Category Archives: Mother and daughter moment

Mwanangu mimi ….!

Unajua saa nyingine huwa siamini kama ni mwanangu ?? Mwenzenu nimekuza! Nikiangalia tulipotoka na tunapoelekea yani hakuna ninachokiona zaidi ya mkono wa Mungu ukiwa juu ya vichwa vyetu kumimina mibaraka yake.

Namshukuru Mungu sana na nitalitukuza jina lake milele. Kanipa rafiki wa milele. Tumekuwa pamoja, tumejifunza mengi pamoja, haswa kupitia makosa yangu mimi kama mama yake, yakampa somo la moja kwa moja. Mungu ni mwema sana. Nimevuka stage ya kuwa strictly mama; sasa hivi ni mama plus rafiki. Tunaongea na kuelekezana kirafiki tu! Kama malezi niliyompa kabla ya miaka 18 hayakumuingia na kumtengeneza kuwa kiumbe bora basi katika umri huu hakuna kitakacho mbadili zaidi ya kumuombea tu! Namshukuru Mungu sanaaaaaaa, mwanangu hajawai kunisumbua hata kidogo. Mungu kanibariki na mtoto msikivu, mwenye hofu ya Mungu, yani ni mtoto mwema mnoooo ndio maana saa nyingine siamini kama nimemlea mimi! ?? such a beautiful, humble, strong, smart, intelligent, classy, loyal, hard working, independent, charming young lady. I mean the list can go on and on but glory and honor all to Almighty God! ??

Leo nimejisikia kupost picha zetu haswa zahuyu mrembo wangu! ?? Kwani kunatatizo?! ?? sikuhizi nimeachana na kupost picha za watu haswa tusio na undugu, urafiki au mazoea. Ndio maana mnaniona sipost mara kwa mara. Nafanya mambo yangu mengine ambayo yananipa furaha na amani zaidi na hayo ndio nitakuwa napost humu.

??

Nimejisikia kumpost kuweka kumbukumbu ?? si blog ya mama yake jamani! ?? Ndio raha yakuwa na kitu chako mwenyewe ulicho kitengeneza wewe mwenyewe kwa utashi wa akili zako na mikono yako miwili. Hakuna atakaye kupangia nini cha kufanya labda huyo mtu ni punguani! ?? ………… Mungu azidi kumbariki sana na kumpa afya njema. ??

Safari ya mama Washington DC

 Siku iliyofuata, tuliamka na kupata breakfast, kisha tukaendelea na mizunguko yetu.     Nilitaka mama aone Washington DC yote kila jengo la office na majumba ya matajiri wa huko. Bahati mbaya au nzuri mama alikataa kutembea alidai amechoka kwasababu ya mizunguko ya jana yake. Hivyo, ikabidi tuchukue tour bus ambayo ilituonyesha sehemu zote tulizopenda kuona. Of course, nimuhimu kusalimiana na wapendwa wako pale unapopata nafasi. Basi hapa tutakutana na cousin yangu (mtoto wa mama yangu mkubwa, mama yake ni wapili kuzaliwa katika familia ya mama yangu) Dr. Joseph Obure yeye anafanya kazi hapo Washington DC. Mama na wanae Mama na kijana wake  wakisogoa story za miaka mingi ? 

Mama na binti yake katika pozi ?


Siku ilyofuata, tulianza kwa kununua green tea na pumpkin bread (my all time favorite breakfast) katika cafe ya Starbucks, tuliungana na aunt yangu aitwaye Sophie au mama AnnaD na baadaye kuanza safari ya kuelekea Makao Makuu duniani ya kanisa la Wasabato.  

Hili eneo ni kubwa sana kama utabahatika kutembelea basi panga angalau masaa azidi ya matatu ili uweze kufaidi na kujifunza kidogo. Mama yangu alifurahia sana. 

  

Basi safari yetu kwa siku hii ikaishia napa, tukaenda kula na kufanya mizunguko kidogo ya dakika za mwisho kwani muda wetu ulikuwa unatupa mkono.    
Nawatakieni maandalizi mema ya Sabato na Sabato njema kwa waumini wote wa dhehebu la Wasabato duniani ?

