Category Archives: Maneno ya hekima!

Mungu azidi kuwa nanyi, soon to be Mr and Mrs Majizzo!Hayo ?  ni maneno yake kaka yangu RC Paul Makonda! Wow! Hongereni wote maharusi watarajiwa lakini zaidi hongera sana Lulu! Jamani! Jamani! Binadamu watakesha wakitaka kukuangusha lakini Mungu atakapoamua kukuinua hakuna anayeweza simama mbele yako! Jinsi watu alivyokuwa wakikucheka kuwa unamkosi leo hii the same people wapo busy kukupongeza! Dah! Watanzania Mungu atusaidie. Hivi kama haya si mapenzi ya kweli mtasema ni kitu gani?!! Hizi ndizo katika tabu na raha ambazo Biblia inazungumzia. Siyo kupigana mangumi na kuchinjana mapanga!! Wanaume kama Majizzo ni wanaume wachache sanaaa haswa kwa watu wa Africa!!  Ubarikiwe sana Majizzo kwa kuonyesha mfano bora haswa kwa vijana wa leo. Hongera Lulu enjoy every single moment ya maandalizi yako mpaka harusi. Make sure you got your dreamed wedding wala usiogope. Huu ndio wakati wako wa kuinuliwa juu simama kishujaa tena kwa madaha. Mungu awamiminie neema zake! ?

**Mimi na dedicate wimbo huu wa Hezekiah  Walker " God favored me" kwako Lulu** ?

wakati wao wakiendelea kutoa fact kuna wengine wanapiga hatua za vitendo ~~~~~ Zamaradi Mketema

Wabishi waliishi miaka mingi sana, chunguza hata katika wengi waliofanikiwa sio wenye elimu iliyopitiliza ama waliotoka kwenye familia zenye uwezo PEKEE hapana, ila ni wale waliokomaa na NDOTO ZAO haijalishi background zao ni zipi, leo hii wasomi wangapi wameachwa mbali na watu kutoka streets tu, wakati wao wakiendelea kutoa fact kuna wengine wanapiga hatua za vitendo kupigana na haya maisha na WANAFIKA, lengo ni kukupa moyo wewe uliekata tamaa ya maisha eti kwakuwa hukupata nafasi ya kusoma kutokana na uwezo, ama umetokea mtaani tu kwenye familia ya kawaida/maskini, huna connection nakadhalika, usiitumie hiyo kama excuse, nataka nikwambie INAWEZEKANA hebu taja baadhi ya waliofanikiwa KIUKWELI kutoka MITAANI hata kama hawajulikani ili kuwapa NGUVU wale waliokata tamaa na kuhisi Dunia ni ya watu fulani tu.

 

Kila mtu ni muhimu!~~~~~ Zamaradi Mketeme

Kuna watu hujishusha thamani wanapoangalia wengine wanaoonekana wamewazidi nafasi bila kujua wao huenda ni MUHIMU kuliko hata wanaowaangalia sababu ndio wanaowasababishia UKAMILIFU, 

Natamani ujue kitu kimoja hapo ulipo iwe wewe ni Mpishi, housegirl, shamba boy, messenger ama mwajiriwa tu wa ofisi fulani, thamini na RINGIA unachokifanya na usiruhusu mtu akudharau, hiko unachokifanya Boss wako hata awe na mamilioni bado hawezi kufanya na hiyo ni NGUVU. Ukichukua muda kuchunguza utagundua hakuna alie muhimu zaidi ya mwingine na KILA MTU NI MUHIMU, vipi leo mahousegirl wakigoma wote hata thamani ya hela yako utaiona!? 

