Category Archives: Mahusiano

Sherehe ya kipekee ya kumuaga Dorice Sassi Igogo!

Ameagwa rasmi! Siku ya Jumatano, tarehe 06/02/2021 zilisikika nderemo na vigelegele vingi sana kutoka kwa familia ya Mr. Emmanuel Agonda Sassi (marehemu) na Mrs. Magreth Cornel Awiti a..k.a Mrs Agonda, a.k.a Mrs Sassi pamoja na wanaukoo wote wa Adol Igogo. Ilikuwa ni furaha ya kumuaga rasmi binti yao kipenzi Mwalimu Dorice Sassi Igogo ambaye anakwenda kuanzisha rasmi kaya (familia) yake.

Dorice akiwa na mtarajiwa wake

Ndoa ni jambo la kheri, ndio maana wazazi hufanya sherehe ya kipekee kabisa ili kumuaga mpendwa wao, kama njia mojawapo ya kuonyesha furaha yao na shukrani kwa Mungu.

Dorice a.k.a Vumilia ni binti aliyezaliwa katika familia ya watoto (3) watatu, yeye akiwa mtoto wa pili kuzaliwa na msichana pekee.

Mtoto wa kwanza ni Yustor Sassi (Kulia), Dorice, na Joseph (kushoto). Katika picha hii inaonyesha makaka wakimlisha keki dada yao, na mama mzazi akiwa pembeni anaangalia.

Yustor akiwa nafuraha nyingi wakati wa kulishwa keki na dada yake.

Joseph naye akifurahia kulishwa keki na dada

Yustor akimpigia saluti mdogo wake, kwa heshima kubwa kama afanyavyo huko jeshini!

Tazama jinsi kaka wa bibi harusi mtarajiwa akitoa saluti kwa mdogo wake kwa furaha na ushupavu wa kijeshi.

Bibi harusi mtarajiwa akielezea historia yao, wapi walikutana na nini kiliwakutanisha.

Zawadi kwa bwanaharusi mtarajiwa

Bibi harusi mtarajiwa akiwa na Mc wa shughuli hiyo ajulikanaye kama McKatokisha

Wamazazi wa upande wa bibi harusi mtarajiwa

Yani mdogo wangu huyu kwa kuchakarika aaah! Ni Mwalimu na pia ni mjasiriamali wa nguvu. Hii keki ametengeneza mwenyewe kwa mikono yake kupitia kampuni yake ya isadoricakes and sassyjuice! Izidi barikiwa kazi ya mikono yake.

Mtarajiwa akikata keki

Akilimlisha mama mzazi kwa unyenyekevu na upendo mwingi

Akimpatia mama mzaa chema keki yake kama ishara ya upendo na ukarimu wake kwake na ukoo wa mumewe mtarajiwa.

Mama mzazi naye alipata kipande chake

Mama wazaa chema na binti yao

Wamependeza kwakweli

Haya ngoja nikusaidie kidogo kama haujui, bibi harusi mtarajiwa ni mtoto wa mama yangu mdogo. Mama yake ndio kitinda mimba kwa uzao wa bibi yangu mzaa mama. Sasa basi, kama ilivyo kwa mama yake Geoffrey Kateti (kama mnamkumbuka) ndivyo ilivyo kwa mama yake na bidada hapa. Mama yake naye alifuata nyayo za dada yake (mama yangu) akaolewa Utegi! Utegi oyeeee! ?? Tofauti na mama yake Geoffrey, mama yake Dorice ameolewa ukoo mmoja na dada yake ?? chezea ukoo wa Odol! Hivyo Dorice ni mdogo wangu pande zote; kwa baba na kwa mama.

Mapenzi ya Mungu yalitimizwa baba yangu mdogo (baba wa bibi harusi mtarajiwa) aitwae Emmanuel Agonda Sassi, alishalala usingizi wa mauti takriban miaka 4 iliyopita. Twamshukuru Mungu kwa yote.

Once again, hongera sana mdogo wangu, shemeji tunakukaribisha kwetu kwa mikono miwili. Mungu awe nanyi siku zote. Amen! ????

?@lush___makeup

? @mckatokisha

? Decor@lillies_luxe_decor

#FBF

Embu tujikumbushie mambo yalivyo kuwa siku ya kuvikana Pete ya ahadi ya ndoa /uchumba, siku ya Jumatatu ya mwezi wa kwanza tarehe kumi na mbili mwaka huu, 01/12/2021. Love is the beautiful thing.

Kitchen party ya RHoda Igogo

Bibi harusi mtarajiwa Rhoda Alexander Igogo

Wakati tukisubiria picha kutoka kwa wataalamu waliolipwa kufanya kazi hiyo, basi tuanze na tulizonazo.

Siku ya jumapili tarehe 05 /16 /2021 ilifanyika sherehe ya kumfunda mwali (bibi harusi mtarajiwa) a.k.a Kitchen party ya Rhoda Alexander Igogo. Sherehe hii aliandaliwa na mama yake mlezi akishirikiana na ndugu na jamaa pamoja na marafiki. Ilifanyika kwenye makazi ya wazazi walezi huko Segerea ambapo bibi harusi mtarajiwa ndipo anapo ishi na ndipo atakapotokea kwenda kwa mwenza wake.

Akiingia ukumbuni mwenye nyuso ya furaha na tabasamu kama lote ndio mama mzazi wa Rhoda na Isaka, Mrs Joyce Alexander Igogo. Ni mke wa marehemu baba yangu mkubwa (wapili kuzaliwa kwenye familia yao baba, watoto bibi Rhoda Nyakanga Olwengo). Babu yangu mzaa baba (Marehemu mzee William Olung’a Igogo) alikuwa na wake watano (5) ??? usishangae sana maana marehemu babu yake baba (my great grandfather) Chief Sarungi Igogo yeye alikuwa na wake 19 ??????? welcome to our ukoo ?? …… Rhoda ndio mtoto wa mwisho kwao. Akitoka kuzaliwa Isaka ndio Rhoda anafuata. Na harusi zao zimekuwa ndani ya mwezi mmoja. Familia hii inajumla ya watoto 7 walio hai, mmoja alifariki. Grace a.k.a Anyango, Aphino a.k.a Nyawade, Kenneth (Marehemu) a.k.a Ukombozi, William a.k.a Mzee, Dr. Obadiah, Isaka, na Rhoda a.k.a Nyolwengo, na Emilia Igogo! ….. Mungu ni mwema sana.