Mother’s Day 2018: Je, ungependa ku-share nasi hadithi / shukrani ya mama yako mpenzi?

Mother and daughter moment: Mother's Day inakuja ni jumapili ijayo, je umepanga kufanya nini au kumfanyia nini mama yako? Mimi binafsi nitakuwa Washington, DC niki enjoy kidogo na mama yangu! Kwani hii itakuwa Mother's Day ya kwanza kabisa kwa mama yangu kuwa hapa Marekani pamoja nami; hivyo nitaitumia nafasi hii vyema. Sasa basi tuambie kuhusu wewe. Je, ungependa kuShare nasi stori ya mama yako au kutoa shukrani zako kwa mama ukiambatanisha na picha ya mama yako? Basi wasiliana na alphaigogo.com kwa kutuma ujumbe kwa njia ya blog, Instagram DM, au Facebook nasi tutaweka ujumbe wako. 

**Zoezi hili linaanza rasmi leo hii mpaka JumaMosi.**
Asanteni 
Pichani ni mdogo wangu Janeth na binti yake Essy. #TBS 2017

 

Mama na mwana

Regrann from @monalisatz - Dear Mama, Najisikia mwenye bahati mno kuwa mtoto wako.Umekuwa mama bora kwangu,bibi mzuri kwa watoto wangu,rafiki yangu wa karibu, mfanyakazi mwenzangu, kila kitu kwangu. Sijui ningekuwaje bila wewe?
Mungu akutunze mama yangu.
Nakupenda kila saa,
Nakupenda kila siku.
Happy birthday Mama @natashamamvi - #regrann

Mother and daughter moment

Pretty-pretty-pretty! Such a lovely priceless moment, mama Cookie na Cookie wake! ???....... Jamani Valentine's moments unaweza ukachagua mtu yoyote umpendaye  uka dedicate mwaka huu kwake! Anaweza akawa mama yako mzazi, baba, dada, mtoto wako n.k! Yoyote yule amabye yupo karibu na ndani ya roho yako! Ila kama ni mume / Mke lazima awe amehalalishwa na mamlaka husika kama serikali, kanisa, au msikitini!  

Mama Mbuna: Mungu wangu ninaye mtumikia akubariki milele yote

Wooh Mungu ni mwema mno. Ilikuwa siku kama ya leo (Alhamisi), tarehe kama ya leo (11/01/ mwaka uleeee, mnamo saa 09:30 mchana, mvua yenye utulivu ikiwa inanyesha, nikiwa pale Ocean Road Hospital, BWANA alinipatia mtoto mzuri wa kike tunayemuita Foster Mbuna Mkapa. Aliyefanya CV yangu ibadilike na kuanza kuitwa mama Foster tangu siku hiyo.  Nakutakia baraka zote za rohoni na za mwilini unapoisherehekea siku yako hii ya kuzaliwa. Kwa imani nakutamkia neno hili kwamba "hakuna silaha yoyote itakayo inuka juu yako ambayo itafanikiwa." Mungu wangu ninaye mtumikia akubariki milele yote. HAPPY BIRTHDAY TO YOU. MUMMY LOVES YOU!!!!!!

Cookie Moses Iyobo nionee huruma mwenzio!

Jamani Cookie binti wa Moses Iyobo na aunty Ezekiel ni nini unanifanyia mwenzio! Embu nionee huruma my darling, wewe hujasikia wenzio ndoa zinavunjika hawataki kuzaa kwa uchumi huu wa Babu yako Trump na Dr. Magufuli ?? maisha magumu  mwanetu ??.   

Tatizo ni jinsi wewe ulivyo mzuri yani mpaka unanitia katika vishawishi  mwanangu wee! Nitakuwa mgeni wa nani mie maisha yenyewe haya ya paycheck to paycheck, Niki miss paycheck moja tu nakuwa homeless  ????????‍♂️ You are beautiful and photogenic fulani amazing kweli kweli! Mungu akulinde, ukuhepushe na manyang’au ya hii dunia! Amazing! BTW, happy belated birthday mama Cookie, Ubarikiwe sana.

