Category Archives: Birthday wishes

Muhtasari wa kumbukizi ya siku ya kuzaliwa Mercy.

Birthday girl herself

Siku ya tarehe 02, 04, 2023 ilikuwa ni siku ya kumbukizi ya mfanano wa siku ya kuzaliwa mwanangu Mercy.

Birthday girl akiingia kwenye mgahawa

Kama video inavyo onyesha hapo juu πŸ‘†πŸΏ Alianza kusherekea siku moja kabla ya siku yake maaalum kuwasaili, ambayo siku hiyo ilikuwa ni Jumosi ya tarehe 04/01/2023. Sambamba na marafiki zake walikuwa pamoja chakula cha usiku katika mgahawa ujulikanao kama TourΓ£o Brazilian Churrasqueria uliopo downtown Houston, Texas. 😍😍

Mtu na mama yake

Basi siku yenyewe ilipofika tulikuwa na muda mzuri pamoja asubuhi na jioni tukaenda tena kufanya kile twapendelea kufanya zaidi 😍😍 Kwakweli sina kingine mwaka huu zaidi ya kusema Asante Mungu wangu. Sifa na utukufu zote ni zako wewe Baba muumba wa Mningu na nchi na vyote vilivyoko. πŸ™πŸΏπŸ™πŸΏ

Asante Baba yangu. Asante Mungu wangu, Asante.

Happy 70th birthday Sir O.O Igogo!

Birthday boy himself 😍

“HAKIKA mimiπŸ‘† Unipendaye, LEO tumshukuru Mola wetu Muumba na mpaji wa UHAI, kwa kuniwezesha kuhitimu elimu maisha ya MIONGO 7πŸ™πŸΏπŸ™πŸΏNikiwa na Afya ya mwili na akili njema siku zote. Furaha niliyo nayo moyoni ni Upendo na Heshima unayonipa kamaπŸ‘‰πŸΏBaba&Babu&Best wako #001 NAKUSHUKURU SANA, SANAπŸ‘πŸΏ” ***Sir O.O Igogo***

Naam, hapo juu hiyo ilikuwa ndio salamu yake mzee O.O Igogo siku ya leo ambapo Mwenyezi Mungu amemjalia kutimiza umri wa miaka 70. Kusema ukweli siku zote nilikuwa nikasikia ndugu na marafiki wakisema kuwa baba/mama/bibi yangu ametimiza miaka 70 au 75 basi nafurahia sana. Chaajabu hata siku moja sikuwahi kuwazia wazazi wangu kufika umri huu. πŸ˜…πŸ˜… Sio kwamba sikujua kuwa wataufikia, hapana! Nivile tu sikuwahi kuwatengenezea picha ya kufikirika wakiwa katika umri huu. Sounds weird eh! πŸ™ˆ Twamshukuru Mungu kwa kutupa afya njema ambayo imetuwezesha kushuhudia siku hii ya leo.

Mimi mwenyewe na birthday boy

Nami nilimuandikia ujumbe wakumtakia kheri kwa siku hii muhimu. …”Happy70th birthday to the most influential man in my life! I’m blessed to call you dad. You deserve all that’s beautiful and precious in life. I wish you nothing but absolute happiness, love, peace, and good health on this superb milestone. Happy birthday Jategi, love you much. Otieno Igogo”⁷

Kwakweli tunashukuru sana Mungu kwa kutupa mbaraka huu wa pekee. Tunamtakia maisha marefu yaliyojaa furaha, amani, upendo, na afya njema.

Baba, Blessing, na mama

Recap: Mzee 0.O Igogo 70th birthday πŸ‘†πŸΏ …… Thank you so much, Robin Thomas Edson, @pixelspro_films, for capturing all these beautiful and precious moments on our dad’s 70th year of life journey on this planet.  Ubarikiwe sana.

Masaa kadhaa kabla ya kumbukizi ya kuzaliwa kwake niliamua kuangalia na ku-share tena baadhi ya video za Mzee O.O Igogo zilizo nivutia na kunikosha moyo 😍😍 na πŸ‘†πŸΏ πŸ‘‡πŸΏ ni sehemu ya hizo baadhi zilizo zipenda zaidi. Haya enjoy them 😜😜

Muhtasari-Sehemu ya 4: Tulisherekea kumbukizi ya siku ya kuzaliwa kwao.