Haya embu tufurahishe macho kwa hizi tilizonazo!

Pichani ni Dia Alex Odemba na bibi yake mama Igogo.

Dada kama dada! Huyu ni dada yake Rhoda aitwae Aphino.

Dia Alex Odemba katika ubora wake!

Mama wa isadoricakes_and_sassyjuice. Dogo langu Mwalimu mwenye ujasiriamali wake! ??

bibi harusi mtarajiwa akikata cake yake

Kwamahitaji yako ya Cake nzuri zenye ubora wake, juice fresh tamu, na Mc wa kitchen party, tafadhali husisite kumtafuta @isadoricakes_and_sassyjuice ndio habari ya taifa! ???

Kutoka kushoto ni mama yangu mzazi, akifuatiwa na mdogo wangu Vumi Sassi, anayefuata ni mdogo wake mama yangu (kitinda mimba kwa familia yao) napia ni mama yake Vumi aitwaye Magreth Cornel Awiti a.k.a Mrs Agonda Sassi, na anayefuata ni mdogo wangu kipenzi Magreth Rhoda-Nyasungu a.k.a Mrs Massawe.

?? mama zangu hao! ??

Rhoda akiingia ukumbini kwa furaha kabisa

Mama mlezi wa Rhoda

Mrs Vetto Igogo (kushoto) pamoja na Mrs Isaka Igogo (kulia). Mmemuona bibi harusi wetu wa wiki iliyopita?! ?? Miguu imeiona? Miguu halisi ya Kiafrika! Yani wana miguu ya bia kama mawifi zao! ??

Baba naye hakutaka kupitwa na matukio katika picha ?? akiwa na furaha kubwa pamoja na binti zake akitaniana na ucheshi wa hapa na pale.

Mtu na wifi zake! Mrs. Massawe kwa mbele hapo, Mrs Vetto Igogo mtu kati, na Mrs Isaka Igogo nyuma hapo.

Wifi karibu sana Utegi!

Watu wakiserebuka kwa raha zao!

Mke ya Mrombo! ??

Mwenye nguo ya njano, anayecheza kwa hisia zote, ni dada wa bibi harusi mtarajiwa, aitwaye Grace Alexander Igogo a.k.a Anyango, yeye ndio mzaliwa wa kwanza kwa familia yao. Anafurahia kusindikiza kitinda mimba kuanzisha familia yake. Pembeni yake ni mama mlezi wa Rhoda.

Mama naye hakutaka kujivunga kwani wimbo wenyewe siunausikia? ???

Haya tunamtakia Rhoda safari njema katika kuhitimisha kilele cha sherehe za kuagwa kwake na familia yake mpaka siku ya harusi. Jumapili hii ni Send-off yake na Jumapili ijayo ndio harusi. Mungu awatangulie katika kila jambo!

BTW, hii siyo mara yakwanza kwa familia yetu kuwa na harusi mbili kwa mpigo (double wedding), kaka yangu mkubwa Vetto Igogo na dada yangu Elline Igogo harusi zao zilipishana wiki tu, tuliserebuka kwa wiki mbili mfululizo! Yani tulianza na kitchen party ya dada Elline, ikafuta harusi ya kaka Vetto, ikaja Send-off party ya dada Elline kisha harusi yake. Na baada ya hapo ikafuata sherehe ya kuvunja kamati. ??? I tell you, this familia loves to partyyy! Nahiyo ni miaka ishirini na mbili (22 yrs ago) iliyopita. Na sherehe zao Ilikuwa kubwa kweli kweli hizi ni chamtoto! Mama zigi-zig catering na Dotnata Catering walipika mpaka walishangaa. ???

***Updates: picha za nyongeza***

Rhoda na binamu yake Honorable Madam Judge Dr Modesta Opiyo.

Rhoda na mama yake mzazi

Juu ni mama mkwe wake Rhoda Mrs Scola Oguna Ollal.

Mawaidha ya akina mama, shangazi, na wanawake wachanga kwenye ndoa.

Mama mdogo Mrs O.O Igogo akitoa ombi la kwanza.

Mama mdogo Mrs Agonda Sassi akitoa ombi la mwisho. Walianza na Mungu wakamaliza na Mungu. Amen!

Kwa picha zaidi bonyeza ????

https://RHEVANSTUDIO2021.pixieset.com/pendokitchenpartyphotos/

Rhoda na rafiki yake, hizi ni pre-wedding pictures

Blessing latika ubora wake

Wadada hao! ??

Kwa picha zaidi bonyeza ????

https://RHEVANSTUDIO2021.pixieset.com/rhodapresendoffphotos/

Hongera sana Isaka na Sarah!

Mr and Mrs Isaka Alexander Olung’a Igogo

Hayawi hayawi sasa yamekuwa! Wamehalalishwa duniani na Mbinguni yakwamba wawili hawa ni mwili mmoja!

Sarah akila kiapo kitakatifu

Agano hili takatifu lilifanyika siku ya Jumosi tarehe 05 /08/2021 katika kanisa la viziwi lililopo huko Bunguruni, Dar es salaam. Tunawaombe baraka nyingi sana katika familia yao hii mpya walio ianzisha!

Bibi harusi

Bwanaharusi akihakikisha je kweli ni yeye?! Kabla ya kula kiapo, maana hukawii kubadilishiwa mke kama Jacob (Yakobo)! ? mjini mambo mengi jama! ?

Bwanaharusi amehakikisha na ameridhia! ?? Kama hujawahi sikia kisa cha Jacob (Yakobo) basi chukua Biblia yako na ufungue kitabu cha mwanzo sura 29 yote itakupa stori kamili!

Kwaufupi ni kwamba, Jacob baada ya kutumikia miaka saba kwa mzee Labani kama mahari ya kumuoa binti yake Rachel (Raheli), siku ya harusi akakuta amebadilishiwa mke anaye mpenda kwa dhati na kupewa Lea ambaye alikuwa ni dada wa Rachel (Raheli). Kwani kulingana na mila na desturi za kabila na ukoo wa mzee Labani ni kuwa mkubwa lazima aolewe kwanza ndipo mdogo anafuata. Kwa maana hiyo Jacob ilibidi atumikie miaka 7 mingine ili aweze kumpata Rachel. Kwa maana hiyo Jacob alitumikia miaka 14 kwa mzee Labani kama mahari ya kumuoa kipenzi cha roho yake! …… Sikilizeni wanawake wenzangu, kama mwanaume anakupenda basi hakuna gumu wala zito mbele ya macho yake! He will move mountains just to have you! Tena bila hiyana yoyote! Wanawake wazuri ni wengi sana lakini Mke ni mmoja tu ambaye kila mwanaume anajua hilo!