Wamama wangapi nyumba zitawashinda, Jiulize Unaweza kufanya wanachokifanya wao fully!? Maana unaitwa Boss sababu kuna watu WALIOKUBALI kukutumikia, Ama hata Kama una ofisi wafanyakazi wakaondoka wote unaweza kufanya kwa ufanisi hiko wanachokifanya wao!?? Kitendo chochote cha kuweza kufanya asichoweza mwingine ni UPEKEE, na upekee ni NGUVU haijalishi unachokifanya ni kitu gani, hivyo usijidharau wala kuona kuna wanaostahili na wasiostahili.. hata kama we ni mpika maandazi mazuri mtaani RINGA, usijidharau halafu ukamuheshimu mama anaepaki gari kila siku kununua maandazi yako kwa kuhisi yeye ndio bora hapana, yeye hawezi kupika kama wewe ndiomana anapaki kwako, na huo uliopewa ni upekee mkubwa ambao wewe ndio wa kuamua uutumie vipi ili uwe na faida sababu hakuna mwingine anaepika kama wewe, 

MUNGU AMEKUPA NGUVU YAKO KUBWA kwa kukutunukia uwezo wa tofauti, hakuna alie BORA zaidi ya mwengine ila tuna MAJAALIWA TOFAUTI, asiekuwa na hiki unakuta ana kingine and viceversa, hivyo heshimu ulichonacho na UJITHAMINI, na zaidi tafuta njia ya kukifanya kwa UKUBWA hata kama ni kitu kidogo kiasi gani maana ndicho ulichopewa na MUNGU!! penye upekee wako ndipo UTAJIRI ULIPO. Haina maana kwakuwa UNATUMWA ukahisi wewe sio muhimu ama anaekutuma ndio mtu hapana, haijalishi unachokifanya ni nini since unaemfanyia hawezi kukifanya mwenyewe basi jua wewe ni wa muhimu pia.

Matatizo yanaweza kuisha na kuwa furaha ~~~ Jackline Mengi

Kwanini usononeke na kukata tamaa kwasababu ya matatizo uliyonayo leo wakati unafahamu kuwa maisha yanaweza kubadilika, matatizo yanaweza kuisha na kuwa na furaha inawezekana? Unaamini haya kwasababu tumeshaona mifano mingi ya waliopitia kwenye shida na taabu nyingi lakini ikafika wakati wakawa na furaha na ndoto zao zikatimia. Hata kwako wewe inawezekana. Mkumbushe unaempenda na unaedhani anahitaji kusikia maneno haya leo.

“watu wema wengi huishia kuwa na sifa ya UBAYA vinywani mwa watu lakini kwa kuwa MUNGU NDIE ANAELIPA!!”>>>> Zamaradi Mketema

Tenda wema unavyotenda, kuwa mwema unavyokuwa, mpende binaadamu unavyoweza, muoneshe kumjali kupitiliza, niamini kitu kidogo kitamsahaulisha yote makubwa tena hakuna ajabu kukuta kinachomfanya akuone mbaya ni haki yako, hakuna anaefanya jema kwa mtu ili alipwe, ila kuna ile hali ya KUONA na kuthamini juhudi anazofanya mtu ambapo hiyo inapokosekana ndio unakuta mtu unakuwa dissapointed kwa namna fulani, maana mara nyingine mtu unatoka hadi nje ya njia zako kumridhisha mtu ama hata kujinyima mara nyingine ili wengine wafurahi hata kama ni kwa kidogo, huenda ndio uwezo wako ulipoishia, lakini hakuna hisia mbaya na zinazoumiza kama kujihisi HUTOSHI ama huna unachofanya hasa kwa mtu ambae deep down unajua unafanya nini na unajali kiasi gani. Nilichogundua ukiwa mwema sana unaowafanyia mara nyingi wanakuonea, watakugandamiza, wata-take advantage of you na zaidi watavuka hadi mipaka yako mara nyingine hata kwa vile vitu vya kutumia tu akili, kiufupi watafanya hadi yale ambayo kihalali wasingeweza kuvumilia kufanyiwa na watu wengine na ukiongea ni KOSA, unakuwa mbaya, tena mara nyingine unaweza hata ukanuniwa, wanataka hata wanapokugandamiza unyamanze UKAE KIMYA hata kama ni haki yako kuongea. Ikikutokea usiumie na wala usiache kutenda pale inapostahili, watu wema wengi huishia kuwa na sifa ya UBAYA vinywani mwa watu lakini kwa kuwa MUNGU NDIE ANAELIPA!! Usiache kujitoa, uzuri yupo na ANAONA!!

