kaya kwa watani (Wajukuu) wangu wa mkoa wa kagera lakini naunga mkono kwa utani maana tulilia pamoja wakati wa msiba sasa ni lazima niwatanie kidogo kipindi hiki cha matanga.

Naamini hata Mkuu wa Kaya alikuwa anawatania ili kuwarudisha katika hali ya Kazi Tu ingawa bado sijafahamu kama Mkuu wa Kaya ni mtani wenu kikabila au kisiasa, naendelea kufanya utafiti kwa kina.

Huu ndio utani wa kisiasa, wanasiasa wana tabia ya kubadilika badilika kama walivyo wananchi wenyewe (No guarantee at all)Ni Utani tu kwa Wajukuu zangu, dont take seriousl

TANZANIA INAHITAJI MIFUMO IMARA KULIKO VIONGOZI IMARA- Peter Sarungi

Bara la Africa ni moja kati bara lililo wahi kutawaliwa na viongozi washupavu, majasiri na imara kwa muda mrefu bila mafanikio. Historia imeshuhudia viongozi jasiri na imara kama Mandela, Kwame Nkuruma, Gadafi, Idd Amini, Nyerere, Samwel Doo, Samora, Patrick Lumumba, Mugabe, Kawawa Simba wa vita, Mobutu Seseko, Savimbi, Karume, Kabila sr, Kenyatta sr, Obotte, Kagame, Satta na wengine wengi ambao walitikisa Afrika wakati wa utawala wao na wengine wapo mpaka sasa. Historia inaonesha kuwa watawala hawa walikuwa Imara ingawa wengine walitawala kwa mabavu, vita, mauaji ya alaiki na wengi walitawala nje ya mfumo wa demokrasia kupitia chama kimoja. Pamoja na uimara na ujasiri wa hawa viongozi bado Afrika imeendelea kulia na kuteseka na umasikini, maradhi na ujinga kwa viongozi na wananchi wao, Bado Afrika imeendelea kumwaga damu yao wenyewe kwa wenyewe, Bado Afrika imeendelea kuwa dhaifu kutokana na utengano dhidi ya mataifa ya magharibi na Asia, Bado Afrika imeendelea kuwa tegemezi katika afya, elimu, teknolojia, biashara, uchumi, utawala na mengi ambayo yanatoka nje ya afrika.

Tanzania tumebahatika kupata kiongozi imara, shupavu, jasiri na mwenye msimamo. Kiongozi anayeweza kufanya maamuzi na akasimamia maamuzi yake bila kutetereka hata kama yatakuwa na makosa, kiongozi anayethubutu kupita viongozi watatu waliopita. Huyu ni Dr John Pombe Magufuli (Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania), Mimi binafsi namkubali sana Mhe. JPM ingawa ana baadhi ya mapungufu kama binadamu lakini bado ameonesha kuwa yeye ni imara. JPM kwa sasa amekuwa ni gumzo kwa bara letu la Afrika na dunia kwa ujumla. Nimepata kuona taarifa nyingi sana kutoka nchi zingine Afrika na Duniani kuhusu uimara wa JPM na hata mwaka uliopita JPM amekuwa ni Raisi wa Afrika aliyejadiliwa na kupata umaarufu mkubwa kuliko maraisi wengine. Hii ni tunu na sifa nzuri kwa utawala wake.

Pamoja Uimara wa JPM, Bado Tanzania tumendelea kulia kilio cha uchumi duni, afya mbovu, elimu duni, demokrasia na udikteta, uhuru wa kujieleza, upatikanaji wa haki mahakamani, utawala bora, utumiaji wa nguvu na vitisho, wajibu wa bunge na wabunge, uelewa wa haki na wajibu wa raia, uchaguzi huru na wa haki, uzalendo na utaifa. Haya ni mambo yanayo endelea kurudisha nyuma maendelea ya taifa letu kwa kasi kubwa sana.

Hii ina sababishwa na Mifumo mibovu, kandamizi na yenye mianya ya kutenda maovu. Mifumo inatoa nguvu nyingi kwa kiongozi mmoja bila kuwa na njia za kudhibiti akikosea, mifumo inayo elekeza kiongozi kuwa juu ya sheria kwa kauli na matendo, mifumo inayo weza kuyumbishwa mda wowote bila kujali athari, mifumo inayo unganisha chama na serikali kuwa kitu kimoja, Mifumo tegemezi katika taasisi za nchi.