Twamshukuru Mungu kwa pumzi ya uhai anayotupatia kila siku ambayo ilituwezesha kuona na kusherekea siku ya kumbukizi ya kuzaliwa wapendwa wetu. Kulikuwa na birthday tatu mwezi wa Nane. Yakwanza ni ya mdogo wangu Janeth kama video inavyo onyesha hapo juu πŸ‘†πŸΏ,

Tulikutana Johari Rotana hotel tukala, tukanywa, na kufurahi pamoja sisi kama madada na wifi yetu mke wa kaka yetu. Yani hapo katika madada aliyekosekana ni Blessing peke yake. 😍😍

Ikafuatiwa na ya mume wake Janeth, shemeji Tobby mtu kati hapo juu!

kisha ya mama yetu mkuwa Mama Sarungi. Tulifurahi sana.

Twamshukuru Mungu kwa yote. πŸ™πŸΏβ€οΈπŸ™πŸΏ

Happy 10th birthday my twin!

Babysister 😍😍

Two digits counting has officially begun! Happy 10th birthday twin babysister! Wishing you a marvelous year and many more to come. Happy birthday mdogo wa mimi. 😘❀️

sisterhood!.😍😍

Mimi mwenyewe na pacha wangu nyumbani Kibada. 😍😍

Pachaa kama pacha! Kwaraha zetu ndani ya Serena hotel, Dar es salaam.

Blessing katika ubora wake 😍

Happy birthday beautiful we all love you. 😘❀️❀️

Kheri ya siku ya kuzaliwa kwa mama yangu mimi!

Leo kazaliwa mama yangu mzazi, kipenzi cha roho yangu! Kwabahati mbaya afya yake imeleta shida kidogo. Lakini pamoja na yote hayo bado twamrudishia Mungu shukrani zetu za dhati kwani anastahili sifa zote na utukufu mkuu!

kama anavyoonekana hapo kwenye hiyo video akiwa mnyonge, ni baada ya kutoka hospital. Na mzamini wa pendo lake akiwa amemletea zawadi ya saa mpya na simu. ??

“Tumefika nyumbani. Mzaliwa mpya, aliye mgonjwa tumemkuta anaendelea vyema. Kapokea zawadi za Birth Day toka kwa Baba/Babu/Mfadhili na rafiki.” …. Maneno yake mzee O.O Igogo baada ya Kufika nyumbani akitokea safari.

Wazazi wangu ni wapenzi wa saa za RADO! Hii ndio aina ya saaa toka na kuwa mpaka leo hii naona wanazivaa tu! Sijawahi kujua kwanini labda siku nidodose! ?? Sindio “upaparazi” wenyewe huo! ??

Happy birthday mama, tunakupenda sana, na tunakuombea afya njema. Birthday itarudiwa pindi mjukuu wako number moja akifika hapo kesho kutwa. Tunaamini Mungu atakuwa amesha kuponya. Amen!

Happy birthday Mercy!

Leo ni siku kazaliwa mrembo wangu! Alizaliwa siku ya JumaMosi kuu (siku moja kabla ya Pasaka). Saa tisa mchana katika hospital ya Tanzania Matertenity Service (Siku hizi inaitwa Tanzania Matertenity Hospital), chini ya uangalizi wa marehemu Dr Amood na Dr Kapesa.

Mercy!

Kalinitesa na uchungu haka, sitokaa nisahau! ?? Niliwekewa chupa mbili za maji ya uchungu ndipo kakatoka! ?? Alikuwa kanona ndani ya tumbo la mama yake na mama mwenye alikuwa na mwili mdogo. Nilikuwa napenda kula chips na kachumbari kupita maelezo! Yani ndio kilikuwa chakula changu kikuu kila usiku! Maharage yalikuwa hayapitiii, yani nikijilazimisha kula natapika bila kujijua! ?? Halafu utamsikia mama Igogo akisema “vipi? Mjukuu kakataa maharage?” ???