“Usiache kumsifu kwa UKUU na UTUKUFU wake pale unapobarikiwa.” -Zamaradi Mketema

Kuna kipindi unasali sana KUOMBA, halafu kuna kipindi unasali sana KUSHUKURU, katika maana maombi yanakuwa machache na shukran zinakuwa nyingi zaidi, na hapo ndipo unapogundua MUNGU ametenda kitu kwako. kama uko kwenye position ya kushukuru endelea na usiache wala kupunguza speed, kama ulivyokazana kwa machozi mbele za MUNGU kuomba akutendee basi lia kwa machozi ya furaha na shukurani mbele zake kwa miujiza aliokuonesha, muombe MUNGU alinde hizo BARAKA zinazokufanya ushukuru, usiache kumsifu kwa UKUU na UTUKUFU wake pale unapobarikiwa.

“Kuwa imara, hakuna alichokiumba Mungu asicho na kusudi nacho”~~~ Faraja Nyalandu

Live your life thinking of who you think you are and not what others think of you. Ukiishi kwa mawazo ya wengine wanavyokufikiria, kuna siku utaishi kama malaika na siku nyingine utaishi kama shetani. Kwasababu binadamu ana uwezo wa kufikiri vyote viwili juu yako. Kuwa imara, hakuna alichokiumba Mungu asicho na kusudi nacho. #WeekendWisdom P. S my country is BEAUTIFUL ?? #Kilimanjaro

“Kazi ya kuajiriwa ni nzuri lakini sio yako ni ya mwajiri wako.” Dina Marios

Naomba niongee na wale ambao tumeajiriwa.Pamoja na kuwa tupo katika ajira tujitahidi kuestablish biashara au mradi wako nje ya ajira yako.Angalia katika mazingira yako vitu gani unaweza kufanya ili kuongeza kipato cha pembeni.Kuna wazee wetu ambao labda wanasoma hapa wameshapitia hizi hatua za maisha.Ila wapo vijana wenzangu humu ambao bado hujastuka au kujipanga sawa sawa.

Binadamu unaouwezo wa kufanya mambo mengi sana ukiamua.Hivyo usijibane sana spread your wings hata kama unalipwa mshahara mkubwa ofisini.

Kazi ya kuajiriwa ni nzuri lakini sio yako ni ya mwajiri wako.Mwajiri wako anaweza kudai kazi yake au hata kuifuta wakati wowote na ukabaki unambwela mbwela tu usijue la kufanya.Mpaka uanze kutafuta kazi sehemu ingine hali inakuwa ngumu lakini kama una miradi na biashara zako zingine wakati unasubiria kupata ajira ingine unaendelea na shughuli zako tena na ukaamua kabisa No kuajiriwa.Nakuomba usijisahau unapokuwa kazini ukamfanyia kazi muajiri wako tu na ukaacha kuanzisha jambo lako mwenyewe.Unaweza kuwa na shamba,biashara yako,ufugaji au una talent fulani ukaitumia.

Kuna dada ameajiriwa lakini hodari sana wa kutengeneza pilipili.Ana biashara ya pilipili/chachandu ambayo inamuinguzia kipato.Tena wateja wakubwa ni ofisini kwake na maofisi mengine jirani.Zipo supermarkets kadhaa na min supermarkets.Ananiambia kwa jinsi anavyopata pesa kwenye pilipili hata mshahara wake ana muda hajaenda bank kuugusa.