Hii mifumo mibovu ndio chanzo cha wana nchi kuendelea kulia vilia vilivyo zoeleka. Kwa aina ya mifumo hii, hata aje malaika kutoka mbinguni kuja kutawala bila kubadili ni sawa na kutwanga maji ndani ya kinu. Tunaweza kuwa viongozi imara kam JPM hata 50 lakini kwa mifumo yetu bado tutaendelea kuumia kila siku.

Peter Sarungi a.k.a The Next Speaker-Baba Pilato!

#MyTake

Bora kuwa na Mifumo imara itakayo weza kulinda maslahi ya nchi na wananchi wake hata kama kiongozi wa mfumo atakuwa legelege, bado mfumo utamnyoosha na kumlinda kuliko kuwa na kiongozi imara ndani ya mifumo dhaifu, maana siku kiongozi imara akibadilika basi nchi itarudi nyuma tena.

Mhe. JPM ni kiongozi Imara lakini mifumo ya serikali na taasisi zake bado zinaonesha udhaifu mkubwa na ndio maana utumbuaji ni mkubwa mno, Yaani kila kiongozi anayeguswa katika taasisi ni kama ameoza kwa rushwa, uzembe, uvivu na mengine mengi.

Tunahitaji mifumo imara kama ya jirani zetu Kenya na Zambia wanaoweza kusimamia matakwa ya wana nchi kisheria bila kutetereka.

BADILIKA, THIS IS 2017–Daniel Sarungi

 

 • Kipenga kimeshapulizwa wenye mbio zao wameshatoka, wewe bado uko kitandani unaandika happy new year kwenye mitandao ya kijamii
 • Kipenga kimeshapulizwa wewe maliza bajet yote leo kwenye starehe alafu uanze kulalamika eti Mwezi wa kwanza Mgumu utadhani umeubonyeza
 • Kipenga kimeshapulizwa wenzako wanaenda na kasi ya Magufuli, wewe bado unapiga vibomu alafu unalalamika uchumi mbovu
 • Kipenga kimeshapulizwa wenzako wanaenda porini kutafuta pesa na kuja kuzitumia mjini wanaenzi ule msemo wa Mali utaipata shambani /porini wewe unatafuta pesa kati kati ya mji, my friend utapata nauli tu
 • Kipenga kimeshapulizwa wanasiasa wenzako wanaleta matokeo chanya kwenye jamii, wewe umekwama na siasa zako za Maigizo, utaisoma namba vizuri
 • Kipenga kimeshapulizwa wenzako wanatengeneza ajira na kulipa mishahara, wewe umeajiriwa mwaka wa 10 unasubiri bonus, increment na kubagain ongezeko la mshahara alafu bado unataka kuwa celebrity, my friend labda celebrity wa mikopo
 • Kipenga kimeshapulizwa wenzako wanatafuta matatizo ili yawe fursa kwao, wewe ukiona changamoto unakimbia na kuilalamikia serikali, utasubiri sana
 • Kipenga kimeshapulizwa wenzako wanatafuta kazi kwa kufanya kazi za kujitolea kujenga nchi, wewe unasubiri interview, hiyo experience utaipata ndotoni
 • Kipenga kimeshapulizwa wakati wenzako wanahojiwa na forbes magazine wamewezaje kuleta impact Africa nzima, we unakazana kujisifu unafollowers wengi instagram alafu Huna hata mmoja ambae ni rafiki wa kusaidiana.
 • Kipenga kimeshapulizwa wakati wenzako wakipost kwenye mitandao yao ya kijamii wanalipwa, wewe kazi yako ni kuretweet/kurepost na kulike siku nzima bila kupata faida yoyote
 • Kipenga kimeshapulizwa wenzako wanaoipenda nchi yao wanachangia matembezi ya tembo na faru yatakayofanyika Morogoro kwa kununua tshirt, wewe bado unazungusha bia na nyama choma alafu unalalamika watalii wamepungua, unataka waje wakuangalie wewe?

BADILIKA This is 2017 my friend. Sarungi 2017

HUU NI MWAKA WA KUONGEZA NA KUTENGENEZA MAHUSIANO MAZURI NA WANA WA NCHI WA TANZANIA- Peter Sarungi

Kila mwaka una lengo kuu endelevu linalotimizwa kuanzia mwanzo wa mwaka hadi mwisho wa mwaka. Kwa mimi Simba wa Utegi na Babu wa Kagera nimeamua kuweka mwaka huu 2017 kuwa mwaka wa kutengeneza mahusiano ya kijamii, kisiasa na kiuchumi na wananchi. Mahusiano yanatengenezwa kwa kupitia mawasiliano.