Namshukuru Mungu kwa zawadi ya hichi kiumbe! Nilizaa mtoto mwenye afya njema nikampa jina Mercy. Jina hili nilikuwa inspired na rafiki yangu ambaye tulisoma naye Kowak Girls Secondary school, yeye anaitwa Mercy Msofe, kwasasa anaishi Arusha. Pia anajina lingine ambalo alipewa na babu yake (baba yangu mzazi), alimpa jina la Theresia a.k.a Teddy. Nijina la marehemu shangazi yangu. Baba yangu kwao (tumbo la mama yake) walizaliwa wavulana watatu na msichana mmoja. Kwakua Mercy ndio mjukuu wa kwanza kwa wazazi wangu akaamua kumuenzi marehemu dada yake ambaye alifariki mwaka mmoja kabla ya Mercy kuzaliwa. Basi Mercy na Teddy yote ni majina yake. Na lakilugha ni Obworo! Ni nickname ya marehemu shangazi yangu, Theresia Obworo!

Mimi namuombea maisha mazuri sana yaliyojaa baraka nyingi na utukufu wa Bwana Mungu. Mwenyezi Mungu amuhepushe na pepo zote. Akalitukuze jina la Muumba wake siku zote za maisha yake. Naomba kwa imani katika jina la Yesu, Amen!

Happy birthday beautiful girl, nakupenda sana nawe wajua hivyo! ?❀

Zifuatazo ni baadhi ya salamu za kheri kutoka kwa :-

Kutoka kwa babu!

“Me & U, are 41 years older and younger than one another, that is what inspired me to wait until all has exhausted their best wishes to you on this very special day, when you have seen the 27th anniversry. As I strive to reach my 95th anniversary to come, my wishes are that you shall celebrate 68th anniversay while healthier with sound knowledge, richer in heart, wealthier in charity, and sorrounded with numerous loving family members as it is with me today, on this wonderfull good friday which filled with happiness of sharing my love with you. UWE NA SIKU MURUA SANA, AHEROI MOKALO NYAKWARA MOKUONGO. ☝️? With all my Love?From ? Babu.”

Aunt Janeth!
Kutoka kwa aunt Mage
Kutoka kwa cousin-sister Sarah

Happy birthday Mercy!

Happy birthday baba!

Leo ni siku kazaliwa mzee O.O Igogo wengine umuita mzee wa Utegi Tech! Na wanawe walimpa jina la utani “mzee wa pamba”! ?? Amegonga miaka 68 leo. Tunamtakia maisha marefu zaidi, mema sana, na yenye baraka nyingi sana. Happy birthday to him. ……. zifuatazo ni salamu kutoka baadhi ya watoto na wajukuu!

Ujumbe toka kwa binti yake, Alpha.

Baba naye akafurahia picha iliyoambatanishwa na salamu za kuzaliwa kwake, ?? I made him smile yeah! ??

Ujumbe toka kwa binti yake Janeth

Salamu za upendo toka kwa mjukuu Sarah, a.k.a Katuko Nyandege

Mziwanda nae hakubaki nyuma! Yeye kampiga picha na kuandika salamu kwa juu! ? smart girl!

Cake maalum kwa ajili ya babu! ??

Salamu kutoka kwa binti yake Magreth Rhoda-Nyasungu

Salamu kutoka kwa mjukuu number moja, Mercy!

Well, kwamara nyingine twamtakia kheri ya maisha marefu! ……. embu tuwakumbishie enzi zake wakati wa ujana wake ??

Mjaluo kama mjaluo! OG from Rorya! ??? Eti dad ake nani huyu?! Kweli umaridadi huficha umasikini! ??

#HappyBirthdayDad. #FBS

Happy birthday Nyasungu!

Happy birthday to the sweetest babysister in the entire world! Thank you for unconditional love and respect you have shown to me that guides me to navigate the joys, the challenges, and understand the responsibilities of being a big sister! Wishing you an extra special day and amazing year! Happy birthday beautiful, love you so very much! ?❀❀❀

Birthday girl herself!
Akiwa na waridi wa moyo wake!
Warombo utawaajua tu!
akiwa na dada yake!
Akiingia kwa birthday dinner yake!

Cake toka kwa wazazi!

Once again, Happy birthday Nyasungu! My mama’s last born, my grandmother namesake, the peace maker, and the charm of our family ?? We love you baby girl! ?❀

Kheri ya siku ya kuzaliwa kwa dada yangu!

Leo ni siku ya kuzaliwa dada yetu, uzao wa pili wa familia yetu. Ni huyo mwenye nguo ya rangi ya Blue. Yeye kwa sasa anaishi Tabora lakini alikuja Dar kwa mambo fulani hivyo mdogo wangu akatumia nafasi hiyo ya pekee kumuandalia chakula cha mchana kufurahia maadhimisho ya siku hii. Tunamtakia kheri na baraka zote, Mungu atembee naye mwaka mwingine na milele zote ????