Huo ni mfano tu Mungu amekusudia kukufanikisha katika mambo yote.Hivyo kujibana katika kazi hiyo tu ni kumuwekea Mungu mipaka ya baraka alizokupangia.Na Mungu mwenyewe anasema usiogope. Jitahidi kabla upepo haujageuka ukaja kukumbuka shuka kumekucha.Maana huwa vinageuka kwa kushtukiza hata kujipanga hujajipanga na kila siku ulikuwa unasema kesho kesho.

Nashukuru Mungu hata mie nje ya ajira nina biashara yangu ya mafuta ya nazi.Dina Marios baby coconut oil bidhaa ambayo naamini miaka kadhaa ijayo itakuwa brand kubwa ya mafuta ya nazi ya watoto.Nina projects nyingi za wanawake na watoto sijatulia kwa sababu Mungu amenipa uwezo na lazima niutumie Sifa na Utukufu ni kwake yeye aliye juu.

Waliniweka niwe mlinzi wa mashamba ya mizabibu,bali shamba langu mwenyewe sikulilinda…wimbo uliobora 1:6

Kila la heri!

HAPPY WOMEN’S DAY 2017- Peter Sarungi

Peter Sarungi (The next Speaker)

 Nitumie siku hii ya leo kuwatakia heri wanawake wote duniani kwa mchango wao mkubwa na wa kutukuka katika kuendeleza dunia. 

Kipekee nimshukuru Mama yangu kipenzi Bi. Martina Sarungi kwa kuendelea kuwa mama bora kwa watoto wake. Nimtakie maisha marefu na yenye furaha na afya tele ili hata wajukuu na vitukuu waje wafaidike kwa busara na maombi yake.

Pia nimpongeze Mama fidel kwa kuchagua kuwa mama mwema na mwenye malezi yenye maadili, nampongeza kwa kuitwa mama na akumbuke kwamba mafunzo yake kwa mtoto wakati wa malezi ndio nguzo kwa mtoto ukubwani. Sipati picha maisha yangekuwaje bila wanawake, fikiria na wewe alafu naamini utajifunza umuhimu wa wanawake duniani.

Leo natoa dedication ya wimbo wa “power of the women” kwa wanawake wote wanao itwa Grace au Neema maana majina hayo yamebeba historia kubwa sana kwangu. Awe ni bibi, mama, dada, mke, mchepuko ama binti yote hayo ni majini lakini yanasimama kwa wanawake. Nawapenda sana na Mungu azidi kuwapa nguvu katika kutimiza majukumu yenu.

Kama unazifahamu tuambie!-Jackline Mengi

“Women are everywhere but Queens are scarce”!

NIWATAKIE HERI YA MWAKA MPYA 2017 WENYE BARAKA NA MAFANIKIO TELE- Peter Sarungi

Peter Sarungi a.k.a The Next Speaker-Baba Pilato!

Kwanza: kabisa, tumshukuru Mungu kwayote yaliyojiri mwaka 2016 yawe mabaya ama mazuri bado tuna wajibu wa kushukuru maana fikra na malengo yetu sio ya Muumba

Pili: Tumshukuru Muumba kwa kuendelea kutupa Uhai usiokuwa na upungufu hata kama upo kitandani ukiwa hoi kwa magonjwa na maumivu makali ama upo bar unakunywa pombe na kufanya starehe mbalimbali, wote yatupasa kumshukuru Muumba kwa huruma yake na upendeleo.

Tatu: Tupeane pole kwa wote tuliopatwa na kuguswa na misiba mbalimbali katika kipindi cha mwaka 2016, tuwaombe wapendwa wetu kwa mungu awarehemu na kuwahifadhi mahala pema mbinguni. Safari ni yetu sote, wao wametangulia tu.

