Leo ni siku ya kuzaliwa dada yetu, uzao wa pili wa familia yetu. Ni huyo mwenye nguo ya rangi ya Blue. Yeye kwa sasa anaishi Tabora lakini alikuja Dar kwa mambo fulani hivyo mdogo wangu akatumia nafasi hiyo ya pekee kumuandalia chakula cha mchana kufurahia maadhimisho ya siku hii. Tunamtakia kheri na baraka zote, Mungu atembee naye mwaka mwingine na milele zote ????
“Wamama na Wababa wa Wajukuu wetu, habarini za asubuhi njema ya leo. Leo nawasalimu kwa salaam ya kipekee, maalum ya kuhitimisha hiyo tafrija ya aina yake, yenye kunikumbusha miaka takriban 45 za Malezi yetu kwa huyo Mdada wenu na Mama wa wajukuu wetu wapendwa. Elline ana historia ya maisha yanayosadifiana na yangu, mie Baba yenu. Maisha yangu duniani yalianza kwa taabu ya afya dhaifu kwa kuwa niliwahi kutengana na lishe ya Mama tumboni mwake, nikazaliwa NJITI??♀️??Nakawa ngangari hadi leo hii bado nadunda japo udogoni nilikiona cha moto, kama Rafiki yangu, Binti yangu mpendwa Mama Min Ji. Alikuwa na afya mgogoro mno udogoni, naye kama nilihadithiwa na Mama kwamba bila huruma na upendo wa Baba yangu, yeye aliisha kata tamaa kwamba nitaishia utotoni tu, naye Nyategi kusema kweli nilimhangaikia vya kutosha utotoni, tukiwa na kipato kidogo mno, hadi hadi katengemaa na leo twasherekea siku yake ya 16,425 hapa duniani, Namuombea azidi kutengamaa na kupata tena siku kama hizo na kuzidi, hapa duniani. ????. Upendo wenu na mshikamano huu mliyonayo iwe ni mizizi inayo sambaa kwenye uzao wetu na kuendelea kwa vizazi na vizazi vijavyo. Nawatakia Sherehe njema, yenye Amani tele na kueneza Upendo wa JK milele.” * Baba mzaa chema -Sir O.O Igogo
Hapa wakiwa Tabora, ambapo mdogo wetu Janeth (aliyebeba mtoto) alikwenda kuwatembelea mwanzoni mwa mwaka huu!