“Wamama na Wababa wa Wajukuu wetu, habarini za asubuhi njema ya leo. Leo nawasalimu kwa salaam ya kipekee, maalum ya kuhitimisha hiyo tafrija ya aina yake, yenye kunikumbusha miaka takriban 45 za Malezi yetu kwa huyo Mdada wenu na Mama wa wajukuu wetu wapendwa. Elline ana historia ya maisha yanayosadifiana na yangu, mie Baba yenu. Maisha yangu duniani yalianza kwa taabu ya afya dhaifu kwa kuwa niliwahi kutengana na lishe ya Mama tumboni mwake, nikazaliwa NJITI??‍♀️??Nakawa ngangari hadi leo hii bado nadunda japo udogoni nilikiona cha moto, kama Rafiki yangu, Binti yangu mpendwa Mama Min Ji. Alikuwa na afya mgogoro mno udogoni, naye kama nilihadithiwa na Mama kwamba bila huruma na upendo wa Baba yangu, yeye aliisha kata tamaa kwamba nitaishia utotoni tu, naye Nyategi kusema kweli nilimhangaikia vya kutosha utotoni, tukiwa na kipato kidogo mno, hadi hadi katengemaa na leo twasherekea siku yake ya 16,425 hapa duniani, Namuombea azidi kutengamaa na kupata tena siku kama hizo na kuzidi, hapa duniani. ????. Upendo wenu na mshikamano huu mliyonayo iwe ni mizizi inayo sambaa kwenye uzao wetu na kuendelea kwa vizazi na vizazi vijavyo. Nawatakia Sherehe njema, yenye Amani tele na kueneza Upendo wa JK milele.” * Baba mzaa chema -Sir O.O Igogo

Hapa wakiwa Tabora, ambapo mdogo wetu Janeth (aliyebeba mtoto) alikwenda kuwatembelea mwanzoni mwa mwaka huu!

Kheri ya siku ya kuzaliwa mama yangu kipenzi!

Leo ni siku aliyo zaliwa mama yangu mzazi, kipenzi cha roho yangu. Ila kwasababu birthday yake imeangukia siku ya kazi na wajukuu wanakwenda shule basi wadogo zangu siku ya jana (Jumapili) wakaamua kum-surprise na birthday cake kama video zinavyo onekana hapo juu ?? ?? …. ukiona mahala kuna upendo basi fahamu kuna Mungu kwani Mungu ni Pendo!

My mama! My MVP! The G.O.A.T! Always triple my blessings when comes to her! Happy birthday Nyarkowak, binti wa Cornel Awiti, muke ya Jategi ?? Mungu akujalie umri mrefu zaidi, maisha yenye furaha na amani zaidi ya jana! Nakupenda mama yangu! ?❀

Ubarikiwe miaka elfu! ??❀

Happy birthday to me!

“Bwana ni mwema sana alitupa mibaraka ya mtoto wa kike usiku wa Alfajiri ya tarehe 26/06/1977 umekuwa mibaraka kwetu, umenifanya kutembea Merikani kama Queen Mungu asingetupa wewe ni nani angenipeleka kwa Hellen G. White, ni nani angenipeleka Washington DC nikaona ikulu ya Trump, ni nani angenifikisha Califonia nikaona Los Angeles, ni nani angenifanya nikaona HOLLYWOOD, na Golden Gate, umenifikisha Chicago, Michigan, Indiana, Houston, nimeona kaburi la mama Hellen G. White (Battle creek, Michigan). Kuishi kwako Merikani Mungu kanifuta machozi nami ninaongea kati ya wanawake. Ubarikiwe 100 times ningekuwa na uwezo ningekutumia nguo ya kuvaa leo lakini endelea kutuombea siku moja nami nikubariki mwanangu. Tunakupenda sana.” I LOVE YOU MORE Mama! ?❀

Blessed beyond measure! Forever grateful ???? #LovingFarther
thank you darling daughter! ?❀

Namshukuru Mungu kwa yote! Nimeuona mwaka mwingine. Happy birthday to me!

Nawatakieni kheri na baraka za mwezi June!