Peter Sarungi a.k.a The Next Speaker-Baba Pilato!

Unaweza kunipata kupitia:

1. Public No & Watsup No. +255 713 037 798

2. Facebook ID : Peter sarungi

3. Instagram ID : peter.sarungi

4. E. Mail : [email protected]

5. Tweeter ID : @psarungi

6. Post Code : 9291- Dar es Salaam

7. Physical Adress : Chanika Village – Dar

Hizo ni baadhi ya njia unazoweza kunipata kupitia mawasiliano yangu rasmi kama Next Speaker mwaka 20…

Karibu tuwasiliane katika kujenga nchi ili hata watoto,wajukuu,vitukuu na vizazi vijavyo vije vipate kula matunda yetu

Imetolewa na:

Idara ya Habari na Maelezo ya Peter Sarungi

Raisi-Jukwaa la Walemavu Tz, Next Speaker. Asante sana kaka yangu mimi pia nitakuwa mmoja wa wafuasi wako!

NIWATAKIE HERI YA MWAKA MPYA 2017 WENYE BARAKA NA MAFANIKIO TELE- Peter Sarungi

Peter Sarungi a.k.a The Next Speaker-Baba Pilato!

Kwanza: kabisa, tumshukuru Mungu kwayote yaliyojiri mwaka 2016 yawe mabaya ama mazuri bado tuna wajibu wa kushukuru maana fikra na malengo yetu sio ya Muumba

Pili: Tumshukuru Muumba kwa kuendelea kutupa Uhai usiokuwa na upungufu hata kama upo kitandani ukiwa hoi kwa magonjwa na maumivu makali ama upo bar unakunywa pombe na kufanya starehe mbalimbali, wote yatupasa kumshukuru Muumba kwa huruma yake na upendeleo.

Tatu: Tupeane pole kwa wote tuliopatwa na kuguswa na misiba mbalimbali katika kipindi cha mwaka 2016, tuwaombe wapendwa wetu kwa mungu awarehemu na kuwahifadhi mahala pema mbinguni. Safari ni yetu sote, wao wametangulia tu.

Nne: Tusikate tamaa kwa matarajio tuliyoshindwa kufikia na wala tusibweteke kwa majarajio tuliyafikia katika kipindi cha mwaka 2016 maana Maisha ni mchakato. Ni harakati za kukusanya mambo manne (4) kwa pamoja ili kupata furaha (happy), mambo hayo ni pesa, heshima, afya na mapenzi. Hivyo jua kama wewe una afya njema jua kina mwenzako yuko maututi, kama wewe unapendwa kwa dhati jua kuna mwingine ana danganywa, kama wewe una pesa ya kukidhi mahitaji yako jua kuna mwingi ni fukara asiye na matumaini na kama wewe una heshimika basi jui kuna mwenzako amekuwa teja anayekosolewa mitandaoni. 

Tano na Mwisho, Niwatakie Mwanzo na mwendelezo mwema wa mwaka 2017 ukiwa na baraka, amani, furaha na mafanikio tele katika mipango yako ya mwaka mpya. Mungu akupe nguvu na ujasiri wa kutambua uwezo na karama yako ili uweze kufanya mambo makubwa na uyapendayo katika mwaka 2017. Mwaka 2017 uwe ni mwaka wa kujivunia tofauti na mwaka 2016 ingawa ni mwaka usio gawanyika kwa 2 kama tulivyo aminshwa na wakubwa zetu hapo zamani.

Mungu awa bariki sana na asanteni kwa kuwa mmoja kati ya marafiki wengi, ndugu wengi na jamaa wengi tulio shirikiana kipindi cha mwaka 2016.

“May you and your family be blessed with an awesome year ahead”-Foster Mbuna

2016 has been great in general, even though there are some things I could have done better. I will not be hard on myself but rather planning to take one day at a time and I choose to be happy in 2017.

I refuse to allow any one to take away my inner peace, joy and happiness.

Apologies to those that I have hurt during 2016 am human I wish I could promise never to repeat again but I know I will be lying. Instead let’s remember that as long as we are humans, who come from different backgrounds such incidents are expected.

To those that I have touched or transformed your lives in a positive way you are welcome and hope I can do better if I will be blessed to cross over to 2017.

The only desire that I have for 2017 is to be closer to God and learn from him more.

Otherwise happy reflective last day of 2016 my Facebook friends and family and hope to be better together in 2017.