Mother and daughter moment!

Mama Gabby na Gabby wake! Beautiful pic

Quote for today: You’re the most beautiful thing I keep inside my heart!

Mama na mwana: Hakika wema na fadhili zako zitanifuata siku zote za maisha yangu!

Ni kwa neema tu! Nasema ni kwa neema yake Mungu kwani akili yangu haikuwai kuwaza kuwa ipo siku kama hii! Hivyo namshukuru sana Mungu kwani ni hakika wema na fadhili zake zitanifuata siku zote za maisha yangu, nami nitadumu ndani yake! Nimeweza kuona ukuu wa Mungu kwa kufanikisha uumbaji wake! Amenibariki na rafiki wa kweli ambaye upendo wetu utadumu milele na milele!  ………Najua tunamipango mingi sana naomba Mungu azidi kutuwezesha katika kila jambo! Moja ya vitu ambavyo nasubiri kwa hamu sana ni passport ya mwanangu!! Yes! her American passport!! Ee Mwenyezi Mungu mimina baraka zako!! Yani can’t wait!! Maana tutatembe hii dunia mpaka ndege zinune  zigome kabisa kuruka ?? ……..Anyway, namshukuru Mungu kwa mbaraka  wa huyu mtoto! Naomba azidi kunilindia na kumuongoza katika kila jambo haswa kiroho, asikae mbali naye!

Mother and daughter moment

Thankful. Grateful. Blessed #LoveOverEverything

Wamenoga eeh! Mama na mwana, Nancy na binti yake Zuri. So pretty!

Quote for today: A daughter is just a little girl who grows to be your best friend.

 

 

Mother and daughter moment

Akothee na mama yake mzazi

?? ngoja nicheke kwanza, maana Akothee ananifurahisha sana! I think she is a sister I need ??? ……. Yani Akothee anajua how to do a “role” change! Akiwa kanisani siku ya Sabato utamjua ndo yeye anavaaga Vi-min na kukatika kwa stage ?? Yani hadi kilemba ile Luo style anafunga siku ya Sabato na sadaka anakusanya.  Na akiwa anakula #bata ni anakula kweli kweli. Sasa kama hapa yupo na mama yake mzazi, muangalie alivyo tega masikio kwa usikivu utafikiri sio yeye. So funny! Wamependeza sana! …….Akothee I know you are my loyal reader, but I want you to be my sister please, I know my sisters love me but they don’t mind to share with you at all ?? We will drive this world crazy, I can tell ??……. Nice pic Akothee, say hello to mama!

Mother and daughter moment!

Nimependa sana hii picha ya Mwamvita Makamba na mama yake! Wamependeza sana. Ilikuwa ni sherehe ya mdogo wake Mwamvita ina itwa “bag” party mie ndo nimeona leo mwe kama kawaida yangu kama kitu nilikuwa sijui basi nawaeleza tu ukweli! Watu walipendeza sana. Nimeipenda!

Mother and daughter moment!

Beautiful Emelda Mwamanga na binti yake Gabby! So nice! Nivizuri kuwapenda watoto wetu zaidi wakiwa katika umri huu mdogo kwani inawajengea kuamini, kutambua thamani yao wakiwa wakubwa,  na kuwa wajasiri! Mtoto yoyote yule anahitaji muongozo, na mipaka lakini pia anahitajika kuwa huru haswa kifikra! Hivyo nijukumu la mzazi kumjenga mtoto wazingira huru ya kujieleza na kutafakari ambayo yana boundaries at the same time!