Wapendwa wasomaji wangu nimekua mvivu sana siku hizi kuandika humu! Natafuta pesa wapendwa, mambo ya kuandika magazeti humu wakati bank kunasomeka negative zero hata hainogi ?? Lakini kama mjuavyo huu si ni mwezi June!! Sasa nitaachaje uwanze bila kuandika kitu humu. Huu sindio mwezi tuliozaliwa viumbe wenye roho za kipekee, viumbe wenye upendo mwingi kuliko viumbe vyote duniani! Viumbe tusiojua kuangaika na mambo ya watu, viumbe wenye furaha na amani muda wote. Viumbe wenye akili za ziada na utashi (Intelligence) wa hali ya juu! Viumbe vinavyo penda kujitegemea zaidi, viumbe vinavyo chukia majungu na umbea ?? Viumbe vinavyo jali na kuheshimu hisia za watu. The Legends ??? Yani ni viumbe fulani amazing kinoma and I am proud of myself to be one of them!

Unaona hiyo picha hapo juu baba mzazi kashanipa baraka zake za kuanzia mwezi. Basi nami naomba niwatakie kheri na baraka zote za mwezi huu wa Sita. Wale tulio zaliwa ndani ya mwezi huu nawatakieni birthday njema, Mungu akawabariki sana ukawe mwaka wa kheri nyingi sana katika miezi iliyo bakia. Mbarikiwe wote. June born babies we truly Rock! ?❀❀

Happy birthday Mercy!

Leo ni siku ambayo mwanangu kipenzi cha roho yangu amezaliwa. Katika kuadhimisha siku hii nimeamua kuweka kumbu kumbu ya post zote za birthday wishes ambazo Niliwahi kuandika huko Facebook. Japo nikawaida yangu kupost siku za birthday yake lakini sijui bbn kwanini nimejikuta nimewaza kama Facebook ikafutika ghalafa hizi kumbu kumbu zote zitapotea. ?‍♀️?‍♀️?‍♀️ Nilipokuwa naziandika niliandika hisia zangu halisi, niliandika vitu ambavyo sio tu vilitoka moyoni bali ninaviamini, hivyo vinabeba uzito mkubwa sana kwangu. Na nilipokua nazisoma tena leo yani mwili unanisiaimka kwa furaha na tabasamu la amani moyoni. ?? Ninawatoto wengi lakini aliyekaa tumboni mwangu na kunifanya ni experience uchungu wa kuzaa ni huyu mmoja tu! Hivyo ana Extra special place in my heart and life!

Mimi huwa nikiandika kitu chochote ambacho kinagusa hisia zangu huwa sirudii kukisoma mpaka muda upite sanaaaa! Yani huwa napenda ku-present my raw feelings! Napenda mtu apate ujumbe kwa jinsi nilivyo jisikia mara ya kwanza. Ndio maana hata kama kuna makosa ya kiherufi (spelling error) huwa naacha hivyo hivyo mpaka nitakapo jiona nipo tayari kusoma hisia zangu katika maandishi ya uhalisia wake! Haya ngoja nitiririke kama ifuatavyo ??


https://www.alphaigogo.com/ni-kwa-neema-tu/

Haya yani hapa nimesha weka kumbu kumbu sawa za toka akiwa na miaka 18 mpaka leo ??? Yani hii hata siku Mungu akinijalia wajukuu basi watakuja ona jinsi nilivyo mpenda mama yao nao itabidi wampende hivyo hivyo, sitaki utani na mwanangu mie ??

Happy birthday Mercy, mjukuu number moja, ubarikiwe sana. Nakupenda leo, nitakupenda zaidi kesho, na milele nitazidi kukupenda.

Keeping up with Blessing: Happy sixth birthday

Happy sixth birthday my twin sister! May God richly blessed you. Love you and missing you terribly!

Happy birthday to my mama!

      
      Shout-out this this beautiful lady, humble soul, prayer worrier, woman who gave birth to me! Today is her birthday, namuombea mibaraka mingi zaidi ya hapa, Mungu azidi kumbariki, naomba uzingatie kuwa nimesema "naomba Mungu azidi kumbariki" kwa I naamini kuwa ameshabarikia kitambo ila naomba Mungu amzidishie isipungue hata moja! Namuombea afya njema na furaha tele. Happy birthday mama, I love you!