Nne: Tusikate tamaa kwa matarajio tuliyoshindwa kufikia na wala tusibweteke kwa majarajio tuliyafikia katika kipindi cha mwaka 2016 maana Maisha ni mchakato. Ni harakati za kukusanya mambo manne (4) kwa pamoja ili kupata furaha (happy), mambo hayo ni pesa, heshima, afya na mapenzi. Hivyo jua kama wewe una afya njema jua kina mwenzako yuko maututi, kama wewe unapendwa kwa dhati jua kuna mwingine ana danganywa, kama wewe una pesa ya kukidhi mahitaji yako jua kuna mwingi ni fukara asiye na matumaini na kama wewe una heshimika basi jui kuna mwenzako amekuwa teja anayekosolewa mitandaoni. 

Tano na Mwisho, Niwatakie Mwanzo na mwendelezo mwema wa mwaka 2017 ukiwa na baraka, amani, furaha na mafanikio tele katika mipango yako ya mwaka mpya. Mungu akupe nguvu na ujasiri wa kutambua uwezo na karama yako ili uweze kufanya mambo makubwa na uyapendayo katika mwaka 2017. Mwaka 2017 uwe ni mwaka wa kujivunia tofauti na mwaka 2016 ingawa ni mwaka usio gawanyika kwa 2 kama tulivyo aminshwa na wakubwa zetu hapo zamani.

Mungu awa bariki sana na asanteni kwa kuwa mmoja kati ya marafiki wengi, ndugu wengi na jamaa wengi tulio shirikiana kipindi cha mwaka 2016.

“May you and your family be blessed with an awesome year ahead”-Foster Mbuna

2016 has been great in general, even though there are some things I could have done better. I will not be hard on myself but rather planning to take one day at a time and I choose to be happy in 2017.

I refuse to allow any one to take away my inner peace, joy and happiness.

Apologies to those that I have hurt during 2016 am human I wish I could promise never to repeat again but I know I will be lying. Instead let’s remember that as long as we are humans, who come from different backgrounds such incidents are expected.

To those that I have touched or transformed your lives in a positive way you are welcome and hope I can do better if I will be blessed to cross over to 2017.

The only desire that I have for 2017 is to be closer to God and learn from him more.

Otherwise happy reflective last day of 2016 my Facebook friends and family and hope to be better together in 2017.

Boarding on Flight 2017 has been announced……

Hope you have checked in only the best souvenirs from 2016 in your luggage….

The BAD and SAD moments if carried, must be thrown away in the garbage bins on arrival …….

The flight will be 12 months long.
So, loosen your seat belts, jingle and mingle.

The stop-overs will be :

✳Health,
✳Love,
✳Joy,
✳Harmony,
✳Well-being
✳Peace.

Refueling will be at
?Giving
?Sharing
?Caring.

The following menu is offered and will be served during the flight…….

✅ Cocktail of Friendship,
✅ Supreme of Health,
✅ Grating of Prosperity,
✅ Bowl of Excellent News
✅ Salad of Success,
✅ Cake of Happiness,

All accompanied by bursts of laughter…
But remember, you will enjoy these meals and the journey better if you talk, share, smile and laugh together. Sitting silent will make the flight seem longer. Wishing you and your family ? an enjoyable trip on board flight 2017…..

?✨??????❤???☔⛄???????

Before Flight 2016 ends,
May you and your family be Blessed With an Awesome Year Ahead.
???????
Stay blessed?

“Wanasema eti Tanzania hatuna demokrasia lakini hawasemi wanatulinganisha na nani?”-Hoyce Temu

screenshot_2016-12-09-10-05-52-1screenshot_2016-12-09-10-01-55-1screenshot_2016-12-09-10-02-06-1????