Maharusi na wapambe wao
Wasimamizi wao
Mchungaji aliye idhinisha ndoa hii

Sarah akisindikizwa na kaka yake aitwaye Alex ambaye ndiye aliyemlea toka wazazi wake wamefariki hadi leo hii anapokwenda kuanzisha nyumba yake mwenyewe. Kwa Sarah hamuoni Alex kama kaka bali ni baba yake mlezi na mke wa Alex ni mama yake mlezi, hao ndio wazazi wa Sarah.

Hapo juu ni baba mlezi wa Isaka ajulikanaye kama mzee O.O Igogo. Yeye ndio amemlea Isaka toka akiwa na miaka 5. Baba mzazi wa Isaka amefariki takribani miaka 7 iliyopita. Mzee 0tieno Igogo ni mdogo wake na marehemu mzee Alexander Igogo ambaye ndiyo Baba yake na Isaka.

Mama mlezi wa Isaka Mrs O.O Igogo akisalimia maharusi, nyuma yake ni mjukuu wake aitwaye Essy.

Mashangazi na mama wakubwa kwa wadogo upande wa bwanaharusi.

Baba mlezi akiwa na furaha nyingi usoni kwa kuongeza mtoto mwingine kwa familia.

Madada, mabinamu, na mashemeji wakiingia kwa shangwe!

Kutoka kulia, ni mdogo wa bwanaharusi aitwaye Blessing, akifuatiwa na mpwa (niece) wa bwanaharusi Essy, akifuatiwa na shemeji mkubwa Mrs. Vetto Igogo, na dada mkubwa (wapili kuzaliwa kwenye familia ya kina Isaka) Aphino Alexander Igogo (Mrs Ogoche).

Mdada mwenye nguo ya blue kutoka kushoto, huyo ndio kitinda mimba kwenye familia ya akina Isaka. Anaitwa Rhoda Alexander Igogo. Naye harusi yake ni mwishoni mwa mwezi huu. Wiki hii ni kitchen party yake.

Bibi harusi mtarajiwa Rhoda Alexander Igogo akiwa na maharusi Mr and Mrs Isaka Alexander Igogo.

Bibi harusi mtarajiwa, bi Rhoda akifurahia kaka kupata “jiko”!

Mama mlezi wa bwana harusi pamoja na baba msimamizi wa ndoa hii mzee Samuel Olung’a Igogo wakitoa nasaha zao.

Baba mlezi akitoa neno kwa niaba ya kamati!

Mama mlezi akiwa na maharusi

Maharusi wakikata keki!

Wapendwa, kwamahitaji yako ya Cake nzuri zenye ubora wake, juice fresh tamu, na Mc wa kitchen party, tafadhali husisite kumtafuta @isadoricakes_and_sassyjuice ndio habari ya taifa! ???

nnnnn

Maharusi wakifungua dancing floor kwa kucheza ziro-diatance music ?? asiye na wake akumbatie chupa ya soda! ???

Meza kuu upande wa bibi harusi

The Olung’as!

Hawa ni baba zake Isaka, wadogo kwa wakubwa. Kutoka kushoto ambaye kichwa tu ndio kimeonekana ni mzee Samuel Olung’a Igogo (baba mkubwa na msimamizi wa ndoa hii), akifuatiwa na mzee Charles Olung’a Igogo (baba mkubwa), akifuatiwa na mzee Otieno Olung’a Igogo (baba mdogo na mlezi wa Isaka), akifuatiwa na Genga Olung’a Igogo (baba mdogo)

Walianza na Mungu, wakamaliza na Mungu. Mama mdogo wa Bwanaharusi Mrs Emmanuel Agonda Sassi Igogo akitoa sala ya mwisho!

Mathayo 19:5 “akasema, Kwa sababu hiyo, mtu atamwacha babaye na mamaye, ataambatana na mkewe; na hao wawili watakuwa mwili mmoja”!

Marko 10:9 “Basi, alichokiunganisha Mungu mwanadamu asikitenganishe” ….. I present to you Mr and Mrs Isaka Alexander Olung’a Igogo

Mc Rhevan mtu kati hapo

picha zote shukrani kwa Mc Rhevan studio. Ukitaka kuona picha za tukio nzima tembelea ????https://RHEVANSTUDIO2021.pixieset.com/isakaandsarahweddingphotos/

Tunawaombea kheri na baraka nyingi!

Bwana harusi mtarajiwa-Isaka akiwa kwenye pozi na bibi harusi mtarajiwa-Sarah

Kesho ndio siku yenyewe kuu, ambapo wawili hawa wataunganishwa kuwa kitu kimoja na koo mbili zitaunganishwa rasmi mbele za Mungu.

Naam, kwamara nyingine tena tunapenda kutoa pongezi nyingi sana kwa watarajiwa hawa kwa kufanya maamuzi mazito yenye busara. Mungu azidi kuwatangulia katika kila jambo ambalo limepangwa kufanyika kesho basi likapatae kibali mbele ya uso wa Bwana na lifanyike kama lilivyopangwa kwa utukufu wa Mungu.

Mwenyezi Mungu mwenye wingi wa rehema na neema awazidishie ulinzi wake na mibaraka yake siku zote za maisha yao. Ndoa yao ikajae amani na furaha, naye Mungu Baba awe mgeni wao siku zote. Wakabarikiwe wao na uzao wao wote. Twaomba kwa imani katika jina la Yesu. Amen! ????

akasema, Kwa sababu hiyo, mtu atamwacha babaye na mamaye, ataambatana na mkewe; na hao wawili watakuwa mwili mmoja!” *** Matayo 19:5

“Kwa sababu hiyo mtu atamwacha babaye na mamaye, ataambatana na mkewe” ****Marko 10:7

Jana ilikuwa siku ya kuagwa kwa bibi harusi mtarajiwa. Bi. Sarah alifiwa na wazazi wake wote wawili akiwa mdogo. Kaka yake Alex akamlea hadi sasa anatokea kwao kwenda kwake na mumewe mtarajiwa. Ni mlemavu wa kusikia na kusema??‍♂️ Hapo anatoa shukrani zake za moyoni kwa walezi wake siku ya kuagwa, na kuwapa zawadi alizomudu kama ishara ya shukrani na kumbukumbu. Mume wake mtarajiwa naye ana historia inayotaka kufanana na yake! Hawa wawili ni kielelezo halisi na ushuda hai kwamba kazi ya Mungu haina makosa.