Boarding on Flight 2017 has been announced……

Hope you have checked in only the best souvenirs from 2016 in your luggage….

The BAD and SAD moments if carried, must be thrown away in the garbage bins on arrival …….

The flight will be 12 months long.
So, loosen your seat belts, jingle and mingle.

The stop-overs will be :

✳Health,
✳Love,
✳Joy,
✳Harmony,
✳Well-being
✳Peace.

Refueling will be at
?Giving
?Sharing
?Caring.

The following menu is offered and will be served during the flight…….

✅ Cocktail of Friendship,
✅ Supreme of Health,
✅ Grating of Prosperity,
✅ Bowl of Excellent News
✅ Salad of Success,
✅ Cake of Happiness,

All accompanied by bursts of laughter…
But remember, you will enjoy these meals and the journey better if you talk, share, smile and laugh together. Sitting silent will make the flight seem longer. Wishing you and your family ? an enjoyable trip on board flight 2017…..

?✨??????❤???☔⛄???????

Before Flight 2016 ends,
May you and your family be Blessed With an Awesome Year Ahead.
???????
Stay blessed?

2016 ULIKUWA NI MWAKA MGUMU SANA ULIOKUWA NA MABADILIKO YA GHAFLA YA JPM by Peter Sarungi

Ni desturi yangu kutathmini mwaka unapofikia mwisho. Nianze kwa kuimba wimbo wangu kwa Tanzania.

“Tanzania eeee, Nakupenda sana x2”

“Hata kama nikilala porini lakini ni ndani ya Tanzania bado nitajivunia”

“Najua wengi wanakutamani ingawa uchaguzi wako bado upo mashakani”

“Nakuaga mwaka kwa maumivu ingawa ni maumivu ya mpito”

“Naamini sasa ni muda wa kula matunda ndani ya mwaka unao anza”

Kwa kifupi mwaka 2016 ulikuwa ni mwaka mchungu na mgumu kwa watanzania masikini na wanyonge wasio jua leo yao itakwishaje na kesho itaanzaje baada ya kuletewa utaratibu wa kufanya kazi kabla ya kula ingawa kazi zenyewe hazipatikani na zingine zinezuiwa kupisha uchunguzi wa HEWA.

Ni mwaka uliokuwa mgumu kwa watumishi wa umma baada ya kulazimishwa mabadiliko makubwa ya utumishi wa serikali na hasa baada ya kuziba mianya mikubwa ya ubadhilifu wa pesa za umma pamoja na kuziba hadi vitundu vidogo vya posho kwaajili ua motisha ya watumishi.

Ni mwaka mgumu kwa wana siasa feki walio ingia kwenye siasa kwa maslahi ya kutajirika. kuna wabunge na madiwani walio tumia nguvu nyingi kupata uongozi, kwa sasa wanajuta ni kwanini walichagua siasa na wengine wana lia hadharani bila kuficha. Lakini pia ni Mwaka mgumu sana kwa wapenda mabadiliko, wana harakati na wapenda demokrasia baada ya kusitishwa kwa shuguli zao za siasa za majukwaa na harakati zingine kama maandamano.

Ni mwaka mgumu sana kwa uchumi wa taifa na wananchi hasa baada ya kutanda kwa UKATA wa hali ya juu sana. imefika mahala ambapo heshima ya ndoa imerejea, heshima ya mshahara imerejea, heshima ya mlo imerejea na hata heshima ya kazi imerejea. Ukuaji wa Uchumi wa nchi kwa mwaka huu nimeufananisha kuwa na kasi  kama ya konokono dhidi ya farasi. Naamini imekuwa hivyo kwa sababu JPM ametumia mwaka huu kuweka misingi sawa, tuangalie mwaka 2017

Umekuwa ni mwaka wa Matamko mbalimbali machungu kwa wanchi katika sekta mbalimbali. Tumepata matamko mengi ya wakuu wa mikoa mbalimbali hasa Dar, matamko ya wakuu katika Mfumo wa Elimu, Afya, Ardhi, Kodi, Usafirishaji, kilimo, Ufugaji, bomoa bomoa, Madini, Umeme na maeneo mengine yaliyo acha alama ya maumivu kwa wananchi.

Tumeshuhudia hadithi za mfalme Juha na simuzili za kusadikika kutoka kwa Polepole, Ben sa8, Yericko nyerere, Faru John, Magoiga, Menuka, Malisa na wengine wengi waliokuwa mstari wa mbele kutupigia hadithi nzuri kwa kila upande kwa mwaka mzima.

