NAILILIA KAGERA (BUKOBA) YA WAJUKUU ZANGU-Peter Sarungi

fb_img_1473861345540
Peter Sarungi

Mimi babu yenu Peter Sarungi kutoka Mkoani Mara wilaya ya Rorya wa kabila la kimataifa la LUO, naandika salamu hizi kwa masikitiko makubwa na huzuni nyingi kwa janga la tetemeko lililowakumba wajukuu zangu. Najua mpo katika huzuni kubwa na inawezekana janga hili limewatonesha vidonda na majeraha makubwa mliyowahi kuyapata miaka ya nyuma, vidonda vilivyosababishwa na MV Bukoba, Vidonda Vilivyosababishwa na Vita vya Idd amin dada na Vidonda vilivyosababishwa na Chimbuko la ugonjwa wa UKIMWI. Hakika majanga haya yameacha vidonda na alama ya huzuni kwa wajukuu zangu kwa kuondokewa na wapendwa wenu wengi mliowategemea na kuwapenda. Niwatie moyo kwa kusema kuwa mimi Babu yenu nawaombea kwa Mungu awafariji na kuwavusha salama kutoka katika kipindi hiki kigumu na awasamehee, kuwalinda na kuwaepusha dhidi ya majanga mengine.

Nawapenda sanafb_img_1473861327089Mungu azilaze roho za wapendwa wajukuu zangu mahala pema peponi…Amin.

Leave a Reply