Mimina neema zako Bwana mimina ????

??? mnaona mama zangu na shangazi yangu aliyegoma kuzeeka pale nyuma na tabasamu kama lote wakikumbushia enzi zao?! ?? so sweet!

Wababa nao hawakubaki nyuma! ??

Picha zote shukrani kwa Mc Rhevan , mtembelee Instagram @mc_Rhevan au website yake ???? https://mc.rhevan.com/

“mpenzi yoyote yule anayekupiga kuna siku ATAKUUWA TU sio mtu wa kumchezea”

Regrann from @lemutuz_superbrand  -  LIVE STRAIGHT TALK: FACTS The Art of Love and Hate takwimu zinaonyesha kati ya Mwaka 2016 na leo 2018 Jumla ya Wananchi 341 wameuliwa na Wapenzi wao kati yao ni Wanawake ndio waliouliwa zaidi yaani Wanawake 247 na waliobaki ni Wanaume waliouliwa ni 94 wote wamekufa kwenye mapenzi na hasa ndoa inasikitisha sana ...kinachosikitisha sana ni the fact that Jamii imenyamaza kimya Wabunge wetu hawana hata habari na Wanasiasa wetu ndio wamekuwa mabubu kabisa sababu? ni Maadili yetu zaidii ya kuficha mapungufu ya Ndoa kwa Mwanaume kulalamika kwa jamii kuwa hamuelewi mke wake ni Aibu sana na Mwanamke kulalamika kwa jamii kuwa hamuelewi mumewe pia ni Aibu ya kuahindwa kuficha mambo ya ndani ya ndoa na matokeo yake ndio haya Taifa limepoteza Nguvu kazi ya Wananchi 341 ...nani anatakiwa kuhusika na afanye nini? ndipo tunapokwama na ninarudia tena na tena kwamba huu ni wakati muafaka Serikali ikaanza kulitupia macho hili tatizo ambalo chanzo chake ni Mapenzi na hata kwenye kuua huwa wanajiamini kwamba wanafanya kitu sawa kwa niaba ya mapenzi yao kwa wanaowaua ...tunatakiwa kuimarisha our Social Welfare Services ziwe na Professionals wanaoweza kusuluhisha matatizo ya Ndoa mara wanapoarifiwa tu na hata wapewe nguvu za kisheria za kuwaweka Rumande Wanaume na Wanawake waanaonekana kuwa chanzo cha matatizo ya kufikia kupigana katika ndoa au mapenzi ....ninasema hivi hatuwezi kuwa na Viwanda imara kama hatuna Wananchi Imara na sisi wananchi its about time sasa tukaanza kuamka usingizini hakuna mapenzi ya kupigana pigana mpenzi yoyote yule anayekupiga kuna siku ATAKUUWA TU sio mtu wa kumchezea I mean mpenzi anayepiga ni hatari sana ni most of the times ni kwa sababu amekulia kwenye ndoa ya Mama yake kupigwa na Baba yake au Baba yake kupigwa na Mama yake guys usicheze na mpenzi wa aina hiyo cause atakuuwa ....ndio maana USA watu wa namna hii wakifungwa jela huwa hawachiwi maana hakuna Therapy wala Rehab inayoweza kuwasaidia isipokuwa kuishi jela tu ...kwa mnaopigwa na Wapenzi wenu please take action now kama hawezi kuacha muwache cause ataishia kukuuwa! - @lemutuz_superbrand  - #regrann

Zari don’t be fooled, stay awake!

Okay! I believe we all had a chance to listen to Diamonds ft Ravvyn new song #Iyena kwangu mimi naona wimbo upo kawaida japo video ni nzuri na nafikiri uwepo wa Zari mule umeongezea mvuto kwa kiasi kikubwa! Kama hujaona tazama ?

Lakini sijali sana kuhu wimbo, ujumbe wangu ni kwa Zari kwani nineona mashabiki "maandazi" wanavyo ongea eti "warudiane" na Diamond ?? I am like for real!! Who in a right mind will dare to say that?! Seriously people?  let us be real here for a second!! Hivi ni huyu huyu Diamond aliye m-cheat Zari na kuzaa nje baadaye akaomba msamaha Zari akamsamehe kwa moyo mkunjuvu na akasema "I made peace with his mistakes"!! Baada ya hapo nini kilitokea?!! Sindio akarudi kutoka South nakupokelewa na Wema Sepetu ukumbini na familia yake yote ikiwepo na Wema?! Na hapo ni baada ya mama Diamond kukaa South Africa kwa Zari zaidi ya mwezi pamoja na mumewe halafu kafika Bongo ndio huyo yupo busy na Wema? (With all due respect to Wema, mimi sinaga mambo ya timu bali nataka nifikishe ujumbe wangu vizuri ndio maana namtaja) Na bado picha na video akiwa na wanawake wengine zilirushwa kwenye mitandao na kila mtu anaona! Nyie watu acheni mzaha!! 
To you Zari, I'm not sure if you consider yourself "a celebrity" or a business lady who happened to be a "celebrity"! Celebrity is a culture, if you want to live a  celebrities culture then forget about your integrity, take Diamond back and prepare to lose respect from many people! What I am trying to say here you're way better off without Diamond! You stand as a very strong and powerful woman right now than those days you used to  zoom around  with Diamond everywhere like a homeless lady!!

You have added your value by showing people who you real are, how strong you can be, please don't trap kwa mama Diamond childish games! Adults, young girls and boys are looking up to you so do your children please don't let them down eti kisa nyimbo! Think about your daughter, you are laying a foundation of how boys and men should treat her be wise like snake! Build good foundation that every man will think twice before holding your daughter's hand! Teach young boys that women are not tools but rather are fellow human beings treat them with respect and dignity, not using them as "money making" machines!! Please, find a healthy  co-parenting way with Diamond and his family but don't take them back as family. That family is perfect but not for you, is perfect for those other women (if you know what I mean)! Achana nayo kabisa they don't deserve you even for a second. You were raised by a strong woman, whom she raised all those strong children alone why letting her down!! Usiseme eti watoto hata yatima pia ni watoto lakini wanakua!! That family isn't a healthy family to raise children with labda uwe unavuta bangi! Money is good but Not all money is great!! Choose your paycheck wisely! 