Ulikuwa ni mwaka mchungu sana kwa watumishi wa umma zaidi ya 300 walio tumbuliwa mwaka huu kutokana sababu mbalimbali kupitia kauli mbiu ya KUTUMBUA inayoongozwa na mkuu wa kaya akisaidiwa na wasaidizi wake kila idara.

Ulikuwa ni mwaka mchungu sana kwa wafanya biashara za utalii, mahoteli, mabasi, nguo, bar, ujenzi, usafirishaji wa mizigo, wamachinga, madalali, vyuo na mashule, biashara za mitaji na biashara za Bank. Maana tumeshuhudia taatifa za kufilisika kwa baadhi ya biashara hizo kwa sababu ya mdororo wa uchumi. Tusife moyo, mwaka ulikuwa ni wa mapito.  

Peter Sarungi a.k.a The Next Speaker-Baba Pilato!

#MyTake

Mwaka umekwisha na changamoto zake, ikiwa mwaka unao anza utakuwa na changamoto hizi basi tujue ni sisi wenyewe tutakuwa tumezitengeneza. Huu ulikuwa ni mwaka wa majaribio ya mabadiliko makubwa, naamini tutajipanga sasa kukubali na kukabiliana na magumu yanayotokana na Mabadiliko haya kutoka kwa Mkuu wa Kaya…….Mwaka 2017 ukiwa mchungu tena kwako basi jua ni kati ya wewe au serikali kuna mmoja atakuwa ni mzembe wa mabadiliko.

How do you forget?!

How do you forget?

 • The same qualifications you have, diploma, degree, masters, that which gave you that job you have are the same qualifications that your friends have too , but they don’t have the job you have. How do you forget?
 • The same pastor who officiated your marriage and blessed it, today you have even children is the same pastor who officiated and blessed even your friend’s marriages but they don’t have children and eventually divorced . How do you forget?
 • The same prayer you offered to God and God answered you is the same prayer that your friends have been praying, but up to now they haven’t recieved any answer and still praying , how do you forget?
 • The same road you use to travel to places and safely you reach home, is the same road that many people have died on, how do you forget?
 • The same church you go to worship God to and God has blessed you, is the same church that your friend goes to worship God too, but up to now his life is still miserable, how do you forget?
 • The same bed you used in the hospital and you got healed is the same bed that your friends used too but they died in there ,how do you forget?
 • The same voice you have and you can sing songs, you can preach, you can talk and so on, is the same voice that your friends also had but eventually stopped singing,preaching because they had cancer of throat, how do you forget?
 • The same rain that made your field to produce good crops and you had bumper harvest is the same rain that destroyed your friend’s fields, how do you forget?

How do you forget, how do you forget?
Come back to your God and thank Him for his kindness. Whatever you have is not by your power, nor your intelligence, nor your qualifications but the Grace of God. Because what made you where you are and what you have today, your friends have them too, but they are still suffering. Remember the Giver of everything you have, don’t just foolishly boast because He can take them away if He so wishes!
Shalom

JINSI YA KUJENGA JAMII DHAIFU NA BONGOLALA- Peter Sarungi

Nchi za Africa bado zitakuwa na kazi ngumu sana ya ki utawala katika kuunganisha jamii tatu katika nchi ambazo ni Wenye Nchi, Wana siasa na Wana Nchi ili kifikia maendeleo ya kweli. Kwa bahati mbaya kumekuwepo na udanganyifu mkubwa unao fanywa na Wana siasa walio pewa wajibu wa kuunganisha na kuleta mahusiano mazuri katika jamii hizi ili ziweze kufanya Kazi kwa ushirikiano hatimaye kuleta maendeleo ya nchi.

Wana Siasa wengi wa Africa wamevuruga nchi zao kupitia mifumo wanayoiweka katika kuongoza nchi. Wana nchi wengi bado hawajui athari za mifumo mbalimbali katika kuendesha maisha yao ya kila siku. Mifumo hii huanza kuathiri maisha ya wana nchi tangu wanapo zaliwa, ukuaji wao, kuelimika kwao, uchumi wao, afya zao, uhuru wao hadi uzee wao. Mifumo hii inaweza kuamua ni kwa kiasi gani wananchi waelimike, wapate afya nzuri, waajiriwe, wajitegemee, wapate uhuru na mengine mengi yakiwemo yanayohusu siasa. Ndio maana kuna msemo unasema ukiona wafuasi ni wabovu basi jua wametengenezwa na kiongozi wao na ukitaka kujua ubovu ama ubora wa nchi basi chunguza athari zinzowapata jamii husika kutokana na mifumo ya kuendesha nchi.

