Safari ya mama Washington DC

Siku ya tarehe 13 mwezi huu wa Tano, mimi na mama yangu tulisafiri kidogo kwenda mji mmoja unaitwa Washington DC. Huu mji ni makao makuu ya U.S.A hivyo nilikuwa nakwenda kumuonyesha mama Makao Makuu ya Marekani na pia kwa kuwa ilikuwa ni siku ya wakina mama duniani hivyo ikawa pia kama sehemu ya Mother's Day treat! Safari yetu ilianzia Houston, Texas hapo kwenye picha ni mama akiwa kwenye train kuelekea terminal ambayo tulipandia ndege. Kitu ambacho nimejifunza katika changamoto za kutaka kufurahia maisha  na kuwa na amani na watu, nikuwa siku zote kama unataka kufurahia matembezi yako binafsi basi nivizuri uwe umejiandaa kufurahiya bila kubugudhi watu wengine. Labda kama kweli unaamini hakuta kuwa na maneno ya chini au kuchafuana kwa majungu basi fikia kwa mwenyeji wako lasivyo Starehe kwa size ya Wallet yako ??? Nasema haya kutoka na experience ambazo nimewahi kuzipata au nimeona baadhi ya watu wakipata (Hii ni topic nyingine kabisa ipo siku nitaileta). Kiufupi hapa ndipo nilipo amua kufika.  Hapa tulikuwa tukipata Mother's Day dinner @Tony Cheng's restaurant.  Mama yangu anamatatizo ya tumbo, tupo extra careful na nini anakula. Kwasasa Chinese food ndio vipo salama kwa tumbo lake. Hapa tulikuwa tukipata Chinese menu kwenye restaurant moja iitwayo Tony Cheng's ndani ya Chinatown, hapo Washington DC.  Mimi mwenyewe baada ya kula, nguvu tele ya kuzunguka kidogo kabla ya kurudi hotelini.    Baada ya kula na kuzunguka kidogo Chinatown nikampeleka mama kuona WhiteHouse ya Marekani. Kwasababu hatukuwa na huwakika lini tungekwenda hivyo ilikuwa ngumu kwangu kuweka appointment ya kupewa tour ya ndani ya WhiteHouse. For security purposes inahitajika at least one month appointment kabla ya kwenda. Lakini hata hii tu ya nje ya jengo alifurahia.  Mama yangu hanaga makuu ??

*** hii ni part one, nitamalizia nyingine baadaye***

Leave a Reply