After all, you look more matured, focused, and well kept right now than ulipokuwa na Diamond. He stressed you out, took the strength out of you, misused your love, you didn't have peace at all.  Try to look at your old pictures you will agree with me!! They degraded you to accommodate and keep up with their uncivilized characters!! Trying to make money by destroying every woman that Diamond is involving with, I hope you are awake enough to smell the nasty coffee!!
Plus this babydaddy of yours care less about your life, he doesn't care if he would leave your children motherless perhaps even no parents at all that why he can't use any kind of protection-HIV is real woman! And what about Hippies, and Hepatitis C for God's sake!! Look how he was fooling around  with those ladies, let them recorded him with no fear or shame then shared them in social media?!! Guess what, that is the PROOF THAT HE DOESN'T LOVE YOU!! He is just using you! Selfish to the core!! If someone loves you will care about you, will always think about you before taking any action!! No one is perfect but some people are evil!! This is nothing but pure evil!!

You can do business with him but make sure every thing is clearly written and well documented. Make sure he is not a beneficiary of any of your money even if you happen to die today! Let ALL your children be the first beneficiaries, and your sisters legal guardian. You're better than this  Zari don't let this family destroy the woman you are!! ..... In the end, it's your life we are just cheerleaders!!


Mungu azidi kuwa nanyi, soon to be Mr and Mrs Majizzo!



Hayo ?  ni maneno yake kaka yangu RC Paul Makonda! Wow! Hongereni wote maharusi watarajiwa lakini zaidi hongera sana Lulu! Jamani! Jamani! Binadamu watakesha wakitaka kukuangusha lakini Mungu atakapoamua kukuinua hakuna anayeweza simama mbele yako! Jinsi watu alivyokuwa wakikucheka kuwa unamkosi leo hii the same people wapo busy kukupongeza! Dah! Watanzania Mungu atusaidie. Hivi kama haya si mapenzi ya kweli mtasema ni kitu gani?!! Hizi ndizo katika tabu na raha ambazo Biblia inazungumzia. Siyo kupigana mangumi na kuchinjana mapanga!! Wanaume kama Majizzo ni wanaume wachache sanaaa haswa kwa watu wa Africa!!  Ubarikiwe sana Majizzo kwa kuonyesha mfano bora haswa kwa vijana wa leo. Hongera Lulu enjoy every single moment ya maandalizi yako mpaka harusi. Make sure you got your dreamed wedding wala usiogope. Huu ndio wakati wako wa kuinuliwa juu simama kishujaa tena kwa madaha. Mungu awamiminie neema zake! ?

**Mimi na dedicate wimbo huu wa Hezekiah  Walker " God favored me" kwako Lulu** ?

“Ni ushauri wa bure chukua au niachie”

Regrann from @lemutuz_superbrand – FACTS: 

  • To you all Mamen Mwanamke anayekupenda atakupigia simu wakati wowote katika siku na ukiona hakupigii eti yupo busy sana ujue muongo HAKUPENDI
  • First date dinner out mara Mbebezz kaja na wenzake ujue hakupendi ni Muongo
  • Ukiona Mbebezz anaogopa kupiga picha na wewe na ana visingizio vingi kama naogopa mitandao babe! ujue ni Muongo anaogopa mtu wake kwako kaja kupima kama una mzigo kuliko mtu wake
  • Akikuambia hana mtu ni muongo hakuna mbebez super hapa mjini ambaye hana mtu kwako kaja kupima tu kama una mzigo kuliko mtu wake wa siku zote
  • Ukiona mbebezz anaogopa kukukaribisha ofisini kwake au hata ukienda hakutambulishi kuwa ni mtu wake ujue sio hakupendi ila ana mtu pale ofisini anayetaka kumtingisha tu kwa kukutumia wewe
  • Ukiona anaogopa kuonekana na wewe Serena Hotel au Kempisk ujue huko ndiko mtu wake anakokua sana
  • Ukionasimuyakeikiliaanakimbiapembeniujue ni mtu wake huyo
  • Ukiona mbebezz hapatikani kwenye simu yake saa za usiku ujue yupo na mtu wake
  • Ukiona Mbebezz hapatikani kuanzia Ijumaa anaanza kukutafuta tena Jumatatu ujue alikua na mtu wake amebanwa
  • Ukiona mbebez hataki kukupa namba yake ya simu au eti hana simu ujue ana mtu
  • Ukiona mbebebzzz anakuwa mkali sana akisikia umesema unatoka naye ujue hakutaki ana mtu anaogopa utamharibia
  • Now guys haya hayahitaji Mwanaume kuwa na PhD ukiona Mbebezz ana hata moja tu ya hizi dalili WACHANA NAYE atakusumbua tu mbele ya Safari UTAPAGAWA! …..ni Ushauri wa Bure Chukua au Niachie …Good Morning! – @lemutuz_superbrand – #regrann

??? nani kaibiwaaaa? It’s  a long weekend ukiona kimya ujuwe ninebanwa ???

 

“Mwanaume ambaye hawaheshimu Wazazi wake jua hatakuheshimu wewe kama mke wake na hatawaheshimu Wazazi wako pia”

Regrann from @lemutuz_superbrand - FACT: To you all my dear Sisters.......Mwanaume ambaye hawaheshimu Wazazi wake jua hatakuheshimu wewe kama mke wake na hatawaheshimu Wazazi wako pia ....Mwanaume asiyejua kuheshimu Traffic Signs anapoendesha gari lake barabarani ujue hatakuheshimu hata wewe...yaani Mwanaume asiyejua Stop Sign...asiyejua Red Light....asiyejua Zebra yaani kusubiri watembea kwa miguu wapite .....atakufanyia hayo hayo kwenye Ndoa au Relationship ....Ukiumwa hatasubiri upone ataku Cheat ...Ukisafiri kikazi hatasubiri urudi ataku Cheat! ..Ukifiwa ukaenda Msibani hatakusubiri urudi ataku Cheat tu! ....Kama Mwanaume wako anagombana sana na madereva wengine barabarani ujue ATAKUDUNDA TU kama Mpenzi au mke wake ....kama anakaripia karipia watu kwenye simu ujue atakukaripia na wewe ....I mean kama vipi MUWACHE CAUSE ATAKUSUMBUA MBELE YA SAFARI I mean ni Ushauri wangu wa bure Uchukue au Niachie ...ila usije kulia lia kuwa hukujua au hukuambiwa! - @lemutuz_superbrand - #regrann

Mkuki kwa Nguruwe kwa binadamu mchungu……. !

