Category Archives: Pongezi

Sherehe ya kuagwa kwa Rhoda Igogo!

Siku ya Jumapili ya tarehe 05/23/2021 ndio ilikuwa siku rasmi ya kuagwa kwa bibi Rhoda Alexander Igogo. Sherehe hiyo ilifanyika nyumbani kwa baba yake mlezi huko Segerea. Zifuatazo ni baadhi ya picha na video kutoka kwenye tukio hilo. Picha hazipo kwenye mpangilio rasmi nimeweka tu!

Bibi harusi mtarajiwa akiingia ukumbuni

Mr Victor na mkewe mtarajiwa!

Rhoda na mpambe wake bi. Oliver Chumo

Oliver

Baba mubwa wa Rhoda, mzee Charles Olung’a Igogo

Wazazi wa bwana harusi mtarajiwa, Mr and Mrs Ollal

Wanandoa wapya Mr and Mrs Isaka Alexander Igogo

Mama mdogo wa Rhoda, Mrs O.O Igogo akipungia wageni

Baba mkubwa wa Rhoda, mzee Charles Olung’a Igogo (kushoto) pamoja na baba mlezi mzee O.O Igogo

Dada wa bwanaharusi mtarajiwa Ms. Aphino Alexander Igogo, pamoja na mdogo wa bibi harusi mtarajiwa Blessing Igogo wakimkaribisha shemeji yao kwa furaha.

Rhoda na mama yake mzazi

Bwanaharusi mtarajiwa akiwa na bibi yake mzaa mama yake.

wageni waalikwa wakiwa na mwenyeji wao mzee O.O Igogo

Mc Rhevan katika ubora wake

Bibi harusi mtarajiwa number 2 akitoa ombi la mwisho.

Rhoda akitoa zawadi ya keki kwa Mkurugenzi Mkuu wa Utegi Technical Ltd, Mrs Margaret Mabada kwa niaba ya wafanyakazi wote wa Utegi ambapo Rhoda ameajiriwa.

Rhoda akicheze na wafanyakazi wenzake

Baba na binti yake wakicheza

Kwa picha zaidi bonyeza ????

https://RHEVANSTUDIO2021.pixieset.com/rhodasendoffpartyphotos/

NYONGEZA: HARUSI YA ISAKA NA SARAH.

Video hapo juu ni muhtasari wa harusi ya Isaka na Sarah, imetengenezwa na studio za Mc Rhevan.

Mr and Mrs Jacob Massawe

Zifuatazo ni baadhi ya picha za ziada na video zilizotengenezwa na camera binafsi za wanandugu. Naziweka humu ili ziwe sehemu ya kumbukumbu. …… Hapo juu ni dada wa bwanaharusi Magreth Rhoda-Nyasungu a k.a Magreth Otieno Igogo a.k.a Mrs Massawe akiwa sambamba na laazizi wake ambaye ni Shemeji wa bwanaharusi. #Warombo #SweetMangi ??

Mama Dia a.k.a Cheusi akiwa na best ake mama Igogo

Dia Alex Odemba akideka kwa bibi yake.

Mrs. Massawe

Shemeji yake Isaka, Mr. Massawe (kushoto) akiwa na kaka zake Isaka, Mr. Albetus Ajee Chuche (mtu kati) na Mr. Guka Otieno Igogo (kulia).

Mashabiki wa Simba nao walipewa haki yao! ?

Hongera sana Mh. Jokate Mwegelo

#RepostSave @jokatemwegelo with @repostsaveapp  Amini Mungu ni mwingi wa rehema kamwe hamtupi amtumainiye yeye!! Ahsante Mungu Wangu.

Labda ni-share kitu kidogo, kuna muda mwaka jana mwishoni nilikuwa so down nilitamani kukata tamaa na kila kitu kwenye maisha nilikuwa pia sijaelewa vizuri hatma yangu kwenye siasa. Nilikuwa kwenye mkutano mkuu wa chama kuna mdada mmoja kutoka Arusha akanikimbilia na kunikumbatia kwa nguvu sana alikuwa na mama mmoja hivi walikuwa wamekuja kupiga picha namimi. Huyo dada mdogo hivi akasema ananipenda sana sana na mimi ndio nilimfanya aingie kwenye siasa na akagombea nafasi kupitia mkoa wa Arusha akashinda!! Nikabaki natabasamu. Ikanipa nguvu kubwa ya kupiga moyo konde na kusonga mbele. Nilifurahi kuona kuna mdada nimeweza kumhamasisha na kumpa ujasiri wa kugombea. Unaweza ukawa unapitia mitihani migumu sana kwenye maisha yako lakini inakubidi usikate tamaa saa zingine kwasababu tu ya wale wanaokutegemea, wanaokuangalia na kuvutiwa nawe na kujifunza kupitia maisha yako. Lakini zaidi kwasababu safari ya mafanikio ina milima na mabonde, inabidi upambane na kiukweli hakuna mafanikio yasiokuwa na changamoto. Na kuna muda changamoto ndio haswa zinatengeneza “character” zetu. .

