Jokate Mwegelo: Muhimu kujipanga kutumia fursa hizi zinazotengenezwa na serikali zetu hizi

Jokate Mwegelo
Tarehe 14/01/2018. Rais Magufuli wa Tanzania alimkaribisha Rais @paulkagame wa Rwanda, Dar es Salaam- Tanzania katika ziara ya kikazi.  Katika ziara hii walirejea mazungumzo juu ya ujenzi wa reli kati ya Isaka na Kigali lakini pia reli hii itaenda mpaka Musongati- Burundi kupitia Keza. Reli iliyopo hivi sasa ni kati ya Isaka ambako kuna bandari kavu na Dar yenye urefu wa kilometa 970- reli ya kati. Na hii reli mpya kati ya Isaka na Kigali itakuwa ya urefu wa kilometa 494. Ujenzi huu utasaidia usafirishaji wa bidhaa na watu kwa urahisi na kupunguza gharama za usafirishaji lakini pia itasaidia kuboresha maendeleo ya kiuchumi. Nchi za Rwanda na Burundi na mpaka DRC ambazo ni “landlocked” watazidi kuona unafuu katika kutumia bandari yetu kutokana na usafiri kuwa wa kuaminika. Mradi huu unabeba pia dhima za EAC, CEPGL na COMESA zenye kuhamasisha “inter-state transportation structures”. Hizi ni hesabu nyepesi. Kwa miaka mingi maendeleo ya biashara ya bidhaa, huduma na usafirishaji wa mazao ya kilomo, madini mbalimbali n.k kati ya nchi za Afrika zimekuwa zikikabiliwa na changamoto ya gharama kubwa za uzalishaji ambapo pamoja na sababu nyingi zingine zimechangiwa sana na ukosefu wa usafirishaji wenye kueleweka. Ujenzi huu utasaidia kufungua maeneo haya na kugusa makundi mengi hasa vijana kiuchumi. Muhimu kujipanga kutumia fursa hizi zinazotengenezwa na serikali zetu hizi. Tufuate kule serikali inapowekeza na kuona jinsi gani tutaweza faidika. Pia tupende kujifunza juu ya mipango ya serikali na tuone tunanufaika vipi na tuhoji. Niwatakie siku njema. ❤️ 

Leave a Reply