Kuna watu wanajifanyaga kuwa wao wanajua jinsi ya kufanya maamuzi mazuri kuliko wenzao, wako wepesi sana kusema matatizo ya watu na kuhukumu wengine kwa maamuzi wanayo fanya! Sasa ikatokea maamuzi uliyofanya hayakuzaa matunda mazuri mbona utakoma! Lakini ikiwa yeye ndio  kafanya maamuzi ambayo siyo sahihi atatafuta kila njia ya   Ku justify hayo makosa na kutumia gharama zote kuficha makosa yao. Sasa huyu Tamar Braxton ni mmoja ya watu wenye tabia kama hizo. Yani huyu alikuwa mwepesi sana kusema dada zake kuwa wamechagua wanaume wasiofaa  na ndio maana ndoa zao zina matatizo. Msikilize hapa ?

Kuna siku pia alimuita Ex husband wa dada yake kuwa ni "baby sitter" kwamba hana faida yoyote kwa dada yake wala watoto zaidi ya kuwa kama mfanyakazi wa kulea watoto. Dada yake alichukia sana na kuwambia kuwa Andre anaweza asiwe mume mzuri lakini ni baba mwema sana kwa watoto wao na hato weza kumvumilia kuona anamdhalilisha baba wa watoto wake. Tizama hao ?

Sasa leo hii yamemkuta matatizo kwenye ndoa yake mpaka anadai talaka sasa amekuwa MBOGO! Hataki hata kuongea na familia yake kuwaelezea ukweli kuwa ndoa yake naye ilikuwa ni mbovu tu kama yao ila alikuwa anaficha. Yamemkuta yale yale aliyokuwa akiwaambia dada zake, kwa aibu anashindwa hata kuwaambia dada zake kuwa amekwenda mahakamani kudai talaka. Dada zake wamejua kuwa mdogo wao amekwenda mahakamani kudai talaka  baada ya kusoma  kwenye mitandao.  Halafu dada zake wanapotaka kumuuliza ili wajue ukweli anakuwa mkali kama pili pili!  Majibu ya shortcut huku akitumia Mic kama "defensive" mechanism! Embu mtazame hapo ?

Unajua kama hayajakufika kama hujui ku sympathize na matatizo ya watu basi ni bora ujifunze kunyamaza kuliko kuhukumu wenzio unafanya wajione  like something is wrong with them! Wakati jambo kama hilo au tatizo lolote lile linapokukuta unakuwa mkali hutaki kuulizwa  wala husikii kitu!

Nasikia Tamar amekuwa very sensitive na ame withdrawal kutoka kwa familia yake. Yupo very protective kulinda image ya mume wake.

Masikini Vince anatia huruma! Anataka ku fight for his marriage. Nafikiri ni vile anajiona yeye ni yatima na amekuwa kwenye Braxton family karibia miaka 20 na zaidi. Kumbuka Vince alikuwa Manager wa Toni Braxton kwa takribani miaka 10. Mkataba wake wa umeneja ulisitishwa baada ya kuamua kumuoa  Tamar kwani Toni alisema hawezi kuchanganya undugu na kazi akimaanisha Vince amekuwa shemeji yake. Wakati huo huo kunatuhuma za domestic violence kati ya Vince na Tamar ambazo zimetolewa na mama yake Tamar. Kama asemacho mama mkwe wake  ni ukweli basi nitakuwa nimeshangaa sana!! Kupiga mwanamke?! No! big No!

Mmh! Wishing her the best, nimefurahi sasa atajifunza kutokana na makosa. Maybe she will learn to put her ego down because she learned her lesson in a very hard way!

Zamaradi Mketema: Mtazamo wangu- Part 1

Regrann from @zamaradimketema - PART 1

Wanawake kulegalega kwenye majukumu yao kunachangiwa sana na wanaume kuacha na kusahau WAJIBU wao ndani ya nyumba, lazima tuwe wakweli hivi vitu vinaenda pamoja

Kumekuwa na malalamiko mengi juu ya wanawake sikuhizi kuwa si watu wa kujali nyumba zao kama ilivyokuwa awali, na mzigo mkubwa wa lawama unatupiwa wanawake bila kuangalia kulia na kushoto kwenye MIANYA ya VYANZO vya namna hii

Katika majumba mengi sikuhizi ni ngumu kutofautisha nguvu ya mwanamke na mwanaume katika kile kinachowekwa mezani (kipato), zamani ilikuwa Baba ndio anaengaliwa kwa macho yote lakini sikuhizi wamama wamekuwa na mchango mkubwa sana kwenye familia nyingi, kitu ambacho ni kizuri na wote tunakubali, TUNACHOSAHAU kila Zuri linakuja na athari zake, tusifurahie tu mazuri halafu tukataka kufumbia macho NGUVU ZINAZOTUMIKA na JASHO LINALOTOKA katika kuleta mazuri hayo.

Hata vitabu vya MUNGU naamini vya pande zote vilizungumza juu ya MWANAMKE KUZAA KWA UCHUNGU na MWANAUME ATATAFUTA KWA JASHO. Lakini leo hii vitu ni tofauti, mwanamke haangaliwi kama mwanamke tena, na ndiomana hata waoaji wengi wa sikuhizi (sio wote) wanataka mwanamke atakaekuwa angalau na mchango kwenye familia, matokeo yake mwanamke anabeba misalaba yote na zaidi, atazaa kwa uchungu, atalea kwa mapenzi, na sio watoto tu hadi Baba, ataangalia na kulinda nyumba, na majukumu yote ya mwanamke yanayoonekana ni ya kwake, na pamoja na hayo yote BADO ATATAFUTA KWA JASHO, ambalo si jukumu lake, na kwa jinsi wanawake wa sikuhizi wanavyoweza kuchakarika hakuna ajabu ya kuona anachokileta nyumbani yeye ni kikubwa kuliko cha baba, kweli bila hata kufikiri mara mbili unaendelea kulaumu nwanamke wa namna hii kuwa labda hakai chini kumfulia mumewe n.k, hebu jiulize kuna MAJUKUMU MANGAPI yasiyo ya kwake anayojikuta ameyabeba!! 

