Kesho ndio siku yenyewe kuu, ambapo wawili hawa wataunganishwa kuwa kitu kimoja na koo mbili zitaunganishwa rasmi mbele za Mungu.
Naam, kwamara nyingine tena tunapenda kutoa pongezi nyingi sana kwa watarajiwa hawa kwa kufanya maamuzi mazito yenye busara. Mungu azidi kuwatangulia katika kila jambo ambalo limepangwa kufanyika kesho basi likapatae kibali mbele ya uso wa Bwana na lifanyike kama lilivyopangwa kwa utukufu wa Mungu.
Mwenyezi Mungu mwenye wingi wa rehema na neema awazidishie ulinzi wake na mibaraka yake siku zote za maisha yao. Ndoa yao ikajae amani na furaha, naye Mungu Baba awe mgeni wao siku zote. Wakabarikiwe wao na uzao wao wote. Twaomba kwa imani katika jina la Yesu. Amen! ????
“akasema, Kwa sababu hiyo, mtu atamwacha babaye na mamaye, ataambatana na mkewe; na hao wawili watakuwa mwili mmoja!” *** Matayo 19:5
“Kwa sababu hiyo mtu atamwacha babaye na mamaye, ataambatana na mkewe” ****Marko 10:7
Jana ilikuwa siku ya kuagwa kwa bibi harusi mtarajiwa. Bi. Sarah alifiwa na wazazi wake wote wawili akiwa mdogo. Kaka yake Alex akamlea hadi sasa anatokea kwao kwenda kwake na mumewe mtarajiwa. Ni mlemavu wa kusikia na kusema??♂️ Hapo anatoa shukrani zake za moyoni kwa walezi wake siku ya kuagwa, na kuwapa zawadi alizomudu kama ishara ya shukrani na kumbukumbu. Mume wake mtarajiwa naye ana historia inayotaka kufanana na yake! Hawa wawili ni kielelezo halisi na ushuda hai kwamba kazi ya Mungu haina makosa.
Mimina neema zako Bwana mimina ????
??? mnaona mama zangu na shangazi yangu aliyegoma kuzeeka pale nyuma na tabasamu kama lote wakikumbushia enzi zao?! ?? so sweet!
Wababa nao hawakubaki nyuma! ??
Picha zote shukrani kwa Mc Rhevan , mtembelee Instagram @mc_Rhevan au website yake ???? https://mc.rhevan.com/