Kikubwa zaidi wakati wa changamoto tukumbuke kuwa wanyenyekevu, wenye kujishusha na kumuomba Mungu aendelee kutupa imani, hekima na busara ya kusubiri wakati wake. Tukumbuke Mungu hamtupi mja wake. Nawatakia Jumapili Njema. Nawapenda Sana. Ahsanteni ??”

Ninafuraha sanaaaa! Hongera sana mdogo wangu Muheshimiwa Jokate Mwigelo kwakuteuliwa kua  Mkuu wa Mkoa wa Kisarawe. Mwenyezi Mungu akuzidishie mibaraka yake, ukaongoze kwa hekima, na busara kwa faida ya wana Kisarawe na taifa la Tanzania kwa ujumla, zaidi ya yote utukufu wa Mungu ukapate onekana mbele za watu. Hongera sana tena sana! #WanawakeTunaweza

Hongera sana Mh. Jerry Muro

"Namshukuru Mungu kwa Kunipa Kibali cha Kumsaidia kazi Mhe, Rais, Dkt. John Pombe Magufuli katika Nafasi Ya Ukuu wa Wilaya ya Arumeru, Nakushuru Mhe, Rais, Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na Viongozi wote Waandamizi wa Serikali kwa kunipa Jukumu Hili la kuwatumikia wananchi wa Meru.#WakatiWetu #MeruYetu #TanzaniaYetu"
Naomba kutoa pongezi zangu za dhati kabisa kwa Mkuu wa wilaya mpya wa Arumeru Mh. Jerry Muro. Nakuombea uongozi bora wenye haki na tija  kwa maendeleo ya wilaya ya Arumeru na taifa kwa ujumla!. Hongera sana!

Mama Keagan: Asante Mungu

Regrann from @nikypal8585  - Asante Mungu wewe ndio uliyenipa huyu mtoto  keagan P .Makonda ? wewe ndio mtendaji na msemaji wa mwisho.Umefanya kwa wakati ulio ona ni sahihi ???? umenipa mtoto wangu Keagan  najua ulikuwa na sababu kwanini haikutokea wakati nilipotaka mimi. Mimi ni ushuhuda kamili katika maisha ya kila mwanamke au msichana aliyekata tamaa. Usiogope  kaa kimya jipe moyo tamka hili neno moyoni mwako MIMI NI USHUHUDA  ULIOKAMILI SITA TETEREKA KAMWE MUNGU NITENDEE  JAMBO LANGU KWA WAKATI  ULIOSAHIHI NA ULIO UPANGA  WEWE  AMEN???????  -  
Asante Mungu kwa ajili ya mume wangu Paul (Baba keagan)hakika wewe ni jeshi lisilo tetereka kwani imani yako imepimwa kwa njia tofauti ila ulisimama imara??kwa machozi ya kishujaa,ulinitia moyo  sana ukuchoka kusema mke wangu wakati  wa Bwana huwa ni sahihi pangusa machozi mshukuru Mungu kwani  alikuwa amekuandalia faraja ya kudumu.Hakika nimemwona Mungu kila wakati nilipo pata jaribu nilijifunza kukaa kimya na kujipa moyo wa ushujaa na kusema hakuna mwanadamu anayeweza kukamilisha hii furaha ya mimi kuitwa mama na kupakata mtoto aliyetoka kwenye tumbo langu.Nasema tena  na tena upendo wa Mungu kwangu hauna kipimo kwani kanipa kicheko na rafiki wa kudumu .Nawapenda wanangu #PK nitawaleanakuwaombea daima ❤️❤️❤️❤️❤️❤️ASANTE MUNGU????  - #regrann

Hongera Mh. Janeth Masaburi

Well! Kama nilivyo wahi sema huko nyuma kuwa kuna ndugu zagu ambao ni wanasiasa, hivyo inapofikia kwenye kutoa pongezi basi sina budi! Kwa maneno hayo, napenda kuchukua nafasi hii kumpongeza my aunt Mrs Janeth Masaburi kwa kuteuliwa kuwa Mbunge wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania. ......Hongera sana, natumaini kuona sheria nzuri za kulinda na kutetea watoto na wanawake haswa katika kutimiza malengo ya dunia ya uchumi wa viwanda kwa wanawake!