Na huenda yalistahili kufanywa na mwanaume, Kazi yake sio kutafuta kwa jasho lakini anatafuta, na huenda bila yeye kuhangaika watoto hawatasoma inavyostahili, mbali na hiyo bado atahangaika kuhakikisha kila kitu kiko sawa nyumbani hata anapokuwa mbali, hali ya kuwa Baba ni Baba tu na jukumu lake moja tena mara nyingine HALIFANYI INAVYOTAKIWA, maana wanaume wengine utakuta aki

Zamaradi Mketema: Ni Makosa yetu wanawake

Miriam Kinunda author of  Taste Of Tanzania: Modern Recipe for the West https://www.instagram.com/miriamkinunda/

Regrann from @zamaradimketema -Kwenye comments nimegundua wanawake wanalalamika na mzigo wanaoubeba wao kwenye majukumu ya familia, ila MAKOSA mara nyingi yanaanzia kwetu, wanawake wengi WANAWALEMAZA sana wanaume wao wenyewe kwa kuhisi wanawasaidia, kwa bahati mbaya hii haina faida kubwa mbele ila hasara.

Tukirudi kwenye nature mwanamke ameumbwa kutunzwa hata vitabu vyote vya Dini vinasema hivyo, na ndiomana ikiwa tofauti madhara tunayaona, mwache mwanaume awe mwanaume hata kama umemzidi kipato, nature ya mwanaume ni KUTOA na kujihisi ANAMILIKI na ndio uanaume wake unapokuja, anapokutunza anafeel uanaume wake, hata uwezo wa kunguruma anaupata ndani, mpe hiyo nafasi usimnyime, hata kama wewe una mia yeye ana kumi hakikisha katika kumi yake lazima utaratibu wake wa kulisha nyumba ubaki palepale kwa kidogo chake hikohiko, we utatumia tu akili jinsi ya KUMSAIDIA ila usimlemaze akaona wewe ndio kilakitu na kumpa nafasi ya kutulia, hakikisha kila anapotoka anaacha kinachostahili hata kama ni mia tano, mfanye awe mume, maana athari za wewe kuibeba familia mara nyingine zinaenda pabaya zaidi hadi kuharibu mahusiano.

Na ndiomana kuna fikra isiyo rasmi kuwa wanaume wengi wanaoishi na wanawake wenye uwezo zaidi yao hutafuta nyumba ndogo pembeni za hali ya chini na kuzihudumia kwa hikohiko kidogo, lengo ni kutaka kuutoa uanaume wake, anataka mamlaka yake yaonekane, anataka akiongea asikilizwe, mpe nafasi hata kama una uwezo, hiyo ndiomaana ya kuwa KICHWA mfanye awe kichwa kwa vitendo, hata kwa umasikini wake onesha unamtegemea yeye na umtie moyo afanye kadiri ya uwezo wake, sio ndio unazo basi yeye anakuwa kama mtoto mdogo sasa ndani unamuacha moja kwa moja hapana, au unajifanya huhitaji kitu kwake unakosea. Ukitaka kujua hii ni nature hata kwa upande wa wanawake ndiomana hakuna feeling nzuri kama kupewa/kutunzwa na mwanaume wako hata kama una kilakitu, sababu nature iko hivyo!! Ndiomana si ajabu kukuta mwanamke tajiri lakini akamtamania mwenzie wa hali ya chini kwa kununuliwa mkufu tu, pamoja na kupata kilakitu kwa jasho lake bado kuna kitu kinamiss, kuona mtu anasimama kwake kama MLINZI na mtunzaji wa maisha yake, MUNGU ndio kaumba hivyo!! Ila siku hizi eti wanaume ndio wanalindwa. Ni Kosa!! Regrann from Zamaradi Mketema

Nguvu iliyowekwa ndani ya mwanamke inaweza kumpa furaha na amani kila mwanaume atakaye ijua nguvu hiyo!

IFIKE MAHALA WANAUME TUWAHESHIMU WANAWAKE KWA JINSIA YAO na sio kuwapa kipaumbele kwa haja zetu za ki mwili, Mwanamke hatajwi kama kiburudisho cha Mwanaume, Mwanamke anatajwa kuwa UBAVU WA MWANAUME... Mchukulie Mwanamke kuwa sehemu ya Maisha ya kila mwanaume aliye timilifu "RIJALI" na hapo ndipo heshima ya Mwanamke itapatikana ndani ya akili yako, Mwanaume kumchukulia Mwanamke kama chombo fulani ni kujilaani mwenyewe maana NGUVU ILIYOWEKWA NDANI YA MWANAMKE INAWEZA KUMPA FURAHA NA AMANI kila mwanaume atakaye ijua nguvu hiyo. Mwanamke anazo nafasi nyingi kwa Mumewe ikiwa atapewa heshima, kutomheshimu Mwanamke ni kujishusha ki akili maana Mwanzo wa Mwanamke ni DADA na baadaye anakuwa MAMA achilia mbali hayo Mwanamke ni PAMBO LA MOYO WA MUME! Kumuacha Mwanamke akihangaika na kuteseka na watoto "FAMILIA" ukaangukia kwenye uhuni usokuwa na maana ni kujiwekea laana na mahangaiko siku zote za maisha yako, Mwanamke anapokuwa ametelekezwa MAISHA YAKE YOTE HUISHI KWA MASONONEKO na mpweke, Hakuna mtihani mgumu kwa Mwanamke kama KUOLEWA NA MWANAUME ASOJUWA SABABU YA NDOA... Hakuna Mtoto hupatikana kwa bahati mbaya maana maandalio ya mtoto yanapatikana kwa muingiliano wa ki mwili baina ya Mwanaume na Mwanamke "TENDO LA NDOA" inapofika mahala wanaume wanashindwa kutambuwa majukumu yao ya ulezi kwa watoto wao ilihali wakati wa mahitaji ya ki mwili aliweza kupambana juu ya ushawishi ni DHAMBI! Nanyi wanawake muwage mnaangalia na wanaume mnaokutana nao, Saa zingine SURA HUONGEA na muda mwingi MTU MBAYA HUJIKITA KWENYE UONGO ili kuificha tabia yake halisi.

#Elista_kasema_ila_sio_sheria ?

***Imenukuluwa kutoka Elista Realif For Heart*** 

Joyce Kiria: Haya MACHOZI yangu namlilia Mungu wangu aliye juu, yeye ndo ataamua

@Regranned from @joycekiriasuperwoman - Changamoto kubwa 2018 #Kipigo
Sikutegemea kama ipo siku kwa mkono wako ungeunyanya KUNIPIGA @kilewo2020mwanga ???? * Ukasahau kabisa! Ukasahau yooooote.. nimeharibu career yangu kupigania ndoto yako kwa kugawa watu wangu kwenye biashara zangu, nimepoteza ndugu jamaa na marafiki, umeniachia nimebeba mzigo wa familia kwa muda wote... Malipo yako ni KUNIPIGA/ KUNIDHALILISHA/ KUNITOA MACHOZI???