Watawala wengi wa Africa wamekuwa na uturatibu wa kutengeneza jamii dhaifu na masikini katika kuhoji, kushauri, kufikiri, wasi jitambua na wasio jua wanachokitaka. Watawala wamekuwa wakitengeneza jamii hizi ili kuendeleza malengo yao ya kutwala dola kupitia mifumo. Na kwa bahati mbaya mifumo hii imeweza kuwaathiri hadi wenye nchi na kujikuta wakitumikishwa na Wana Siasa, ndio maana utakuta kuna idadi kubwa ya wanajeshi walio ishia darasa la saba na kidato cha nne kuliko wale waliofika kidato cha sita na kuendelea. Wote hawa hujikuta wakitawaliwa na wana siasa kwa maagizo hata ya kutekeleza jambo kwa mnyonge kwa maana mfumo waliofundishwa na kuapa ni wa kutii bila kuuliza.

Watawala wengi wa Africa wameweza kupitisha na kuhalalisha mifumo ya kuzalisha jamii dhaifu na Bongolala kupitia njia tatu….fb_img_14819059905521. KUDHOOFISHA ELIMU KWA JAMII
Watawala wengi wa Africa wana amini kuwa kutawala jamii iliyo elimika kupitia Elimu bora ni ngumu sana na ina waweka katika riski kubwa ya kutawala milele, hivyo hulazimika kutengeneza jamii kubwa isiyokuwa na elimu ili kudhoofisha uelewa wao na uwezo wao wa kufikiri. Watawala hawa wana vuruga mfumo wa elimu kwa makusudi na kuweka mifumo dhaifu yenye kutoa nafasi ndogo ya wana nchi wachache kupata elimu hadi ngazi za juu na hata hao wanaopata nafasi hiyo hawapati Elimu inayostahili na kumkomboa karika utegemezi.

2. KUDHOOFISHA UCHUMI WA JAMII
Ni ukweli usio pingika kuwa Uchumi imara ni nguvu nzuri kwa jamii. Jamii yenye uchumi imara inaweza kuelimika kwa gharama yoyote ile ikiwa uchumi wao ni imara. Jamii yenye uchumi imara inaweza kuamua kufuatana na maslahi yao hata inaweza kupinga mifumo dhalimu ya nchi na hata kuwapinga watwala. Kwa kuhofia vikwazo hivyo, Viongozi wengi wa Africa wamekuwa wakidhoofisha uchumi wa jamii zao ili kuwafanya wanyonge wasioweza kuhoji ubaya ama uzuri wa watawala. Viongozi wengi wamekuwa wakikusanya pesa nyingi kupitia kodi na kujilimbikizia wao pamoja na utawala wao kama alivyofanya hayati Mobutu Seseko wa Congo. wanapenda sana kuona pesa nyingi zikiwa kwao kuliko kwa wana nchi na ndio maana hata sekta binafsi zina zorota katika kuchangia maendeleo ya jamii.

3. KUDHOOFISHA UHURU WA KUTOA MAONI
Watawala wengi wa Africa hawapendi kusikia maoni tofauti na waliyo nayo wao, hawapendi kusia ukweli walio uficha, hawapendi kupingwa kwa namna yoyote ile. Hivyo watawala hawa wataingiza sheria na taratibu za kuua uhuru wa kutoa maoni kinzani. Inaaminika kuwa kuna watu hata ukiwa dhoofika ki uchumi na ki elimu lakini bado wanaweza kiwa wajasiri wa kutoa maoni yao hata kama ni ya kupinga utawala bila kujali vikwazo walivyonavyo. Hivyo ili kuto ruhusu riski hiyo, watawala huweka mifumo ya sheria za kukandamiza Uhuru wa kutoa maoni na hata Uhuru wa kujieleza kwa jamii.

Peter Sarungi a.k.a The Next Speaker-Baba Pilato!
Peter Sarungi a.k.a The Next Speaker-Baba Pilato!

#MyTake
Africa kama ilivyo nchi ya kisadikika, ina safari ndefu sana ya kubadili mifumo ya nchi. Mabadiko hayo huletwa na jamii iliyovuka vikwazo vitatu hapo juu yaani lazima uwe vizuri kichwani, uwe vizuri mfukoni na uwe na njia nyingi tata za kutoa maoni yako. Kinyume na hapo itakugharimu wewe na familia yako.

