Pumzika kwa amani ya Bwana mtoto wa dada yangu!

Kutoka kushoto: Alpha mkubwa, Alpha mdogo (R.I.P) na dada Pendo Igogo (mama Alpha).

Pumzika kwa amani ya Bwana wajina wangu Alpha! Ilikuwa heshima kubwa sana pale ulipo zaliwa, dada yangu Pendo Igogo akasema huyu mwanangu nampa jina Alpha kumuenzi mdogo wangu anipendaye sana. Ilikuwa ndio njia pekee ya yeye kunionyesha upendo wake kwangu na jinsi anavyo shukuru kwa upendo wetu kama madada.

Kutoka kushoto: Janeth Igogo, Alpha mkubwa, dada Pendo, Alpha mdogo, na nyuma ni mama yake Pendo mke wa marehemu baba yangu mkubwa.

Alpha, kifo kimeumbiwa mwanadamu lakini sikutegemea maisha yako yangekuwa mafupi namna hii! Leo hii umemuacha dada yangu akiwa si tu mlemavu wa viungo bali moyo uliyojaa maumivu makali sana. The only child she had! Ulizaliwa kama miujiza kwani wengi hata madaktari hawakuweza kuwamini mwanamke mwenye ulemavu wa viungo aina ya mama yako angeweza kubeba mimba kwa miezi tisa na kujifungua mtoto! Na sasa umemuacha mama mkiwa!

Kutoka kushoto: Magreth Igogo, Alpha mkubwa, dada Pendo, Alpha mdogo, na nyuma ni mama yake Pendo mke wa marehemu baba yangu mkubwa.

Baba yako ndie mwanaume aliyempenda dada yangu na akamuoa na Mungu akaibariki familia yao kwa kuwapa mtoto Alpha. Leo hii wote wewe na baba hamponae tena mmemuacha kama alivyo! Kweli maisha ni fumbo na Mungu mwenyewe ndio mwenye kuweza kulifumbua! Nasikiaga wakisema kuwa “ng’ombe wa masikini hazai” na leo umenifanya niamini huu msemo kwa viwango vingine kabisa!

Pumzika kwa amani mrembo, tutakutana asubuhi njema!

Bwana ametoa na Bwana ametwaa jina lake litukuzwe milele! ????

Leave a Reply