Umenipiga kwa sababu Mimi Ni MNYONGE siyo! SINA NGUVU, kwa sababu ni MWANAMKE Sina nguvu za kupigana na MWANAUME ... Umeniumiza mwili wangu unauma kila mahali umefiria damu na kichwa ukanigongesha kwenye gari, ili iweje? Nia yako ilikuwa ninini? kuniua??? Mungu amenipigania.

 Haya MACHOZI yangu namlilia Mungu wangu aliye juu, yeye ndo ataamua...?????? Kama NI Mimi niliandamana na watoto, nikakufanyia kampeni na deni kubwa nikaingia mpaka nikafungiwa Kipindi hewami, ninakutunza wewe na Watoto wako kwa miaka yote, MUNGU YUPO.... LEO UMENIPIGA @kilewo2020mwanga ??? Sawa watakusifia hao wanaokusifu ujinga, wanaokuambiaga Mimi sikuheshimu, badala wakwambie ufanye kazi utunze familia, Leo watakuona wewe ni MWANAUME kwa KUNIPIGA... - #regrann

Zamaradi Mketema: Kumbuka details ndio zinazotengeneza PACKAGE, na package ya ukweli unayoifahamu ni wewe

@Regranned from @zamaradimketema – Ukiona MAAMUZI yako yanaangalia sana watu ujue una hatihati ya kuharibu maisha yako, kuna watu wanategemea sana ushauri na APPROVAL za ndugu, jamaa wa karibu na marafiki katika kila kitu bila kuchuja mengine aone ni ya kwake na yanamuhusu yeye tu, tusichofahamu linapokuja swala la hisia na mahusiano hakuna ubaya wa kusikiliza lakini fata kulingana na moyo wako, wengi wanaokushauri watakushauri kulingana na interest zao juu ya huyo mtu au vile wanavyomuona nje, lakini kumbuka wewe ndio unaishi nae na ndio mwenye moyo. Na zaidi kuna vingi unavyovijua ambavyo wao hata wawe karibu kiasi gani hawatakaa wavione, na hata kama mnahadithiana mara nyingi mnaongelea matukio na sio DETAILS, na kumbuka details ndio zinazotengeneza PACKAGE, na package ya ukweli unayoifahamu ni wewe, ila kwa kutaka kuridhisha watu unaweza jikuta unaacha kufanya maamuzi sahihi kwakuwa fulani kakwambia sio sawa tena kwa kuangalia tu kile ULICHOMUAMINISHA NACHO ama kumwambia, mwisho wa siku athari za UKWELI unabaki nazo wewe. Kumbuka tu Washauri ni wengi kwenye maisha lakini hawana msaada wowote na wewe pale linapokukuta, watu wapo kila siku lakini hupaswi kuwazingatia kiasi mpaka ukasahau lenye umuhimu na wewe kwa kuwapendezesha wao, wao wanafanya ya kwao bila kujali utawahukumu vipi na ya kwako yatakapoharibika utakaekaa ndani kulia ni wewe peke yako, na zaidi hawatakuwepo muda wote kwa ajili yako. – #regrann

Joyce Kiria: Maisha ya Ndoa bana yana mambo jamaniii mwee……!

Joyce Kiria

Maisha ya Ndoa bana yana mambo jamaniii mwee, unaanza vizuuri kabisa kuwa “Mke” mtamuuuuu, kisha Polepole unakuwa “mama Fulani” Mke wa mtu, kisha taratiiibu unakuwa “Mlinzi” baadae “mlezi” kuna “mtunza nyumba” kuna “Mpishi” kuna “mfuaji” kuna “furniture” uuuuuuwwwwiiii nkinkiiii ruwa mangiiii ?? (Usiombe Mume awe chini ya Miaka 45?) utashaaaaaaaaaa…. — Jipe tuu Furaha mwenzangu, tuishi kama single flani amazing, akiwepo sawa akisepa sawa, tusingoje Furaha Toka kwa Mwanaume.. Tutaiskia kwenye filamu! Akili za usiku #NaesabuBati ?? #NikoDirishani ##AnatokeaWapiNifungueMlango

ASANTE SANA @didavitengewear kwa mwonekano wa kitenge… @rosebrazilian kwa Nywele… Twende SAWA… Kama una neno lolote weka hapa

 

“Ukiniuliza Mimi nitakuambia huyo asiyekua lolote wala chochote Leo ndio mzuri….”~~~Rose Shaboka

Nguo unayoinunua dukani ikiwa READY MADE wakati mwingine sio rahisi kuirekebisha iwe exactly unavyotaka. Lakini nguo unayoenda kushona kwa Fundi kuanzia mwanzo ni rahisi sana kuitengeneza ikawa exactly kile unachotaka. Msichana unayetaka na kuomba mwanaume ambaye tayari ana kila kitu (ready made) hujui unachokiomba. Sio vibaya ukipata mtu ambaye ana kila kitu tayari lakini nakuambia usimkatae wala kumdharau huyo ambaye hana kitu Leo. Ukiniuliza Mimi nitakuambia huyo asiyekua lolote wala chochote Leo ndio mzuri na ukishirikiana na Mungu vizuri unaweza kumtengeneza akawa unavyotaka na anachotakiwa kuwa kirahisi sana kuliko yule ambaye ameshatengenezwa usivyotaka. Mimi kama Fundi ukiniletea hicho kitambaa ambacho hakijashonwa ni rahisi kutengeneza unachotaka kuliko ukiniletea nguo ambayo ilishashonwa kitu kingine niitengeneze iwe kitu kingine. Huyo mwanaume asiye na chochote Leo ni kitambaa kipeleke kwa Fundi anaitwa Yesu akutolee style moja matata itakayokutosha katika hali zote ambayo macho hayajawahi kuona, masikio hayajawahi kusikia wala akili za mwanadamu hazijawahi kufikiria Yale mambo Bwana amewaandalia wampendao.

#mchungaji anapokua Fundi cherehani hata kwenye vitambaa vya kushona anapata mafunuo#
#kila jambo lina majira, hata kukosa kuna mwisho hatakua maskini milele, usimdharau#
#pastors new day church, power house#
#victoria petrol station#