Hongera Jesca Wahuru: Mwenyekiti wa vijana mkoa wa Iringa (CCM)!

Jesca Wahuru: Mwenyekiti wa vijana mkoa wa Iringa

“Tareh 22.9 2017 Mungu aliweka historia nyingine kwenye maisha yangu. Ukijishusha Mungu atakuinua na ukijikweza Mungu atakushusha. Asanteni kwa kunikopesha kura zenu nawaahidi nitawalipa utendaji……..  Asanteni kwa kuniamini”~~~~~~~~~ Jesca Wahuru

Mimi siyo mwana siasa nawala sitegemei kuingia kwenye siasa maishani mwangu! Just show me where “money” is; I will meet you there! Better be 100% genuine though ?? I’ve my daughter and a life to live, for that prison ain’t my favorite place to be ??……….Ok! Back to our story! Japo mimi si mwana siasa lakini nina ndugu zangu ambao wanapenda siasa, na wengine siasa ndio carrier zao. Mfano mzuri ni huyu wifi yangu Jesca Wahuru, yeye ni Mwalimu kwa taaluma lakini siasa pia ipo kwenye damu yake. Anapenda siasa sana, na chama chake kipenzi ni CCM! Sasa juzi kati alichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa vijana mkoa wa Iringa. Kwa maana hiyo naomba nichukue nafasi hii kumpongeza sana kwa hatua hiyo. Namuombea awe kiongozi mzuri ambaye ataweka maslahi ya nchi yake mbele na chama nyuma! UZALENDO! UZALENDO! Niwajibu wa kila raiya kuwa mzalendo kwa nchi yako, hivyo muwe wazalendo! Hongera sana. #WanawakeTunaweza

Dr. Ntuyabaliwe Foundation yakabidhi Library!

Naamini wengi mtakuwa mmesikia kuhusu hii giving back to community foundation ambayo inakwenda kwa jina la “Dr Ntuyabaliwe”. Kama hujawahi kusikia habari hiyo basi huu ni mfuko ulio anzishwa na Jacqueline Mengi kumuhenzi baba yake mzazi ambaye alikuwa medical Dr I believe alikuwa Gynecologist  (please kama nimekosea unaruhusiwa kunisahihisha) lakini naamini alikuwa Gynecologist. Anyway, Jacqueline amekuwa anasaidia mambo mbali mbali kwenye jamii kwa kutumia mfuko huu.  Amekuwa akitoa vifaa vya hospitali (incubator)  vya kutunzia watoto ambao wanazaliwa premature / njiti, madawati ya shule na vifaa mbalimbali vinavyotumika mashuleni. Wiki iliyopita alikabidhi Maktaba / Library kwa shule ya awali ya Makumbusho iliyopo jijini Dar es salaam. Na hii ilikuwa mara ya pili kwa Jacqueline kujenga library kwa shule kwa kutumia mfuko huu wenye jina la baba yake. Kama picha inavyo jieleza hapo ilikuwa wanakabidhi library ya kwanza. Hongera sanaaaaaa Jacqueline, such an inspirational. Kama unafatilia hii blog basi utakumbuka huko nyuma niliwahi kusema kuwa sasahivi Jacqueline yupo kwenye “public eyes”  hivyo jamii itapata nafasi ya kumjua Jacqueline ni nani haswa ( her character) and I have to  admit the more I look at her the more I love her! Just lovely and beautiful. Haya na Molocaho hiyo inakwenda Dubai kwa maonyesho. Mungu akisema Yes hakuna wa kukuzuia! You go girl! Hongera Sanaaaaaa ??

Matukio katika picha: Hongera Dr. Nai kwa kuvishwa pete ya uchumba!

fb_img_1474806992131screenshot_2016-09-25-07-37-15-1fb_img_1474807010314Hongera sana Dr Nai, nakutakia baraka tele katika safari ya hii ya maisha yako mapya unayo tarajia kuanza. Mungu akutangulie katika kila jambo na mipango yote uliyo nayo! screenshot_2016-09-25-00-45-46-1 Fundi / designer wako anajua sana ku-designe na kushona nimeangalia nguo zake kadhaa kwakweli ni mtaalam! fb_img_1474807000925The Doctors themselves! Pendeza sana…….hongera pia kwa mama Dr. Victoria Kisyombe kwa kule binti na sasa unamuozesha. Mungu kumbariki sana. And once again congratulations to you Dr. Nai!