Mtoto siyo mdoli jamani, mfunze mtoto maadili mema, na jinsi y kuweza kukabiliana na hali zote za maisha. Kwamfano hapo Gabby unaona amefundishwa kupika na kuchanganya vitu kwa kutumia blander hivyo hata akienda kwa watu ambao wanatumia "high tech" kitchen appliances hashangai sana. Napia anajua jinsi ya kutumia mikono yake kushika vitu! Nilishawahi kuona kwa macho yangu mtoto wa miaka nane (8yrs old) bado anatawazwa akimaliza kutumia choo ?? Yani anajisaidia haja kubwa halafu anita dada wa kazi au mama yake amsafishe! And the mother was very OK with it ?? Jamani!! Anyway, those are rich people problems, maskini kama sisi tutayawezea wapi? ??

 

Ndugu wanapokutana…….!

Pale ndugu wanapokutana ni furaha kwa kwenda mbele! ........mama akipata kumbukumbu ya picha na binti yake kwa furaha ya kuonana tena baada ya miezi kadhaa kupitia! Magreth akimpokea dada yake Elline kwa furaha sana!..........  kwafaida ya wasomaji wangu, Elline ni dada yetu mkubwa, mimi ndio namfuata. Yeye alikuwa anaishi Geita lakini mwezi uliopita wamehamishiwa kikazi Makao Makuu (Dodoma). Hivyo sasa ni wakazi wa Dodoma! ........Tunamshukuru Mungu kwa yote! 

Mother and daughter moment!

Mama na mwana wakiwa katika mazingira safi kabisa ya Kisumu International Airport, hapo nchini Kenya! Hii Airport kwa muonekano tu wa nje inaonekana ni safi zaidi ya ile ya kwetu pale Bongoland! Japo hii ipo nje ya mji wa Nairobi lakini inavutia kwa usafi sana........Ni nini haswa tatizo letu sisi Watanzania! Maana hata mazingira yatengenezwe mazuri vipi haichukui muda utashangaa jinsi yalivyo chafuliwa, na kuharibiwa! Saa nyingine tunailaumu serikali kwa mambo ambayo ni sisi wenyewe ni tatizo! Kweli aliyeturoga kafa!.........Picha hii imepigwa week na siku kadhaa sasa wakati mama Igogo alipokuwa amekwenda kwenye msiba kwa wakwe zake na binti yake!

Motherhood!

Mama na mwana! Pendeza sana mama yetu so beautiful!  Happy belated Mother’s Day to you mama yetu we love you ? Btw, Dinnah na mimi tulisoma wote CBE Marketing major natulikuwa roommates.  Dinnah ni ana akili usipime hata waliosoma naye UD watashuhudia! Plus msafi sana kama mimi vile ??

 

Mother and daughter moment

What a beautiful picture of Hoyce Temu and her beautiful lovely daughter Rubby! Priceless! Happy Mother’s to Hoyce Temu

Mother and daughter moment

Nimependa sana hii picha ya Nambua Cassandra na mama yake mzazi mama Mlaki. Hii ilikuwa wiki iliyopita kwenye babyshower ya Nambua. Mmh! So touchy, lovely, and priceless moment. Happy Mother’s Day to both of them!

Mother and daughter moment: Mama Essy na Essy

Ain’t they cute! Lawyer Janeth Igogo and her beautiful daughter Essy looking beautiful in a custom made African print dress! Wamependeza sana ??

Mother and daughter moment!

Wema atinga Chadema bega kwa bega na mama yake! Limekuwa si jambo la kushangaza sana kuona mama Sepetu akiwa mguu kwa mguu katika maswala yanayo muhusu binti yake Wema Sepetu, japo kwa safari hii imekuwa tofauti kidogo na matukio mengine anayo yafanya!…….Wema amemwaga manyanga ya CCM na kubeba manyanga ya Chadema juu tena kwa madaha na mbwembwe nyingi huku mama yake mzazi akiziunga mkono na kuzibariki mbwembwe hizo!…….  Je, nguvu ya mrembo huyo yatosha kumng’oa Magufuli  / CCM madarakani?!! Mimi sijui kwani Siasa isn’t my cup of StrawberryMango smoothie! Bali naweza sema tuombeane uzima ili tushuhudie mambo 2020!……wishing her the best in her handover!