Asanteni sana, ngoja niendelee kutunisha mfuko wangu ili itakapo hitajika kubadili mfumo nami niwemo.

Womanhood!

screenshot_2016-12-14-14-39-09-1screenshot_2016-12-14-14-39-02-1screenshot_2016-12-14-10-47-12-1 screenshot_2016-12-13-08-18-37-1screenshot_2016-12-13-08-18-15-1

Happy 70th Annivessary to UNICEF! Thank you for serving and protecting children!

screenshot_2016-12-14-10-46-15-1screenshot_2016-12-14-10-44-58-1screenshot_2016-12-14-10-45-37-1screenshot_2016-12-14-10-45-28-1screenshot_2016-12-14-10-44-04-1screenshot_2016-12-14-10-44-21-1screenshot_2016-12-14-14-48-03-1screenshot_2016-12-14-14-41-26-1screenshot_2016-12-14-14-48-26-1

The art of confidence by Lemutuz

screenshot_2016-12-12-09-19-16-1screenshot_2016-12-12-09-19-32-1screenshot_2016-12-12-09-19-44-1Asante Lemutuz kwa kuongea ukweli bila chenga! Mimi si mpenzi wa muziki ya rap! Si maanishi ni mibaya hapa my brain doesn’t comply with them lol! Honestly, I have selective mind problem hivyo kuna vitu siwezi sikiliza au tazama yani brain yangu ikigoma haivitaki basi mie huwa I keep a distance from them! Mfano mmoja lilishawahi toa huko nyuma kuwa mie sipendi strong bright colors  huwa napata headache kabisa!……….Anyway, turudi kwenye mada!……Binafsi hili swala la watu kutafuta “Kiki” kwa kutumia scandals zisizo na kichwa wala mguu lina nikera na nalichukia mno! Actually I’m a victim of hawa watu wanao tafuta #Kiki!! Watu wameondokewa na hofu ya Mungu kabisa!! Wanacheza na Mungu kama walivyo mchezea mzee Kikwete!!! The devil has corrupted people’s mind mpaka inaogopesha!!………. Huwezi amini kuna watu wapo teyari kucheza na ndoa walizo kula kiapo kanisani / Msikitini mbele za Mungu  ili kutafuta umaharufu!! Hivi ndoa Siniagano takatifu???!!! Watu wamepewa dhamana ya kutumikia wana nchi lakini wapo teyari kucheza na kazi na vyeo walivyopewa kutumikia wana nchi ili kupata stupid attention??! Wasichana na wanawake wazima wanakubali kudhalalishwa ili kupata umaharufu??!!! Tena wengine wanadai wao ni “Wachungaji” lakini matendo yao yatakuacha hoi!! Hiyo yote wanatafuta umaharufu! mmmh! Eeh Mungu tusaidie! Its sad!  This needs to end kwakweli! Naamini katika uongozi huu wa baba yangu Dr Magufuli hawa watu watanyooshwa tuu ?? Sorry Shingongo tafuta biashara nyingine ?? Enough is enough!!

Hongera sana kaka #Darassacmg kwa mfano mzuri wa kuigwa katika jamii yetu!   #Inawezekana  #ItBeginsWithYou

“I’m so proud of you my guardian, sis and mentor” -Jokate Mwegelo

screenshot_2016-12-12-09-17-29-1screenshot_2016-12-12-09-17-20-1Nice! Congrats to her!

Hongera sana Rebeca Ngyumi! 2016 African Women Of The Year in Civil Society And Activism!

