Mungu ndiye muhasisi wa #Democracy

Demokrasia ni mfumo ulio hasisiwa na Mungu Mwenyezi. Mungu alikuwa mtu wakwanza alieanzisha Democracy pale kwenye bustani ya Edeni. 

Pamoja na kumpenda mwanadamua sana, na akampa masharti ya jinsi ya kuishi katika bustani ile ya Edeni lakini alimpa Adamu Uhuru wa kuchagua #Democracy kati ya mema na mabaya. Adamu alitumia uhuru wake kufanya maamuzi aliyo yafanya. 

Mimi huwa siku zote nasemaga sina "role model" ambaye natamani kuwa kama yeye isipokuwa Yesu mwana wa Mungu. Huyu ndio "role model" wangu siku zote, natamani kuwa kama Yesu na si mwanadamu mwenzangu. Don't get confused, kuna watu wengi sana wana ni inspire au motivate katika mambo mbalimbali na mtu wa kwanza au watu wakwanza kabisa ni Wazazi wangu! 

Kwanini Yesu ni "role model" wangu? Kwasababu, Yesu alitumwa na Mungu kuja kutuonyesha jinsi gani ya kuishi maisha yetu hapa duniani, siyo tu kiroho, kiakili, kiafya, na kimwili. Yesu alizaliwa kama mwanadamu mwingine yeyote yule, aliishi maisha yake kama mwanadamu, na alikufa kama mwanadamu. 

Hivyo, ametuonyesha ni jinsi gani tunaweza ishi na watu ambao hawana mtazamo wa mawazo kama sisi. Ametuonyesha jinsi gani tunatakiwa kuwapa watu uhuru wa kuamua nini wanataka nakuheshimu maamuzi yao hata kama hatukubaliani nao. Ndio maana Yesu alishiriki katika sherehe za harusi za ndugu zake na marafiki ambao walikuwa ni walevi japo Yeye binafsi si mlevi. #Democracy ilitumika! Alihubiri injili ya neno la Mungu lakini hakuwatenga au kuwachukia walio ikataa! Again, #Democracy ilitumika.

Shetani alikuwa mmoja wa Malaika waimbaji wakuu Mbinguni lakini alitumia uhuru wake na kufanya maamuzi kwa kutumia kiburi kumdharau Mungu. Na akachagua kuja duniani kutengeneza majeshi yake kama yanavyo onekana katika tabia za watu mbali mbali.

Kwa kumalizia, nasema mtu yeyote yule anayependa kuwapa watu #Democracy  basi atakuwa anatabia za 'kimbingu'! Kila mtu anahaki ya kuwa huru kufanya kile apendacho ilimradi hawaingilii uhuru, privacy za watu wengine au kuvunja sheria ya nchi husika. Demokrasia ni rahisi sana kuisema lakini kuitekeleza ni ngumu sana.  Mungu atusaidie!

Leave a Reply