Happy birthday Mrs Mapigano Peter

"Women are many, but wifely women are not only few, but they are very rare. Actually, true wives are gotten from God, im not hesitant to declare you are wife from God. Your blessings are innumerous to me since we got wedded. I cant mention all, among them being the peace i enjoy being with you, the beautiful kids you gave me, the great care you manifested to both live and stay with my great mummy something that few women could do.I pray that God gives us a gift to inherit the kingdom of heaven together with our beautiful kids. That when God comes the 2nd time, we together meet the Lord in the granduer of heaven and in surpassed glory of our Lord Jesus Christ. HAPPY BIRTHDAY MY DEAR GREAT WIFE! Amen. Salome Achayo" ~~~ from caring husband Mapigano Peter

Happy birthday Mrs Mapigano, Mungu wa rehema akuzidishie baraka zake katika kila utendalo na utamanialo. Uzidi kuwa baraka sio tu kwa mumeo na familia yenu bali kwa kila mtu aingiaye ndani ya malango yako na popote pale upitapo. Happy birthday Salome!.... Napenda sana nikiona kama zangu wakimimina hisia zao kwa wake zao kwa upendo na furaha kama hivi mbele ya jamii. Inaonyesha mwanaume anaye jitambua, kujiamini, kujali, na kumpenda mkeo bila kuogopa. Nashindwaga kuelewa wale waliokula viapo vya ndoa mbele ya kadamnasi lakini hutakaa umsikie hata siku moja akimsifu au kumshukuru mkewe mbele za watu! ?? Mwanaume wa kweli lazima amsifu na kumshukuru mkewe in public and in private! Lasivyo kunashetani ananyemelea ndoa yenu ?

 

Happy birthday Cookie

Happy birthday mwanangu Cookie Moses Iyobo! Mungu akujalie afya njema, maisha mazuri yaliyojaa amani na furaha, na zaidi ya yote akujalie kumjua na kumtumikia yeye Mungu muumba wa Mbingu na Dunia. Happy birthday beautiful, much love from aunt Alpha. Β @auntyezekiel naomba copy ya movie ya Cookie (Mama) nasi tutizame please

Neema Ndepanya: HAPPY BIRTHDAY Mwanamke uliyenifanya niwe hapa nilipo

Regrann from @neema_ndepanya  -  Niandike nini sasa kuhusu wewe mwanamke jamani??Β My mom

My Everything

My woman

Mungu wangu wa pili duniani

Am speechless???

HAPPY BIRTHDAY Mwanamke uliyenifanya niwe hapa nilipo...

Nakupenda sana mama angu!!

@kisa_ndepanya @kisa_ndepanya  - #regrann Β 

Nami naomba niungane na Movie Director wanguvu kumtakia mdogo wangu kipenzi Kissa Ndepanya kheri na baraka ya siku ya kuzaliwa kwake. Mwenyezi Mungu aliyejaa neema akuzidishie baraka zake kimwili, kifedha, na kiroho. Happy birthday Kissa, love you babysister ?❀

Lady JayDee: I cherish your love and care because you have made me stronger in my daily trials. You’re my rock

Regrann from @jidejaydee –Β Today is a special day because it marks your birthday. I’m wishing you good health, success in your business and many more years in your life. For a period that we have been together, you have proved to be a true pillar of support during my struggle. I cherish your love and care because you have made me stronger in my daily trials. You’re my rock. Thank you for always being here when i need a shoulder to cry on . I love you today , tomorrow and yesterday β™₯️β™₯️β™₯️β™₯️β™₯️

Happy birthday @spicymuzik

#WeBelongTogether – #regrann

Happy birthday Tanzanian Princess and African pride!

Regrann from @jokatemwegelo – March Baby ??. March Queen ????‍???‍?. Soon to be somebody’s Wife ??and Mummy??. God is Great and Faithful. Grown but forever a baby girl ??. Ni kwa neema tu na rehema. Thank you loves for dragging me out to take these @divaglam_beauty @petefarasi9 @jacquescollection Nawapenda ❀ ~ otherwise I couldn’t be bothered ? #Kidoti #Kidoti2018 – #regrann

Happy birthday to our one and only one Jokate Mwegelo, Tanzanian Princess and African Pride! Wishing you abundantly blessings, endless happy momoments, and forever love! ……. Awwih! Am happy to hear the good news please usininyime mualiko hata kama sina hela nitakopa kwa baba yangu Dr Magufuli ili tu nije Β kwa send off na harusi yako ??? (I am very serious though). Nakutakia kheri milele zote. Love you sanaaa ?❀