HAPPY WOMEN’S DAY 2017- Peter Sarungi

Peter Sarungi (The next Speaker)

 Nitumie siku hii ya leo kuwatakia heri wanawake wote duniani kwa mchango wao mkubwa na wa kutukuka katika kuendeleza dunia. 

Kipekee nimshukuru Mama yangu kipenzi Bi. Martina Sarungi kwa kuendelea kuwa mama bora kwa watoto wake. Nimtakie maisha marefu na yenye furaha na afya tele ili hata wajukuu na vitukuu waje wafaidike kwa busara na maombi yake.

Pia nimpongeze Mama fidel kwa kuchagua kuwa mama mwema na mwenye malezi yenye maadili, nampongeza kwa kuitwa mama na akumbuke kwamba mafunzo yake kwa mtoto wakati wa malezi ndio nguzo kwa mtoto ukubwani. Sipati picha maisha yangekuwaje bila wanawake, fikiria na wewe alafu naamini utajifunza umuhimu wa wanawake duniani.

Leo natoa dedication ya wimbo wa “power of the women” kwa wanawake wote wanao itwa Grace au Neema maana majina hayo yamebeba historia kubwa sana kwangu. Awe ni bibi, mama, dada, mke, mchepuko ama binti yote hayo ni majini lakini yanasimama kwa wanawake. Nawapenda sana na Mungu azidi kuwapa nguvu katika kutimiza majukumu yenu.

Leave a Reply