“Vijana wa sasa hampendani kabisa ni chuki na wivu tu ni hatari sana kwa maendeleo ya society yetu”-Lemutuz

screenshot_2016-10-07-12-15-10-1-1screenshot_2016-12-03-16-24-12-1screenshot_2016-12-03-16-24-45-1

Manhood!

screenshot_2016-11-25-16-21-33-1 screenshot_2016-11-25-16-01-34-1

Manhood!

fb_img_1480017723731Everyday we’re given an opportunity to make a positive impact on the people and communities that surround us. What was your impact today? // Kila siku tunapewa nafsi ya kufanya jambo lenye matokeo mema kwa watu na kwa jamii zinazotuzunguka. Leo umefanya jambo gani jema? —Mo

fb_img_1480017757090Good morning my friends
NAWATAKIA SIKU NJEMA NA BARAKA ZA MUNGU JUU YAKO, WEWE ULIYE NA KAZI FANYA KWA BIDII KWA MAANA WAPO WENGI WANAOITAMANI KAZI KAMA YAKO NA HAWAJAIPATA, NAWE USIYE NA KAZI USIKATE TAMAA ALIYEWAPA WAO BADO HAJABADIRIKA NI YULEYULE NA WEWE ZAMU YAKO ITAFIKA. Nawapenda Sana Rafiki Zangu.

Wapo wakukupa umbea, lakini wakukupa pesa hakuna!

screenshot_2016-11-21-12-31-05-1??? UMBEA ni bidhaa cheap sanaaa ndiyo maana inagaiwa kama njugu! Uwezi amini kuna watu unaweza waheshimu sana kama hujakaa nao karibu yani uwaone kwa mbali tu maana ukiwavuta kwa karibu unaweza TAPIKA NYONGO ??? Wana elimu na CV za kufa mtu lakini Mwe eee! ???Wanamajungu mfano hakuna!! Wanapenda umbeya utafikiri walizaliwa kwenye mitalo! Wana elimu lakini hawajaelimika!! Sasa chuki kwa watu ndo usiseme kabisaaaa! Furaha ya wengine ni msiba kwa maisha yao hivyo kila siku iyendayo kwa Mungu wao ni vilio, misiba na matanga yasio isha!!……..Hawa watu wahivi ni wakuwahurumia tu, tuwaombee tu kwakweli kwani hakuna amani ndani ya roho zao!…… WAPO WAKUKUPA UMBEA LAKINI WAKUKUPA PESA HAKUNA!! Jitambue, jithamini, jijenge kwa kukataa umbea, kwa kukataa majungu! fb_img_1479752624163TAFADHALI: Hii picha ya jirani yangu Janeth haina huusiano wowote na story hii au nilicho andika! Nimependa uzuri na urembo wake wa ASILI ndiyo maana nimetumia!!

“Picha hii imenikumbusha mbali sana wakati nasoma primary kijijini” ~~~Hoyce Temu

screenshot_2016-11-21-08-37-13-1???  Nimecheka siyo kwamba ni mazuri bali nimejisikia “kafaraja kidogo” ndani ya moyo wangu kuwa kumbe siyo mimi tu peke yangu ndio nilisoma shule za #Kata au za watoto wa “walala hoi” wakati wa kutafuta elimu ya msingi. Kumbe hata Hoyce Temu naye alisoma kwenye shule za mazingira haya?!  Wow! Kweli ulikotoka hakuna tija bali uendapo ndio mambo yote!?? Kumbe hata sisi tuliosoma shule za #kata huwa tuna ndoto ya kufanya mambo makubwa na kufanya dunia kuwa sehemu nzuri ya kuishi?! Kha! Kumbe inawezekana eeh!…….. Asante Hoyce kwa kutumege kidogo story yako! Naomba Mungu awajalie viongozi wote wa bara la Africa roho ya imani na utu ili waweze kutumikia watu wao kulingana na maadili ya uongozi na matakwa ya Mwenyezi Mungu. Africa bila vita inawezekana! Africa bila njaa inawezekana! Africa bila unyanyasaji kwa wanawake na watoto inawezekana! #UsikateTamaa #ItBeginsWithYou

screenshot_2016-11-21-08-37-43-1

Are you “ordinary” or “extra ordinary” person?!

fb_img_1476361401001Mmmmh ? akili ni nywele kila mtu anazakefb_img_1476157240029