screenshot_2016-12-05-12-56-12-1

Hongera sana Rebeca kwa tuzo ulizopata! Wow! Wanawake Watanzania ndio watakao ubadilisha na kuondoa mfumo dume wa unyanyasji wanawake na watoto ndani ya Tanzania na Africa kwa ujumla! Umeonyesha ujasiri mkubwa sana, mfano mzuri mno kwetu sote! “Sina ambacho nitahathirika endapo serikali itasema hii sheria iendelee lakini nafikiri tunajukumu kama wana nchi kuhakikisha tunaweka mifumo mizuri ya sheria ambayo inalinda wana nchi wengine nasiyo tu sisi peke yetu”! Nimependa sana hayo maneno yako! Tatizo kubwa linalo sumbua Bara la Africa ni UBINAFSI! Tuondoe ubinafsi kuwa hilo halinihusu! Sikiliza nikwambie ee mwanamke mwenzangu; kama limemkuta mwanamke au msichana mwenzio basi hilo pia ni LAKO LINAKUHUSU SANA! Kwani laweza kutokea kwako wakati wowote ule au kwa vizazi vyako! Ngoja niseme ule msemo wa Mboni Masimba kuwa “Sauti ya mwanamke ni sauti ya jamii”!! Hivyo ondoa ubinafsi kwa faida ya taifa lako!screenshot_2016-12-05-12-55-33-1Kitu ambacho nimeshindwa kuelewa ni kwanini serikali ilikata rufaa?!! Baba yangu Dr. Magufuli hawa waliokata rufaa nao ni #JIPU tu wanahitaji kutumbuliwa kwakweli!!……….. Unajua hizi bangi za ukubwani ni shida sana, mie hapa ninakaribia kugonga 40 na ndoa bado naigopa kama gereza la Keko halafu eti watu wanapinga maamuzi ya Mahakama?! Kha! Natamani niwajue hawa watu, walikuwa Wanaume au Wanawake? Na nini haswa ilikuwa nia yao!screenshot_2016-12-04-13-19-13-1

Wanawake kwa pamoja tunaweza badilisha Africa lakini kumbuka kuwa siku zote mabadiliko huanza na wewe!!………Hongera sana Rebeca, well done! Very well deserved!!

 

Hongera sana Lyne Charles

screenshot_2016-12-04-17-33-36-1screenshot_2016-12-04-17-29-16-1Hongera sana Lyne Charles kwa kuwa mfano bora kwa vijana wengi haswa watoto wa kike! Taifa letu linahitaji wanawake wengi kama wewe, tafadhi usije acha ku-share njia ya mafanikio yako kwa wengine!

“Stop telling your big dreams to small-Minded people”-Steve Harvey

screenshot_2016-12-04-17-37-45-1

Ushauri umetolewa na Steve Harvey kuwa acha ku-share ndoto zako na watu wenye UFINYU wa mawazo au kwa lugha ya kisasa wanasema watu wenye MAWAZO MGANDO!………. Wanaposema “small-minded” people haina maana kuwa ni watu wenye shida ya pesa au hawana elimu! Hapana! Small-minded people niwale watu ambao hawapendi kuona mwingine anafanikiwa! Niwale watu ambao wana roho za kwanini na yuko tayari kufanya lolote lile ili kumuangusha au kumuumiza mwingine kwasababu tu ya chuki binafsi juu ya maendeleo ya mwingine! Ni watu ambao wanapenda kutoa kasoro kwa mambo ya watu bila ku-offer any solution. Ni watu ambao wanaona mapungufu ya wengine lakini si ya kwao! Ni watu ambao hufurahia anguko la mwingine. Watu wenye elimu lakini hawajaelimika! Hawezi msaidia mtu bila kunyamaza lazima watu wote wajue kuwa alikusaidia………….Kuna watu ambao ni masikini wa pesa lakini tajiri wa roho! Watu kama hawa siku zote wanaamini katika ule msemo usemao WEMA HAUOZI! Kwani kwayeye kutenda wema kwako ndipo Mungu naye atambariki katika mambo yake. Kwahiyo unaweza ukawa hauna pesa lakini una akili na roho kubwa!…,,Stop Telling Your Big Dreams To Small-Minded People!

Kama hauna mazuri ya kuangali kwenye maisha yako binafsi ni vigumu sana kuyaona mazuri kwenye maisha ya mwingine!-Lemutuz

screenshot_2016-11-30-00-06-31-1screenshot_2016-11-30-00-05-38-1screenshot_2016-11-30-00-05-50-1

You don’t belong at the wedding!

screenshot_2016-11-29-23-29-45-1Binasfi nachukulia harusi ni swala personal sana, yani ndugu zako pekee na  wale watu ambao kweli wamegusa maisha yako au wenye kukutakia mema siku zote ndio wanatakiwa kuja kwa harusi yako! Harusi ni kitu kina tokea mara moja katika maisha yako (if no divorce) hivyo lazima uifanye iwe na kumbukumbu za watu au marafiki ambao kweli wana umuhimu kwako……….Kama hujaalikwa kaa kwako utulie!fb_img_1479752684072Tafadhali hii picha haina huusiano wowote na story hii. She is my niece!

“Capitalism au ubepari bado unaendelea kuwa a foreign concept kwa Wabongo”-Lemutuz

screenshot_2016-11-29-10-55-49-1 screenshot_2016-11-29-10-55-18-1screenshot_2016-11-29-10-55-37-1